Uchaguzi mkuu October 2025,labda tuendelee kusubiri lakini suala la mtu au watu si hoja kwasasa.
Ninachoangalia ni mpangilio mahsusi wa hizi kesi za kufungia chama.
Kesi ya Mwenyekiti na muda wa kampeni na hatimaye uchaguzi.
Tatizo la Watanganyika au Watanzania wengi ni kupenda kusikia kinachowapendeza.
Mfano mzuri ni ujanja unaotumika kuvuta muda kesi ya Lissu.Utabaini hakuna kesi pale wanataka kuiweka chadema busy huku wakikosa muda wa maandalizi ya uchaguzi.
Ukitazama wachangiaji wengi mpaka sasa hawana majibu ya namna chama kitakavyoweza kukabiliana na changamoto za kesi za michongo.
Chama hakina plan B iwapo Mwenyekiti ataendelea kusota rumande.
Chama hakina plan B iwapo Tume wataamua kubadili kanuni mbovu za uchaguzi.
Chama mpaka sasa nakiona kikiwa kimejikita kusikiliza na kufuatilia kesi za Lissu.
Makamu Mwenyekiti anatia huruma hajui afanye nini zaidi ya kutoa matamko ambayo hayana impact na maamuzi ya mahakama.