manake nini? eti aina kajifunze kwanza hata kiswahili sanifuSiasa aina adui wa kudumu wala rafiki wa kudumu .
dr slaa vipi hajazimia kwa aibu?
mnakuja kwa kasi kama saloon na lugha zenu za mipashooooo na nchi ndo mtaachia tuMnyika toa tamko CDM kususia kununua sato na sangara?
Mkuu sidhani kama ni ushindi wa Tsunami, maana tofauti ni kura tatu, 11/8, mie ni mkazi wa kata ya Mkolani, najua siasa za Nyamagana, na kama hujui , huyu jamaa kabebeshwa zigo kubwa sana ambalo sijui atalibeba vipi. Siasa za Mwanza ni zaidi ya ushindi, acha tusubiri tuone kama ni kitu cha kushangilia ama ni kumuonea huruma. Tutaona kama huo weledi unaosema na utumishi uliotukuka utaonekana, maana ni mwanzo tu, na kwavile siasa za mwanza ni zaidi ya ushindi, nitapenda nisikie tena hili ulilotabiri Mkuu.MODS ; Hii thread msije kuichakachua na kuiunganisha na zingine kwani zile ni za matokeo na hii ni hali halisi ilivyo mwanza hizi sasa
Ndugu wana JFKama mlivyo kwisha sikia katika mitandao ya kijamii na vyombo mbali mbali vya habari, cdm wamebwagwa kwa ushindi wa sunami na ccm kwenye kiti cha meya wa jiji la mwanza ambacho ndio muhimu kuliko hata kile cha ilemele ambacho kitatoa mwenyekiti wa manispaa. Kwa hali ilivyo hivi sasa haya ndio yaliyotoke na yanayo endelea kutokea:
1. baada tu yakutangazwa matokeo ndani ya ukumbi wa uchaguzi, dr Slaa ambae alikuwapo wakati wa uchaguzi alionekana ni mwnye huzuni na simanzi kubwa , na hakukaa tena bali aliondoka haraka. Hata waandishi wa habari walikuwa wanamtafuta wamuhoji hakuonekana tena, sasa sijui ni aibu yakushindwa ama lipi.
2. baada ya matokeo kutangazwa vifijo na nderemo vilikuwa vingi kiasi cha kwamba watu walikuwa hawasikilizani kabisa. Na hapo basi , sherehe za ushindi zilihamia mpaka nje na kusambaa katikati ya jiji la mwanza na kufanya shughuli nyingine kusimama, mpaka sasa shughuli zimesimama na sherehe zimetapakaa mji mzima huku foleni za magari zikiwa ndefu.
3. meya mteule wa jiji la mwanza anategemewa kuongea na wananchi wa jiji kutoa shukrani zake na imani yake yakulitumikia jiji hili kwa weledi mkubwa na uliotukuka
Kwa sasa ni hayo tu, ntawaletea kitakacho jiri zaidi.
ama kweli chadema ni cha tawala yaani ccm kushinda imekuwa kitu cha ajabu sana yaani sawa na manyema fc kuifunga simba au yanga watashangilia sana..vita vinaendelea....
Uwezekano wa CDM kushinda ulikuwa finyu ukichukulia walishajipunguzia idadi ya kura kwa kuwafukuza uanachama madiwani. Lakini kufukuzwa kwao kwa nia ya kuweka nidhamu katika chama ni sahihi zaidi, ni heri kutokuwa nao kuliko ufitini na uharibifu waliokuwa wanauendeleza ndani ya chama. Ni maamuzi magumu yanayowezekana CDM tu kwa ajili ya uendelevu kisiasa,ni sawa na kukatwa mguu au mkono ili kuokoa saratani isisambae mwili mzima. Kwa mbeleni CDM tuwe waangalifu tunapopitisha wagomba katika ngazi mbalimbali