Ilani ya chama isiwe mali ya chama na isibadilishwe mara kwa mara

hagau

JF-Expert Member
Dec 17, 2023
390
1,310
Napendekeza kusiwe na Mabadiliko ya ilani ya chama kinachokuwa madarakani mara kwa mara.

Na ilani ya chama iwe ni mali ya Serikali (Umma).

Aidha, tunapoenda kwenye chaguzi na kumaliza uchaguzi tuendelee na ilani iliyokuwepo ispokuwepo Rais anae ingia Madarakani aseme kwa kila kipengele cha ilani atatekeleza asilimia ngapi ndani ya mwaka, miaka 2, n.k


Faida za mpango huu wa kuepuka kutengeneza ilani kila mara.


1. Tunakuwa na mwongozo wa kutuonesha wapi tulipokuwa, tulipo na wwpi tunatakiwa kwenda

2. Itapunguza ufisadi kwa kiasi fulani, kwa sababu imeonekana baadhi ya vipengele vya ilani kwa miaka ya hapo nyuma vililenga kujibu au kutoa fursa kwa wezi wa mali za umma.

3. Itatuondolea garama kubwa zinazotumika kukusanya maoni, kuandaa na kusambaza ilani husika.

4. Itasaidia kuonesha usirious wa serikali tofaut na ilivyo sasa hata watu wa serikali wakipita kukusanya maoni ya kuandaa ilani wananchi wanapuuza maana hawaoni mantiki ya ilani iliyoisha muda wake.

Hivyo nashauri ilani iliyopo iliyo anadaliwa awamu ya 05 iwekewe mchakato kuwa mali ya Umma na utekelezaji aake utahusu uongozi wa mtu au chama chochote kitakachokuja madarakani.


Aidha, hii tunajifunza kutokana na mataifa ya wenzetu yaliyopiga hatua kubwa waliamua kustiki katika malengo mahususi kwa muda mrefu na kuja kupata matokeo makubwa.


Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom