Kuelekea kusomesha Historia ya Uhuru wa Tanganyika bila Khiyana

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,920
30,263
KUELEKEA KUADHIMISHA UHURU WA TANGANYIKA SEHEMU YA PILI: KUSOMESHA HISTORIA BILA KHIYANA

Nina wajibu wa kusomesha historia ya uhuru wa Tanganyika kwani wengi hawaifahamu.

Nimekuwa nikisomesha wanafunzi wengi wala idadi yake siijui.

Naweka hapa chini muongozo ninaotumia unaojulikana kama "Biographical Approach," kufundisha.

Yeyote mwenye maswali na aulize:

"Napoanza kusomesha historia ya uhuru wa Tanganyika naanza na hawa watu wawili: Dr. Kwegyr Aggrey na Kleist Sykes mwaka wa 1924 walipokutana Dar es Salaam na Dr. Aggrey akamshauri Kleist kuunda African Association.

Kleist aliunda African Association 1929 na 1933 akaunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika).

Hapo huwafungulia wanafunzi wangu Dictionary of African Biography (2011)nikawaambia wasome historia ya Dr. Aggrey wamfahamu ni nani na nini mchango wake katika historia ya Afrika.

Kisha nawaambia wamsone Kleist Sykes katiki hiyo Dictionary of African Biography wajue nini mchango wake katika siasa za Tanganyika.

Hapa wanafunzi wangu wanakutana na historia ya Kleist Sykes na wanae ambao wote walikuja kuwa viongozi katika TAA mwaka wa 1950.

Nikifika hapa nawapa kitabu kingine cha kusoma: "Modern Tanzanians," (1973) kitabu kilichohaririwa na John Iliffe wasome historia ya Kleist Sykes: "The Townsman Kleist Sykes," mwandishi Aisha Daisy Sykes.

Nini kinapatikana hapa?

Mwanafunzi wangu hapa namuelekeza asome barua ya Mzee bin Sudi President wa African Association aliyomwandikia Secretary wa African Association Kleist Sykes mwaka wa 1933.

Barua hii imeanza na "Bismillah Rahman Rahim."

Mzee bin Sudi (1896 - 1972) anamkumbusha Kleist Sykes (1894 - 1949) kuwa wameunda African Association kwa nia ya kuikomboa Tanganyika.

Kinachopatikana ni historia ya Sykes baba na Sykes watoto katika uhuru wa Tanganyika.

Hawa hawakuwa viongozi tu bali walikuwa wafadhili wa harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.

Baada ya hapa ndipo nawaingiza katika KAR Burma Infantry 6th Batallion Kalieni Camp nje kidogo ya Bombay wakisubiri kurejeshwa makwao.

Vita vimekwisha hapa mkesha wa Xmas 24th December 1945 Abdul Sykes akawakumbusha askari wenzake kutoka Afrika ya Mashariki na kwengineko kuwa wakifika makwao waanze harakati za kudai uhuru wa nchi zao.

Hii ndiyo siku Abdul Sykes alipozungumza kuunda TANU na haya ameyaandika katika shajara (diary) yake.

Nawapa wanafunzi wangu kitabu cha kusoma: "The Making of Tanganyika," (1965) mwandishi Judith Listowel."

Tusimame hapa kwa sasa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom