CCM yahaha kuimaliza CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yahaha kuimaliza CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lukolo, Nov 21, 2010.

 1. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  • CHENGE ABEBESHWA MZIGO KUWASILISHA HOJA BINAFSI

  na Mwandishi wetu

  SIKU moja baada ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Chiligati, kueleza mkakati wa kutaka kuwaondoa bungeni wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), chama hicho tawala sasa kinajiandaa kuleta hoja binafsi kuwaondoa wabunge wa CHADEMA, Tanzania Daima Jumapili imeelezwa.

  Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima Jumapili imezipata kutoka ndani ya CCM, zilisema chama hicho kimetoa maagizo kwa wanasheria wake ili waandae hoja binafsi itakayowasilishwa bungeni na mwanasheria, Andrew Chenge, kisha kupiga kura ya kutaka wabunge hao waondolewe bungeni.

  "Mchezo uliopangwa kufanyika ni kama ule aliofanyiwa Zitto Kabwe alipotoa hoja ya Buzwagi. Licha ya utetezi wake mzuri, aliondoka. Safari hii kazi hii atapewa Chenge, tumepania lazima wabunge wa CHADEMA waondoke bungeni hadi hapo watakaposema wanamtambua rais," alisema mmoja wa makada wa CCM.

  Kwa mujibu wa habari hizo, mpango huo unasubiri baraka za Katibu Mkuu, Yusuf Makamba, ambaye alitarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam jana baada ya kuwa nje ya ofisi yake kikazi.

  Kada huyo alipohojiwa ni kifungu gani cha Katiba au cha kanuni za Bunge kilichovunjwa, alishindwa kujibu, lakini alisisitiza kuwa chini ya mkakati huo, CCM itahakikisha inamtumia spika wake mtiifu, Anne Makinda, kuhakikisha wabunge wa CHADEMA wanashughulikiwa.

  "Hakuna kitu kilichomuumiza rais kama kitendo cha wabunge wa CHADEMA kusimama na kuondoka kwa dharau. Bora wasingekuja bungeni na katika hilo chama kimedhamiria, Bunge lijalo moto utawaka," alisema mpashaji habari huyo.

  Naye Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Benno Malisa, amelaami kitendo hicho na kusema ni ishara ya utovu wa nidhamu kwa wapiga kura waliowachagua.

  Hata hivyo, uamuzi huu wa CHADEMA kususa matukio yanayomhusisha rais umemfadhaisha na kumsumbua rais mwenyewe na CCM mbele ya umma na macho ya kimataifa.


  Source: Tanzania Daima

  My Take
  Iwapo CCM watatekeleza mpango huu, nafikiri wanaweza kuwa wamejichimbia kaburi kwa kuwa CHADEMA hawataongelea bungeni tena bali watakwenda kwa wananchi. Kitendo cha kuitisha mikutano na wananchi na kuwaeleza ni namna gani serikali iliyopo madarakani inadhulumu haki ya watanzania, kitaamusha hasira miongoni mwa wananchi na kuweza kupelekea kuvunjika kwa amani. CCM wafikirie upya juu ya mkakati wanaotaka kuuchukua, maana unaweza ukawagharimu, wakajikuta wanashindwa kuongoza nchi.
   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hayo uanyosema ni upupu tu, Chadema isha jimakiza yenyewe, kama unabisha, subiri ujionee, miaka mitano ijayo watabaki kama NCCR mageuzi, una kumbukumbu za vipi Mrema alikuwa? Utajaza mwenyewe.
   
 3. F

  Far star Senior Member

  #3
  Nov 21, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani mambo yanafanywa kwa kuzingatia sheria na kanuni,sasa kama hawajavunja kanuni,sasa hawa ccm wanatakakuchomekea kwa kulalamikia nini,swala la kuondoka bungeni sio tatizo kabisa ilimradi hawajavunja kanuni,haijalishi wakati wanaondoka aliekuwepo ni raisi au nani.

  Amani ikivunjika wakulaumiwa ni ccm na sio chadema, maana kinachojadiliwa hapa sio tatizo kati ta chadema na kikwete,no hapa issue ni mfumo uliotumika wala hakuna mwenye bifu na kikwete.
   
 4. W

  We can JF-Expert Member

  #4
  Nov 21, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kila kitu kwa wakati wake. Bila shaka jambo hili limetokea kwa idhini ya Mungu.

  Hakuna haja ya kulazimisha watu waandamane kupinga, kwani ni sawa na kujipinga mwenyewe! Umesema, unalaani CHADEMA kutoka nje ya Bunge, lakini hapohapo unataka watu waandamane....zote hizo ni PROTEST!

  Jaji Mkuu kashasema, what CHADEMA did was legal, sasa kwa nini kutafutiza makosa? Namna ya kupunguza umaarufu wa counterpart wako ni kukaa kimya! CCM wanapolivalia bango suala hili kwa jinsi hii, ni kuonyesha kuwa HAWAJAKOMAA ktk misingi ya demokrasia? La, hasha, CCM wamekomaa sana, ispokuwa MAFISADI wanawayumbisha.

