Besta Mlagila
Senior Member
- May 29, 2018
- 101
- 191
Ikiwa ni siku moja imepita tangu kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi wa kitaifa wa CHADEMA na viongozi hao kupatikana, aliyekuwa mgombea wa nafasi ya mwenyekiti na kushindwa Mhe. Cecil Mwambe amesema kuwa, ameshindwa kwenye uchaguzi huo kwa kuwa 'uwanja haukuwa sawa'.
Amesema "Mhe. Mwenyekiti (Freeman Mbowe) aliongoza vikao mfululizo kwa nafasi yake(Mwenyekiti), na muda wote vikao hivyo vilikuwa ni sehemu ya kampeni, kuongea na wanachama kwa nyakati tofauti, halafu mimi nikapewa dakika 5 niombe kura na maswali matatu, jumla dakika 8"