Jamani tuwekeeni hapa alichokisema Mbowe tuone propaganda za Chiligati.
Mbowe alisema Kikwete na kamati yake wanaficha mambo kuhusu EPA kwa kuwa kuna mambo yalihusika na kampuni yake. Alimtaka Kikwete ajisafishe kwa kuweka mambo yote hadharani. Pia alilaumu kwa Kikwete kuchunguza EPA pekee wakati kuna ufisadi mwingine mwingi uliofanyika BOT. Kikwete anajua kabisa kuwa sehemu ya fedha za Kagoda, Deep Green, Meremeta, Tangold nk zilikwenda kwenye kampeni zake. Ni Kikwete alijua ufisadi wa IPTL. Kikwete alijua ufisadi wa kwenye madini.
Mtakumbuka Rais Jakaya Kikwete amekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia Desemba 2005. Kabla ya kuwa Rais, Mheshimiwa Kikwete alikuwa Waziri wa Mambo Nje na Uhusiano wa Kimataifa kuanzia 1995 hadi 2005, Waziri wa Fedha 1994 hadi 1995 na Waziri wa Maji, Nishati na Madini kuanzia mwaka 1990 hadi 1994. Kama Waziri wa Maji, Nishati na Madini, Mheshimiwa Kikwete alishiriki moja kwa moja katika kusaini mikataba mibovu ya madini na makampuni ya madini ya kimataifa ambayo kwayo taifa limeendelea kupoteza utajiri mkubwa na kuinyima Serikali uwezo wa kifedha wa kuhudumia wananchi. Kwa mfano, mnamo tarehe 10 Aprili 1990, Major Jakaya Mrisho Kikwete aliingia mkataba wa madini ya kampuni ya SAMAX Limited ambapo kampuni hiyo ilipewa leseni ya kuchimba dhahabu katika eneo la Lusu, Wilayani Nzega Mkoa wa Tabora. Matokeo ya mkataba huo, maelfu wa wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu waliokuwa eneo hilo waliondolewa kwa nguvu na vikosi vya FFU na bila ya kulipwa fidia yoyote. Hadi leo wananchi hao hawajalipwa fidia yoyote licha ya miaka zaidi ya kumi ya kufuatilia haki zao. Baada ya kutwaa utajiri wa dhahabu wa eneo hilo, SAMAX Limited iliuza eneo hilo kwa kampuni ya Ashanti Goldfields ya Ghana kwa dola za Marekani milioni 253. Ashanti Goldfields nao wakauza eneo kwa kampuni ya Resolute Limited ya Australia kwa kiasi kisichojulikana cha fedha za kigeni. Resolute Limited ndio waliojenga na wanamiliki Mgodi wa Dhahabu wa Golden Pride ulioko eneo la Lusu, Nzega hadi sasa na ambao ulifunguliwa mwezi Novemba 1998.
Mnamo tarehe 5 Agosti 1994 Luteni Kanali Jakaya Mrisho Kikwete aliingia tena mkataba na kampuni ya madini Kahama Mining Corporation Ltd., kampuni tanzu ya kampuni ya Sutton Resources ya Canada. Ijapokuwa mkataba huu unaonyesha wazi kwamba ulikuwa unahusu eneo la Butobela Wilaya ya Geita Mkoani Mwanza, mwezi Agosti mwaka 1996 Kahama Mining Corporation wakisaidiwa na vikosi vya FFU walivamia eneo la Bulyanhulu, Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga na kuwaondosha kwa nguvu watu takriban laki nne waliokuwa wakiishi na kuchimba dhahabu katika eneo hilo. Baada ya kutwaa eneo hilo kwa nguvu za kijeshi, Sutton Resources iliiuza Kahama Mining Corporation na Bulyanhulu kwa Kampuni ya Dhahabu ya Barrick Gold Corporation ya Toronto, Canada kwa dola za Marekani milioni 280. Leo hii Bulyanhulu ni moja ya migodi tajiri kwa dhahabu katika Bara la Afrika.
JK anahusishwa na hili kwa mazingira yaliyopo na yeye amekaa kimya anapima uelewa wa watu wa Tanzania .Kauli za JK na kila mara Tume na mara wanaanz akurudisha pesa kimya kimya nk lazima tuhoji.Utetezi wake wa Lowasa kwamba ni mchapa kazi na yaliyo mpata ni ajali kazini .Ajali ipi ? Aseme .JK anauhusima kama anasema yeye ni msafi afanye kweli .Mbona akina Hosea na Mwanyika bado wanapeta ? Mbona mafisadi kibao kama Chenge kawarudisha kazini ?
Kuna mambo mengi ya kujioji ya kumweka au kumwondoa mtu mkubwa kwenye Kitanzi.
1.0 Urafiki wake na RA ulianzia wapi?
2.0 Ni kwa nini alimteuwa EL kuwa waziri mkuu licha ya wananchi kutokupendezwa naye tangu 1995? Lakini kwa nini hakujihoji ni nini kilichopelekea Mwl. kuhoji mipesa ya EL hasa baada ya kujilimbikizia mali muda mfupi baada ya kuingia pale AICC?
