CHADEMA ibadili slogan ya itikadi yake haraka kuelekea 2015

CHADEMA ibadili slogan ya itikadi yake haraka kuelekea 2015

Yerriko ntachangia baadae nikimaliza kazi yangu hapa mara moja!
 
Hivi itikadi ya CCM ni nini? Mmeliua azimio la Arusha kwa Azimio la Zanzibar,mkajimilikishia raslimali za nchi kwa ulafi wenu.
Acha porojo FaizaFoxy,nini mnachoamini CCM kama chama tawala? Miiko ya uongozi iko wapi? Acheni kutoa rushwa wala kutumia nafasi zenu serikalini,acheni kutumia vyombo vya dola kutisha wananchi. Fanyeni siasa kama vyama vingine kwenye neutral ground,tuone matokeo.

Itikadi ni kupeleka mahawara bungeni kwa viti maalum.
 
Hivi Slaa atamkaribia Mwenyekiti wako wa Chama kwa uzinzi?Hivi yule Vick Kamata wa Mwanza Ubunge wa viti maalum aliupataje?

Wewe punguani kweli kweli, kwa hiyo nyinyi ndio wapinzani wenye itikadi? eti kwa kuwa CCM wamefanya na nyinyi mfanye? huo ndio upinzani? Loh!

​
 
Kama siasa huzijui siuache tu.Maisha binafsi ya mtu hayakuhusu.hata kama mtu na mkewe wanavunjana viuno ikulu haikuhusu.

Tatizo lako kubwa hujui maana ya itikadi ni nini.
 
Haujaelewa nini mkuu?

Sehemu ya kwanza tu nimeeleza haya hapa,

"ITIKADI ya CHADEMA ni itikadi ya MRENGO WA KATI, Ninashawishika kusema kuwa kile kiambata cha uenezi wa itikadi ya Chadema ambacho ni haki za raia, utawala wa sheria, na vita dhidi ya ufisadi, kimepungua uthabiti na ushawishi katika jamii na hakina nguvu tena ya kuiondoa ccm madarakani 2015",

ndugu yeriko ndiomana nilitaka kujuwa itikadi ya cdm ni ipi kabla ya ku jb
chama au tasisi yoyote ni lazima iwe na itikadi namini huwezi kusonga mbele bila kuwa na itikadi kwangu mimi ufisadi sio itikadi kwa sababu ni jambo linaloweza tokeya au lisitokeye kabisa sasa hapo sijui chama kitabaki itikadi ipi wakati hakuna ufisadi

itikadi ni msimamo au mrengo ulioegemeya kwa mfano

1 raisi wa zimbabwa bwana mugabe alianzisha sera ya chama chake au mrengo wa chama ni kuchukuwa mashamba toka mikononi mwa wazungu kwenda kwa wafrika hiyo ni itikadi

2 chama kuweka msimo wa kusimamia wazawa kwanza kwa jambo lolote lile la ajira au kituchochote kile kwanza wazawe ndio kipaumbele hio inaitwa itikadi au mrengo wa chama

3 nikupe mfano wa cuf kama ulivyo sema cuf husimamia msimamo wa zanzibari kamili yenye mamlaka yake hiyo ni itikadi ya cuf japo huwa wanaingiza swala la muungano hilo kwangu mm huwa nawaona swala la muungano huwa wanaingiza tu kiujanja ujanja ilikutokuweleweka kuwa hawapingi muungano lakini sera yao kabisa ni zanziba huru yena yenya mamlaka kamili hapo nako unasema ni itikadi ya chama

tunakuja upande wa cdm mimi naamini chama kilikuwa hakina itikadi ufisadi sio itikadi ndio mana mlifeli maneno ya ufisadi ni kama joto muilini hupanda kwakasi sana na linashuka mwili unabaki kama ulivokuwa
swala hilo walisha sema siku nyingi san malalamiko ya ufisadi vimepwaya hamkusikia na ww ulikuwa wa kwanza kupinga na maneno yako ninayo hadi sasa ninaweza kuweka aliyo coment zzk akilalamika chama kutokuwa na sera zaidi ya ufisadi ww ukampinga na maneno ya kashfa ss naona umerudi njia ileile aliopita zt ukipinga naweka hapa watu waone
 
