GE2025 CHADEMA inakwenda shimoni

GE2025 CHADEMA inakwenda shimoni

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Heshima sana wanajamvi.

Nimekaa pale natafakari na kujiuliza mambo mengi sipati majibu.

Natazama hizi kesi za michongo na hukumu za michongo naiona chadema inapitia mkondo ule ule wa NCCR-MAGEUZI.

Ngongo kwasasa Tanga Michungwani.
Ungejua hata Mitume na Manabii walipitishwa katika mitihani mikubwa,sasa hivi hata mtu akitaka kuhamia Chadema anajiuliza mara mbilimbili,ndiyo maana wengi wanaenda ACT WAZALENDO na CHAUMMA
 
..dhana kwamba tukae tukisubiri upinzani wa kweli utoke ndani ya Ccm ni potofu.

..kwanza tumetokea katika mfumo ambao kabla ya 1992 kila Mtanzania mtu mzima alikuwa ni mwana Ccm.

..kwa hiyo vyama karibia vyote vya upinzani vilianzishwa na watu waliotokea Ccm. That is a HISTORICAL fact.
Na hawa ambao ni upinzani, wanarudi CCM kwa direct au indirect way. Wachache walio dhamiria ndio hao kina Lissu unawaona wanachofanyiwa na hadi na watu ambao waliaminika na upinza walivyo piga U-Turn
 
Heshima sana wanajamvi.

Nimekaa pale natafakari na kujiuliza mambo mengi sipati majibu.

Natazama hizi kesi za michongo na hukumu za michongo naiona chadema inapitia mkondo ule ule wa NCCR-MAGEUZI.

Ngongo kwasasa Tanga Michungwani.
Prof Ngongo habari za huko😅
 
Na hawa ambao ni upinzani, wanarudi CCM kwa direct au indirect way. Wachache walio dhamiria ndio hao kina Lissu unawaona wanachofanyiwa na hadi na watu ambao waliaminika na upinza walivyo piga U-Turn

..tusiwalaumu wanaorudi au wanaohama upinzani kwenda Ccm.

..kuna mateso na dhuluma ambayo wapinzani wanapitia na kusababisha wengine wakate tamaa na kwenda Ccm.

..tuilaumu Ccm kwa matendo yake ya kikatili, kinyama, na dhuluma, wanayowafanyia viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani.
 
Heshima sana wanajamvi.

Nimekaa pale natafakari na kujiuliza mambo mengi sipati majibu.

Natazama hizi kesi za michongo na hukumu za michongo naiona chadema inapitia mkondo ule ule wa NCCR-MAGEUZI.

Ngongo kwasasa Tanga Michungwani.
JK alijaribu akashindwa.
Jiwe alijaribu akashindwa.
Mbowe + Samia + CCM + Ngongo + Fundi Mchundo wamejaribu, wanaendelea kujaribu, lakini matokeo ni yale yale, mnashindwa.
 
Heshima sana wanajamvi.

Nimekaa pale natafakari na kujiuliza mambo mengi sipati majibu.

Natazama hizi kesi za michongo na hukumu za michongo naiona chadema inapitia mkondo ule ule wa NCCR-MAGEUZI.

Ngongo kwasasa Tanga Michungwani.
Ah, Hapo michungwani msalimie Ali Samkonje, Wasalimie hapo wahuni wanaokaa chini ya miembe apo sunrise wanao toboa mifuko ya sukari, mchele, sabuni, nk.

Wasalimie hapo Rembo, Wasalimie hapo juu wanapo uzaubwabwa wa nazi nimepasahau jina.

I Miss the place for quite longer.
 
Heshima sana wanajamvi.

Nimekaa pale natafakari na kujiuliza mambo mengi sipati majibu.

Natazama hizi kesi za michongo na hukumu za michongo naiona chadema inapitia mkondo ule ule wa NCCR-MAGEUZI.

Ngongo kwasasa Tanga Michungwani.
Mkuu Ngongo heshima kwako.

Bila shaka wewe ni mdau mkubwa wa CHADEMA uliyeshiriki kujenga chama hicho kwa dhamira kubwa kivitendo tofauti na baadhi ya wadau wanavyokuhisi hapa. LAKINI sidhani kama umepatia kulinganisha mkondo inaopitia CHADEMA hivi leo na ule iliopitia NCCR-Mageuzi enzi zile. Labda kama unataka kuonesha kutofurahia kwako jinsi chama kilivyo na kinavyoenenda nyakati hizi.

Muhimu kwako katika uzi wako huu ni kutoa mawazo na mikakati jinsi CHADEMA inavyoweza kuepuka kwenda shimoni (kama unavyoona). Usipoteze muda kujibu michango yenye jazba. Be positive. Umeleta uzi, utendee haki; toa hitimisho lenye tija.

***********

Binafsi, tangu dola iamue kukamilisha michakato yote ya chaguzi mezani/ofisini na wananchi kutangaziwa matokeo tu, sioni kama CHADEMA wala chama chochote cha siasa kinaweza kufanya shughuli za siasa kwa haki nchini. (Hata CCM wamenywea). Wawakilishi wa wananchi ni wale wanaopitishwa na dola pekee. Ushahidi ni 2019, 2020, na 2024.

