CCM yanguruma Busanda; Wapinzani chali!

Dr Slaa,
Kwa waliosikia kauli ya rais juzi akiwa Misungwi kuhusu ushindi wao Busanda, haishangazi kwa nini wahalifu waliachiwa na Polisi pamoja na uhalifu wote walioufanya. Ni bahati mbaya sana kuwa viongozi wengi wa Afrika wamekuwa na dharau sana kwa wananchi wao na kugeuka watumishi wa hao wanaoitwa nchi wahisani/wafadhili.

Halitakuwa jambo baya kama uovu wa watawala wetu, sambamba na kuwajulisha wananchi, pia mtawajulisha na mabalozi wa hizo nchi za hao wafadhili wao.
 

Mzee MKJJ, nimesoma kijarida cha cheche lakina nimeshindwa ku connect dots na bolded info. yako hapo juu.
 

Heshima kwako Dokta,
Maelezo yako yameelemea sana katika matendo CCM waliyofanya kuhakikisha ushindi. Na nadhani wengi tutakubali ni matendo yanayoweka doa kubwa katika chaguzi za kidemokrasia na yapaswa kukemewa kwa hali na mali.
Lakini, mimi binafsi ningependa pia kuona Chadema inachacharika zaidi katika msakato mzima wa uchaguzi. Sina uhakika wa ukubwa wa base yenu hapa nchini. Lakini nadhani kama Chadema ingeweka kundi la watu ambao inahakikisha ndio wako targeted katika sera, ingesaidia sana katika kuimarisha nguvu ya chama. Nadhani mnatumia sana slogan ya vijana katika kampeni zenu. Lakini katika wapiga kura wote, vijana wanachukua asilimia ngapi? Waliojiandikisha ni wangapi? Na wanaotoka kupiga kura ni wangapi? Sina uhakika wa data mnazokuwa nazo katika uchaguzi, na nisingependa kuwaeleza ni jinsi gani ya ku-run kampeni yenu, lakini nadhani ingesaidia kuweka angalau asilimia kadhaa ya kura mfukoni mwenu tayari, kama mtakuwa na a 'target' group. Swala hili unalionaje mheshimiwa?
 
Dr. Slaa kama haya yote uliyoyasema yametokea na mna ushahidi (kama ilivyokuwa Kiteto) kwanini mnataka kushiriki uchaguzi mdogo wa Biharamulo? Mnatarajia kutakuwa na tofauti?
 
CCM imewaliza tena Watanzania. Ili kuwe na maisha bora, ni lazima kuanza upya. Bila CCM.

As Obama says, you cannot do things the same way over and over again and expect a different result. As long as the same “wenzetu” continue to steal elections and to rule us, and in the same way, we shall continue to be one of the five poorest countries in the world.

Watanzania wameelemewa na CCM, na CCM imeelemewa na corruption. Ili Watanzania waweze kudhibiti corruption, itabidi kwanza waondokane na CCM. Hilo linakuwa gumu kwani CCM inaiba kura, tena kwa kutumia vyombo vya uma!

Nchi inayotawaliwa na wezi itaendeleaje?
 

Sawa, Hilo linajulikana, swali ni 'what to do'?
 
Bila shaka wanatupeleka kule tusikotaka kuwa. Watafurahi tukitumia nguvu kuwanyang'anya dola na hapo watapata nafasi ya kusema upinzani ni vita. Lakini uonevu huwa na mwisho ndugu zangu, na ukifika mwisho mnabashiri nini? Subirini hawa vijana wanaomaliza shule na vyuo sasa ambao kwao wakikosa uvumilivu ugoma na kutumia nguvu kutafuta haki watakapofikia umri wetu, sisiemu watajua nini nasema!
 
Sawa, Hilo linajulikana, swali ni 'what to do'?

Ni swala zuri, Mtoto; Nini cha kufanya!

  1. Wakati Dr. Lamwai alipogombea na kuchukua Jimbo la Ubungo, wapiga kura wake waliweza kuthibiti wizi wa CCM. Itabidi wananchi wajitolee kulinda haki yao. Nadhani hilo lilifanyika Musoma vile vile.
  2. Uongozi wa Chadema umefanya vizuri kukusanya ushahidi na mashahidi wa ujangili uliofanywa na CCM. Dr. Slaa anajua wanavyofanya hawa CCM. Tunatarajia atumie mahakama sasa kufichua angalau sehemu ya ufisadi uliofanyika. Tuko wengi sana ambao tunasema TUMAINI LETU NI SLAA.
  3. Tunatawaliwa na watu hatari sana. Inapofikia Mzee Mzima kama Malechela anaongoza kundi la watu wanaowapiga wapinzani visu, basi ujue hawa wanazungumzia amani, lakini wenyewe hawaijali hata kidogo. Polisi wakikataa kulinda usalama wa wapinzani, basi itabidi wapinzani wajilinde kwa njia zao wenyewe.
  4. CCM ni kizazi cha nyoka. Tufikishe huo ukweli kwa wananchi. Njia mbali mabali zinaweza kutumika. Hata hapa JF ni mahali pazuri pa kuanzia. Wako wanahabari wengi wanaosoma hapa.
 

- Mkuu Moshi habari za siku nyingi umepotea sana vipi mkuu? Huku Busanda uchaguzi ulishaisha na CCM ilishinda tena hata Chadema wamekubali kwamba ulikuwa ni uchaguzi wa haki bin halali, sasa tunajitayarisha kuelekea Biharamulo, cha msingi ni wapinzani kusimamisha mgombea mmoja tu, ama sivyo yatakuwa ni yale yale tu,

Otherwise ujumbe wako ni mzito sana.

Respect.

FMEs!
 