Mie navyoelewa Itikadi yoyote inaendana na mda kama ulivyosema mwenyewe na kwa vyovyote vile ni lazima Itikadi iwe dynamic pia,na hii inakuwa influenced na kumaliza ngwe moja ama imefanikiwa ama mazingira yamegoma kuruhusu ...kwahiyo basi,kwa mazingira ya leo yanakulazimisha ama uwe mkomunist,liberali, ama wa kati,hiyo ndo main pillar na labda kuongezea kama kaulimbiu hiyo iongezwe kwa zile za usawa,haki na nguvu ya umma make unaposema Itikadi na kaulimbiu ni vitu viwili tofauti kidogo
 
mada ndeeefu kama hadithi za alfulelaulela...jipange kaka

Hii inaonyesha ni jinsi gani hauwezi kusumbua kichwa kufikiri mambo yakitaifa au yamsingi unapenda shortly ndio maana ukisoma mchanganuo mlefu hauelewi.Nawatu kama wewe ndio misukule ya Ccm kwa sababu umedumaa ubongo.Polesana na ulaaniwe!
 
Mkuu nirudie kusema kuwa ITIKADI ya CHADEMA ni itikadi ya MRENGO WA KATI.

Hii haiwezi kubadilika, ni kama maandiko matakatifu ya kiroho vile,

Hapa ninachokijadili ni slogan ya kuieneza itikadi ndio ibadilike,

Slogan inaweza kubadilika hata kila baada ya mwaka, hii itategemea sanana mazingira ya mahitaji ya kisiasa.
 
ITIKADI ya CHADEMA ni itikadi ya MRENGO WA KATI, Ninashawishika kusema kuwa kile kiambata cha uenezi wa itikadi ya Chadema ambacho ni haki za raia, utawala wa sheria, na vita dhidi ya ufisadi, kimepungua uthabiti na ushawishi katika jamii na hakina nguvu tena ya kuiondoa ccm madarakani 2015,

Nilipofundisha somo la siasa hapa jamvini nilieleza kwa kirefu namna itikadi inavyoenezwa na umuhimu wa itikadi katika siasa kwa ujumla.

Sehemu ya somo hilo ilipembua kinagaubaga hasa juu yayo, na hata sasa nasisitiza hili kwa chama changu.

Ili itikadi iweze kuenezwa/kuuzika ni lazima iende sambamba na hitaji kuu la umma unaoufanyia siasa, hapa ndipo vyama vyetu vinapofeli na kujikuta vinakuwa vyamsimu.

Kwa Afrika ya leo imekubwa na ombwe la vyama vya siasa kutokuwa na itikadi inayoaminiwa na wanachama wa vyama husika, Tatizo hili limeikumba hata siasa ya nchi yetu kwa sasa, Leo tuna vyama visivyokuwa na itikadi inayoeleweka ya vitendo.

CCM ilifanikiwa ki-itikadi chini ya mfumo wa chama kimoja kutokana na itikadi urithi ya kihafidhina iliyolenga ukombozi wa nchi na Utaifa (chini ya TANU); baadae siasa ya Ujamaa na kujitegemea ililenga kumwinua Mtanganyika.

Tangu kupigwa mweleka kwa azimio la Arusha mwaka 1992 na kuzaa azimio ls Zanzibar la mwaka 1992, CCM imekuwa inahubiri itikadi ya Ujamaa, lakini upande mwingine, inatekeleza itikadi ya soko huru, tena bila ya mchujo (ubepari).
Ukosefu huu wa msimamo kiitikadi wa ccm ndio tiketi ya mparaganyiko wa chama hiki na sasa kinaelekea ahera kabisa, huku chagizo la Ufisadi likisindikiza kifo hicho kwa ccm.

Lakini tuna vyama vilivyopata umaarufu kutokana na sababu ambazo hazihusiani na UMMA kubaini ubora wa itikadi ya chama baada ya kufananisha na itikadi za chama/vyama vingine vilivyopo, Badala yake, umaarufu wa vyama hivi unatokana na UMMA kuvikubali kwa sababu nyingine nje kabisa ya ubora wa itikadi zao. Mathalani ni umaarufu wa NCCR miaka ya 1995 na ule wa Chadema miaka ya 2005 – hadi sasa.
Ili somo letu liende vizuri ni vema nifafanue baadhi ya mambo katika hili, neno ‘kujipatia umaarufu’ badala ya ‘kujipatia mafanikio’, ni kwasababu tofauti na ‘mafanikio’ ambayo hutokana na itikadi, mara nyingi ‘umaarufu’ hutokana na vitu vya mpito, na huwa haudumu kwa muda mrefu.

Wanachama na wafuasi wenzangu wa Chadema, mtakumbuka umaarufu wa NCCR miaka ya 1995; umaarufu wa Chadema hauna tofauti kubwa sana kwa sababu mafanikio tunayoyaona hayatokani na watu kuipokea kwa uthabiti wake itikadi ya chama, bali kwa vitu vya msimu ama matukio tu, ambavyo vinaweza meguka kirahisi.

Pia tuna vyama vilivyopata mafanikio kisiasa (sio umaarufu) kutokana na itikadi zao. Lakini vyama hivi vina udhaifu mmoja mkubwa juu ya itikadi zao: Itikadi hizi zinaendana na hali halisi ya upande mmoja tu wa jamii badala ya jamii nzima. Mathalani CUF na mafanikio ya kiitikadi visiwani ambayo imekuwa vigumu kuyarudia Bara. Mafanikio ya sasa ya CUF visiwani Zanzibar hayana tofauti kubwa na mafanikio ya TANU Tanganyika miaka 1960. Mafanikio ya CUF yanatokana na itikadi inayohanikizwa na Utaifa /Ukombozi dhidi ya Utawala wa Tanganyika. Pamoja na mafanikio yake huko Zanzibar, itikadi ya CUF haina mashiko upande wa Tanganyika kwakuwa haina hanikizo la hitaji la umma wa Watanganyika.

Udhaifu wa itikadi ya CUF utapitia hatua tatu za maisha: (1) Itikadi ya uhuru na Utaifa iliyozaa matunda hadi sasa Zanzibar, (2) baada ya utaifa kupatikana, CUF itakumbwa na changamoto za kutekeleza ahadi ilizozitoa wakati wa mapambano ya kudai utaifa kutoka Tanganyika na hali itazidi kuwa ngumu zaidi iwapo patatokea vyama vingine vya upinzani upande wa Zanzibar, (3) Iwapo vitajitokeza vyama vipya vyenye nguvu Zanzibar, itikadi ya CUF itazidi kuishiwa makali kutokana na kushindwa kutekeleza ahadi za ukombozi (kama ilivyotokea kwa CCM), na vyama vitabaki kukosoana huku CUF ikionekana sio lolote na vyama vya upinzani Zanzibar vitaendeleza kasumba yakusahau kabisa kwamba adui yao ni itikadi zenye kuishi maisha marefu.

Udhaifu huu wa ki-itikadi ndani ya vyama vya siasa unawakosesha wananchi fursa ya kuunda muono na mtazamo wa kisiasa unaofuatana na imani za kiitikadi zinazotambulika, na nyepesi kueleweka au kutofautisha. Hii ndio sababu kubwa inayopelekea wananchi kuunga mkono watu au vyama kishabiki zaidi kuliko kuunga mkono vyama hivyo kutokana na kushiba itikadi za vyama.

Tofauti na nchi zilizokomaa kisiasa, kwa Tanganyika na Zanzibar suala la wanachama kuhama hama vyama ni suala la kawaida. Kama vyama vingekuwa vinaendesha siasa za ki-itikadi, jambo hili lisingetokea kwani itikadi ya vyama nchini kwamjibu wa katiba zao inatofautiana kabisa.

Katika demokrasia iliyokomaa na yenye kuendeshwa ki-itikadi, kitendo cha wanasiasa kuteteana kwa sababu binafsi, au wanasiasa kuhama hama vyama, ni kitendo cha kujimaliza kisiasa. Ni katika nchi kama Tanganyika na Zanzibar pekee ambapo leo mwanasiasa anaweza jitoa CHADEMA, CCM, au NCCR na kwenda chama kingine bila ya hofu yoyote na akaendelea kuhudumu siasa za kitaifa tu. Hiki ni moja ya vielelezo vikubwa juu ya udhaifu wa vyama vyetu ki- itikadi.

Katika mazingira ya kawaida, kitendo cha kiongozi kuhama chama ni sawa na kukana imani (itikadi) yake na kukumbatia imani (itikadi) nyingine. Kwa mwanachama kufanya hivi sio jambo la hatari sana, lakini ni la hatari sana kwa viongozi.

Ni mapungufu haya ya ki-itikadi ndiyo hupelekea vyama vyetu kunadi ilani na sera zinazofanana, badala ya kuwa na ushindani mkali wa mtazamo unaotokana na itikadi. Katika siasa za sasa, vyama vyote vinashindana kwenda Ikulu, sio kuleta jambo jipya linalotokana na itikadi zao, bali kutekeleza sera zile zile za soko huria zilizojaa uholela.

