Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 142,025
- 285,577
cdm iko tayari kupokea wazo lolote zuri litakalosaidia kuing'oa ccm 2015 , asante sana kaka .
Hiyo ni sahihi kwakuwa ndio tafsiri ya itikadi ya mrengo wa kati inayoaminiwa na Chadema.
Yericko kwanza nikupongeze
Nadhani utakubaliana nami chadema kwanza inabidi ifikilie njinsi ya kuingia ikulu.Pili inabidi chama kijihoji je ni watu gani watakaotufikisha ikulu? jibu la haraka ni wanachi kupitia sanduku la kura.
Sasa tukija kwa wanachi wengi wa tanzania hawajali itikadi ya chama kama inafuatwa mfano sera ya ccm ya mwaka 2015 walikuwa na sera ya maisha bora kwa kila mtanzania lakini wanachi hawakuhoji kabla ya kusema maisha bora kwa kila mtanzania je ni vip hayo maisha bora yatakuja hata wale wasomi ambao walijua haiwezekani waliwakumbatia na awamu ilipoisha wakasema sasa ni kasi zaidi,nguvu zaidi na ari zaidi lakini watanzania hawakuhoji je mlisema maisha bora kwa kila mtanzania sasa mnasema kasi zaidi je hicho ambacho mmekifanya kipo wap ili tuwape ridhaa mfanye zaidi.
Watanzania wengi hawajui ubora wa sera ya vyama ili wapime ni chama kipi chenye sera bali wanaangalia ni jamaa,ndugu gani wa karibu wamsapport ili ya yeye apate kutoka kimaisha kibinafsi.lakin pia wanagalia atampa nini ili atoke kimaisha
Nikija kwenye slogan unayopropose ya tanganyika huru na zanzibar huru.Itakuwa ngumu kuwafikia wananchi wengi wa vijijini ambao ndio wapiga kura wengi maana hawaoni nini faida wanapata faida ya tanganyika kwa sababu hawaoni faida ya muungano hivyo itakuwa vigumu wa tangayika lakina kwa zanzibar inawezekana
hiyo slogan ya peoples power ina uhusiano gani na huo mrengo wako wa kati?
cdm iko tayari kupokea wazo lolote zuri litakalosaidia kuing'oa ccm 2015 , asante sana kaka .
View attachment 157320
Kaa utulie ule mafao ya CCM yenu ila kumbuka kuwa this is your last term. 2015 mnaachia kwa nguvu ya Ballot Box.
Na nyie misukule changieni vibakuli vinavyopitishwa kwenye mikutano ya M4C, Slaa ameigeuza Ufipa kuwa ni saccos, Josefina ana NGO ina fedha kuliko chadema. Mbowe anapeleka hawara kula nae bata Dubai.
Endeleeni kushangilia majanga!
Jibu la swali lako ni rahisi saaaana.Tutumie itikadi gani sasa ili tuweze kuongoza taifa lililoliwa na ccm miaka 52
Utakuwaje na itikadi wakati hata nidhamu za maadili huna?
Wewe unaeongelea itikadi wewe una itikadi ipi? Ya uongo? Ulikuja humu JF ukadanganya kuwa Nyerere ni baba'ko mzazi. Mpaka Andrew Nyerere akasema kauliza Msasani hawakujui, alipoenda Mwitongo akauliza hawakujui. Akasema akamuuliza mpaka Butiku (naona hapo alitaka kuhakikisha kama Nyerere alikuwa na katoto ka siri nje) nae pia akasema hakujui, jibu alilopewa ni kuwa wengi wapo wanatumia majina tu.
Ikiwa wewe uliyeleta mada huna itikadi wala hujui itikadi ni nini, hivi leo una ubavu wa kuongelea itikadi ndani ya chadema na CCM?
Huoni haya?
