CCM yapasuka? Kinana ang'atuka...

Siku zote kazi ya ofisi ya mtu kama Nape katika chama ni kule KUTIA MAFUTA PALE PANAPOONEKA KUELEKEA KUPAUKA kimaslahi katika taasisi inayompa kula.

Hivyo, mpaka hapo ukweli tumeshaupata kamili humu na kile anachokifanya Nape hapa nacho tumeshakielewa vizuri sana tu.

Hakika ni hizi funika funika za CCM ndizo zilizotufikisha hapa tulipo kama taifa na ht kupamba kisichopambika.

Kesho tu utasikia wamemlazimisha mzee wa watu kwenda Press Conference kukiokolea sura CCM. Karibu Nape, mhadhara huu ni wako tngu sasa endelea kutiririka upendavyo.
 
Niliwahi kuwashauri CCM kuharisha uchaguzi huu wa chama unaotalajiwa kufanyika ili kupisha hatua za kumaliza migogoro ndani ya chama, hawakunisikiliza. Sasa dalili za migogoro hii kukitafuna chama zinaanza kuonekana waziwazi.


Source>>> https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/182285-ushauri-uchaguzi-wa-ccm-2012-usogezwe-mbele.html
 
Hawezi ku multi task? nina uhakika sasa hivi ni mawasiliano ya hali ya juu yanaendelea ndani ya hao magamba, na vikao ili kujaribu kuona kama wanaweza kuliokoa jahazi.Kuna watakaoombwa na kupigiwa magoti,kuna watakaotishwa nk.Ila mwishowe watakuwa na majibu tu na ukweli utafahamika.Hapa ni popcorns tu kwa mwendo wa mbele.

Binafsi ninaamini Nape ndiyo mzushi,na huko alipo anajaribu kufanya "damage control".Usikute usawa huu amemvutia waya JK wanajadili,na kama hicho kipengele cha ufamilia kipo,usishangae hiyo barua ikafanyiwa mizengwe.Hapa wanaliana timing tu.
 
Wanajamvi,
Nnauye jr amekuja hapa haraka kutokana na thread iliyosema ' Kinana ang'atuka.... kuachana na siasa uchwara'.
Alichokifanya Nape ni kukubali kuwa Kinana ameng'atuka na hapo tu amethibitisha kuwa ile thread ina element za ukweli kama si ukweli kamili.

Asichokubaliana nacho ni matumizi ya neno 'kuachana na siasa uchwara'. Amenukuu maneno ya Kinana bila kutueleza yametoka katika kikao, FB au katika barua.

Pasco ameuliza, je ni kweli barua imeandikwa au ni uzushi? Nape amekimbia hataki kujibu hilo wala wapi maneno ya Kinana yanapatikana. Hadi hapo unaweza kuona namna alivyojichanganya.

Kwanini Nape amekuja kwa kasi? Jibu ni kuwa vikao vya chama vinaendelea na habari hizi kuvuja JF zinaufikia umma kwa haraka sana. Kitakachotokea ni wale wenye hati hati ndani ya chama kujipanga kabla ya kumalizika vikao.
Ni kuzuia mkakati uonaonekana kuwa una sababu maalumu. Mtu kama Kinana hahitaji kutangaza, angekuwa na option ya kutochukua fomu basi hilo tu lingetosha kumuondoa katika nafasi.

Kitendo cha Kinana kusema hayo aliyoyasema kinaashiria ujio wa jambo zito. Anaweza kuwa amefanya hivyo kwa kukusudia baada ya kutathmini hali ya chama na mustakabali, au anaweza kuwa amefanya hivyo ili ku-set tone kwa maamuzi yanayoonekana kuwa mazito na yenye madhara 'repercussions'.

Kwahiyo msibabaike sana ujio wa Nape ni katika mkakati wa 'pre-emptive strategy' hasa baada ya JF-Leak.
Nisomeni vizuri, Jumatano na Alhamisi zitakuwa siku zenye habari nyingi za kisiasa, siku zitakazoonyesha hatima ya CCM na wale waliokubali kubeba jeneza na kibao cha R.I.P.

Nasema R.I.P kwasababu damage ya chama ni kubwa sana kiasi kwamba kinachohitajika ni injini mpya na si bodi.
Hilo halitatokea katika makundi yaliyopo na kuparaganyika ni jambo la kwanza hata kama litafunikwa na maneno 'tumeingia wamoja tumotoka wamoja'. Underneath there is a big rift for the part to stand tall as it used to be.
 
Nashukuru kwa kujitokeza haraka kuweka kumbukumbu sawa katika jukwaa hili.
Mh Mbunge wangu, mimi naona ni mapema mno kumshukuru Nape kwa hili, kumbu barua ya Kinana inatambuliwa zaidi kuliko haya maneno mawili ya Nape.

