CCM wasema takrima sasa basi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM wasema takrima sasa basi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwikimbi, Sep 5, 2008.

 1. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  CCM wapiga marufuku takrima
  Tausi Mbowe

  CHAMA cha Mapinduzi (CCM), kimepiga marufuku wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya jumuiya zake na wapambe wao kwenda mikoani na wilayani kujinadi au kuwanadi wagombea


  Naibu Katibu Kuu wa CCM (Bara), Kapteni George Mkuchika, alisema kuwa imebainika kuwa kuna vitendo vichafu vya rushwa vimeanza kufanywa na baadhi ya wagombea kwa lengo la kuwashawishi wajumbe wawapigie kura katika uchaguzi ujao.


  "Wapo wagombea wanazunguka mikoani na wilayani kujitangaza wakati hata majina yao hayajateuliwa na vikao husika. Wakiwa huko hukutana na baadhi ya wajumbe na kuwapa takrima,"alisema na kuongeza:


  "Wengine wanatumia wapambe na kuwagharamia kili kitu ili kufanikisha mipango yao ya kuingia madarakani kwa rusha".


  Mkuchika alisema wagombea wengine wanapakana matope, kuwa kutoleana lugha chafu kwa lengo la kuchafuana, jambo ambalo ni kinyume na maadili ya chama hicho.


  "Sisi katika CCM tunaamini kwamba viongozi wazuri na watakaoweza kukisaidia chama ni watakaochanguliwa bila rushwa, wanaochanguliwa na rushwa hawawezi kukisaidia chama kwasababu watashindwa kukemea rushwa, hivyo kuwa sehemu ya tatizo kwa jumuiya zao na chama," alisisitiza Mkuchika.


  Mkuchika alisema ni marufuku wagombea na wapambe wao kujihusisha na vitendo vya rushwa ya aina yoyote pamoja na kutoa takrima au bahasha kwa wajumbe.


  Alisisitiza kuwa ni marufuku kutumia lugha za kupakana matope katika kipindi chote cha mchakato hadi uchaguzi kwa sababu chama kinataka kuwa na viongozi safi.


  Mkuchika aliwaonya wagombea watakaobahatika kuteuliwa kugombea nafasi mbalimbali kuheshimu dhamana waliyopewa na chama kwa kutojiingiza kwenye rushwa, vinginevyo atakayebainika atafutwa.


  Alisema wagombea wote watapata nafasi ya kujieleza na kujinadi katika vikao vya uchaguzi kabla ya kupigiwa kula hivyo kujinadi nje ya vikao hivyo ni kosa.


  Hii ni kauli nzito kuwahi kutolewa na CCM tangu kuanza kwa chaguzi mbalimbali ndani ya chama hicho.


  Mkutano wa tatu wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM), kwajili ya kuchuja majina ya wagombea uongozi wa umoja huo kinatarajiwa kukutana kesho kutwa mjini Dodoma huku kukiwa na taarifa kuwa Kamati ya Utekelezaji iliyokutana mwezi uliopita chini ya Uwenyekiti wake Dk Emmanuel Nchimbi kuwaengua baadhi ya wagombea akiwemo Nape Nnauye anadaiwa kupewa alama 'E' kwa kigezo cha umri


  Katika hatua nyingine mkataba wa ujenzi wa jengo la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), unaodaiwa kusainiwa kwa njia ya ufisadi umejadiliwa katika kikao cha Kamati Kuu ya CCM (CC) baada ya wanasheria wa chama hicho kuutiza upya mkataba huo.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,851
  Likes Received: 83,275
  Trophy Points: 280
  Bora wafunge chama chao tu na kupotea katika anga za siasa za Tanzania. Matatizo mengi ndani ya nchi yetu yanasababishwa na hiki chama cha mafisadi.
   
 3. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #3
  Sep 5, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hawa mythlocated kind of cuckoo's wamekosa ajenda kabisa!Walijifanya wanajua Kiswahili sana wakatungia rushwa jina jipya kwa kuiita Takrima and now wanaona vidagaa ndio vinagombea ndio wanaona ndio wakati wa kuipinga hiyo Takrima!
  Very Stupid!
  Sorry for the strong language!
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Sep 5, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Sio kweli...!
   
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  Sep 5, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Heri mimi sijasema
   
 6. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #6
  Sep 5, 2008
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Maneno matupu hayavunji mfupa.

  CCM wakifanikiwa kuondokana na tatizo la takrima/rushwa watakuwa wamezika chama chao rasmi na kuunda chama kingine cha siasa chenye wanachama wataojiengua kwa kuwa wao CCM ndio walioweka msingi wa hiyo takrima ili kukibinafsisha chama chao (CCM) kwa matajiri.

