Chadema Iringa Mei 19, 2011: Picha na Matukio

Chadema Iringa Mei 19, 2011: Picha na Matukio

tunasubiri kwa hamu picha kamili za maandamano na mkutano, mliopo huko eneo la tukio mtujuze kadili mtakavyoweza!
 
IMG_8161.JPG
 
kazi nzuri - asante mkuu

Duh Kumbe Iringa nako kuna WACHAGA wengi hivi.

kazi kwako nape...
 
Asante Sana Francic (fmpiganaji). Nimeziona. Najihisi kama niko Iringa. Big up wana Iringa.
 
bora huyu anawapa maneno ya hekima huku kasimama nao kuliko kuwagawia pipi akiwa kwenye VX kama mzee wa kaya.
 
CHADEMA hawana uchungu na wananchi kwa sababu;-
1. Kipindi cha kilimo wameenda Nyanda za Juu Kusini na kutibua harakati za wananchi kujitafutia ridhiki kupitia mashambani.

2. Kuwafanya watoto washindwe kwenda shule na kufuata gari lao la matangazo. Hapa Dr. Slaa anatoonyesha mfano mbaya kwa kuwapotezea taifa la kesho muda wao wa kwenda shule na kupata elimu.

3. Viongozi wa CDM hawana utashi wa kulipa kodi ingawa ni hodari wa kula mapesa ya wananchi kupitia ruzuku.

HAWA CDM waogopwe kama kipindupindu!!!!!

Ina maana Nape na Mukama hawakuyajua hyao walipokuwa Singida na Mara?
 
picha zote hizo ni mwanzo kabisa mwa maandamano
 
si kuna chama kilikuwa na mgombea wake alikuwa anakaa kwenye mavumbi anakumbatia wadada walemavu..hivi ni wa chama gani yule
 
CHADEMA hawana uchungu na wananchi kwa sababu;-
1. Kipindi cha kilimo wameenda Nyanda za Juu Kusini na kutibua harakati za wananchi kujitafutia ridhiki kupitia mashambani.

2. Kuwafanya watoto washindwe kwenda shule na kufuata gari lao la matangazo. Hapa Dr. Slaa anatoonyesha mfano mbaya kwa kuwapotezea taifa la kesho muda wao wa kwenda shule na kupata elimu.

3. Viongozi wa CDM hawana utashi wa kulipa kodi ingawa ni hodari wa kula mapesa ya wananchi kupitia ruzuku.

HAWA CDM waogopwe kama kipindupindu!!!!!

Nenda ukawaambia wananchi haya maneno yako ya kejeli uone kitakachokupata, watu wameshajichokea - maisha magumu hawana matumaini tena wewe unaongea usharobaro...

Wewe ulishawahi kushika jembe, ulishalala njaa hata siku moja? ulishawahi kukosa ada ukakaa nyumbani term nzima? ulishawahi kuugua ukakosa buku mbili za kujiandikisha kwa daktari?
 



KWA wiki kadhaa sasa, viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamekuwa wakifanya mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali ya Tanzania ambako wanazungumzia masuala mbalimbali yanayohusu uendeshaji wa nchi na kama ilivyotarajiwa, wakiikosoa Serikali pamoja na chama tawala katika masuala mbalimbali, ikiwamo uendeshaji na usimamiaji wa uchumi wa nchi.

Mambo mengi yamezungumzwa na viongozi na makada wa chama hicho katika mikutano hiyo, lakini jambo lililovutia wengi na kuchukuliwa kwa uzito wa hali ya juu na vyombo vya habari ni kauli zilizotolewa na mmoja wa makada wake, Fred Mpendazoe, aliyejiunga na chama hicho mapema mwaka jana.

Mpendazoe, ambaye alikuwa Mbunge wa Kishapu kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), aliamua kubwaga manyanga na kuondoka CCM Machi mwaka jana, akijiuzulu ubunge huku akitangaza kujiunga na chama kipya kilichokuwa kikijulikana kama Chama Cha Jamii, kwa kifupi CCJ, ambacho kuanzishwa kwake kuliandikwa sana na vyombo vya habari kwamba kimeanzishwa na baadhi ya vigogo kutoka CCM.

Hata wakati akitangaza kujiondoa CCM, Mpendazoe alisema wazi kwamba yeye amekuwa mtu wa kwanza kujitokeza hadharani kujiunga na chama hicho na kwamba baadaye, wenzake wengi wazito kutoka ndani ya CCM, wangemfuata na kujiunga naye kama ilivyokuwa imeandikwa katika vyombo vya habari.

Lakini kwa bahati mbaya, chama hicho kilishindwa kupata usajili wa kudumu ili kishiriki katika kinyang’anyiro cha Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa kubaini kasoro nyingi, ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa wanachama waliokuwa wameorodheshwa na chama hicho katika maeneo mbalimbali nchini. Chama hicho kikafa.

Kuona hivyo, Mpendazoe akaamua kujiunga na Chadema ili ashiriki katika uchaguzi na akagombea ubunge katika Jimbo la Segerea jijini Dar es Salaam, ambako kwa bahati mbaya aliangushwa na mgombea wa CCM, Makongoro Mahanga. Kesi ya kupinga matokeo hayo bado ipo mahakamani.
Mpendazoe ameibuka katika mikutano ya Chadema, kwanza ule uliofanyika wilayani Mbinga, Mkoa wa Ruvuma, alikomtaja Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM, Nape Nnauye, kama mmoja wa watu walioshiriki kikamilifu kuanzisha CCJ, huku akiahidi kuwataja viongozi wengine wa CCM aliowaita wasaliti na wapenda vyeo.

Mjini Njombe, kada huyo wa Chadema aliwataja Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe kama miongoni mwa viongozi wengine kutoka CCM walioshiriki moja kwa moja katika kuianzisha CCJ. Anadai kuwa mwanzilishi halisi, aliyejitolea muda na mali kuanzisha chama hicho ni Sitta.

Kwa vyovyote vile, kwa chama makini kama CCM, tuhuma za aina hiyo ni nzito sana kwa sababu kama ni za kweli, basi zinaashiria kuwapo kwa wasaliti ndani ya chama ambao wapo tayari kuanzisha chama kingine kwa lengo la kutimiza ndoto zao za kisiasa.

Chama Cha Mapinduzi sasa kipo katika harakati za kujivua gamba kwa kuondoa kenge waliovamia kwenye msafara wa mamba na tunadhani usaliti katika chama ni moja ya dhambi kubwa zinazotakiwa kupatiwa adhabu ya hali ya juu ikiwa ni pamoja na kuwaondoa wahusika wote ndani ya chama.

Si kazi yetu kuwafundisha kazi viongozi wa CCM, lakini kama kweli kina nia ya dhati ya kujivua gamba, kinatakiwa kizifanyie kazi kwa kuzichunguza kwa makini tuhuma hizi nzito zinazotolewa na Mpendazoe na kama ikibainika kuwa kuna ukweli ndani yake, basi hatua zinazofaa zichukuliwe ili kufanikisha falsafa yake ya kujivua gamba.
 
Heading haijakawa sawa, rekebisha kwa ku-specify nani azichunguze
 
Asije akaiona hii post kuwa ili watoto wamshangilie ni lazima awagawie pipi ina maana hata mvuto hana

baada ya milipuko ya mabomu ya gongo la mboto, kikwete alitembelea hospital moja lengo ni kuwapa pole cha ajabu akiwa anazunguza na wahanga hao alimuona mtoto akimyweshwa uji basi ki kwete akachukua kijiko kutoka kwa mama aliekuwa akimywesha mtoto huyo, akachota uji ili amyweshe mtoto yule alikataa kabisa basi kikwe te akaondoka kwa aibu..
 
Back
Top Bottom