Mimi ningeshauri ajibu vema maswali ya bwana Pasco ndio ashukuruwe au ashutumiwe nasi.

Mwisho kumbuka Nape nimtaalamu wa propaganda chafu, anaweza kubisha/kukanusha chocho i;limradi tu umpe jukwaa.
 

kwa habari hii iliyo hapa mbele yetu, THIBITISHA kwamba ni uongo! Nape katuthibitishia ni ukweli, haya lete uthibitisho wako wa uongo
 
Kinana ni mwanasiasa mzoefu na makini. Miaka 25 ni mingi. Uamuzi wa kupumzika siasa ni wa busara na unafaa kuigwa. Nitamkumbuka kwa ushauri na nasaha zake kama mlezi wa Chama Mkoa wa DSM.

uzoefu wa siasa za kinafiki,fitina na uwongo,angekuwa mtu anayeona mbali angekwisha achana na siasa zaidi ya miaka 5!
 
Ni kuzuia mkakati uonaonekana kuwa una sababu maalumu. Mtu kama Kinana hahitaji kutangaza, angekuwa na option ya kutochukua fomu basi hilo tu lingetosha kumuondoa katika nafasi.
Hapo ndo kwenye mzizi wa fitina,there is no such a thing as "kujiuzulu kugombea",magamba bana.
 

teh teh..nacheza na JF?Jf ni serious business..hata mizaha humu ndani watu wanapewa tasks ngumu kwa hilo.Hapa pasco anaonekana kapata habari nzuri sana kwa mgombea wake.Utajuaje kuwa hii habari inahusiana na hii pic, ama ndio kaitwa kajibu haraka?
Ze komedi kama si machokoraa fulani baada ya abush ndio wanajipongeza kwa kukutana tena wakiwa hai,pengine na msala walioacha ndani hauwahusu.Bongo kuna wapiga picture wana imaginations.pengine wakuu wa kaya wameziona na kuwataka vijana na wazee (watoto) warudi ndani upesi na msala unawahusu.
 
Kinana ni mwanasiasa mzoefu na makini. Miaka 25 ni mingi. Uamuzi wa kupumzika siasa ni wa busara na unafaa kuigwa. Nitamkumbuka kwa ushauri na nasaha zake kama mlezi wa Chama Mkoa wa DSM.

Endelea kumkumbuka lakini njia nzuri ya kumuenzi ni kufuata yale anayoyaamini hasa hili la kuchoshwa na Siasa uchwara ndani ya CCM. Kuna kundi kubwa la wazee wamesayaona haya, wameamua kukaa pembeni. Sidhani kama kuna siasa safi ya kushabikiwa na vijana wa aina yako ndani ya CCM.
 
Kuhusu kujiudhuru sijui kungatuka kwa kinana bila kufata la nape wala la wanaosema siasa uchwara.
Hivi Kinana amejiuzulu ama kung'atuka kitu gani?Alikuwa ana madaraka gani ndani ya chama hadi usawa huu?Msaada tutani tafadhali.
 
Kuna dhoruba inaikumba ccm mda si mrefu sasa kinana hataki kuwa sehemu ya waathirika wa dhoruba hiyo.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Mungu ni wa ajabu sana, ana njia nyingi za kuwanusuru waja wake zidi ya madhalimu na udhalimu wao,ata binadamu walipofanya kiburi cha kujenga mnara wa babeli aliwavuruga kila mmoja akaongea lugha yake sasa ameamishia miujiza yake kwenye ukombozi wa watanzania.
 
Kwa statement hii ya Nape,good thing JF is on "another level",na siasa uchwara haziwezi kuiaffect!
Naona atakuwa anajaribu "kuthibitisha habari hizi na uongozi wa juu",kaazi kweli kweli!
 

As long ni mechi nzuri kuangalia .mimi nitaangalia kwa makini.CDM wakiohold any more time CCM itakufa kabla hawaajarushiwa konde na CDM.
 
Me naomba hiyo barua iwekwe hapa ndani najuwa watu wanayo.......
 
Hivi Kinana amejiuzulu ama kung'atuka kitu gani?Alikuwa ana madaraka gani ndani ya chama hadi usawa huu?Msaada tutani tafadhali.

Kavunja kamati ya kampeni rasmi.Pengine hajasema alivyokereka na kuomba kila sent kwa prince kwa kipindi chote cha kampeni.Halafu leo ndio najikuta akitakiwa jikomba NEC wakati teammates wake wakichuku nafasi NEC.
 
jmushi1 hawa CCM ndio wameamua kila kukicha kuongeza at least one enemy kutoka ktk list ya media.By the time wanafikia 2015,watakuwa ktk position ya CUF.

Sasa hivi they are up for something fishy with another media.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…