Elections 2010 CCM yatoa tamko kuhusu kitendo cha wabunge wa CHADEMA

chama cha mapinduzi, ccm, kinaandaa tamko na mkakati rasmi kuhusiana na kitendo cha wabunge wa chama cha demokrasia na maendeleo, chadema, kuondoka katika ukumbi wa bunge hapo jana wakati rais alipokuwa akilifungua bunge hilo rasmi kwa ajili ya vikao vya awamu ya 2010 - 2015.

Katibu wa itikadi na uenezi wa ccm, kapteni mstaafu john chiligati amekutana na waandishi wa habari leo huko dodoma na kusema ccm inapindana na hatua ya wabunge wa chadema kuondoka bungeni.

Amesema kwamba chama chake kitapeleka tamko rami bungeni ili ikiwezekana kwa mujibu wa sheria, kanuni na taraibu za bunge, basi wabunge wa chadema waondoshwe katika ushiriki wa shughuli na vikao vyote vya bunge hadi hapo watakapotambua kuwa aliyechaguliwa kwa asilimia nyingi zaidi katika uchaguzi uliopita ni jakaya mrisho kikwete na ndiye rais halali wa jamhuri ya muungano wa tanzania.

hapo ndio pazuri chadema ilipopataka tuingie katika mgogoro wa kikatiba, ili kila upande utoe madukuduku yake. Kwa wale wote waliokuwa wakionyesha wasi wasi na hatua hii ya chadema mnaona we nyewe jinsi ilivyowagusa? Mpaka wantaka kukaa na vyama walivyowaulia wanachama wao 2001. Big up chadema!!!!!!!!!!!!!!!
 
wanaanda ili walipeleke bungeni, kuwashitaki chadema ili wafukuzwe wasiingie bungeni na pia waondolewe kuwa kambi ya upinzani (As if its possible, Watu bana, very very confusing)
 
haya yalitarajiwa na nina imani kabisa kwamba chadema watanyang'anywa hadhi ya kuongoza upinzani bungeni.

Kwanza hali itakuwa mbaya sana kwa chadema bunge litakapoanza kujadili hotuba ya jk.
Watajikuta katika wakati mgumu wa kuwepo bungeni wakati wa majadiliano ya hotuba waliyoisusia.

Wakisusa kuwepo wakati wa mjadala huo ni sawa na kujipalia makaa zaidi.

Tulishauri tukapuuzwa. 'negative implications' tulizokuwa tunazitolea angalizo ndio hizi sasa.
naomba kifungu cha kanuni za kudumu za bunge kitakachotumika kufanya hivyo, ustuletee ukihiyo wa kiccm hapa? Hata chiligati amesema kuwa wataomba chadema wamatambue raisi kwanza hayo wewe umeyatoa wapi?. nakupatia kanuni za kudumu za bunge letu ili ufute ukihiyo wako.

massage tayari imeshakuwa sent, by february 2011 wakati hotuba inajadiliwa hata wabunge wa ccm watakuwa hawapo makini kwa hotuba hiyo ila kujijenga kwa mawaziri wapya new emerging administration (urais 2015) .

Utaona hotuba hiyo itakuwa haina wachangiaji wengi.
 
Jamani patamu panakaribia Chadema hit the target kumbe imewauma walipokuwa wanazomea walidhani Chadema wanatania wamelala usiku walipoamuka ndipo wameanza kuyasikia maumivu na bado. CCM ilizoea vyama vya hewala baba sasa wamekutana na chama kilicho serious.
 
watu pipoooozzzz....pawaaaaaaaa.... MKUKI KWA CHADEMA MTAMU KWA CCM MCHUNGUUU...waende mahakamani... bungeni kuna sheria zake...mwaka huu mpaka 2015 watatujua sie nani au manyani...

TUKIWAAMBIE KATIBA MBOVU HAWATUELEWI...bungeni tunajadiliana sio kufungiana..na wakitufungia TURUDIE UCHAGUZI afterall about 60% ya wananchi hawakupiga kura nahisi watahitaji kupiga kura na kuwakilishwa bungeni na rais pia wampendaye....

HAPO NDIPO PATAMU NA NI PALEEE PALIPOINGIA SHUBIRI ILHALI ASALI BADO YAPENDWA NA WENGI
 
Bad move kwa ccm,good move kwa chadema na wapambanaji.
Kwanza Chadema hawajakurupuka,wanazijua sheria na wanjua nin wafanyacho.
Pili kama ccm na vibaraka wo watalazimisha ikawa hivyo basi ndo mwanzo wa machafuko maana ndo itakuwa maandamano nchi nzima kupinga uchakachuaji wa kura na hatua hiyo ya bunge.Kitakachofuata ni polisi kutumia nguvu na kusababisha umwagikaji damu au usuluhishi ambapo moja kwa moja matakwa ya Chadema kwa niaba ya wananchi ni kura za urais zihesabiwe upya kwa mujibu wa matokeo ya majimboni,jambo ambalo litapingwa vikali,alternative itakuwa ni katiba ibadilishwe.
 
