Leak
Platinum Member
- Feb 22, 2012
- 52,942
- 43,601
Ndio maana nikasema bora kukosa umayer kuliko kukaa na nyoka ndani ya nyumba!
Sahihisho: habari yapaswa kuwa KAFU +CCM waibwaga CDM Nyamagana.
last week RAIMWEMA liliandika.....
HUKU kikiwa na mvutano wa ndani na madiwani wake wawili kiliowafuta uanachama, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinakabiliwa na mtihani mzito katika kutetea nafasi Meya wa Jiji la Mwanza dhidi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.
Uchaguzi huo unaofanyika baada ya kugawanywa kwa Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kuunda Halmashauri ya Jiji na Manispaa ya Ilemela unatarajiwa kuwa na mvuto wa aina yake katika siasa za Mwanza, ukitiwa chachu na hatua ya CHADEMA kuwafukuza uanachama madiwani wake ambao kwa namna fulani wanaweza kuathiri matokeo ya uchaguzi huo.
Wakati CHADEMA wana uhakika wa kutwaa nafasi ya meya na naibu wake katika Manispaa ya Ilemela ambako pamoja na kumvua uanachama Diwani wa Kitangiri, Henry Matata, bado idadi ya madiwani wake ni wanane akiwamo mbunge wao dhidi ya madiwani sita wa CCM na mbunge wa viti maalumu mmoja wa CUF, shughuli pevu itakuwa katika halmashuri ya Jiji la Mwanza ambapo CUF ndiyo wenye turufu ya kuamua nani anakuwa meya.
Kwa upande wa Halmashauri mpya ya Jiji la Mwanza, inayoundwa ndani ya mipaka ya Jimbo la Uchaguzi la Nyamagana, awali kabla ya CHADEMA kumvua uanachama Diwani wa Kata ya Igoma, Adam Chagulani, kilikuwa na wajumbe wanane sawa na CCM ambacho pia kilikuwa na idadi hiyo ya wajumbe wa Baraza la Madiwani, ambapo sasa baada ya Chagulani kuvuliwa uanachama CHADEMA kinabaki na wajumbe saba.
Hata hivyo bado turufu ya nani anakuwa Meya wa Jiji hilo bado iko mikononi mwa CUF ambao wana wajumbe wawili ndani ya baraza hilo, ambao wakiamua kuunga mkono upande wowote huo ndio utaibuka na ushindi katika kinyanganyiro hicho.
kabla ya chagulani ilemela
CCM=8 CDM=8 CUF=3
baada ya Chagulani na ndoa ya CUF+ CCM=11
so hata kama huyo chagulani angekuwepo bila kula za CUF CDM wangeishia kula 8 tu. na hamna ambalo lingebadilika
ujanja wa CCM uliazianza baada ya kugawanya JIJI kuwa na Nyamagana na Ilemela kupitia waziri mikuu ambaye ni CCM. so turufu ikabaki kwa CUF ambao ni maswahiba na wenza wao (unabisha haupo TZ!)
kabla ya kugawa jiji
ccm=15
cdm=19
cuf=3
so piga ua CDM ingeshinda mwanza! wanaakili sana lakini wanashau kuwa hata kama unaakili watu wakichoka hauwezi badili watu! so kina chagulani walitumika kuharibu hali ya hewa hili watu wasiojua ukweli wanaone chadema si chama cha maana, arafu uchaguzi wa meya urudiwe ili CCM washindwe. Sasa najiuliza Chagulani na mwenzako mmefurahi nini?