RockSpider
JF-Expert Member
- Feb 16, 2014
- 6,859
- 2,762
Hiyo itikadi uliyoitoa hapo juu haitakuwa na mvuto wa kutosha kwa kwa watanganyika kwa sababu mpaka sasa huu muungano hauna impact yoyote kwa mtanganyika wa kawaida. Itakadi ya chADEMA inatakiwa iwe radical zaidi. Mfano uchumi na rasimali za nchi kumilikiwa na wananchi. Na hapa sasa kutekeleza ipasavyo sera ya ugatuaji madaraka kwenda katika serikali za mitaa. Maanake sasa wananchi wfaidi moja rasimali zinazotoka katika maeneo yao.Na hii ndio maan hasa ya nguvu ya umma. Tutunge sera zitakazoweza kuzalisha matajri wengi zaidi wa kitanzania ili faida inayopatikana kwenye rasimali zetu ibakie hapa nchini na hivyo kukuza uchumi na ajira. Watu km kina Muhongo waeleimishwe kwamba ili nchi iendelee lazima iwe na uwezo wa kutengeneza matajiri wengi zaidi wa kizalendo. Naposema matajiri naamanisha matajir kweli km kina Bakhresa, na mengi. Tunatakiwa tuwe nao km mia moja hivi! Hata hivyo sijui km Bakresa anawekeza faida yake yote hapa nchini.
Mkuu nakubaliana na wewe 100%... mimi napendekeza slogan iwe " Mali za Watanzania kwa Faida ya Watanzania"... Wasiogope mabwana wa dunia hii kwani nguvu ya umma siku zote hushinda ...Haiwezekani eti wanakuja wazungu wapiga picha hapa wanalipwa mishahara mikubwa na mabonus ya kufa mtu wakati engineers wetu wanalipwa fedha kiduchu huku wakikamuliwa kodi za kufa mtu...