CHADEMA, huu ni wakati wakuwa Radio na TV ya Chama

DATAZ

JF-Expert Member
May 25, 2012
2,453
5,988
Ninyi ni Chama kikuu Cha upinzani na Chama mbadala wa CCM, kuwa na media yenu itasaidia sana kueneza Sera na elimu mbalimbali kwa wanachama na wananchi. Uenezi wa Chama unahitaji vyombo vya uhakika vya habari.

Ni aibu kwa Chama Kikuu, kikongwe kama hiki, kutoa matamko yake kwenye Twitter huku mkijua wanachi wengi wako vijijini na hawana Access na hivyo vitu.

Kama tulivyochangia uendeshaji wa Kesi ya Mwenyekiti mbowe na matukio mengine, hatushindwi kuchangia na kufanikisha uwepo wa radio na Tv ya Chama, if need be.

Leo vijana wadogo kqma Zamaradi ana Tv, Majizo ana Tv, Why not CHADEMA.
Hili pia linawahisu ACT-Wazalendo.
 
Wapinzani wao chama tawala watakubali kuwapa masafa? Maana serikali ni ya ccm, labda kama dhana ya masafa ya umma hapo itabidi wawe nayo tu. Hawana hata pro media za kueneza sera zao
 
Wapinzani wao chama tawala watakubali kuwapa masafa? Maana serikali ni ya ccm, labda kama dhana ya masafa ya umma hapo itabidi wawe nayo tu. Hawana hata pro media za kueneza sera zao
Wangetimiza na kufuata matakwa na vigezo vyote vya kuanzisha TV & Radio, then wakikwamishwa ndio warudi kwa wananchi..sasa zingine Watz tupunguze kulalamikalamika ,tujifunze kufuata taratibu na kuchukua hatua na pia tupunguze HOFU na hisia hasi
 
Ni wazo zuri lakini utekelezaji wake ni mgumu sana kwa mazingira yetu ya kisiasa.
 
Ninyi ni Chama kikuu Cha upinzani na Chama mbadala wa CCM, kuwa na media yenu itasaidia sana kueneza Sera na elimu mbalimbali kwa wanachama na wananchi. Uenezi wa Chama unahitaji vyombo vya uhakika vya habari.

Ni aibu kwa Chama Kikuu, kikongwe kama hiki, kutoa matamko yake kwenye Twitter huku mkijua wanachi wengi wako vijijini na hawana Access na hivyo vitu.

Kama tulivyochangia uendeshaji wa Kesi ya Mwenyekiti mbowe na matukio mengine, hatushindwi kuchangia na kufanikisha uwepo wa radio na Tv ya Chama, if need be.

Leo vijana wadogo kqma Zamaradi ana Tv, Majizo ana Tv, Why not CHADEMA.
Hili pia linawahisu ACT-Wazalendo.
Vyombo vikuu vya habari hawatangazi shughuli za Chadema. Siyo haki kwa TBC na hata ITV kufamya kazi kama mali ya CCM.

Ni muhimu Chadema kuanzisha vyombo vyao vya habari. Sina shaka kukiwa na TV Chadema itapata watazamaji wengi sana.

Siyo kazi ndogo kuanzisha TV lakini Chadema siyo chama kidogo. Buy an existing TV company if you can
Hili neno!, angalia hili ni bandiko la lini Elections 2015 - Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni ...
17. Sasa ili kuwafikia Watanzania wote na kuwaamsha waliolala, Chadema haiwezi kuwafikia Watanzania wote kwa kutegemea mikutano ya hadhara na mass media za wengine. Chadema lazima wawe na mass media yake ambayo ita propagate the message of changing the mindset ya Watanzania. Chadema wana all the resource kumiliki media yake lakini very unfortunately they are myopic, hawana vision ya kuona mbali kuangalia nje ya box and see a bigger picture. Hawajui kupanga priorities zao. Bei ya gari moja tuu la M4C linatosha kununua transmitter ya Digital ya redio na TV. Chadema bila media yake, ni kutwanga maji kwenye kinu, CCM ina media yake na TV yake TBCCM, radio zake na magazeti yake, Chadema bila media yake, ikulu wataendelea kuisikia tuu kwenye bomba, 2015 ni CCM tena! .

Wasalaam.

Paskali
hivyo alipokuja Mwamba wa Kaskazi nilisema Elections 2015 - Mabadiliko Chanya ya Ujio wa Lowassa: CHADEMA Kuhama Ufipa!, Kuwa Makao Yake, Kituo cha TV na Redio!
Wanabodi,

Ukipiga hesabu ya jumla ya ruzuku yote ambayo Chadema imekuwa ikipokea, ukajumlisha na zile fedha za Sabodo alizoipa Chadema kujenga ofisi za makao makuu zenye hadhi, na kulinganisha ruzuku hiyo imekuwa ikifanyia nini, utakubaliana na mimi, kuwa fedha hiyo, ingetosha kabisa kujenga jengo jingine la maana na lenye hadhi kwenye eneo la kutosha. Hali hii imetokana na upangaji mbovu wa vipaumbele vyake, hali iliyopelekea matumizi mabovu ya ruzuku, kama yalivyofafanuliwa kwenye ripoti ya CAG.

Mabadiliko hayo chanya ya ujio wa Lowassa sio tuu kwa Chadema kumiliki jengo lake lenyewe, bali pia Chadema itamiliki media zake yenyewe kikiwepo kituo chake cha Redio na Televisheni pamoja na magazeti yake yenyewe, kwa sababu Lawassa hapo alipo tayari anamiliki by proxy, familia kubwa ya media, yenye vituo vya Redio, TV na magazeti lukuki!, hivyo sasa pia vitatumiwa kuisupport Chadema kwa kuanzia tuu, wakati mchakato wa umiliki rasmi wa vyombo vyake yenyewe ukiendelea!.

Ama kweli mgeni njoo, mwenyeji apone!.

Hongera sana Lowassa!.

Hongera Chadema.

Ikulu 2015 ni ya UKAWA!.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali

Ushauri huu niliwapa toka 2012!, asante sana kwa kuliona leo 2023!.
Mungu ibariki Chadema iweze!
Mungu ibariki Tanzania

P
 
Back
Top Bottom