CHADEMA ibadili slogan ya itikadi yake haraka kuelekea 2015

CHADEMA ibadili slogan ya itikadi yake haraka kuelekea 2015

Bakora nafikiri Mod angemsimamisha kidogo watu tunapata somo yeye anaweka ujinga YN endelea kamanda namapambano maana tuko kwenye wakati wakujikomboa
 
Ni wazo zuri sana japo naona umekazia zaidi kwenye wimbo wenyewe kuliko waimba huo wimbo .Nyongeza yangu kwenye wazo lako ni kwamba,Chama kiandae watu walio na utaalamu mzuri wa kugundua wanasiasa wenye vipaji vya siasa na uongozi ambao kama wakichaguliwa kuwa wagombea wa chadema aidha kwenye nafasi za ubunge au udiwani basi wawe na uwezo mkubwa kuelezea sera,mawazo na mipango ya kimaendeleo ya chama kwa wananchi na wakaeleweka vizuri tena na wananchi wa kutoka kwenye makundi mbalimbali ya kijamii kama vile wanafunzi wa shule za sekondari,vyuo,wafanyakazi,wafanyabiashara na wakulima.Kwamba wagombea hawa wawe wepesi kubadili lugha na ujumbe kulingana na mazingira na aina ya hadhira/umma wanayoongea nayo.Mwisho,Ni vyema CHADEMA kuanzia sasa wakaanzisha utamaduni wa kuandaa mikutano maalum ya ndani maaruf kama HALL MEETING kwaajili ya kujadiliana/kuelimishana na wananchi wa makundi mbalimbali ili waweze kuyaelewa malengo ya chama kwa undani zaidi.Let us say Siku flani mnaandaa HALL MEETING na kundi la wafanyabiashara wakubwa,next mnakutana na wafanyabiashara wa kati kisha mnakutana na wafanyabiashara wadogo wadogo,Kupitia mikutano ya namna hii ambayo itatoa fursa ya kujadiliana,maswali kuulizwa na majibu yake kupatikana itawawezesha wafanyabiashara kuelewa kwa kina sera,mawazo na mipango ya maendeleo ya CHADEMA na wakivutiwa nayo wafanyabiashara hawa wanaweza kugeuka kuwa mawakala wa uenezi wa itikadi za chama kwa wengine.Hivyo ndivyo vyama vyote makini vya siasa duniani vilivyofanikiwa kujenga majeshi yao yenye nguvu ya kiitikadi,Walianza kuyaelimisha makundi madogo ndani ya jamii kisha makundi haya yakageuka kuwa jeshi imara la uenezi wa itikadi za vyama husika kwa jamii pana zaidi.

Umeongea mambo mujarabu na yakujenga sana mkuu,

Asante sana kwaushauri wako mzuri.
 
Bakora nafikiri Mod angemsimamisha kidogo watu tunapata somo yeye anaweka ujinga YN endelea kamanda namapambano maana tuko kwenye wakati wakujikomboa

Niliona tangazo la ajira kwa Jamii Media kampuni mama ya Jamiiforums, moja ya malengo katika kuboresha jf ilikuwa ni kudhibiti wavuruga mijadala kama huyu kijana.
 
Sasa ni kwa kiasi gani Itikadi zitakua na madhara kuelekea uchaguzi mkuu ujao wakati toka mwaka 1992 itikadi hazikuwahi kupewa kipaumbele kwenye siasa zetu ndio maana CCM walishindwa kugutuka hata walipojikuta wametoka nje ya itikadi yao?

Ili msukumo wa Itikadi uwe na nguvu tunahitaji kujenga misingi imara kwa wanachama na wafuasi wetu zaidi ili iwe benchmark ya kubadili political landscape

Leo hii ukimuuliza mwananchi wa kule kijijini Malampaka kuhusu Itikadi atakuambia nina njaa au sina ajira hiyo itikadi ina msaada gani wa haraka kwa mwaka huu au miaka 2 ijayo.It's bitter but the truth
 
  • Thanks
Reactions: jme
Mleta mada hajui anataka kufikisha ujumbe upi. Ni porojo tupu.
 
