CCM yawatosa Watuhumiwa bila Ushahidi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yawatosa Watuhumiwa bila Ushahidi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 11, 2007.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 11, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Wakati serikali ya CCM ikidai kuwa watuhumiwa wasichukuliwe hatua yoyote au kuhukumiwa kwa namna yoyote hadi vyombo vya sheria vitimize kazi yake, habari zinazoingia KLH News ni kuwa Kamati Kuu imeamua kuwatosa waliokuwa wa Bunge wa Mkoani Arusha ambao walikuwa wanakabiliwa na TUHUMA ZA RUSHWA. Chama hicho tawala, hakikutaka kusubiri maamuzi ya mahakama au kuacha mchakato wa sheria ufuate mkondo wake na badala yake imeamua kuwa mtoa taarifa, hakimu, polisi, na Mnyongaji!!

  Taarifa zaidi baadaye....
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2007
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Hii mpya na kali. ukiona kukurupuka usingizini ndiko huku, enewei tuone kitakachojiri....
   
 3. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2007
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  hayooooooo...

  yanawatokea puani na double standard zao!
  Mbona wasisubiri mahakama na vyombo vya sheria vifanye kazi?
   
 4. M

  Mtu JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2007
  Joined: Feb 10, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Aisee inamana wale akina Elisa Mollel? wametoswa vipi mkuu?
   
 5. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  haya tunasubiri hizo nyuzi nyingine, itakuwa kama ile ya mara ya kwanza !
   
 6. m

  mTz JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2007
  Joined: Aug 20, 2006
  Messages: 283
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Those are sacrificial lambs hoping that will appease the masses that something is being done on the whole "ufisadi". Now let us wait for the reaction from the very masses.
   
 7. YournameisMINE

  YournameisMINE JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2007
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 2,451
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 145
  Hivi si juzi tu 'muungwana mwendo mdundo' kaleta stori kule Arusha?? sasa hii ni nini tena....anataka kumkoroga nani?
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Oct 11, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Chetu ni chao na chao ni chao.. Kwenye "Shamba la Wanyama" kuna sheria zinazohusu wanyama wote, lakini kuna sheria nyingine haziwahusu wote kwani kuna wanyama wengine ambao wana haki zaidi kuliko wengine.

  Kada.. ndiyo habari za hivi sasa... kama watageuza kibano hilo jingine.. ila ndiyo hivyo tena..
   
 9. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2007
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mzee wa kijiji, hapa sijakupata vema, kwamba wamefukuzwa uanachama? ama wamesimamishwa ubunge? fafanua kidogo mkuu.. ama habari bado ziko jikoni sana?

  Na kikao kipi kime fanya maamzi hayo mbona ile k/kuu ilisema wataendelea na ubunge hizo ni tuhuma tu?
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Oct 11, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Rwabugiri tangia jana kuna kikao cha Kamati Kuu ambacho kilikuwa kinaandaa mkutano wa Halmashauri Kuu ambao utaangalia mipango ya Mkutano Mkuu. Sasa habari ni kuwa kikao cha Kamati Kuu kimeamua kuwavua Uanachama and hence wanapoteza Ubunge mara moja, kwani Kamati Kuu haiwezi kuwavua Ubunge!
   
 11. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2007
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Mbona hilo lipo wazi? nashangaa MKJJ kulishikia bango...!
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Oct 11, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Lipi lipo wazi?
   
 13. a

  alles JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2007
  Joined: Oct 14, 2006
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanajaribu kufukia mashimo ya Buzwagi na BOT.Wamesahau kwamba "la kuvunda halina ubani, hata wakiendelea kupaka manemane litaendelea kunuka tu".
   
 14. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #14
  Oct 12, 2007
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Asante Mkijiji,

  Hapo kazi imeanza vyama mbadala inabidi vifanye kweli... taratiiibu kuja kufika 2010 mambo hayatakuwa haba!. na haya majimbo kuyachukua ni rahisi sana, kwani hao wabunge wana support kubwa ya watu wao nao wanadai wameonewa!! kwahiyo ni rahisi kusaidia upande wa pili.. na hasira ya wale wanao ungana nao kwamba wameonewa inaweza malizikia kwa kuwapa mbadala...

  oh.. lovely!
   
 15. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #15
  Oct 12, 2007
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  SISIEMU lazima washikiwe Bango wasilete zao.

  Hata Fisi kwa Uroho wake wa nyama hali Nyama ya Fisi mwenzie ni kweli aweza mkata gino la tako lakini si kula nyama yake.

  SISIEMU wameanza kulana wenyewe bila kufuata Utaratibi Kanuni na Sheria.

  Jamaa wakishinda Kesi waipeleke SISIEMU Mahakamani kupinga kufukuzwa.
   
 16. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #16
  Oct 12, 2007
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Umesikiliza maneno ya Muungwana... au hupendi tu?
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Oct 12, 2007
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,681
  Likes Received: 82,533
  Trophy Points: 280
  Kwa speed hii itakuwa vizuri kama Muungwana akiwatosa Karamagi, Meghji, Balali, Msolla, Magufuli, Mramba na wengineo wote ambao hawana credibility machoni mwa Watanzania ili kusafisha awamu yake. Vinginevyo itakuwa yale yale ya usanii. Kwa wengine sheria inatumika kwa speed kali sana wakati huo huo kwa wana mtandao na washkaji hawaguswi na wanaendelea kupeta.
   
 18. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #18
  Oct 12, 2007
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  Nadhani kama sisiemu wamechukua hatua hiyo, sio haki kwa watuhumiwa, kwa sababu kesi yao bado iko mahakamani, wangesubiri. Na iwapo uchaguzi wa majimbo ya hawa wabunge utafanyika, huenda kura nyingi zikaenda kwa wapinzani, maana Tanzania ya 2007 haitabiriki.
   
 19. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #19
  Oct 12, 2007
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Ukiwa mnafiki na fisadi hata siku moja huwezi kubadilika. Kila siku tulikuwa tunasema gavana wa benki kuu asimamishwe ili uchunguzi ufanyike walisema ni majungu lakini leo kwa sababu wengine ni binadamu zaidi ya Watanzania wengine hiyo ni sawa kuwasimamisha bila ushahidi.

  Tunataka watu ambao wamefanya makosa ya uhujumu wa uchumi kama Karamavi na timu yote iliyohusika na mkataba wa Buzwagi wafukuzwe mara moja na uchunguzi zaidi ufanyike kwenye makampuni yote ya madini na mikataba yote ambayo haina faida ifutwe. MBONA JK ANAONA KIGUGUMIZI KWA HILI?
   
 20. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #20
  Oct 12, 2007
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  nadhani hii ameitoa huko arusha na akaamua kuwa hao wabunge watoswe as mfano ingawa sie wananchi tunaona baaaado kweli kweli. Kama akimtosha white head na RA pamoja na vicheche wengine walah tutaona angalau atapata kura moja in 2010.

  ...haya maneno nakumbuka nilishawahi kuyasikia akisema siku fulani mwanzoni mwa utawala wake, tena akasema anawajua kwa majina halafu kikapita kimya mpaka sasa....


  ....Naye anawalaumu kina slaa kistaili. Akumbuke kuwa hiyo ndiyo impact ya kuishtaki serikali kwa wananchi, walidhani ni mchezo, angalau wangekubali kuundwa kwa tume bungeni lakini kwa kuwa hawajui majira ya vuli na masika basi wanaambulia fedheha.... Sisi wananchi tunaamua ktk sanduku la kura.

  Tena hapo juu naona muungwana amekwenda mbali kidogo maana akina slaa hawajatoa hukumu bali wameshtaki kwa wananchi ambapo nasi hatujatoa hukumu mpaka siku ya uchaguzi ifike. Na je alitegemea kuwa watoa tuhuma wasifanye upelelezi?? Naamini kuwa wanapaswa wajiridhishe kuwa taarifa wanazotoa kwa umma ni sahihi na usahihi huu lazima waangalie rangi halisi ya carpert baada ya kulifunua.
  Namshauri muungwana awatimue washauri wake maana wamekosea kumshauri ktk hili.
   
Loading...