3.0 Mkataba wa madini Nzega Golden Pride uliyosainiwa na mkuu wakati ule kule Nzega ulifanikishwa na nani?
4.0 Je, watambua kuwa Igunga anakowakilisha RA ni karibu na machimbo ambayo Mh. white house alisign?
5.0 Je, watambua kuwa RA alikiri kuwatambua DOWSONS (jina-kampuni iliyoirithi Richmond) kwa kuwa wako sehemu moja/wanafanya kazi pamoja na kampuni yake CASPIAN?
6.0 Je, watambua kuwa wafanyakazi wawili wa CASPIAN ndiyo walihusika na kusajili Kagoda Agriculture wale wababe wa EPA?
7.0 Je, wajua kuwa kampuni ya CASPIAN ipo kwenye migodi ususani kwenye mgodi uliyosigniwa na Mh. Mkuu huko Nzega Golden Pride? Kama ulivyotajwa na Dr. Slaa kwenye orodha ya mafisadi.
8.0 Je, wajua kuwa inadaiwa fedha hizi ziliisaidia CCM kwenye Kampeni za uchaguzi wa 2005. Fedha za EPA na Zile zingine za Deep solution?
9.0 Je, wajua kuwa wadadisi wanadai fedha hizi wakati zinaingia kwenye Chama kuelekea kwa walengwa Mh. Katibu wa CCM enzi hizo hakujua na alikanusha kutokujua lolote?
10.0 Je, umeshawai kujiuliza kuwa kama Katibu wa Chama hakujua, je vipi Kuhusu Mweka hazina wa chama?
11.0 Je, watambua kuwa baada ya Kikosi kuingia madarakani RA aliteuliwa kuwa Mweka Hazina wa Chama na Ng Mkuu wa mkoa wetu miaka ile kupewa Ukatibu? (Huyu bwana siku mh. ameteuliwa Dom na chama chake alidaiwa kutoweka ktk Gari la mkuu huyu)
12.0 Je, umeshawai kujioji ni kwa nini Mweka hazina wa wakati ule ambaye angejua lolote juu ya mapesa ya Kampeni ni kwa nini alienguliwa wadhifa wake, na yuko wapi leo hii kutusaidia sisi watanzania kuhusu fedha za kampeni kuhusishwa na Kagoda na Deep?
13.0 Je, wajua kuwa imedaiwa kuwa ile kampuni hewa ya deep solution iliyochota mapesa mengi BOT ilisajiliwa na wanasheria wenye Kampuni ijulikanayo kama IMMMA?
14.0 Je, wajua kuwa waziri wa mambo ya Ndani mh. Lawrence Masha kijana toka Sengerema (Mtoto wa Dr. Masha yule wa UDP aliyekuwa akiibiwa kura na CCM kule sengelema. Dr. William Shija ndo alikuwa mbunge wa jimbo hili lakini mpinzani wa Mh. Bush wetu kwenye mchakato wa CCM)ni mmoja wa watu wanene pale IMMMA?
15.0 Je, wajua Masha alipelekwa sengelema mahususi kumwengua Dr. Shija na kupanua wigo wa mtandao? (This time Baba hakugombea lakini alipewa ulaji fulani japo sikumbuki lakini alisaidiwa na CCM, may be mbunge wa EA or else. Lakini cheki Cheo-bwana Mapesa na yule Bibie wa UDP aliyehoji mfuko wa Mama Mkapa bungeni Teddy Kasela Bantu walivyopewa ulaji. Cheo umsifia sana Kikweta for WHAT?)
16.0 Je, umejioji juu ya Masha kupewa wadhifa from no where na Kijana wa Mkuu kuwa mmoja wa staff wa IMMMA. Si mbaya lakini kwa nini IMMMA, mtoto, deep na waziri hapa hapa?
17.0 Je, watambua kuwa wakati wa BM mwanasheria aliyekuwa anakamata dau la selikali ni mzee wetu wa Musoma Vijijini ambaye aliingia bungeni na kupiku wadau wengine, je, kwa nini chombo kingine cha sheria Bungeni wakati wa term hii ya Bush yaani waziri? wote wamehusishwa na mapesa ya BOT.
Sasa CCM watuambiye huyo mtu msafi yuko wapi? Kura za watanzania hazina macho lakini haimaanishi ndiyo tulimweka msafi wakati alikuwa anafanya kazi kwenye jiko lenye masizi akiwa amevaa nguo nyeusi. Hatuoni masizi lakini nguo inanuka uvundo.
Ndugu Agao madai mazito haya .Yanaleta hisia nzito .Kwa kukusaidia tu ni kwamba ni Deep Green na si deep Solution.Asante sana kwa hoja zako .CCM wanacheza na watanzania
Jamani tuwekeeni hapa alichokisema Mbowe tuone propaganda za Chiligati.