  Hakuna kosa kubwa la karne kama HATA KUANZISHA MJADALA WA KUWATOA BUNGENI CHADEMA, Hii ni sawa na kutoa tangazo la kujadili kina cha kaburi la CCM, I advice, NEVER EVEN INTERTAIN THAT IN THE HOUSE OF ALL TANZANIAS, BUNGE.
   
 5. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #5
  Nov 21, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wanaotoa hukumu ya kweli kuhusu nani awajibike kwa kuhatarisha amani ya nchi ni wananchi watanzania wenyewe.

  Kwenye hili sisiem isijione kwamba ndio kila kitu na kwamba wanachoamua hata kama ni kwa dhuluma iwe hivyo hivyo, kwa maoni yangu walichofanya CHADEMA ni salamu kwa mwizi au mnufaika na mfumo mbovu wa tume ya uchaguzi.

  Mtu hachaguliwi jinsi ya kumshughulikia mwizi wake, ukiamua kumpiga ni sawa ingawa ni kinyume cha sheria (unatakiwa kumpeleka polisi) ukiamua kumzomea hii ni nzuri zaidi hasa kama ni mtu mwenye jina lake kwenye jamii hii nii sawa kabisa.

  Inashangaza kuona kwamba mtu aliyeiba kura kutosikilizwa na aliye waibia imekuwa habari lakini suala la walioibiwa watu wote hawaichukulii kama habari.....jamani mwizi ni mwizi tu hakuna jina mbadala,demokrasia ya kweli ni box la kupigia kura na sio kuchakachua.

  Unawaibia watu kura zao halafu unategemea wakusifie..bullshit....tuvumiliane jamani kuibiwa kunauma sana. Lini watanzania maoni yetu kwenye box la kura yataheshimiwa?
   
 6. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #6
  Nov 21, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Tunawajua CCM kuanzia mkwere hadi wapambe ni watu wa visa. Sitashangaa nikiona haya yanatekelezwa. Wajue kabisa kuwa wananchi wataangalia bunge na kuwa na maoni yao kwa kila kitakachoendelea. Miaka mitano si mingi kama waccm walivyoambiwa na mungu wao. Wajue kuwa wanazidi kuchochea hasira za wana wa nchi na mwisho wa siku watachinjiwa kwenye ballot box. Safari ijayo kitaeleweka tu! Na itafahamika tu! Wao wacheze na hii miaka mitano kuleta bifu na chama cha wananchi-CHADEMA. Watashangaa wamepoteza majimbo 200. Watanzania ni watu wa kimya kimya. Jenerali said it all kwenye waraka wake w pili kwa Jakaya
   
 7. k

  kamalaika Senior Member

  #7
  Nov 21, 2010
  Joined: Mar 16, 2007
  Messages: 187
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tafakari kabla ya kuchukua hatua, msije mkawasha MOTO ambao mtashindwa kuuzima.
   
 8. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #8
  Nov 21, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,207
  Trophy Points: 280
  CCM badala ya kuhaha kutibu makovu ya chama chao wanahaha kuimaliza chadema
   
 9. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #9
  Nov 21, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  • chondechonde ccm. Chondechonde jk. Tafadhali vitendo vyovyote vya ubabe vitahatarisha usalama, amani na utulivu ambao ulijengwa na mwalimu kwa ufundi sana. Ccm isigeuzwe kuwa sawa na mkoloni wa 1954 -1961 ambapo chadema ikawa kama tanu ya kipindi hicho. Nchi yetu haikumwaga damu kuupata uhuru. Vivyo hivyo tunatarajia ccm na ukomavu wake ianze mchakato kwa amani na bila masharti wa kurekebisha kasoro za taratibu za uchaguzi na ikibidi katiba. Itakuwa inafanya hivi kwa faida ya kizazi kijacho. Kwa kufanya hivyo ccm iajijengea heshima kubwa kwa kizazi kijacho. Vinginevyo ikitumia ubabe leo itakuwa imepandikiza bomu ambalo litakimaliza kizazi kijacho.
   Hadi sasa tuna statesmen 2: Mwalimu kwa kuwezesha kuleta uhuru bila kumwaga damu 2. Mzee wetu rahim mzee mwinyi kwa kuleta mageuzi makubwa ya siasa na kiuchumi bila damu kumwagika. Chonde chonde jk uwe statesman wa tatu katika kuleta mageuzi ya katiba ambayo itaendelea kuitunza amani hii na kuleta maendeleo makubwa zaidi ili kizazi kijacho kikukumbuke. Acha ubabe na usiwasikilize wanaokuchochea ufanye ubabe. Dira yako iwe ni kizazi kijacho. Ili jk afanikiwe kuwapuuza wapinzani ni kufanya hayo mageuzi - ataona kama watakuwa na kuu jipya. ​
   
 10. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #10
  Nov 21, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 11. m

  matawi JF-Expert Member

  #11
  Nov 21, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Bonge la picha hili. Asante teja la JF
   
 12. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #12
  Nov 21, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  CCM hawana akili kabisa ..yaani imewauma sana kuona JK kaaibishwa hahaaaaaa.JK sio rais halali na hilo linaeleweka...wajaribu waone kitakachotokea..
   
 13. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #13
  Nov 21, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  DSM, labda nikukumbushe tu kwamba mimi ni mwanaCCM wa siku nyingi wala kadi yangu ya CCM bado sijairudisha, nimeshahudhuria vikao vingi sana vya ndani vya CCM, kwahiyo ninajua ni chama gani ni cha upinzani cha kweli na ni chama gani ni geresha. Ni makosa makubwa sana kuilinganisha CHADEMA na NCCR mageuzi. Kama kweli wewe ni mwanaCCM basi waulize wakubwa wako CHADEMA ni nini na NCCR Mageuzi ni nini, naamini watakwambia.
  MS, upo dada or sorry kaka?? Sidhani kama CHADEMA inawekwa kapuni hivi sasa. Badala yake kitendo cha CCM kuendeleza hili zogo na CHADEMA, inazidi kukijenga na kukipamba. Kwa mtindo huu watu watataka kujifunza zaidi kama CHADEMA ni nini, na mwisho wa yote wakijua ukweli wa kile ambacho CHADEMA inakipigania, CCM haitakuwa na kwa kupeleka pua. Kuweni makini, CCM ndiyo inakufa hivyo.
   
 14. M

  Mkorosai Member

  #14
  Nov 21, 2010
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM wakifanya maandamano ya kulaani kitendo cha wabunge wa CHADEMA kutoka nje ya ukumbi wakimsusa Rais, Viongozi wa CHADEMA nao waitishe maandamano ya kuwaunga mkono wabunge wao na kulaani Tume ya Uchaguzi kwa kuchakachua matokeo!! Halafu tuone nani zaidi.

  Angalizo katika hili, polisi iruhusu maandamano hayo na itowe ulinzi kwa wote. Kikwete apokee maandamano hayo kama mwenyekiti wa CCM na Mbowe apokee maadamano kama mwenyekiti wa CHADEMA!
   
 15. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #15
  Nov 21, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Ngoja nikapake mate ya mamba kabisaa
   
 16. m

  mgalisha Member

  #16
  Nov 21, 2010
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kama wanataka kubip amani ya hii nchi baadhi ya maeneo ikoje wafanye hivyo kwa kupeleka Hoja hiyo Bungeni ili wawaondoe kwa wingi wao, waone muitikio utakavyo kuwa kwa jamii,
  tafadhari msikurupuke na maamuzi uchwara,
   
 17. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #17
  Nov 21, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  jamani nasisitiza ccm hawawezi kuwatowa wabunge wa chadema bungeni,kwani ni kifungu kipi kinawafunga wabunge wa chadema? kama mlinukuu vizuri bwana mbowe mtajuwa kuwa hawa jamaaa wa ccm hawawezi na haitatokea,chadema wanamtambuwa raisi na wanatambuwa kuwa hawawezi kwenda mahakani kuhoji kutokana na katiba,wao wanacho pinga ni mchakato mzima wa tume ya uchaguzi nec na matokeo ya uraisi,na hata kutoka kwao bungeni ni kufikisha ujumbe kwa jamii na dunia kwa ujumla.

  haya msubilini makamba akulupuke then muwashe moto ambao hautozimika labda kwa petrol


  mapinduziiiiiiii daimaaaaa
   
 18. M

  Mkorosai Member

  #18
  Nov 21, 2010
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mapinduziiiii ...............Tanzania daimaaaaaa!!
   
 19. K

  KunjyGroup JF-Expert Member

  #19
  Nov 21, 2010
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Sisiem wangekuwa na akili timam wangetumia hizo nguvu kuleta maendeleo. Thats why i agree with people who say sisiem wamepoteza mwelekeo. Hawajui hata watanzania wanaitaj nin. Wao kwa akili zao ndogo wanatumia pesa za umma kupambana na Chadema. Thats why i question kama kweli chama chao kina watu wenye hekima.
  Rais wao aliiba kura, kwanin wanalazimisha aeshimiwe?
   
 20. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #20
  Nov 21, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mzee, yote umeyasema, CCM ni lazima wajifunze kusikia! Wanapoambiwa kitu kizuri kwa lugha ya ustaarabu wanatakiwa waone mantiki ya walichoambiwa badala ya kupindisha ukweli na kuingiza propaganda za kijinga!!! Hivi sisiem mtaendelea kuwadanganya Wadanganyika hadi lini? Hivi hamjui kuwa mnajichimbia kaburi wakati hawa mnaodanganya watakapong'amua ujanja wenu kuwa mmekuwa mkiwadanganya tu??
   
Loading...