zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 19,156
- 28,895
Nikipita mitandaoni nimekutana na video ya kiongozi wa CHADEMA anaitwa ndugu Daniel Ngogo Naftali akitoa press statement kuhusiana na masuala ya Tegeta Escrow na ufisadi uliofanyika kimfumo.
View: https://www.youtube.com/live/M1HNMuJN6mU?si=RKFzHIKMCwmmn5Gq
Hoja zake ni nzito sana lakini kilichonishangaza anatoa maoni sio kama kiongozi wa CHADEMA huko mkoani Rukwa ila kama mratibu wa NGO yake binafsi. Suala hili pia analifanya Mdude Nyagali kutumia mwavuli wa "Sauti ya Wananchi". Huko nyuma pia Ben Saanane naye alikua akitoa matamko sio kama Mkurugenzi wa sera na tafiti CHADEMA ila kama mratibu wa NGO ya "Kizazi cha kuhoji". Huko BAWACHA pia kuna binti mmoja machachari sana anaitwa Dorcas Francis anayo "Bavicha Queens" .
Hizi vuguvugu ni nzuri na zinaongeza initiatives za vijana kwenye kujitegemea kimawazo bila kusubiri support ya CHADEMA. However, changamoto ni kwamba inaleta mgongano wa kimaslahi maana kuna misimamo ya CHADEMA kama taasisi inaweza kinzana na misimamo ya initiatives za hao vijana.
Mfano Mdude alitaka maandamano ya kupinga mkataba ila chadema walikua na ratiba ya mikutano huko kanda ya Nyasa. Sasa haya mambo yanaweza kuwa madogo ila huko mbele utashangaa hizi NGO zinasema washiriki uchaguzi huku chama hakitaki chaguzi bila tume huru. Madhara yake ndio kama yale ya kina Halima Mdee unashangaa maamuzi rasmi ya chama hayaheshimiki kabisa sababu kuna taasisi ndani ya taasisi.
Ningeomba CHADEMA mkemee hili swala mapema, kama wana NGOs zao basi waachie viongozi wengine watoe matamako. Lakini hili la kwamba kila kiongozi anakuwa na taasisi binafsi na yenyewe inakua frontline ilihali ana access na resources za chama haikai vizuri.
Naomba kuwasilisha