Elections 2010 CCM yatoa tamko kuhusu kitendo cha wabunge wa CHADEMA

wao wanatoa TAMKO kama nani?

Sijaelewa hapa!


Mkuu safari hii nchi yetu itaona maajabu mengi sana. Naona sasa vyama vinaanza kufanya kazi ya spika, sijui kama vyama vina nafasi bungeni au wabunge kutoka vyama mbalimbali ndio wananafasi, tunaanza kuona vioja vya matokeo ya uchaguzi.
 
mtanukuu vingi tu. Mkuwa walokole wanaochukua verse moja na kuwa sera ya dini. To go out means there is no goverment to chadema. Wakienda bungeni ni kufuata posho tu. chadema wanaojua na kutokutaka aibu hiyo hakuwafuata posho namely Ndesa, zitto, shibuda, mdee, lucy etc.
 
Siku moja kabla Nilimwuliza Zitto, Mnyika na Dr. wa kweli kama kunamadhara ya kisheria wakiingia bungeni na wakati Mkwere akianza hotuba wato nje na niliuliza hivyo kwa sababu Mbowe alisema wange sikiliza hotuba hiyo Zitto akanijibu wanajadili.Kwa mantiki hiyo mambo yakisheria yalikuwa miongoni mwa mjadala wao. sasa wewe Chiligati unafahamu sheria zaidi ya Lissu, Marando na Dr. ? hata nyie mnayeshabikia tamko la chiligati hamjisitukii kama ni wazushi?
 
kilichofanyika jana ni kwa manufaa ya Chadema si wananchi walio watuma. Loud and clear
 
Kuchangia hotuba au Hoja yoyote BUNGENI ni maamuzi ya mtu, wa hulazimishwi, ndo maana bunge la TISA kuna watu hawajawahi kuchangia hata hoja moja, mfano ROSTAM AZIZI

Mkuu huyo jamaa sio kuchangia tu sidhani hata kama alikuwa na mahudhurio mazuri huko bungeni
 
Taarifa ya Tbc ya sa2 usiku mjumbe wa Nec,chiligati amesema Chadema wakiendelea ivo wabunge wa ccm wataagizwa kuwafukuza bungeni wabunge wa chadema. Pia kaongeza kusema kuwa wamevunja katiba,ila ajafafanua wamevunja katiba ya nchi gani maana mpaka sasa napekua katiba sijaona kipengele kilichovunjwa. Kwa iyo inapaswa kuwepo katiba mpya itakayokuwa na kipengele cha kuwabana wabunge kumheshimu rais wakati anahutubia bunge. Kuwepo kwa katiba mpya chadema itakuwa imepata dai lake la kwanza. Pili kapt.Chiligati amesema Rais ni sehemu ya Bunge kwa iyo chadema kutoka bungeni imekimbia ofisi yake ya kazi. Ila katiba ninayoijua mimi ya Jamhuri wa muungano wa tz inasema taasisi ya rais itakuwa mhimili mmoja na mihimili 2 ni Bunge na Mahakama. Hapa kuna kitu pia kinaitwa "seperation of power" na "checks and balance" je kweli chiligati ni mbumbumbu wa kuchanganua au ni udikteta au ni utukutu au hakuyaona madarasa ya shule. Great thinkers,bila kujali itikadi zetu za kisiasa,ebu tuelezane ukweli hapa maana sisi ni wasomi na weledi. Nawasilisha.
 
This is country ndio maana aliendelea kkuhutubia nbila mtikisiko,move yote ilikuwa wazi kabla, alikuwa anajua before kufika pale

Sina uhakika kama alikuwa anajua maana alikuwa anashangaa pia kama hakuelewa kilichokuwa kinatokea
 
Chiligati is another bogus in CCM, hana issue huyo. he is just rabish like Makamba and so many useless people inside CCM
 
Tusijidanganye. CCM know what they are talking about.
Itakuwa vigumu kwa wabunge wa Chadema kufanya kazi bungeni iwapo chama chao hakiitambui serikali inayotawala.
Cha ajabu ni kwamba walishaapa kuilinda katiba ambayo ndiyo iliyomweka Rais wasiyemtambua madarakani.
Motion inayopelekwa na CCM itapita na wabunge watafukuzwa bungeni. Take my word.

Mnaojiita wasomi, weledi, bla bla ... hamlioni hilo?

Liko wazi hata kwa sisi wa kawaida.
 
Chiligati is another bogus in CCM, hana issue huyo. he is just rabish like Makamba and so many useless people inside CCM

I totally I agree. Where does CCM party pick these kind of joke leaders? Hiki chama kisipojiangalia kitakufa kwakuwa hata viongozi wake ni wavivu hata kusoma na pia kusoma nyakati. Chadema hawawezi kufanya haya pasipokujua madhara. Dude lolote kufa huwa halifi ghaflani kwa stage. CCM ndio inakufa hivi. Tupo hapa wote na sisi ni mashuhuda
 
Hakuna la kushangaza kwa hili toka kwa Chiligati kwani ndo walewale vihiyo wa sheria. ila ukihiyo wao unachangiwa sana na kuchanganyikiwa na kunusa harufu ya kupoteza nafasi yao ya hatamu ya nchi..huyo anaweza kuitwa LAP SOKWE. ongeza pale kwenye lap dog, lap kenge list ni kubwa zingatia boguses wote wa CCM...:bump::bump::bump::bump::bump:
 
Huyu mzee naye anazeeka vibaya, hajui alitendalo, hakika saa ya ukombozi wa Tanganyika huru upo mikono mwetu, wajaribu kufanya wanachotaka kufanya ndipo watakapo jua wantanzania ni kina nani na wamebadilika kiasi gani, wakati umefika wa kutotishwa kwa kelele za mwenye nyumba, lazima wawe na heshima, kuna njia nyingi za kuwatoa madarakani.

Tumedhamilia na tupo serious na hili, CCM tumewachoka tunahitaji mabadiliko ya kweli kwa manufaa ya nchi yetu, kazi kudanganya wananchi ambao hawadanganyiki.
 
kishongo huna jipya rudi kwenu kalime shule yako ni ndogo hainaa manufaa kwa jamii go to hell
 
Mwanakijiji, hujakosea kabisa, walisema hivyohivyo, wataenda watarudi. Ukweli ni kwamba, CCM ktk mambo ambayo hawakuyategemea ni lile la wajumbe wa CDM kutoka hotuba ya JK. Walipigwa na Butwaa na hata JK mwenyewe. Lile somo la CDM ni somo ambalo watanzania wote jana wamejifunza na hata kudhubutu kufahamu kuwa, kumbe mtanzania ana uhuru wa kutokukubaliana na Rais, kitu ambacho wengi wao walikuwa hawakijui. Kama ni somo la Uraia (Civics) basi CDM wataingia ktk historia ya watanzania.

MY TAKE: CCM naomba wasome alama za nyakati.....ukweli ni kwamba ugumu na ubishi wao ktk kukubaliana na hali halisi, kutatuletea matatizo hapa nchini. Na ikiwa kama watafanya hayo ya kutaka Bunge liwasimamishe wabunge wa CDM, wafahamu kuwa, wanawanyanganya mamillioni ya watanzania haki yako ya kuwakilishwa Bungeni na wala si wale wabunge 56 wa CDM. Na hapo sasa, itabidi watanzania watafute njia muafaka nyingine ya kudai haki zao. Kama NEC ilichakachua kura, wasidhani inawezekana kuchakachua pia wabunge wa CDM pale mjengoni: Naona hali inavyozidi kwenda, waliowengi wanachoshwa na mambo haya ya ukandamizaji, chonde chonde, watu wakipoteza uvumilivu hapatakalika hapa. Na kwanini tufike huko?? Kwa ukweli, kila siku matamko ya hao waheshimiwa, yanaifanya hali ya siasa nchini kuwa tete...., Wenye masikio ya kusikia na wasikie kwani wasidhani watakuwa salama!

Ndugu, hapo ndipo haswa kwenye the heart of the matter!!
Huu ndio mwanzo wa kumwondolea Mtanzania wingu la ujinga na uoga ambao ccm haitaki utoke kwa majority ya watanzania. Hili wingu litatoka tuu! na muda wa kutoka ndio huu.
ccm wana option mbili:
1. wakubali tufanye mambo kwa ustaarabu wa karne ya 21, (katiba mpya yenye manufaa kwa watanzania wote), au
2. Wajifanye kama mugabe na kibaki .... matokeo wanayajua!!
 
Jamani atupe basi ni kifungu gani cha katiba na hasa ni kanuni gani ya bunge imevunjwa?
 
Tusijidanganye. CCM know what they are talking about.
Itakuwa vigumu kwa wabunge wa Chadema kufanya kazi bungeni iwapo chama chao hakiitambui serikali inayotawala.
Cha ajabu ni kwamba walishaapa kuilinda katiba ambayo ndiyo iliyomweka Rais wasiyemtambua madarakani.
Motion inayopelekwa na CCM itapita na wabunge watafukuzwa bungeni. Take my word.

Mnaojiita wasomi, weledi, bla bla ... hamlioni hilo?

Liko wazi hata kwa sisi wa kawaida.
Hivi wewe ulifaulu mtihani wa form two.
 
Back
Top Bottom