CHADEMA: Bila Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi, hakuna Uchaguzi Mkuu

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesisitiza bila katiba mpya na tume huru ya uchaguzi basi hakutakuwepo na uchaguzi mkuu nchini.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara mjini Musoma leo Jumapili, Januari 22, 2023, Naibu katibu mkuu wa Chadema bara, Benson Kigaila amesema msimamo huo tayari ulishatolewa na chama chake pamoja na magumu waliyopitia katika kipindi cha miaka saba iliyopita msimamo huo haujabadilika.

"Serikali ya CCM inapoendelea kuvuta miguu juu ya suala la katiba mpya sisi tunaendelea kupiga mstari pale pale tulipokwisha uchora ni kwamba bila katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, uchaguzi hautafanyika huo ndio msimamo wetu," amesema.

Amesema katiba mpya ni hataji la Watanzania hivyo hakuna sababu ya Serikali kupuuzia hitaji hilo badala yake inatakiwa kutekelezwa kwa maslahi ya Watanzania na nchi kwa ujumla.

"Moto haufichwi kwenye shuka pamoja na kifungo cha miaka saba lakini leo mmekuja hapa mkidai na kuitaka katiba mpya hivyo ni lazima ipatikane kwani bado hamjachoka na hamtochoka kuidai," amesema.

Naye katibu mkuu wa chama hicho, John Mnyika amesema endapo kungekuwa na katiba mpya inayodaiwa na wananchi basi leo wananchi wangekuwa na uwezo wa kuwawajibisha wabunge wengi ambao amedai wameingia bungeni kwa njia zisizokuwa halali.

"Katiba ya Jaji Warioba imetamka wazi wananchi wanataka wawe na uwezo wa kuwawajibisha wabunge wasiowajibika na kama hiyo katiba ingekuwa inatumika basi hadi sasa tungekuwa tumewawajibisha wale wabunge walioingia bungeni kimagumashi," amesema.

MWANANCHI
 
Sidhani kama CDM wanajua wanachosimamia Kwa sababu suala la katiba Mpya sio kama mkate wa kununua dukani tu ghafla, najua viongozi wao wanalijua hilo lakini wanajitoa ufahamu na kutumia katiba Mpya Kwa ajili ya popularity
 
Rekebisha hapo juu ndugu,

Katiba pendekezwa ya Warioba ilichakachuliwa. Ni mbovu.

Rasimu ndo Iko vizuri kabla haijaingia Bunge la Katiba,

Tunapambana tuanze na Rasimu ya Warioba ndipo tupendekeze njia ya Kupata wabunge wa kuingia Bunge la Katiba.
 
Serikali ya CCM inapoendelea kuvuta miguu juu ya suala la katiba mpya sisi tunaendelea kupiga mstari pale pale tulipokwisha uchora ni kwamba bila katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, uchaguzi hautafanyika huo ndio msimamo wetu," amesema
Wao ccm waendelee na utaratibu wao wakujipangia wabunge, madiwani na Rais.

Sio razima chadema tushiriki.
 
Sidhani kama CDM wanajua wanachosimamia Kwa sababu suala la katiba Mpya sio kama mkate wa kununua dukani tu ghafla, najua viongozi wao wanalijua hilo lakini wanajitoa ufahamu na kutumia katiba Mpya Kwa ajili ya popularity
Rais akiamua hata ndani ya miezi sita inapatikana katiba bora kabisa.
 
Ungejua yajayo, ungeanza kujiandaa mapema.

Bt nasikitika, yajayo ni dhahiri, Yako wazi bt yamefichwa kwako usiyaone na kuyaepuka.
Tatizo mmejijaza sana imani kwa hao wanasiasa wenu uchwara badala ya kuwa neutral, mnawaona kma malaika vile.

Hiyo katiba isiwe kigezo cha wao kususa huo ni upumbavu.