 
FMES,

Heshima mbele mkuu! Mie nipo, ila nazidi kuumia zaidi ninavyoona wananchi wenzangu wanavyoonewa. Iweje watu wa CCM wamkamate mtendaji wa CHADEMA, wamfunge kamba na kumchoma kisu, na Polisi wasiwakamte wahalifu? Kumbe mikutano aliyoongoza Mzee Malechela ilikuwa ya kupanga namna ya kufanikisha uhalifu kama huu?

I am completely convinced now that the greatest and most debilitating corruption in Tanzania is that of CCM. This group of evil doers sign secret deals with people who rape us, embezzle funds from the national coffers, and rig elections! There is no limit on what this den of vipers could do!
 
 
Hapa najifanyia tathmini nilisema nini kuhusu Wapinzani ile 2009 na kulinganisha hiki kinachoendelea UKAWA.

Pasco
 
John Pombe Magufuli aliyepiga kampeni kwa Kisukuma lugha ambayo wanaielewa .
Baada ya John Pombe Magufuli kupitishwa kuwa mgombea wa CCM, nimeukumbuka huu uzi, nimemkumbuka John Pombe Magufuli alivyokuwa akipiga kampeni kwa lugha ya Kisukuma!.

Ndugu zangu wapinzani, wakati mnatafakari mtamleta nani wa kushindana na Magufuli kwenye urais, pia jiandaeni kuangalia mtakavyo yaokoa majimbo yanayoshikiliwa na upinzani kwenye kanda hii ya Ziwa, kwa nilichokishuhudia kwenye kampeni hizi za kanda hii, uchaguzi wa mwaka huu, Magufuli atayarudisha CCM, majimbo yote yanayoshikiliwa na wapinzani!.

Ila pia Tanzania tujiandae kushuhudia ukabila wa ajabu Magufuli akiishaingia Ikulu yetu. Kama kwenye kampeni NEC imepiga marufuku kuhutubia kwa kutumia lugha za makabila, lakini Magufuli amehutubia kwa Kisukuma, ni uthibitisho tosha huyu jamaa ni mkabila, hivyo subirieni tutakuja kukumbushana


Pasco
 

Kwa ujumla ccm zaid ya kupoteza majimbo mengi kwa upinzani hakuna wanachoweza kufanya
 

Mkuu Pasco mbona unazidi kujidhalilisha sana?.Kwa muda mrefu humu ulituaminisha eti ccm lazima impe Lowasa urais.Leo tena uko kuzusha uongo kuhusu majimbo ya ziwa.Ni hivi Chadema itayatetea yote na kuongeza mengine!!
 
Pasco nazidi kukuzarau usiwe mwepesi kubadilika kama kinyonga. Juzi hadi kamati kuu inaendelea wewe ulikuwa upande wa mh lowassa... Kama wewe aupo kimaslahi ni bora muda mwingine ukanyamaza kwa sababu sio lazima kila kinachokujia ubongoni mwako ukiandike hapa ... Nyani Ngabu message yake inasema miafrika ndivyo tulivyo na ihii ni kweli akuna watu wabaya duniani kama waafrika wanacheka,wanakula,wanakunywa na wewe lakini dakika moja inatosha kukusaliti tatizo ni ufukara wa akili na mali za dunia ihii.... Najua sasa hivi unajipendekeza kwa mh magufuli kusaka ukuu wa wilaya au mkoa hongera sana ...ila unajizalilisha kwa ukigeugeu kama kinyonga hata wiki bado ushakuwa na mahaba na magufuli na kumsahau mzee el kabisa .... Haya maisha haya rafiki wa kweli ni ndugu yako wengine akuna kitu zaidi ya unahaaaaaaa
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Pasco mbona unazidi kujidhalilisha sana?.Kwa muda mrefu humu ulituaminisha eti ccm lazima impe Lowasa urais.Leo tena uko kuzusha uongo kuhusu majimbo ya ziwa.Ni hivi Chadema itayatetea yote na kuongeza mengine!!
Mkuu , wengi wa wachangiaji humu are theoretical, not practical!, idadi kubwa ni wishful thinkers tuu kuwa 2015 wapinzani wataingia ikulu, ukiuliza how?, hawana majibu!. Mimi ni realist, kazi yangu ni kuwaletea ukweli nilioushuhudia kwenye ground, nikawatolea mfano wa jimbo la Busanda, na kueleza CCM ilishindaje!. Vitu vingine ni kuelezana tuu humu ndani, yakitimia tujakuja kukumbushana tuu!.

Pasco
 
Mkuu kwanza naomba nikuhakikishie kuwa Pasco wa jf, huwa hajipendekezi kwa yoyote!. Kama unadhani Magufuli ndio nimeanza kumzungumzia baada ya kupitishwa juzi, nenda kanisome hapa, uangalie huu uzi ulipandishwa lini humu!. Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" .

Hili la ukuu wa wilaya nalo neno!. Kaangalie mshahara wa DC shilingi ngapi kwa mwezi, kisha nenda Brella kaangalie mmiliki wa kampuni inaitwa PPR ni nani, hapo Brella pia utaona hiyo PPR iko jengo gani!. Baada ya hapo nenda NHC kaangalie kodi ya pango ambayo PPR inalipa NHC, kisha ulinganishe na mshahara wa DC!, na baada ya hapo malizia kwa kwenda TRA ukaangalie hiyo PPR inalipa kodi kiasi gani!, baada ya kuyajua yote hayo, ujiulize huyo jamaa wa PPR anajipendekeza ili awe DC akapate nini?!. Kwa taarifa yako huyo DC naweza kumuajiri na kumlipa mshahara mkubwa kuliko anaolipwa!.

Pasco
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…