Katika mazingira haya, sioni kingine wanachoweza kufanya CHADEMA labda nao waamue kuwasaliti wananchi kama wanavyofanya CCM na vyama vingine washirika wao. Yaani waache kudai marekebisho (reforms) badala yake wapange foleni ya kuomba huruma ya dola kugawiwa viti vya uwakilishi!

Ni mwehu tu ndiye anayeweza kuamini kuwa 2020 CHADEMA ilipata mbunge mmoja (1) tu! Kama ni kuwa shimoni basi CHADEMA ilitumbukia tangu Oktoba 2020. (Linganisha matokeo ya 2015 na 2020).

Nilishangaa baada ya Oktoba 2020 kusikia CCM na serikali bado inatambua CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani nchini huku kikiwa na mbunge mmoja tu na halmashauri 0! Halafu 2021 yanaanzishwa mazungumzo ya "maridhiano" kati ya serikali na CHADEMA! Sitashangaa baada ya Oktoba CHADEMA bado ikiendelea kutambuliwa kama chama kikuu cha upinzani huku Msajili akiendelea kujiumauma kuhusu kuifuta kwenye rejesta!
 
..tusiwalaumu wanaorudi au wanaohama upinzani kwenda Ccm.

..kuna mateso na dhuluma ambayo wapinzani wanapitia na kusababisha wengine wakate tamaa na kwenda Ccm.

..tuilaumu Ccm kwa matendo yake ya kikatili, kinyama, na dhuluma, wanayowafanyia viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani.
Kutokea hapa, baada ya kuliona tatizo. Tujikite katika njia gani kupata solutions?
 
Kutokea hapa, baada ya kuliona tatizo. Tujikite katika njia gani kupata solutions?

..tuwaunge mkono na kuwatia moyo wapinzani.

..tulaani na tupinge ukatili na udhalimu unaofanywa na Ccm dhidi ya wapinzani.

..kuwalaumu na kuwabeza wapinzani ni kuwawezesha Ccm ktk udhalimu wao.
 
Heshima sana wanajamvi.

Nimekaa pale natafakari na kujiuliza mambo mengi sipati majibu.

Natazama hizi kesi za michongo na hukumu za michongo naiona chadema inapitia mkondo ule ule wa NCCR-MAGEUZI.

Ngongo kwasasa Tanga Michungwani.
Utakwenda shimoni wewe. CDM ni imani na haijapoteza imani kwa wanachama wake wa kawaida ukiachana na hawa kiduchu waganga njaa
 
Ndio unachotamani eh?

Mbowe mwaka jana alisema hakuna tume mpya hakuna uchaguzi halafu baada ya kushindwa anahudhuria dira ya mama anaulizwa vipi anasema yeye sio msemaji na wakati mjumbe wa kamati kuu ya chama.

Unafikiri ataaminika vipi kama kesi ya mwenyekiti aliyempokea kijiti haendi halafu kwenye hafla za Samia anakuwepo?

Najua watu mtatamani sana CHADEMA ife na hasa huu upinzani feki wa CHAUMMA na ACT uliopewa pesa za msimu kuhadaa watu ila mkae mfahamu watu kwa sasa wamejitambua na watawashangaza sana hamtoamini.

Kama CCM ilivyopoteza mvuto licha ya mabango, media, zinagawiwa pikipiki , baiskeli, miradi inapewa jina la Samia ila bado haiondoi watu wanachofikiria ndio ije kwa hivi vyama shikizi?
 
Matamanio yako dhidi ya cdm baada ya Mbowe kushindwa yanafahamika, ila uzuri sisi wafuasi wa cdm wengi tunajitambua na cdm ni imani. Hizi kesi zitapita maana sio halisi bali ni hujuma za kawaida kwenye nchi zenye vyama vinavyozeekea madarakani. Lakini cdm itazidi kuwa imara. Hiki ni kizazi kingine kabisa boss.
Hawezi kuelewa huyo, Kizazi cha sasa sio kile cha gizani cha NCCR.
 
Ndio unachotamani eh?

Mbowe mwaka jana alisema hakuna tume mpya hakuna uchaguzi halafu baada ya kushindwa anahudhuria dira ya mama anaulizwa vipi anasema yeye sio msemaji na wakati mjumbe wa kamati kuu ya chama.

Unafikiri ataaminika vipi kama kesi ya mwenyekiti aliyempokea kijiti haendi halafu kwenye hafla za Samia anakuwepo?

Najua watu mtatamani sana CHADEMA ife na hasa huu upinzani feki wa CHAUMMA na ACT uliopewa pesa za msimu kuhadaa watu ila mkae mfahamu watu kwa sasa wamejitambua na watawashangaza sana hamtoamini.
Watu wanajitambua sana, hizi hadaa zao zinazofadhiliwa na ccm ili kuihadaa dunia hazitofanikiwa.
Tutaionesha dunia na dunia itatambua kuwa watz hawataki janjajanja kwenye chaguzi
 
Watu wanajitambua sana, hizi hadaa zao zinazofadhiliwa na ccm ili kuihadaa dunia hazitofanikiwa.
Tutaionesha dunia na dunia itatambua kuwa watz hawataki janjajanja kwenye chaguzi
Ngoja muda ni mwalimu mzuri watu wanafikiri wimbi la mabadiliko linanulika kwa fulana na baiskeli mkweche.
 
Back
Top Bottom