CCM achaneni na Samia 2025, leteni mtu mwingine kabla ya uchaguzi afanye reform kwa hali iliyopo, chama kiingie kwenye uchaguzi kikiwa kimeaminika

Nigrastratatract nerve

JF-Expert Member
Sep 4, 2019
1,398
3,907
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa chama chochote cha siasa kikipuuza maoni ya wananchi kitalia kilio ambacho hatakuwepo wa kukinyamazisha

Ni dhahiri CCM imepoteza mwelekeo haijali kabisa changamoto wanazopitia wananchi

wamekuwa wakiwaza tu kuchapisha fomu moja wamesahau hata kutekeleza majukumu yao sawasawa

ukweli ni kwamba Samia hatoshi tena kugombea urais 2025 tena kikawaida angejiuzuru mapema kuruhusu mtu mwingine aje kufanya reform kabla ya 2025 maana CCM kikiingia hivi kwenye uchaguzi kitalia kilio kikubwa Sana
 
maana CCM kikiingia hivi kwenye uchaguzi kitalia kilio kikubwa Sana
Supposedly hoja zako ni kweli, kati ya vyama hivi vilivyopo, ni chama kipi cha kuiliza CCM na kuiletea hicho kilio kikubwa sana?.
P
 
🤣🤣🤣angejiuzulu?
Thubutuuu,kiti kitamu,hata kama unajijua huna uwezo,ila ikitokea unapewa kiti,ndo utajua utamu wake,hata huku maofisini tunaona,wasio na uwezo ndo wanapewa nafasi,na wakishakalia kiti,Cha Moto mtakiona,na atafanya lolote kuhakikisha anaendelea kukalia kiti🙏it's normal
 
Supposedly hoja zako ni kweli, kati ya vyama hivi vilivyopo, ni chama kipi cha kuiliza CCM na kuiletea hicho kilio kikubwa sana?.
P
Amesema CCM watafute mgombea mwingine angalau atakayejali maisha ya Watanzania. Wapo wenye unafuu Polepole, Bashiru Ali, Mpina, Lukuvi, Mtaka nk.

Upinzani yupo Mwakubusi, Dr Slaa, ila hawana platform. Wengine wote waonjoshe asali tu wanakuwa hawana tofauti na CCM.
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa chama chochote cha siasa kikipuuza maoni ya wananchi kitalia kilio ambacho hatakuwepo wa kukinyamazisha

Ni dhahiri CCM imepoteza mwelekeo haijali kabisa changamoto wanazopitia wananchi

wamekuwa wakiwaza tu kuchapisha fomu moja wamesahau hata kutekeleza majukumu yao sawasawa

ukweli ni kwamba Samia hatoshi tena kugombea urais 2025 tena kikawaida angejiuzuru mapema kuruhusu mtu mwingine aje kufanya reform kabla ya 2025 maana CCM kikiingia hivi kwenye uchaguzi kitalia kilio kikubwa Sana
Ushauri wako siyo mzuri. Ni ngumu sana kupata rais kama Dkt Magufuli, ndiyo Dkt Samia ni mzembe sana tena hafai kabisa kuendelea kukalia kiti cha urais kwa sababu kila eneo la kiutawala kashindwa mno mno, ila ukiangalia hakuna mbadala ndani ya CCM wa nje ya CCM. Yaani bora mara 💯 tuendelee na Dkt Samia ambaye tumeshajua siyo nyampara bali ni kiongozi anayetaka kila mtu ajisimamie, ila bahati mbaya sana watanzania karibia wote waliopo serikalini na wafanyabiashara wana vinasaba vya ufisadi, wizi, upigaji kiasi kwamba kwa kiongozi kama Dkt Samia wanafurahia mno. Kwa nini nasema hatutaki zaidi ya Dkt Samia, huyo unayemfikiria akija atataka kuwa kama Dkt Magufuli (atashindwa kuwa kwa sababu Dkt Magufuli alikuwa na kipaji hicho cha kuzaliwa) na atataka kuwa kama Dkt Samia (hawezi kwa sababu Dkt Samia kwa asili yake kama Mwanamke na kuwa ni Mzanzibar ndivyo alivyo lelewa), huo mchanganyiko utaiumiza nchi. Tuendelee na Dkt Samia
 
CCM sio chama cha kianaharakati, ni taasisi, inashinda kama chama. Mafanikio yote ni ya chama.

Hii ni tofauti na chadema ambayo inaendeshwa kiuanaharakati kama HAMAS au Muslim Brotherhood na Jamaa Al Islamiya
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa chama chochote cha siasa kikipuuza maoni ya wananchi kitalia kilio ambacho hatakuwepo wa kukinyamazisha

Ni dhahiri CCM imepoteza mwelekeo haijali kabisa changamoto wanazopitia wananchi

wamekuwa wakiwaza tu kuchapisha fomu moja wamesahau hata kutekeleza majukumu yao sawasawa

ukweli ni kwamba Samia hatoshi tena kugombea urais 2025 tena kikawaida angejiuzuru mapema kuruhusu mtu mwingine aje kufanya reform kabla ya 2025 maana CCM kikiingia hivi kwenye uchaguzi kitalia kilio kikubwa Sana
Sukuma gang kazi mnayo safari hii
 
Back
Top Bottom