Sasa ni kwa kiasi gani Itikadi zitakua na madhara kuelekea uchaguzi mkuu ujao wakati toka mwaka 1992 itikadi hazikuwahi kupewa kipaumbele kwenye siasa zetu ndio maana CCM walishindwa kugutuka hata walipojikuta wametoka nje ya itikadi yao?

Ili msukumo wa Itikadi uwe na nguvu tunahitaji kujenga misingi imara kwa wanachama na wafuasi wetu zaidi ili iwe benchmark ya kubadili political landscape

Leo hii ukimuuliza mwananchi wa kule kijijini Malampaka kuhusu Itikadi atakuambia nina njaa au sina ajira hiyo itikadi ina msaada gani wa haraka kwa mwaka huu au miaka 2 ijayo.It's bitter but the truth

Kwanza kama chama ni lazima tujue na tuyatumikie malengo ya chama,

Ikiwa malengo ni kushika dola na kuwaongoza Watanzania kwa msingi wa itikadi yetu ya mrengo wa kati, basi hatuna budi kusaka njia mujarabu ya kushawishi umma utupe rudhaa yakuongoza, hasa hili tukilitazama zaidi kuanzia 2015.

Njia tuziishizo zimekosa ushawishi na uthabitiwenye malengo 2015,
 
Na sie tusioataka chadema iwepo madarakani tuendeleze itikadi gani ili kama ikiwezakana hii chagadema ipotee kabisaa kwani itikadi zake si hatuzipendagi kwani ni za kazikazini sana
 
Huenda haupo sahihi ama unafanya makusudi tu,

Wapi hujaelewa ili ueleweshwe mama.

Wewe mwenyewe umeelewa ulichokiandika?

Ningewashauri kabla hamjaanza kuhororoja kuhusu itikadi mngeanzia kwa kusafisha madudu mliokuwa nayo ndani ya chadema. Uliona chama kipi cha siasa kinakuwa saccos?
 
ITIKADI ya CHADEMA ni itikadi ya MRENGO WA KATI, Ninashawishika kusema kuwa kile kiambata cha uenezi wa itikadi ya Chadema ambacho ni haki za raia, utawala wa sheria, na vita dhidi ya ufisadi, kimepungua uthabiti na ushawishi katika jamii na hakina nguvu tena ya kuiondoa ccm madarakani 2015,

Nilipofundisha somo la siasa hapa jamvini nilieleza kwa kirefu namna itikadi inavyoenezwa na umuhimu wa itikadi katika siasa kwa ujumla.

Sehemu ya somo hilo ilipembua kinagaubaga hasa juu yayo, na hata sasa nasisitiza hili kwa chama changu.

Ili itikadi iweze kuenezwa/kuuzika ni lazima iende sambamba na hitaji kuu la umma unaoufanyia siasa, hapa ndipo vyama vyetu vinapofeli na kujikuta vinakuwa vyamsimu.

Kwa Afrika ya leo imekubwa na ombwe la vyama vya siasa kutokuwa na itikadi inayoaminiwa na wanachama wa vyama husika, Tatizo hili limeikumba hata siasa ya nchi yetu kwa sasa, Leo tuna vyama visivyokuwa na itikadi inayoeleweka ya vitendo.

CCM ilifanikiwa ki-itikadi chini ya mfumo wa chama kimoja kutokana na itikadi urithi ya kihafidhina iliyolenga ukombozi wa nchi na Utaifa (chini ya TANU); baadae siasa ya Ujamaa na kujitegemea ililenga kumwinua Mtanganyika.

Tangu kupigwa mweleka kwa azimio la Arusha mwaka 1992 na kuzaa azimio ls Zanzibar la mwaka 1992, CCM imekuwa inahubiri itikadi ya Ujamaa, lakini upande mwingine, inatekeleza itikadi ya soko huru, tena bila ya mchujo (ubepari).
Ukosefu huu wa msimamo kiitikadi wa ccm ndio tiketi ya mparaganyiko wa chama hiki na sasa kinaelekea ahera kabisa, huku chagizo la Ufisadi likisindikiza kifo hicho kwa ccm.

Lakini tuna vyama vilivyopata umaarufu kutokana na sababu ambazo hazihusiani na UMMA kubaini ubora wa itikadi ya chama baada ya kufananisha na itikadi za chama/vyama vingine vilivyopo, Badala yake, umaarufu wa vyama hivi unatokana na UMMA kuvikubali kwa sababu nyingine nje kabisa ya ubora wa itikadi zao. Mathalani ni umaarufu wa NCCR miaka ya 1995 na ule wa Chadema miaka ya 2005 – hadi sasa.
Ili somo letu liende vizuri ni vema nifafanue baadhi ya mambo katika hili, neno ‘kujipatia umaarufu' badala ya ‘kujipatia mafanikio', ni kwasababu tofauti na ‘mafanikio' ambayo hutokana na itikadi, mara nyingi ‘umaarufu' hutokana na vitu vya mpito, na huwa haudumu kwa muda mrefu.

Wanachama na wafuasi wenzangu wa Chadema, mtakumbuka umaarufu wa NCCR miaka ya 1995; umaarufu wa Chadema hauna tofauti kubwa sana kwa sababu mafanikio tunayoyaona hayatokani na watu kuipokea kwa uthabiti wake itikadi ya chama, bali kwa vitu vya msimu ama matukio tu, ambavyo vinaweza meguka kirahisi.

Pia tuna vyama vilivyopata mafanikio kisiasa (sio umaarufu) kutokana na itikadi zao. Lakini vyama hivi vina udhaifu mmoja mkubwa juu ya itikadi zao: Itikadi hizi zinaendana na hali halisi ya upande mmoja tu wa jamii badala ya jamii nzima. Mathalani CUF na mafanikio ya kiitikadi visiwani ambayo imekuwa vigumu kuyarudia Bara. Mafanikio ya sasa ya CUF visiwani Zanzibar hayana tofauti kubwa na mafanikio ya TANU Tanganyika miaka 1960. Mafanikio ya CUF yanatokana na itikadi inayohanikizwa na Utaifa /Ukombozi dhidi ya Utawala wa Tanganyika. Pamoja na mafanikio yake huko Zanzibar, itikadi ya CUF haina mashiko upande wa Tanganyika kwakuwa haina hanikizo la hitaji la umma wa Watanganyika.


Udhaifu wa itikadi ya CUF utapitia hatua tatu za maisha: (1) Itikadi ya uhuru na Utaifa iliyozaa matunda hadi sasa Zanzibar, (2) baada ya utaifa kupatikana, CUF itakumbwa na changamoto za kutekeleza ahadi ilizozitoa wakati wa mapambano ya kudai utaifa kutoka Tanganyika na hali itazidi kuwa ngumu zaidi iwapo patatokea vyama vingine vya upinzani upande wa Zanzibar, (3) Iwapo vitajitokeza vyama vipya vyenye nguvu Zanzibar, itikadi ya CUF itazidi kuishiwa makali kutokana na kushindwa kutekeleza ahadi za ukombozi (kama ilivyotokea kwa CCM), na vyama vitabaki kukosoana huku CUF ikionekana sio lolote na vyama vya upinzani Zanzibar vitaendeleza kasumba yakusahau kabisa kwamba adui yao ni itikadi zenye kuishi maisha marefu.


Udhaifu huu wa ki-itikadi ndani ya vyama vya siasa unawakosesha wananchi fursa ya kuunda muono na mtazamo wa kisiasa unaofuatana na imani za kiitikadi zinazotambulika, na nyepesi kueleweka au kutofautisha. Hii ndio sababu kubwa inayopelekea wananchi kuunga mkono watu au vyama kishabiki zaidi kuliko kuunga mkono vyama hivyo kutokana na kushiba itikadi za vyama.

Tofauti na nchi zilizokomaa kisiasa, kwa Tanganyika na Zanzibar suala la wanachama kuhama hama vyama ni suala la kawaida. Kama vyama vingekuwa vinaendesha siasa za ki-itikadi, jambo hili lisingetokea kwani itikadi ya vyama nchini kwamjibu wa katiba zao inatofautiana kabisa.

Katika demokrasia iliyokomaa na yenye kuendeshwa ki-itikadi, kitendo cha wanasiasa kuteteana kwa sababu binafsi, au wanasiasa kuhama hama vyama, ni kitendo cha kujimaliza kisiasa. Ni katika nchi kama Tanganyika na Zanzibar pekee ambapo leo mwanasiasa anaweza jitoa CHADEMA, CCM, au NCCR na kwenda chama kingine bila ya hofu yoyote na akaendelea kuhudumu siasa za kitaifa tu. Hiki ni moja ya vielelezo vikubwa juu ya udhaifu wa vyama vyetu ki- itikadi.

Katika mazingira ya kawaida, kitendo cha kiongozi kuhama chama ni sawa na kukana imani (itikadi) yake na kukumbatia imani (itikadi) nyingine. Kwa mwanachama kufanya hivi sio jambo la hatari sana, lakini ni la hatari sana kwa viongozi.

Ni mapungufu haya ya ki-itikadi ndiyo hupelekea vyama vyetu kunadi ilani na sera zinazofanana, badala ya kuwa na ushindani mkali wa mtazamo unaotokana na itikadi. Katika siasa za sasa, vyama vyote vinashindana kwenda Ikulu, sio kuleta jambo jipya linalotokana na itikadi zao, bali kutekeleza sera zile zile za soko huria zilizojaa uholela.

Vyama pia vinapoteza muda mwingi sana kushindania yasiyo na umuhimu sana yakiwa yametapakaa kama vile haki za raia, utawala wa sheria, na vita dhidi ya ufisadi. Siasa juu ya masuala haya zimekosa uthabiti na kuungamana kutokana na udhaifu wa ki-itikadi. Vile vile kutokana na udhaifu wa ki-itikadi, umaarufu wa vyama mara nyingi (kama sio mara zote), unatokana zaidi na hulka za viongozi waliopo katika vyama hivyo, hasa nguvu zao katika jamii wanazotoka, bila ya kujali vyama wanavyotoka au itikadi wanazoziamini.

Hivyo slogan/msukumo wa itikadi ya Chadema kwa sasa iwe ni Tanganyika HURU na Zanzibar HURU ndio msingi wa MUUNGANO imara na Tanzania IMARA

Hayo unayojaribu kuishauri Chadema ni sawa na kuivalisha maiti suti,miwani,viatu vya thamani na saa kwani kuzimu havitumiki.Chadema ilishakufa.
 
Na sie tusioataka chadema iwepo madarakani tuendeleze itikadi gani ili kama ikiwezakana hii chagadema ipotee kabisaa kwani itikadi zake si hatuzipendagi kwani ni za kazikazini sana

Nyinyi jengeni chama cheni ccm
 
hiyo slogani ya Tanganyika Huru na Zanzibar Huru ndio yakuua muungano sio..... lengo lenu.la.kuua muungano halitafanikiwa...SHAME ON YOU..

Ni mjingaaa sanaa pekee atakayesema CDM inaua muungano, CDM pekee bila kuuungwa mkono na wananchi yaiwezi kuvunja muungano. Na kama wananchi wameunga mkono CDM ina kosa gani???? VIVA CDM VIVA
 
Hayo unayojaribu kuishauri Chadema ni sawa na kuivalisha maiti suti,miwani,viatu vya thamani na saa kwani kuzimu havitumiki.Chadema ilishakufa.

Haya kama ilishakufa basi endeleeni kuwa "mashabiki" wa ccm
 
Nyinyi jengeni chama cheni ccm

Yaani tukijenga chama chetu chagadema itajifia yenyewe ji tukiomba msajili akifute tutakuwa tumekosea? Maana chama hiki kila utakapo enda madalali wake always huwa WACHAGA kwanini kabila zingine hawana nafasi kama wao?
 
Wewe mwenyewe umeelewa ulichokiandika?

Ningewashauri kabla hamjaanza kuhororoja kuhusu itikadi mngeanzia kwa kusafisha madudu mliokuwa nayo ndani ya chadema. Uliona chama kipi cha siasa kinakuwa saccos?

Kwahiyo kutoeleweka kwa mada hii nikutokana na hicho ukiitacho madudu ndani ya chadema?

Je ccm utaiitaje?
 
Nyerere uko sawa kaka ila wewe unafikiri CHADEMA sasa kimekosa mvuto au bado kina mvuto ule ule wa mwaka 2010 na kwanini unasema CHADEMA kama NCCR unamaanisha kuwa sasa chama chako kinakosa uhalari kama NCCR kwanza umekikatia tamaa kimechoka na kimechelewa kufanya mageuzi ya ki-tikadi sasa kuna haja gani ya kuwa na vyama vya upinzani vya msimu si bora kuiachia CCM maana hakuna maana ya upinzani na je tutaweza lini kutengeneza taasisi imara za siasa kama CCM inaonekana tumeshindwa TANZANIA yangu maskini
 
Yaani tukijenga chama chetu chagadema itajifia yenyewe ji tukiomba msajili akifute tutakuwa tumekosea? Maana chama hiki kila utakapo enda madalali wake always huwa WACHAGA kwanini kabila zingine hawana nafasi kama wao?

Rejea kwenye hoja,

Umeelewa nini katika hoja hii??
 
Nyerere uko sawa kaka ila wewe unafikiri CHADEMA sasa kimekosa mvuto au bado kina mvuto ule ule wa mwaka 2010 na kwanini unasema CHADEMA kama NCCR unamaanisha kuwa sasa chama chako kinakosa uhalari kama NCCR kwanza umekikatia tamaa kimechoka na kimechelewa kufanya mageuzi ya ki-tikadi sasa kuna haja gani ya kuwa na vyama vya upinzani vya msimu si bora kuiachia CCM maana hakuna maana ya upinzani na je tutaweza lini kutengeneza taasisi imara za siasa kama CCM inaonekana tumeshindwa TANZANIA yangu maskini

Hapana, umesoma mada lakini bado hujaielewa mantiki yangu,

Nataka chama changu kisifanye makosa yaliyofanywa na vyama vingine huko nyuma.
 
Kwahiyo kutoeleweka kwa mada hii nikutokana na hicho ukiitacho madudu ndani ya chadema?

Je ccm utaiitaje?

saccos huwa na itikadi ipi kisiasa?

Mwenyekiti kumkatisha safari mbunge wa viti maalum (hawara yake) hakuna ndani ya chadema anaeweza kuelezea aliwekwa bungeni kwa vigezo vipi vya kisiasa zaidi ya kuwa hawara wa Bosi, ndiyo unaiita itikadi?

Hivi Mwenyekiti kama huyo utamueleza nini kuhusu itikadi? itikadi hapo ni uzinzi kwa kwenda mbele.
 
Chadema imepoteza ushawishi kwa wananchi kabisa...yaliyokipata nccr miaka hiyo na baadaye cuf sasa yanakipata chadema. Haiponi
 
Back
Top Bottom