CHADEMA ibadili slogan ya itikadi yake haraka kuelekea 2015

CHADEMA ibadili slogan ya itikadi yake haraka kuelekea 2015

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,027
Reaction score
20,518
ITIKADI ya CHADEMA ni itikadi ya MRENGO WA KATI, Ninashawishika kusema kuwa kile kiambata cha uenezi wa itikadi ya Chadema ambacho ni haki za raia, utawala wa sheria, na vita dhidi ya ufisadi, kimepungua uthabiti na ushawishi katika jamii na hakina nguvu tena ya kuiondoa ccm madarakani 2015,

Nilipofundisha somo la siasa hapa https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/640686-darasa-la-siasa-4.html nilieleza kwa kirefu namna itikadi inavyoenezwa na umuhimu wa itikadi katika siasa kwa ujumla.

Sehemu ya somo hilo ilipembua kinagaubaga hasa juu yayo, na hata sasa nasisitiza hili kwa chama changu.

Ili itikadi iweze kuenezwa/kuuzika ni lazima iende sambamba na hitaji kuu la umma unaoufanyia siasa, hapa ndipo vyama vyetu vinapofeli na kujikuta vinakuwa vyamsimu.

Kwa Afrika ya leo imekubwa na ombwe la vyama vya siasa kutokuwa na itikadi inayoaminiwa na wanachama wa vyama husika, Tatizo hili limeikumba hata siasa ya nchi yetu kwa sasa, Leo tuna vyama visivyokuwa na itikadi inayoeleweka ya vitendo.

CCM ilifanikiwa ki-itikadi chini ya mfumo wa chama kimoja kutokana na itikadi urithi ya kihafidhina iliyolenga ukombozi wa nchi na Utaifa (chini ya TANU); baadae siasa ya Ujamaa na kujitegemea ililenga kumwinua Mtanganyika.

Tangu kupigwa mweleka kwa azimio la Arusha mwaka 1992 na kuzaa azimio ls Zanzibar la mwaka 1992, CCM imekuwa inahubiri itikadi ya Ujamaa, lakini upande mwingine, inatekeleza itikadi ya soko huru, tena bila ya mchujo (ubepari).
Ukosefu huu wa msimamo kiitikadi wa ccm ndio tiketi ya mparaganyiko wa chama hiki na sasa kinaelekea ahera kabisa, huku chagizo la Ufisadi likisindikiza kifo hicho kwa ccm.

Lakini tuna vyama vilivyopata umaarufu kutokana na sababu ambazo hazihusiani na UMMA kubaini ubora wa itikadi ya chama baada ya kufananisha na itikadi za chama/vyama vingine vilivyopo, Badala yake, umaarufu wa vyama hivi unatokana na UMMA kuvikubali kwa sababu nyingine nje kabisa ya ubora wa itikadi zao. Mathalani ni umaarufu wa NCCR miaka ya 1995 na ule wa Chadema miaka ya 2005 – hadi sasa.
Ili somo letu liende vizuri ni vema nifafanue baadhi ya mambo katika hili, neno ‘kujipatia umaarufu’ badala ya ‘kujipatia mafanikio’, ni kwasababu tofauti na ‘mafanikio’ ambayo hutokana na itikadi, mara nyingi ‘umaarufu’ hutokana na vitu vya mpito, na huwa haudumu kwa muda mrefu.

Wanachama na wafuasi wenzangu wa Chadema, mtakumbuka umaarufu wa NCCR miaka ya 1995; umaarufu wa Chadema hauna tofauti kubwa sana kwa sababu mafanikio tunayoyaona hayatokani na watu kuipokea kwa uthabiti wake itikadi ya chama, bali kwa vitu vya msimu ama matukio tu, ambavyo vinaweza meguka kirahisi.

Pia tuna vyama vilivyopata mafanikio kisiasa (sio umaarufu) kutokana na itikadi zao. Lakini vyama hivi vina udhaifu mmoja mkubwa juu ya itikadi zao: Itikadi hizi zinaendana na hali halisi ya upande mmoja tu wa jamii badala ya jamii nzima. Mathalani CUF na mafanikio ya kiitikadi visiwani ambayo imekuwa vigumu kuyarudia Bara. Mafanikio ya sasa ya CUF visiwani Zanzibar hayana tofauti kubwa na mafanikio ya TANU Tanganyika miaka 1960. Mafanikio ya CUF yanatokana na itikadi inayohanikizwa na Utaifa /Ukombozi dhidi ya Utawala wa Tanganyika. Pamoja na mafanikio yake huko Zanzibar, itikadi ya CUF haina mashiko upande wa Tanganyika kwakuwa haina hanikizo la hitaji la umma wa Watanganyika.


Udhaifu wa itikadi ya CUF utapitia hatua tatu za maisha: (1) Itikadi ya uhuru na Utaifa iliyozaa matunda hadi sasa Zanzibar, (2) baada ya utaifa kupatikana, CUF itakumbwa na changamoto za kutekeleza ahadi ilizozitoa wakati wa mapambano ya kudai utaifa kutoka Tanganyika na hali itazidi kuwa ngumu zaidi iwapo patatokea vyama vingine vya upinzani upande wa Zanzibar, (3) Iwapo vitajitokeza vyama vipya vyenye nguvu Zanzibar, itikadi ya CUF itazidi kuishiwa makali kutokana na kushindwa kutekeleza ahadi za ukombozi (kama ilivyotokea kwa CCM), na vyama vitabaki kukosoana huku CUF ikionekana sio lolote na vyama vya upinzani Zanzibar vitaendeleza kasumba yakusahau kabisa kwamba adui yao ni itikadi zenye kuishi maisha marefu.


Udhaifu huu wa ki-itikadi ndani ya vyama vya siasa unawakosesha wananchi fursa ya kuunda muono na mtazamo wa kisiasa unaofuatana na imani za kiitikadi zinazotambulika, na nyepesi kueleweka au kutofautisha. Hii ndio sababu kubwa inayopelekea wananchi kuunga mkono watu au vyama kishabiki zaidi kuliko kuunga mkono vyama hivyo kutokana na kushiba itikadi za vyama.

Tofauti na nchi zilizokomaa kisiasa, kwa Tanganyika na Zanzibar suala la wanachama kuhama hama vyama ni suala la kawaida. Kama vyama vingekuwa vinaendesha siasa za ki-itikadi, jambo hili lisingetokea kwani itikadi ya vyama nchini kwamjibu wa katiba zao inatofautiana kabisa.

Katika demokrasia iliyokomaa na yenye kuendeshwa ki-itikadi, kitendo cha wanasiasa kuteteana kwa sababu binafsi, au wanasiasa kuhama hama vyama, ni kitendo cha kujimaliza kisiasa. Ni katika nchi kama Tanganyika na Zanzibar pekee ambapo leo mwanasiasa anaweza jitoa CHADEMA, CCM, au NCCR na kwenda chama kingine bila ya hofu yoyote na akaendelea kuhudumu siasa za kitaifa tu. Hiki ni moja ya vielelezo vikubwa juu ya udhaifu wa vyama vyetu ki- itikadi.

Katika mazingira ya kawaida, kitendo cha kiongozi kuhama chama ni sawa na kukana imani (itikadi) yake na kukumbatia imani (itikadi) nyingine. Kwa mwanachama kufanya hivi sio jambo la hatari sana, lakini ni la hatari sana kwa viongozi.

Ni mapungufu haya ya ki-itikadi ndiyo hupelekea vyama vyetu kunadi ilani na sera zinazofanana, badala ya kuwa na ushindani mkali wa mtazamo unaotokana na itikadi. Katika siasa za sasa, vyama vyote vinashindana kwenda Ikulu, sio kuleta jambo jipya linalotokana na itikadi zao, bali kutekeleza sera zile zile za soko huria zilizojaa uholela.

Vyama pia vinapoteza muda mwingi sana kushindania yasiyo na umuhimu sana yakiwa yametapakaa kama vile haki za raia, utawala wa sheria, na vita dhidi ya ufisadi. Siasa juu ya masuala haya zimekosa uthabiti na kuungamana kutokana na udhaifu wa ki-itikadi. Vile vile kutokana na udhaifu wa ki-itikadi, umaarufu wa vyama mara nyingi (kama sio mara zote), unatokana zaidi na hulka za viongozi waliopo katika vyama hivyo, hasa nguvu zao katika jamii wanazotoka, bila ya kujali vyama wanavyotoka au itikadi wanazoziamini.

Hivyo slogan/msukumo wa itikadi ya Chadema kwa sasa iwe ni Tanganyika HURU na Zanzibar HURU ndio msingi wa MUUNGANO imara na Tanzania IMARA
 
hiyo slogani ya Tanganyika Huru na Zanzibar Huru ndio yakuua muungano sio..... lengo lenu.la.kuua muungano halitafanikiwa...SHAME ON YOU..
 
Tutumie itikadi gani sasa ili tuweze kuongoza taifa lililoliwa na ccm miaka 52

Hapo kunahitajika mkutano wa kitaifa, watu wapige kura kuamua aina ya itikadi wanayopenda kuifuata.

Lakini kama Chadema itaingia madarakani ikiwa pekee yake bila (UKAWA), taifa litaongozwa kwa itikadi ya Chadema ya MRENGO WA KATI.
 
yericko nyerere umechanganyikiwa na ugumu wa maisha
 
hiyo slogani ya Tanganyika Huru na Zanzibar Huru ndio yakuua muungano sio..... lengo lenu.la.kuua muungano halitafanikiwa...SHAME ON YOU..

Mada kama haikuhusu ni bora ukakaa kimya kuliko kutuvuruga hapa,

cc Invisible
 
Last edited by a moderator:
Changia mada kaka acha matusi ili ni darasa katoa yerrico# abakorakamo. Mhaya gani c muelewa?
 
Hiyo itikadi uliyoitoa hapo juu haitakuwa na mvuto wa kutosha kwa kwa watanganyika kwa sababu mpaka sasa huu muungano hauna impact yoyote kwa mtanganyika wa kawaida. Itakadi ya chADEMA inatakiwa iwe radical zaidi. Mfano uchumi na rasimali za nchi kumilikiwa na wananchi. Na hapa sasa kutekeleza ipasavyo sera ya ugatuaji madaraka kwenda katika serikali za mitaa. Maanake sasa wananchi wfaidi moja rasimali zinazotoka katika maeneo yao.Na hii ndio maan hasa ya nguvu ya umma. Tutunge sera zitakazoweza kuzalisha matajri wengi zaidi wa kitanzania ili faida inayopatikana kwenye rasimali zetu ibakie hapa nchini na hivyo kukuza uchumi na ajira. Watu km kina Muhongo waeleimishwe kwamba ili nchi iendelee lazima iwe na uwezo wa kutengeneza matajiri wengi zaidi wa kizalendo. Naposema matajiri naamanisha matajir kweli km kina Bakhresa, na mengi. Tunatakiwa tuwe nao km mia moja hivi! Hata hivyo sijui km Bakresa anawekeza faida yake yote hapa nchini.
 
Hiyo itikadi uliyoitoa hapo juu haitakuwa na mvuto wa kutosha kwa kwa watanganyika kwa sababu mpaka sasa huu muungano hauna impact yoyote kwa mtanganyika wa kawaida. Itakadi ya chADEMA inatakiwa iwe radical zaidi. Mfano uchumi na rasimali za nchi kumilikiwa na wananchi. Na hapa sasa kutekeleza ipasavyo sera ya ugatuaji madaraka kwenda katika serikali za mitaa. Maanake sasa wananchi wfaidi moja rasimali zinazotoka katika maeneo yao.Na hii ndio maan hasa ya nguvu ya umma. Tutunge sera zitakazoweza kuzalisha matajri wengi zaidi wa kitanzania ili faida inayopatikana kwenye rasimali zetu ibakie hapa nchini na hivyo kukuza uchumi na ajira. Watu km kina Muhongo waeleimishwe kwamba ili nchi iendelee lazima iwe na uwezo wa kutengeneza matajiri wengi zaidi wa kizalendo. Naposema matajiri naamanisha matajir kweli km kina Bakhresa, na mengi. Tunatakiwa tuwe nao km mia moja hivi! Hata hivyo sijui km Bakresa anawekeza faida yake yote hapa nchini.

Nakushukuru sana mkuu,

Nakubaliana nawe kabisa mkuu, Lakini nifafanue tena hapo, itikadi haiwezi kubadilika kwakuwa ni "imani", lakini msukumo wa itijadi hiyo (slogan) inaweza kubadilika kulingana na mahitaji ya chama ama umma tunaoufanyia siasa, sasa malengo yetu ni kushika dola 2015, na tukipima tunaona mwitikio wa umma juu ya slogan yetu ile ya miaka 22 iliyopita umepungua uthabiti hii nikuwa watu wameizoea na wanaichukulia kama yakawaida tu, kumbuka mazoea huzaa tabia, hivyo kama chama lazima tuangalie njia mbadala za kueneza itikadi yetu ya mrengo wa kati, na kwakuwa suala la uhuru wa tanganyika na zanzibar tumeungwa mkono kwa wingi na kimtazamo halitaisha leo,basi slogan yetu itembee humo kwa sasa.
 
Kuna point nyingi. sana apa mkuu maana tupo au wapo wengi sana hawaelewi ata itikadi ya vyama vyao wanasubiri PA waende kweny mkutano.

Kutokuwa na watu wenye iman flani katk chama ndo tunazalisha wakimbizi wa kisiasa nchini kwetu.

Maana kiiman kama hujaiva ukibadilishwa huwezi kujisikia aibu wal taabu yyte.

Ila najua kama UKAWA watadumu lazima wataandaa itikadi ya pamoja, i hope itabeba dhima kubwa.
 
Kuna point nyingi. sana apa mkuu maana tupo au wapo wengi sana hawaelewi ata itikadi ya vyama vyao wanasubiri PA waende kweny mkutano.

Kutokuwa na watu wenye iman flani katk chama ndo tunazalisha wakimbizi wa kisiasa nchini kwetu.

Maana kiiman kama hujaiva ukibadilishwa huwezi kujisikia aibu wal taabu yyte.

Ila najua kama UKAWA watadumu lazima wataandaa itikadi ya pamoja, i hope itabeba dhima kubwa.

Ndio mkuu, kama nilivyomjibu mdau mmoja hapo juu kuwa,

Hapo kunahitajika mkutano wa kitaifa, watu wapige kura kuamua aina ya itikadi wanayopenda kuifuata.

Lakini kama Chadema itaingia madarakani ikiwa pekee yake bila (UKAWA), taifa litaongozwa kwa itikadi ya Chadema ya MRENGO WA KATI.
 
nenda global publishers - utazikuta mada fupifupi zinazoendana na akili yako.

Nadhani mods wajitahidi kutuboreshea udhibiti wa mijadala, watu wa aina ya abakorakamo wasipewe fursa ya kuchafua mijadala kabisa
 
Last edited by a moderator:
Ni wazo zuri sana japo naona umekazia zaidi kwenye wimbo wenyewe kuliko waimba huo wimbo .Nyongeza yangu kwenye wazo lako ni kwamba,Chama kiandae watu walio na utaalamu mzuri wa kugundua wanasiasa wenye vipaji vya siasa na uongozi ambao kama wakichaguliwa kuwa wagombea wa chadema aidha kwenye nafasi za ubunge au udiwani basi wawe na uwezo mkubwa kuelezea sera,mawazo na mipango ya kimaendeleo ya chama kwa wananchi na wakaeleweka vizuri tena na wananchi wa kutoka kwenye makundi mbalimbali ya kijamii kama vile wanafunzi wa shule za sekondari,vyuo,wafanyakazi,wafanyabiashara na wakulima.Kwamba wagombea hawa wawe wepesi kubadili lugha na ujumbe kulingana na mazingira na aina ya hadhira/umma wanayoongea nayo.Mwisho,Ni vyema CHADEMA kuanzia sasa wakaanzisha utamaduni wa kuandaa mikutano maalum ya ndani maaruf kama HALL MEETING kwaajili ya kujadiliana/kuelimishana na wananchi wa makundi mbalimbali ili waweze kuyaelewa malengo ya chama kwa undani zaidi.Let us say Siku flani mnaandaa HALL MEETING na kundi la wafanyabiashara wakubwa,next mnakutana na wafanyabiashara wa kati kisha mnakutana na wafanyabiashara wadogo wadogo,Kupitia mikutano ya namna hii ambayo itatoa fursa ya kujadiliana,maswali kuulizwa na majibu yake kupatikana itawawezesha wafanyabiashara kuelewa kwa kina sera,mawazo na mipango ya maendeleo ya CHADEMA na wakivutiwa nayo wafanyabiashara hawa wanaweza kugeuka kuwa mawakala wa uenezi wa itikadi za chama kwa wengine.Hivyo ndivyo vyama vyote makini vya siasa duniani vilivyofanikiwa kujenga majeshi yao yenye nguvu ya kiitikadi,Walianza kuyaelimisha makundi madogo ndani ya jamii kisha makundi haya yakageuka kuwa jeshi imara la uenezi wa itikadi za vyama husika kwa jamii pana zaidi.
 
Back
Top Bottom