Nimekupa link ya darasa la siasa, hebu usiende kama nyumbu mkuu, isome ikubadili
endelea kujitahidi kaka. Mkuu mbowe anakusoma ..uchaguzi ujao atakukumbuka kukupa hata kaujumbe kamati kuu
Hiki ulichokifanya kikongwe wangu inaitwa kitaalamu "ad hominem abusive" yaani unamshambilia mwenye hoja binafsi baala ya kuishambulia hoja> It is a very low type of thinking inayoitwa fallacious reasoning. Mazingira yanayomzunguka mtoa hoja hayapunuzi au kuoneza uhali wa hoja. Je hoja liyoleta nyeyrere hapa inahusu mambo ya maadili? Umefanya kosa lingine tena la kimantiki hapa kwa kuhamisha mjadala. Umedistort original argument ya mleta mada halafu ukaendela kunock down your own distorted argument. Mleta mada hazungumzii habari za maadili hapa!
Jibu la swali lako ni rahisi saaaana.
Kinachotakiwa kufanywa na cdm ni kuwaeleza wananchi juu ya sera za chama chao kuhusu:
1-Afya cdm wakiingia madarakani sera yao ya afya ikoje.
2-Madini Sera ya cdm kuhusu madini ni ipi.
3-Elimu sera ya cdm kuhusu elimu ni ipi
4-Jumuia ya Afrika mashariki-sera za cdm zinasemaje kuhusu hili.
5-Miundombinu Sera ya chama inasemaje kuhusu hili.
6-Maliasili ya nchi-Sera ya cdm imekaa vipi
7-Mambo ya nje-Sera za cdm zikoje
8-Majeshi ya Tanzania kuwa walinda amani nchi mbalimbali dunia-Sera zao zikoje
9-Muungano na z'bar-Sera za cdm zinasemaje.
10-Uchumi-sera za chd zikoje kuhusu uchumi.
Vitu hivi pamoja na vingine vingi,ambavyo kwa ujumla wake ndio MSINGI MKUU,vinapaswa kuimbwa na cdm kila siku,ili wananchi WAJUE NA WAONE TOFAUTI KATI YA ALIYEKO NA ATAKAE KUJA.Kwa kuwapa wananchi comperative advantage ya kujua ajaye ana nini cha kufanya kulinganisha na aliyeko,ndiko kutakako ipeleka cdm ikulu.na si vinginevyo.
Siasa za zima moto ya kudadia matukio kama ndio sera, kamwe haiwezi kuipeleka cdm ikulu.
USHAURI HUU WANGU NI WA BURE.
Mkuu, huende sio mfuatiliaji wa siasa za Chadema,
Hayo yote na mengine mengi, ndio huhubiriwa na Chadema kila uchao kwa miaka 22 sasa,
Mjadala uliopo ni Kaulimbiu/Slogan ya kuendeza itikadi ya Chadema ijulikanayo kama itikadi ya mrengo wa kati.
mambo ya bavicha haya. bavicha na matusi are synonymous.Chizi umejua kuunganisha herufi kwa kutumia keyboard.
ITIKADI ya CHADEMA ni itikadi ya MRENGO WA KATI, Ninashawishika kusema kuwa kile kiambata cha uenezi wa itikadi ya Chadema ambacho ni haki za raia, utawala wa sheria, na vita dhidi ya ufisadi, kimepungua uthabiti na ushawishi katika jamii na hakina nguvu tena ya kuiondoa ccm madarakani 2015,
Nilipofundisha somo la siasa hapa https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/640686-darasa-la-siasa-4.html nilieleza kwa kirefu namna itikadi inavyoenezwa na umuhimu wa itikadi katika siasa kwa ujumla.
Sehemu ya somo hilo ilipembua kinagaubaga hasa juu yayo, na hata sasa nasisitiza hili kwa chama changu.
Ili itikadi iweze kuenezwa/kuuzika ni lazima iende sambamba na hitaji kuu la umma unaoufanyia siasa, hapa ndipo vyama vyetu vinapofeli na kujikuta vinakuwa vyamsimu.
Kwa Afrika ya leo imekubwa na ombwe la vyama vya siasa kutokuwa na itikadi inayoaminiwa na wanachama wa vyama husika, Tatizo hili limeikumba hata siasa ya nchi yetu kwa sasa, Leo tuna vyama visivyokuwa na itikadi inayoeleweka ya vitendo.
CCM ilifanikiwa ki-itikadi chini ya mfumo wa chama kimoja kutokana na itikadi urithi ya kihafidhina iliyolenga ukombozi wa nchi na Utaifa (chini ya TANU); baadae siasa ya Ujamaa na kujitegemea ililenga kumwinua Mtanganyika.
Tangu kupigwa mweleka kwa azimio la Arusha mwaka 1992 na kuzaa azimio ls Zanzibar la mwaka 1992, CCM imekuwa inahubiri itikadi ya Ujamaa, lakini upande mwingine, inatekeleza itikadi ya soko huru, tena bila ya mchujo (ubepari).
Ukosefu huu wa msimamo kiitikadi wa ccm ndio tiketi ya mparaganyiko wa chama hiki na sasa kinaelekea ahera kabisa, huku chagizo la Ufisadi likisindikiza kifo hicho kwa ccm.
Lakini tuna vyama vilivyopata umaarufu kutokana na sababu ambazo hazihusiani na UMMA kubaini ubora wa itikadi ya chama baada ya kufananisha na itikadi za chama/vyama vingine vilivyopo, Badala yake, umaarufu wa vyama hivi unatokana na UMMA kuvikubali kwa sababu nyingine nje kabisa ya ubora wa itikadi zao. Mathalani ni umaarufu wa NCCR miaka ya 1995 na ule wa Chadema miaka ya 2005 hadi sasa.
Ili somo letu liende vizuri ni vema nifafanue baadhi ya mambo katika hili, neno kujipatia umaarufu badala ya kujipatia mafanikio, ni kwasababu tofauti na mafanikio ambayo hutokana na itikadi, mara nyingi umaarufu hutokana na vitu vya mpito, na huwa haudumu kwa muda mrefu.
Wanachama na wafuasi wenzangu wa Chadema, mtakumbuka umaarufu wa NCCR miaka ya 1995; umaarufu wa Chadema hauna tofauti kubwa sana kwa sababu mafanikio tunayoyaona hayatokani na watu kuipokea kwa uthabiti wake itikadi ya chama, bali kwa vitu vya msimu ama matukio tu, ambavyo vinaweza meguka kirahisi.
Pia tuna vyama vilivyopata mafanikio kisiasa (sio umaarufu) kutokana na itikadi zao. Lakini vyama hivi vina udhaifu mmoja mkubwa juu ya itikadi zao: Itikadi hizi zinaendana na hali halisi ya upande mmoja tu wa jamii badala ya jamii nzima. Mathalani CUF na mafanikio ya kiitikadi visiwani ambayo imekuwa vigumu kuyarudia Bara. Mafanikio ya sasa ya CUF visiwani Zanzibar hayana tofauti kubwa na mafanikio ya TANU Tanganyika miaka 1960. Mafanikio ya CUF yanatokana na itikadi inayohanikizwa na Utaifa /Ukombozi dhidi ya Utawala wa Tanganyika. Pamoja na mafanikio yake huko Zanzibar, itikadi ya CUF haina mashiko upande wa Tanganyika kwakuwa haina hanikizo la hitaji la umma wa Watanganyika.
Udhaifu wa itikadi ya CUF utapitia hatua tatu za maisha: (1) Itikadi ya uhuru na Utaifa iliyozaa matunda hadi sasa Zanzibar, (2) baada ya utaifa kupatikana, CUF itakumbwa na changamoto za kutekeleza ahadi ilizozitoa wakati wa mapambano ya kudai utaifa kutoka Tanganyika na hali itazidi kuwa ngumu zaidi iwapo patatokea vyama vingine vya upinzani upande wa Zanzibar, (3) Iwapo vitajitokeza vyama vipya vyenye nguvu Zanzibar, itikadi ya CUF itazidi kuishiwa makali kutokana na kushindwa kutekeleza ahadi za ukombozi (kama ilivyotokea kwa CCM), na vyama vitabaki kukosoana huku CUF ikionekana sio lolote na vyama vya upinzani Zanzibar vitaendeleza kasumba yakusahau kabisa kwamba adui yao ni itikadi zenye kuishi maisha marefu.
Udhaifu huu wa ki-itikadi ndani ya vyama vya siasa unawakosesha wananchi fursa ya kuunda muono na mtazamo wa kisiasa unaofuatana na imani za kiitikadi zinazotambulika, na nyepesi kueleweka au kutofautisha. Hii ndio sababu kubwa inayopelekea wananchi kuunga mkono watu au vyama kishabiki zaidi kuliko kuunga mkono vyama hivyo kutokana na kushiba itikadi za vyama.
Tofauti na nchi zilizokomaa kisiasa, kwa Tanganyika na Zanzibar suala la wanachama kuhama hama vyama ni suala la kawaida. Kama vyama vingekuwa vinaendesha siasa za ki-itikadi, jambo hili lisingetokea kwani itikadi ya vyama nchini kwamjibu wa katiba zao inatofautiana kabisa.
Katika demokrasia iliyokomaa na yenye kuendeshwa ki-itikadi, kitendo cha wanasiasa kuteteana kwa sababu binafsi, au wanasiasa kuhama hama vyama, ni kitendo cha kujimaliza kisiasa. Ni katika nchi kama Tanganyika na Zanzibar pekee ambapo leo mwanasiasa anaweza jitoa CHADEMA, CCM, au NCCR na kwenda chama kingine bila ya hofu yoyote na akaendelea kuhudumu siasa za kitaifa tu. Hiki ni moja ya vielelezo vikubwa juu ya udhaifu wa vyama vyetu ki- itikadi.
Katika mazingira ya kawaida, kitendo cha kiongozi kuhama chama ni sawa na kukana imani (itikadi) yake na kukumbatia imani (itikadi) nyingine. Kwa mwanachama kufanya hivi sio jambo la hatari sana, lakini ni la hatari sana kwa viongozi.
Ni mapungufu haya ya ki-itikadi ndiyo hupelekea vyama vyetu kunadi ilani na sera zinazofanana, badala ya kuwa na ushindani mkali wa mtazamo unaotokana na itikadi. Katika siasa za sasa, vyama vyote vinashindana kwenda Ikulu, sio kuleta jambo jipya linalotokana na itikadi zao, bali kutekeleza sera zile zile za soko huria zilizojaa uholela.
Vyama pia vinapoteza muda mwingi sana kushindania yasiyo na umuhimu sana yakiwa yametapakaa kama vile haki za raia, utawala wa sheria, na vita dhidi ya ufisadi. Siasa juu ya masuala haya zimekosa uthabiti na kuungamana kutokana na udhaifu wa ki-itikadi. Vile vile kutokana na udhaifu wa ki-itikadi, umaarufu wa vyama mara nyingi (kama sio mara zote), unatokana zaidi na hulka za viongozi waliopo katika vyama hivyo, hasa nguvu zao katika jamii wanazotoka, bila ya kujali vyama wanavyotoka au itikadi wanazoziamini.
Hivyo slogan/msukumo wa itikadi ya Chadema kwa sasa iwe ni Tanganyika HURU na Zanzibar HURU ndio msingi wa MUUNGANO imara na Tanzania IMARA
Naomba unitajie kiongozi ye yote wa cdm ambaye amesimama kwenye jukwaa la kuwahutubia wananchi kwamba endapo wakikabithiwa nchi hii kwenye elimu tatafanya hivi,kwenye afya tutafanya hivi,kwenye madini tutafanya hivi.
Mimi nafuatilia sana siasa za hapa kwetu,kingetokea hicho unachokisema,na sera zake nikazichambua kwa kina ,ningekuambia usemayo ni kweli,lakini nasikitika kuwa kinyume chake usemayo sio kweli.
Sasa hivi wamedandia katiba na jumuia ya ukawa.
Kabla ya hayo ajenda zilikuwa mwagosi,ufisadi,richmond,OPERATION SANGARA,M4C,maandamano mpaka kieleweke,nchi haitatawalika,hivyo ndivyo nilivyokuwa naviona na kusikia,LAKINI SIO SERA SERA SERA SERA SERA.
naona unamsapoti muokota makopo mwenzako. tangia kile kipigo kitakatifu cha chopa 3 kata 3 halafu ikafuatiwa na zahama kule kalenga na baadaye kuinua matanga pale chalinze mmechanganyikiwa kabisa. na huo ni mwanzo tu, dhambi ya ubaguzi ni ya kuepukwa kuliko kitu kingine chohcote.Chizi umejua kuunganisha herufi kwa kutumia keyboard.