Vyama pia vinapoteza muda mwingi sana kushindania yasiyo na umuhimu sana yakiwa yametapakaa kama vile haki za raia, utawala wa sheria, na vita dhidi ya ufisadi. Siasa juu ya masuala haya zimekosa uthabiti na kuungamana kutokana na udhaifu wa ki-itikadi. Vile vile kutokana na udhaifu wa ki-itikadi, umaarufu wa vyama mara nyingi (kama sio mara zote), unatokana zaidi na hulka za viongozi waliopo katika vyama hivyo, hasa nguvu zao katika jamii wanazotoka, bila ya kujali vyama wanavyotoka au itikadi wanazoziamini.

Hivyo slogan/msukumo wa itikadi ya Chadema kwa sasa iwe ni Tanganyika HURU na Zanzibar HURU ndio msingi wa MUUNGANO imara na Tanzania IMARA
Duh leo ndo umetambua kudhoofika kwa CDM? kazi kweli kweli
 
Mie navyoelewa Itikadi yoyote inaendana na mda kama ulivyosema mwenyewe na kwa vyovyote vile ni lazima Itikadi iwe dynamic pia,na hii inakuwa influenced na kumaliza ngwe moja ama imefanikiwa ama mazingira yamegoma kuruhusu ...kwahiyo basi,kwa mazingira ya leo yanakulazimisha ama uwe mkomunist,liberali, ama wa kati,hiyo ndo main pillar na labda kuongezea kama kaulimbiu hiyo iongezwe kwa zile za usawa,haki na nguvu ya umma make unaposema Itikadi na kaulimbiu ni vitu viwili tofauti kidogo

Umenielewa vibaya, sijasema "itikadi yoyote huendana na muda"

Kinachokwenda na muda ni slogan ambayo ndio tunayoijadili hapa, sio itikadi.
 
Mkuu nirudie kusema kuwa ITIKADI ya CHADEMA ni itikadi ya MRENGO WA KATI.

Hii haiwezi kubadilika, ni kama maandiko matakatifu ya kiroho vile,

Hapa ninachokijadili ni slogan ya kuieneza itikadi ndio ibadilike,

Slogan inaweza kubadilika hata kila baada ya mwaka, hii itategemea sanana mazingira ya mahitaji ya kisiasa.

Toa mapendekezo Yeriko.

Nilimsoma Dady0000 na kumweelewa. Kwa kifupi itikadi ya cdm iko imara na inakipa nafasi chama uwanja mpana kucheza nayo watakavyo. 2015 si mbali na sidhani kama Watanzania watakuwa wasahaurifu ( japo ugonjwa huo hupo) nguvu ya umma ya cdm ya mwaka 2012 and mid 2013. Suala tu la muda na ni kubaliane nawe kwamba nguli wa siasa za cdm waitane sasa ktk mikakati mipya....ikiwa ni pamoja na mashinikizo ya kisiasa kwa serikali kupata tume mpya ya uchaguzi kama sivyo kupata sheria mpya za uchaguzi.

ccm wanajua karata yao ya mwisho ilikuwa uchonganishi na upandikizaji wa vibaraka ndani ya cdm...now that has failed...wakarukia katiba mpya ambayo tayari cdm is out of their fake game.

CCM wanacho kifanya sasa ni upinzani na kupindisha sera za cdm. Wanajitahidi kufuta nyayo za cdm za mwaka 2012/3 and early Jan this year....tunajipanga kurudi watakapo maliza.
 
Hii inaonyesha ni jinsi gani hauwezi kusumbua kichwa kufikiri mambo yakitaifa au yamsingi unapenda shortly ndio maana ukisoma mchanganuo mlefu hauelewi.Nawatu kama wewe ndio misukule ya Ccm kwa sababu umedumaa ubongo.Polesana na ulaaniwe!

hahaha...we mwenyewe hujaelewa kitu hapo..yericko ameandika pumba tu..
 
Mkuu nirudie kusema kuwa ITIKADI ya CHADEMA ni itikadi ya MRENGO WA KATI.

Hii haiwezi kubadilika, ni kama maandiko matakatifu ya kiroho vile,

Hapa ninachokijadili ni slogan ya kuieneza itikadi ndio ibadilike,

Slogan inaweza kubadilika hata kila baada ya mwaka, hii itategemea sanana mazingira ya mahitaji ya kisiasa.

chadema ina itikadi ya kihafidhina
 
Back
Top Bottom