Chama Cha Mapinduzi, CCM, kinaandaa tamko na mkakati rasmi kuhusiana na kitendo cha Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, kuondoka katika ukumbi wa Bunge hapo jana wakati Rais alipokuwa akilifungua bunge hilo rasmi kwa ajili ya vikao vya awamu ya 2010 - 2015.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Kapteni mstaafu John Chiligati amekutana na waandishi wa Habari leo huko Dodoma na kusema CCM inapindana na hatua ya Wabunge wa CHADEMA kuondoka Bungeni.

Amesema kwamba chama chake kitapeleka tamko rami Bungeni ili ikiwezekana kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taraibu za Bunge, basi Wabunge wa CHADEMA waondoshwe katika ushiriki wa shughuli na vikao vyote vya Bunge hadi hapo watakapotambua kuwa aliyechaguliwa kwa asilimia nyingi zaidi katika uchaguzi uliopita ni Jakaya Mrisho Kikwete na ndiye Rais halali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Chiligati is nut!!!!!!!
 
HATA AFRIKA MASHARIKI WAPINZANI KUTOKA NJE NI KAMA KAZI TUU!!


Uganda Government News: Opposition walk outs criticized

Ultimate Media
First published: 2009/09/25 1:36:01 PM EST

The Members of opposition in Parliament have been criticized for absconding from Parliamentary work through walking out after disagreements with their fellow MPs from ruling National Resistance Movement party members.

The opposition MPs walked out of Parliament yet again this week, protesting against sections of the budget that was being passed.

The MPs in particular protested against the allocation of 6.5 billion shillings to the president's office for promoting patriotism and an additional 10 million shillings for the presidential Banana Initiative.

However, the government Chief Whip, Daudi Migereko says that such behavior of opposition MPs is uncalled for as it is not provided for in the rules of procedure.

Migereko says storming out of Parliament is not an acceptable way of conducting business, adding that there are known procedures for dissenting from positions presented on the floor of Parliament.

Source:Uganda Government News: Opposition walk outs criticized
 
This is country ndio maana aliendelea kkuhutubia nbila mtikisiko,move yote ilikuwa wazi kabla, alikuwa anajua before kufika pale
 
jamani hakuna mwenye video atumwagie ktk youtube? Mi niliikosa hiyo move! Nahisi walkout nyingine nyingi zaja hasa sisi em wakilazimisha kupitisha upuuzi simply kwa kuwa wao na sisi em B wako wengi :lol:
 
CCM siku zote si ni chama cha matamko! Au mmekisahau? Muda si mrefu utasikia mara wazee wa Dar wanaandamana au UVCCM wameandaa maandamano. Uzuri wa haya mambo yote yanaingia ktk historia and the truth will always remain the truth.
 
Tamko linasaidia nini sasa!!! Kama ni goli ccm imeshafungwa mbele ya watazamaji wa kimataifa. Wakae watafakari tu namna watakavyoboresha tume ya uchaguzi ili iwe huru zaidi badala ya kupoteza muda kwa porojo zisizo za maana.
 
Chama Cha Mapinduzi, CCM, kinaandaa tamko na mkakati rasmi kuhusiana na kitendo cha Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, kuondoka katika ukumbi wa Bunge hapo jana wakati Rais alipokuwa akilifungua bunge hilo rasmi kwa ajili ya vikao vya awamu ya 2010 - 2015.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Kapteni mstaafu John Chiligati amekutana na waandishi wa Habari leo huko Dodoma na kusema CCM inapindana na hatua ya Wabunge wa CHADEMA kuondoka Bungeni.


Amesema kwamba chama chake kitapeleka tamko rami Bungeni ili ikiwezekana kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taraibu za Bunge, basi Wabunge wa CHADEMA waondoshwe katika ushiriki wa shughuli na vikao vyote vya Bunge hadi hapo watakapotambua kuwa aliyechaguliwa kwa asilimia nyingi zaidi katika uchaguzi uliopita ni Jakaya Mrisho Kikwete na ndiye Rais halali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Topic: CCM kutoa tamko kuhusu wabunge wa Chadema
 
Kwenye taarifa ya Habari ya TBC FM wamesema CCM kwa kushirikiana na vyama vingine vitaandaa azimio dhidi ya CHADEMA.
Hapa ni proof nyingine kuwa bungeni kuna kambi mbili, CHADEMA vs CCM & Co
 
Back
Top Bottom