Aliyeona CHADEMA wakitoa misaada kwa wananchi wa Hanang kama walivyofanya CCM naomba aniwekee hapa picha au video yake

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,330
9,750
Ndugu zangu Watanzania,

Mpaka sasa tumeona namna chama cha Mapinduzi kilivyofanya kazi kubwa ya uokozi na misaada kwa wananchi wa hanang. tumeona CCM ikitoa faraja kwa kushirikiana kwa ukaribu na wananchi mbalimbali katika kuokoa watu na kuwasaidia majeruhi. Tumeona pia CCM ikitoa misaada ya vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya million kumi kwa wahanga.

Tumeona pia viongozi wote wa CCM kuanzia ngazi ya Taifa wakifika eneo la tukio kutoa pole ,faraja na kuwasaidia wahanga,tumemuona makamu mwenyekiti wa CCM Taifa, kaimu katibu mkuu,viongozi wote ngazi ya mkoa wakiwa eneo la tukio huku mh Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye ni Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania atatembelea na kufika maeneo mbalimbali yaliyoathiriwa ndani ya wiki hii.

Lakini kila mtu ameshangaa kwa chama hiki cha CHADEMA kinachojiita chama kikuu cha upinzani nchini kimeshindwa na hakuna mahali popote pale ilipoonekana CHADEMA na viongozi wake wakitoa hata kilo moja tu ya sukari au unga. Hakuna cha mwenyekiti wa CHADEMA mbowe au makamu ambaye ni lissu au katibu mkuu wake waliofika eneo la tukio zaidi ya kuona akina Lissu wakiwa Dar kutumbua na kutanua maisha na kupiga porojo na blaa blaa zisizo na ukweli wowote ule.

Kiukweli inasikitisha sana tena sana chama kinachojiita chama kikuu cha upinzani kinashindwa kwenda kuwapa faraja wahanga? Kinashindwa kupeleka hata kilo moja ya sukari? Kinashindwa hata kupeleka mablanketi kwa ajili ya watoto wadogo? Kinashindwa kupeleka hata unga kwa ajili ya yatima na wajane walioachwa ghafla?

Kama CHADEMA hakiwezi kulia na watu na kuwapa faraja wakiwa na matatizo na shida kitaanzia wapi kuwapa faraja na kuwafuta machozi kikipewa madaraka? Kitawakumbukia wapi? Kitaanzaje kuhangaika kwenda kwenye matatizo ya wananchi? Mbowe yupo wapi? Lissu yupo wapi? Kwanini hawajaenda mpaka sasa? Mmewaona wapi hawa wapotoshaji wakitoa faraja na msaada kwa wahanga?

Yaani club za mpira kama simba na yanga zisizo tegemea kura za wananchi zimeguswa na kuwa na uchungu na maisha ya watu na yale yaliyo wakuta na kuamua kwenda kutoa misaada ya kibinadamu kama vile unga,mafuta ya kura ,chumvi,sabuni, sukari,pesa n.k. halafu chama kama CHADEMA kinachotegemea kwenda kuomba kura za wananchi kinashindwa kuguswa na kwenda kutoa misaada? Kinashindwa kwenda kuwafuta machozi watu?Hivi inaingia akilini kweli hii? Hivi hiki chama kinajitambua kweli? Kina viongozi wenye hisia? Uchungu? Utu? Ubinadamu? Utanzania?upendo? Ukarimu na kuwa na uchungu na maisha ya watu?

Ndio maana Watanzania wanawapuuza sana CHADEMA maana wanajuwa ni chama cha kibabaishaji tu,ni chama kisichojali wala kuwa na uchungu na maisha ya watu,ni chama ambacho kinaangalia matumbo yao tu na Usaka Tonge tu,ni chama kisicho guswa na matatizo na maumivu ya watu.ni chama ambacho hata wafe wote chenyewe hakina habari zaidi ya kutumbua maisha tu.

Ndio maana wananchi wanaipenda na kuiamini CCM, kwa kuwa wameona na wamekuwa wakiona siku zote namna CCM ilivyo karibu nao,namna ilivyo na uchungu na maisha yao ,namna inavyohangaikia maisha yao,namna inavyoguswa na maumivu yawapatayo ,namna inavyokuwa msitari wa mbele katika kuwapigania na kuwatetea,namna inavyowafuta machozi na kuwapa faraja na matumaini wapitiapo nyakati na vipindi vigumu.

Tanzania na Dunia nzima imeona juhudi , upendo na ukarimu wa CCM kwa wananchi wake. Lakini pia watanzania na Dunia nzima imejionea namna CHADEMA walivyo wababaishaji na wasiojali maisha ya watanzania. Na wamejithibitishia kuwa CHADEMA haipaswi kupewa hata kura za moja ya ndio katika uchaguzi wa aina yoyote ile maana hawaguswi na chochote wala na lolote lile linalogusa maisha na hisia za watu.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Onesha kifungu kwenye katiba ya chadema kinachoelekeza kutoa msaada kwenye majanga kama hayo.
Acha ujinga wako ndugu yangu.kwani hujuwi kitu kinachoitwa ubinadamu na kusaidiana wakati wa shida? Kwanini hamguswi? Sasa hizo kura mtazipata kutoka kwa nani? Nani mwenye akili Timamu atawapa kura yake ya ndio?
 
Tofautisha Chama na Serikali
CCM imekwenda kama CCM na Serikali nayo imefanya kwa upande wake. Vipi CHADEMA imetoa misaada gani mpaka hivi sasa kwa wahanga?

Kwanini hamna huruma ninyi wala moyo wa kuguswa na matatizo ya watu? Yaani hadi club za mpira zinaguswa halafu lichama linalotaka kura za wananchi linashindwa kuguswa linashindwa kuguswa?
 
Back
Top Bottom