CCM inaelekea kufilisika mno haraka na wasipochunga fikra zao mbofu-mbofu, watasababisha maafa kwa watanzania kwa kisingizio cha kupambana na Chadema. Wanashindwa kupambanua kuwa tanzania ndio Chadema, maana hiki ni chama cha watu, umma, na nguvu ya watu.
Wanatakiwa watafakari endapo nchi ina watu zaidi ya milion 45, CCM ni milioni 5 tu, watanzania takribani milion 35 ndio 'taifa' na idadi kubwa ni chadema kwa sasa, na wanaobaki kama milion 5 wanagawana vyama vidogo vikiongozwa na CCM-B, yaani Cuf na wasio na vyama.
Kwa hiyo CCM ijue tangazo lolote la uhasama dhidi ya Chadema ni kupambana na 'taifa nzima' na haina kikomo zaidi ya CCM kutoweka au ku-cease!
CCM wanahaha kuhusu uimara na nguvu ya chadema kwa umma na dhidi ya uhalifu wa CCM, hawana majibu, wana pressure, wanapishana na kugombana wenyewe...na bado!
Siku Chadema watafikia maamuzi, wanatangaze rasmi ufidhuli wa CCM, NEC na UWT wlipoharibu kura za taifa hili, kutakuwa na mshtuko mkuu kwao wote na watatamani kuikimbia nchi maana 'raia' na nchi yao hawatatamani hata kuwasikia kuanzia na JK mweyewe. Achana na akina Chiligati na akina Malisa wanaopanic kabla hakujakucha. Tusubirie...Yetu macho.