Hii ni ishara tosha kwamba JF kuna propaganda watu tunalishwa. Kwa kelele za hapa JF mimi niliamini kabisa CHADEMA wanashinda Busanda.
Ina maana taarifa nyingi tulizokuwa tunaletewa zilikuwa za uongo au za upande mmoja. Pale CHADEMA wanapofanya vizuri habari zake tulikuwa tunaletewa, kule wanakofanya vibaya habari zinafichwa. Hiyo ni propanda sawa tu na TV ya serikali au magazeti ya RA au vyombo vya habari vya Mengi.
Inabidi JF tuwe zaidi ya mambo tunayoyapinga.
Nimeshangaa mkuu Pasco ambaye mimi huwa namwamini kutokana na maandishi yake mbalimbali, ghafla kapotea si ajabu baada ya kuona CCM wanaanza kushinda.
Hapa JF hakuna wapiga kura, lazima tuhakikishe tunapeana habari za ukweli mtupu. Kuja kumwaga propaganda JF haitusaidii kabisa badala yake mnaishia kuumiza mioyo ya wapenzi wenu ambao wanajenga hope kumbe hakuna kitu.
Kama kilichokuwa kinaandikwa kilikuwa sahihi basi kuna mawili, either CCM wameiba kura au wale watu waliokuwa kwenye hiyo mikutano walikuwa mamluki kutoka sehemu nyingine na hawakuwa wapiga kura.
Kitila,So what is your point here bwana mkubwa? Kukua kwa chadema kunakukera au namna gani? Sijakupata kabisa unachojaribu kusema!
Dar hawajalala fofofo. Ni kuwa tangia muamko wa buzwagi hawajapata nafasi ya kuonyesha hasira zao....zinatokota ndani kwa ndani bao.
Vilevile hata katika uchaguzi wa 2005 vyama vya upinzani hawakuwa na wagombea wenye ushawishi wa kuweza kuaminiwa na wanjanja wa mjini. Ni mnyika pekee ndiye aiyekuwa na mvuto kwao.........
omarilyas
...bila ya Malecela huu uchaguzi wangebwagwa tena...nafikiri yule mzee ni asset kwa CCM.
Si uje wewe utoe habari vizuri unapenda kupewa tu. Dawa kama unaona kuna tatizo basi jitahidi ulitatue sio kuomba jirani akutatulie
Hakuna cha kufika hapo NCCR mwaka 1995 ilikuwa chachu kuliko leo 2010 CHADEMA. Huwezi kusema watu ndio wanaanza kuamka wakati 1995 tuliona wabunge wengi wa upinzani.Kusema hivyo nikujaribu kujidaganya tu.
Uwiano Maalum,Unajipunguzia heshima ndugu, kuwa objective na uache kujikomba. Hufanani na maneno uliyoandika hapo.
Ukweli ni kwamba CCM wamejimaarisha maeneo ya vijiji kuliko vyama vya upinzani. Hii ni changamoto kwa upinzani kujiandaa vyema kwa uchaguzi 2010 katika maeneo ya vijijini. Operesheni wanazozifanya bado haziwaamsha wananchi kiasi wawe na imani ya kunyakua viti vingi vya ubunge au hata urais katika miaka mwakani au hata 2015.
Uwiano Maalum,
kwa nilivyoona mimi, tofauti kati ya Tarime na Busanda ni Malecela.
Unaweza usikubaliane na mimi lakini ndio conclusion yangu. Sisemi niko sahihi maana haya mambo huwezi kujua kama uko sahihi au la, lakini naamini Malecela kaisaidia CCM ishinde.
Acha kunifuata fuata. Toa hoja zako badala ya kunifuata fuata mimi.
Mimi si natoa habari za Mbeya ambazo ndio zimekukoroga kichwa chako mpaka unaanza kunifuata fuata? Jibu hoja zangu na achana na kufuata mtu.
Safi sana, tupo moja Kamanda! 😀BTW, hongera CCM kwa ushindi mwingine...
Naona unaanza kutokuwa realistic, huwezi kutegemea CHADEMA kuwa na ofisi kila sehemu nchi hii ghafla kama unavyodhani. Hapo baadaye sawa, tatizo lililopo kwa sasa ni kila mmoja kudhani kuwa kazi ya kuikomboa hii nchi ipo mikononi mwa CHADEMA,nadhani si sahihi.
Hii ni nchi yetu sote, kuanza kuwalaumu wao kama chama ni kosa, tuipiganie sote. Watu fulani wanafanya kadri ya uwezo wao kujaribu kuleta mabadiliko, kuna kundi linafanya kila namna kupinga hayo mabadiliko na kutetea UFISADI na looting. Ni vita unayowapigania watu ambao hata wenyewe hawaelewi kuwa unawapigania. Mpenda mabadiliko yeyote aliyechoshwa na utawala huu ni lazima afanye jambo, hata kama ni kwa kuwashawishi ndugu zako popote walipo waachane na hilo chama lao inaweza kuwa ni hatua ya kuanzia. Nimeanza na babu yangu, ameelewa somo, japo umri umeenda wewe umeanza na nani?
Wewe si umetoa hoja yako ya kutufundisha na mimi nimesema kuwa sisi sio wanafunzi wako hivyo hayo unayotufundisha fanya wewe mwenyewe! unafura du! . sawa mimi ni mshamba nimekubari
By the way Dr anaendele vyema!
FMES na Williams wameishakusoma mkuu.....
Unajipunguzia heshima ndugu, kuwa objective na uache kujikomba. Hufanani na maneno uliyoandika hapo.
Ukweli ni kwamba CCM wamejimaarisha maeneo ya vijiji kuliko vyama vya upinzani. Hii ni changamoto kwa upinzani kujiandaa vyema kwa uchaguzi 2010 katika maeneo ya vijijini. Operesheni wanazozifanya bado haziwaamsha wananchi kiasi wawe na imani ya kunyakua viti vingi vya ubunge au hata urais katika miaka mwakani au hata 2015.
Samahani Busanda hakuna umeme na ki E90 changu kilichemsha sasa ndio nimerudi hewani na matokeo ndio hayo mliyoyasikia.Hii ni ishara tosha kwamba JF kuna propaganda watu tunalishwa. Kwa kelele za hapa JF mimi niliamini kabisa CHADEMA wanashinda Busanda.
Nimeshangaa mkuu Pasco ambaye mimi huwa namwamini kutokana na maandishi yake mbalimbali, ghafla kapotea si ajabu baada ya kuona CCM wanaanza kushinda.
Mjini CHADEMA wana majimbo mangapi? acha hizo
Shalom,
Please ondoa ujinga wako hapa!
Dr kuendelea salama kuna uhusiano gani na thread hii?
Waambie wana JF unachotaka kusema; waambie ile ajali ulikuwa mkono wa Mtanzania.
Pure nonsense! Inatakiwa ukapimwe akili yako.