Mbowe alisema Kikwete na kamati yake wanaficha mambo kuhusu EPA kwa kuwa kuna mambo yalihusika na kampuni yake. Alimtaka Kikwete ajisafishe kwa kuweka mambo yote hadharani. Pia alilaumu kwa Kikwete kuchunguza EPA pekee wakati kuna ufisadi mwingine mwingi uliofanyika BOT. Kikwete anajua kabisa kuwa sehemu ya fedha za Kagoda, Deep Green, Meremeta, Tangold nk zilikwenda kwenye kampeni zake. Ni Kikwete alijua ufisadi wa IPTL. Kikwete alijua ufisadi wa kwenye madini.
Mtakumbuka Rais Jakaya Kikwete amekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia Desemba 2005. Kabla ya kuwa Rais, Mheshimiwa Kikwete alikuwa Waziri wa Mambo Nje na Uhusiano wa Kimataifa kuanzia 1995 hadi 2005, Waziri wa Fedha 1994 hadi 1995 na Waziri wa Maji, Nishati na Madini kuanzia mwaka 1990 hadi 1994. Kama Waziri wa Maji, Nishati na Madini, Mheshimiwa Kikwete alishiriki moja kwa moja katika kusaini mikataba mibovu ya madini na makampuni ya madini ya kimataifa ambayo kwayo taifa limeendelea kupoteza utajiri mkubwa na kuinyima Serikali uwezo wa kifedha wa kuhudumia wananchi. Kwa mfano, mnamo tarehe 10 Aprili 1990, Major Jakaya Mrisho Kikwete aliingia mkataba wa madini ya kampuni ya SAMAX Limited ambapo kampuni hiyo ilipewa leseni ya kuchimba dhahabu katika eneo la Lusu, Wilayani Nzega Mkoa wa Tabora. Matokeo ya mkataba huo, maelfu wa wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu waliokuwa eneo hilo waliondolewa kwa nguvu na vikosi vya FFU na bila ya kulipwa fidia yoyote. Hadi leo wananchi hao hawajalipwa fidia yoyote licha ya miaka zaidi ya kumi ya kufuatilia haki zao. Baada ya kutwaa utajiri wa dhahabu wa eneo hilo, SAMAX Limited iliuza eneo hilo kwa kampuni ya Ashanti Goldfields ya Ghana kwa dola za Marekani milioni 253. Ashanti Goldfields nao wakauza eneo kwa kampuni ya Resolute Limited ya Australia kwa kiasi kisichojulikana cha fedha za kigeni. Resolute Limited ndio waliojenga na wanamiliki Mgodi wa Dhahabu wa Golden Pride ulioko eneo la Lusu, Nzega hadi sasa na ambao ulifunguliwa mwezi Novemba 1998.
Mnamo tarehe 5 Agosti 1994 Luteni Kanali Jakaya Mrisho Kikwete aliingia tena mkataba na kampuni ya madini Kahama Mining Corporation Ltd., kampuni tanzu ya kampuni ya Sutton Resources ya Canada. Ijapokuwa mkataba huu unaonyesha wazi kwamba ulikuwa unahusu eneo la Butobela Wilaya ya Geita Mkoani Mwanza, mwezi Agosti mwaka 1996 Kahama Mining Corporation wakisaidiwa na vikosi vya FFU walivamia eneo la Bulyanhulu, Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga na kuwaondosha kwa nguvu watu takriban laki nne waliokuwa wakiishi na kuchimba dhahabu katika eneo hilo. Baada ya kutwaa eneo hilo kwa nguvu za kijeshi, Sutton Resources iliiuza Kahama Mining Corporation na Bulyanhulu kwa Kampuni ya Dhahabu ya Barrick Gold Corporation ya Toronto, Canada kwa dola za Marekani milioni 280. Leo hii Bulyanhulu ni moja ya migodi tajiri kwa dhahabu katika Bara la Afrika.
14.0 Je, wajua kuwa waziri wa mambo ya Ndani mh. Lawrence Masha kijana toka Sengerema (Mtoto wa Dr. Masha yule wa UDP aliyekuwa akiibiwa kura na CCM kule sengelema. Dr. William Shija ndo alikuwa mbunge wa jimbo hili lakini mpinzani wa Mh. Bush wetu kwenye mchakato wa CCM)ni mmoja wa watu wanene pale IMMMA?
15.0 Je, wajua Masha alipelekwa sengelema mahususi kumwengua Dr. Shija na kupanua wigo wa mtandao?
(This time Baba hakugombea lakini alipewa ulaji fulani japo sikumbuki lakini alisaidiwa na CCM, may be mbunge wa EA or else.
Naona Bwana Ngurudoto ama Kaiza Twalipo ameamua "kumwaga radhi" kabisa, katuonesha hadi uchi wake wa ubongoni na tumeona kilichopo ni EMPTY SET!
Jakaya hatufahamu kama ni Fisadi au laa
VERY FAIR INDEED, LAKINI TUNAHISI.......Very fair!
Na anyefanya hisia zipate nguvu ni yeye mwenyewe.VERY FAIR INDEED, LAKINI TUNAHISI.......
EXACTLY! THAT WHAT I WANTED TO POINT OUT.Na anyefanya hisia zipate nguvu ni yeye mwenyewe.