Yajayo hayawezi kufurahisha kama yatajulikana sasa isipokuwa mpka yatimie.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesisitiza bila katiba mpya na tume huru ya uchaguzi basi hakutakuwepo na uchaguzi mkuu nchini.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara mjini Musoma leo Jumapili, Januari 22, 2023, Naibu katibu mkuu wa Chadema bara, Benson Kigaila amesema msimamo huo tayari ulishatolewa na chama chake pamoja na magumu waliyopitia katika kipindi cha miaka saba iliyopita msimamo huo haujabadilika.

"Serikali ya CCM inapoendelea kuvuta miguu juu ya suala la katiba mpya sisi tunaendelea kupiga mstari pale pale tulipokwisha uchora ni kwamba bila katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, uchaguzi hautafanyika huo ndio msimamo wetu," amesema.

Amesema katiba mpya ni hataji la Watanzania hivyo hakuna sababu ya Serikali kupuuzia hitaji hilo badala yake inatakiwa kutekelezwa kwa maslahi ya Watanzania na nchi kwa ujumla.

"Moto haufichwi kwenye shuka pamoja na kifungo cha miaka saba lakini leo mmekuja hapa mkidai na kuitaka katiba mpya hivyo ni lazima ipatikane kwani bado hamjachoka na hamtochoka kuidai," amesema.

Naye katibu mkuu wa chama hicho, John Mnyika amesema endapo kungekuwa na katiba mpya inayodaiwa na wananchi basi leo wananchi wangekuwa na uwezo wa kuwawajibisha wabunge wengi ambao amedai wameingia bungeni kwa njia zisizokuwa halali.

"Katiba ya Jaji Warioba imetamka wazi wananchi wanataka wawe na uwezo wa kuwawajibisha wabunge wasiowajibika na kama hiyo katiba ingekuwa inatumika basi hadi sasa tungekuwa tumewawajibisha wale wabunge walioingia bungeni kimagumashi," amesema.

MWANANCHI
Hamuna ubavu wa kuzuia uchaguzi. Endeleeni kujitoa ufahamu
 
Sidhani kama CDM wanajua wanachosimamia Kwa sababu suala la katiba Mpya sio kama mkate wa kununua dukani tu ghafla, najua viongozi wao wanalijua hilo lakini wanajitoa ufahamu na kutumia katiba Mpya Kwa ajili ya popularity
Lah!

Sasa wewe unayejua swala la Katiba Mpya "sio kama mkate wa kununua dukani tu ghafla", unawaambiaje hao wa upande wa pili wasiokuwa na nia kabisa hata ya kulizungumzia swala hilo la katiba mpya?

Kwa hiyo kwa maoni yako, CHADEMA waishie tu kwenye mipasho hii ya "mikate"?
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesisitiza bila katiba mpya na tume huru ya uchaguzi basi hakutakuwepo na uchaguzi mkuu nchini.
Uchaguzi Mkuu ni takwa la kikatiba, Chadema, CCM au Chama chochote kinashiriki uchaguzi Mkuu kwa hiyari yake, hakuna chama chenye uwezo wa kusema hakuna uchaguzi Mkuu!, hivyo Chadema hakina uwezo wa kusema bila katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, hakuna uchaguzi Mkuu, kitu wanachoweza kusema ni bila uwepo wa katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, Chadema haitashiriki uchaguzi. Chadema haiwezi kutoa ultimatum ya kufanyika au kutofanyika uchaguzi, kwenye uchaguzi, who is Chadema?, it's just a party and it's nothing!. Hata CCM ambao ni chama tawala, kwenye uchaguzi Mkuu, CCM is just a party, tofauti ya CCM na Chadema ni CCM is something wakati Chadema is nothing!. CCM sio chama tuu, CCM ni chama dola wakati Chadema ni chama tuu!.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara mjini Musoma leo Jumapili, Januari 22, 2023, Naibu katibu mkuu wa Chadema bara, Benson Kigaila amesema msimamo huo tayari ulishatolewa na chama chake pamoja na magumu waliyopitia katika kipindi cha miaka saba iliyopita msimamo huo haujabadilika.
Baada ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kufanya maridhiano na CCM, kabla ya Chadema kukurupuka na mikutano ya hadhara, walipaswa kwanza wafanye semina ya ndani kwa viongozi wake kuwaelimisha kuhusu maridhiano hayo, na Chadema kutoa taarifa rasmi sasa wanautambua uchaguzi Mkuu, wanamtambua Rais Samia, wanalitambua Bunge la JMT, na hivyo kulegeza ile misimamo yake ya awali enzi zile wamesusa na wamenuna, sasa ni wamefurahi na wanacheka.
"Moto haufichwi kwenye shuka pamoja na kifungo cha miaka saba lakini leo mmekuja hapa mkidai na kuitaka katiba mpya hivyo ni lazima ipatikane kwani bado hamjachoka na hamtochoka kuidai," amesema.
Chadema inapaswa iwafunge midomo baadhi ya vilomolomo wake!, haiwezekani Mwenyekiti Mbowe aende kupiga magoti kwa Mama kuomba maridhiano, yamepatikana, halafu kuna mburumatata anakuja na kauli kama hizi!.

P
 
The same story from the same person !!! Upuuzi wa chadema,Kwani wakisusa uchaguzi kuna tatizo gani,cuf wapo watashiriki!!
 
Katiba pendekezwa ya Warioba ilichakachuliwa. Ni mbovu.
Hakuna kitu kinachoitwa "katiba pendekezwa ya Warioba". Kazi ya tume jaji Warioba iliisshia kwenye kutengeneza rasimu tu. Kwahiyo kuna "rasimu ya katiba ya jaji Warioba".

Baada ya hapo rasimu ilipelekwa kwenye Bunge Maalum la Katiba (BMK). Huko ndiko ikapatikana "Katiba Pendekezwa" na hii ndiyo haitakiwi kabisa maana imejaa mawazo ya kihafidhina ya ccm.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesisitiza bila katiba mpya na tume huru ya uchaguzi basi hakutakuwepo na uchaguzi mkuu nchini.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara mjini Musoma leo Jumapili, Januari 22, 2023, Naibu katibu mkuu wa Chadema bara, Benson Kigaila amesema msimamo huo tayari ulishatolewa na chama chake pamoja na magumu waliyopitia katika kipindi cha miaka saba iliyopita msimamo huo haujabadilika.

"Serikali ya CCM inapoendelea kuvuta miguu juu ya suala la katiba mpya sisi tunaendelea kupiga mstari pale pale tulipokwisha uchora ni kwamba bila katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, uchaguzi hautafanyika huo ndio msimamo wetu," amesema.

Amesema katiba mpya ni hataji la Watanzania hivyo hakuna sababu ya Serikali kupuuzia hitaji hilo badala yake inatakiwa kutekelezwa kwa maslahi ya Watanzania na nchi kwa ujumla.

"Moto haufichwi kwenye shuka pamoja na kifungo cha miaka saba lakini leo mmekuja hapa mkidai na kuitaka katiba mpya hivyo ni lazima ipatikane kwani bado hamjachoka na hamtochoka kuidai," amesema.

Naye katibu mkuu wa chama hicho, John Mnyika amesema endapo kungekuwa na katiba mpya inayodaiwa na wananchi basi leo wananchi wangekuwa na uwezo wa kuwawajibisha wabunge wengi ambao amedai wameingia bungeni kwa njia zisizokuwa halali.

"Katiba ya Jaji Warioba imetamka wazi wananchi wanataka wawe na uwezo wa kuwawajibisha wabunge wasiowajibika na kama hiyo katiba ingekuwa inatumika basi hadi sasa tungekuwa tumewawajibisha wale wabunge walioingia bungeni kimagumashi," amesema.

MWANANCHI
Mnyika aliwaambia watu wake wajiabdae na uchaguzi Sasa itakuaje?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom