BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,831
- 287,782
CCM yasikitishwa Rais Jakaya kuhusishwa na ufisadi
Mwandishi Wetu
Daily News; Wednesday,March 12, 2008 @00:03
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesikitishwa na kauli ya kumtuhumu Rais Jakaya Kikwete kuhusika na ufisadi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu (BoT) na kuvitaka vyama vya siasa kuacha kutumia kashfa hiyo kwa malengo ya siasa.
Taarifa yake iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi ya CCM, John Chiligati, ilisema kauli hiyo ya Mbowe aliyoitoa kwenye kongamano la akinamama wa Chadema ina lengo la kumchafua Rais Kikwete na kuwataka Watanzania kupuuza na kuzikataa njama hizo.
CCM tunayo kila sababu kuamini kashfa ya EPA imeanza kutumiwa kwa malengo ya siasa ya kudhoofisha kazi nzuri inayofanywa na Rais Kikwete katika kushughulikia ufisadi na mafisadi kumdhoofisha aonekane hajafanya jambo lolote la maana, njama hizi siyo za kiungwana ni mchezo mchafu, alisema Chiligati katika taarifa yake.
Alisema Rais Kikwete anastahili pongezi na si lawama, kwani yeye ndiye aliyeamuru EPA ikaguliwe na wakaguzi wa nje. Aliunda kamati kuchunguza ufisadi huo, kuchukuliwa hatua za sheria na fedha kurejeshwa na baada ya tume ya uchunguzi kukamilisha kazi, Rais Kikwete atawachukulia hatua waliohusika, alisema.
lakini kabla Tume haijawasilisha taarifa ya uchunguzi, Rais anaanza kubebeshwa lawama na shutuma nzito, kwamba anawalinda watuhumiwa na anashindwa kuwachukulia hatua za kuwapeleka mahakamani.
Lawama hizi siyo sahihi, siyo wakati wake na zina lengo la kutimiza malengo ya siasa ya kulipaka matope jina la Rais machoni mwa umma. Hali hii haiwezi kukubalika machoni mwa jamii ya waungwana kama Watanzania tulivyo.
CCM ingependa tujenge utamaduni wa kukosoana kwa lugha ya staha na uungwana, siyo lugha ya dharau, kejeli na ya kuudhi, kwa mfano kusema rais anafanya uhuni siyo lugha ya kistaarabu, alisema.
Chama hicho kimewataka Watanzania wawe macho na siasa za kuchafuana majina na wazikatae, ikiwamo kuwabeza na kuwapuuza viongozi wanaoendesha siasa hizo chafu. Hata hivyo, chama hicho kiliwataka Watanzania kuwa na subira hadi uchunguzi wa EPA ukamilike na Rais atakapochukua hatua za kisheria.
Kampuni ya Ernst & Young ilibaini upotevu wa Sh bilioni 133 kutoka akaunti ya EPA, hali ambayo ilisababisha Rais Kikwete kumfukuza kazi Gavana Dk. Daudi Ballali na nafasi yake kujazwa na Profesa Beno Ndulu.
Pia aliunda tume kuchunguza makampuni 22 yaliyohusika na ufisadi huo na kutakiwa kukamilisha kazi ndani ya miezi sita, ikiwamo kuwachukulia hatua wote waliohusika na ufisadi huo.
Hadi sasa tume hiyo imeshafanikisha kurejeshwa kwa Sh bilioni 50 kutoka kwa waliohusika na ufisadi huo pamoja na kutambua mali zilizonunuliwa na fedha hizo za EPA. Tume hiyo leo itazungumza na wahariri Dar es Salaam kufafanua kazi yake hadi sasa.