Centre of Tanganyika-umefika hapa?

Lole Gwakisa

JF-Expert Member
Nov 5, 2008
4,728
2,259
IMG_0391.JPG
Kwa wale ma-Vasco Dagama wenzangu , najua hapa mnapajua vema, centre ya Tanganyika.
Kama unatoka hapo nipe salamu!
 
picha nzuri sana ila ukiieweka upside down yaani lami ionekane kwa juu ingekuwa nzuri zaidi!
Usipate tabu mchizi wangu,nyonga kichwa na shingo uitazame picha juu chini au geuza skrini ya kompyuta yako juu chini na uationa picha Kama roho inavyopenda!
 
hapa ni relini ukitokea singida kuingia mji wa manyoni barabara mpya.
wagogo waliungua hapo mwaka juzi wakichota mafuta kwenye lori lililogongwa na treni.
 
hapo ni mji wa manyoni, but ili kufika kwenye centre kabisa ya Tanganyika ni mbele kidogo kama unaelekea Dodoma, karibu na pale unaposhuka bonde la ufa, kuna alama pembeni upande wa kulia kuna chuma kiko mlimani mfano wa Nondo hapo ndipo centre penyewe. Ahsante kwa picha
 
Asante sana mkuu.
Tupo pamoja, ni kweli kabisa sehemu hiyo karibu na Chikuyu unapopanda mlima/ridge ya Saranda, ipo juu ya jiwe lililo kilimani kwa upande wa kushoto.
Nakushukuru kwa umakini.
Hata hivyo picha hii inaonyesha bango jipya badala ya bango lilowekwa na wakoloni karibu sOana na hapo , likionyesha umbali wa miji tofauti toka hapo.
Miji mingi mikubwa ina umbali wa wastani wa km 500 toka hapo mahala.
 
Back
Top Bottom