  Natabiri kuwa wanachama wao wengi watahama na kutafuta chama mbadala chenye wagombea ambao wako tayari kutoa takrima ili kununua uongozi, nachokiona sasa katika CCM ni kuwa kimekuwa Chama cha wenye mapesa ya kununua uongozi na Wanachama wenye njaa wanongojea uchaguzi wagange njaa na kuongeza mlo au kubadilisha menu.
   
 7. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #7
  Sep 5, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mwenyewe kaingia kwa takrima
   
 8. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #8
  Sep 5, 2008
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Rushwa yatanda chaguzi za CCM

  2008-09-05 09:23:29
  Na Futuna Seleman

  Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kimepokea taarifa kwamba, kuna baadhi ya wagombea wake ambao wameanza kujihusisha na mambo yanayoashiria rushwa, ikiwemo kuzunguka mikoani na wilayani kujitangaza wakati majina yao hayajateuliwa na vikao kwa ajili ya kugombea uongozi wa jumuiya za chama hicho.

  Chama hicho hivi sasa kipo katika mchakato wa chaguzi za jumuiya zake katika ngazi mbalimbali.

  Chaguzi hizo zinazohusisha jumuiya za Vijana, Wanawake na Wazazi zinatarajiwa kukamilika Novemba, mwaka huu katika ngazi ya taifa.

  Taarifa ya tamko la CCM kuhusu chaguzi za jumuiya zake lililotolewa kwa vyombo vya habari jana na kusainiwa na Naibu Katibu Mkuu, Kapteni George Mkuchika, lilisema baadhi ya wagombea wanakwenda mikoani na wilayani kuwarubuni wajumbe.

  Aidha ilielezwa kwamba wengine wanatuma wapambe na kuwagharimia kwa kila kitu kuzunguka nchini kote kwa niaba yao kwenda kuwanadi, kugawa bahasha au takrima kwa wajumbe.

  Kapteni Mkuchika aliongeza kuwa wagombea wengine wanapakana matope, mambo ambayo ni kinyume kabisa cha maadili ya Chama hicho.

  ``Sisi katika CCM tunaamini kwamba viongozi wazuri na watakaoweza kukisaidia chama ni wale tu watakaochaguliwa bila ya rushwa, kwani viongozi waliochaguliwa kwa njia hiyo hawawezi kukisaidia chama kwa kuwa hawawezi kukemea rushwa na badala yake wenyewe watakuwa sehemu ya tatizo kwa jumuiya zao na chama kwa jumla,`` aliongeza Kapteni Mkuchika.

  Kufuatia hali hiyo, alisema chama hicho kimewapiga marufuku wagombea wote wa nafasi za uongozi katika jumuiya zake na wapambe wao kuzunguka mikoani na wilayani kujinadi au kumnadi mgombea yeyote, pamoja na kuacha kujihusisha na vitendo vya rushwa ya aina yoyote.

  Pia CCM kimewapiga marufuku wagombea kutoa takrima au bahasha kwa wajumbe, kutumia lugha za kupakana matope katika kipindi chote cha mchakato hadi uchaguzi wenyewe na kuonya kuwa yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo vilivyo kinyume cha maadili ya chama, uteuzi wake utatenguliwa wakati wowote.

  Pia CCM imeziagiza kamati za maadili za chama hicho katika ngazi zote kuchukua hatua mara moja na bila ya kuchelewa kwa watakaaobainika kujihusisha na vitendo hivyo.

  * SOURCE: Nipashe
   
 9. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #9
  Sep 5, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  wana kazi kweli kweli
   
 10. M

  Mtu Kwao JF-Expert Member

  #10
  Sep 5, 2008
  Joined: Jan 15, 2008
  Messages: 258
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mmh...... Eti wakatae takrima,wana kichaa au?maana hawa siku wakiacha takrima na chama ndio kitakuwa kimekufa kabisa.
   
 11. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #11
  Sep 5, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Rais mwenyewe aliingia kwa takrima, sasa ndio wawe hao wa jumuia za chama?

  Dawa ni kuunda chombo huru ambacho kitashughulikia rushwa Tanzania. Kutegemea fadhila za rais, tusitegemee kitu. Wataweka ndani watu wadogo huku vigogo wanaendelea kuchukua madaraka kwa kutumia pesa zao.
   
 12. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #12
  Sep 5, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,694
  Trophy Points: 280
  Lakini hata JK nimemgundua kwamba zile njia zake haramu alizoingilia na kuukwa ukulu,leo anajaribu pia kuzizuia na si kwa kuwa ana mapenzi mema na nchi,no just because hataki wengine watumie huo mwanya kumletea balaa uchaguzi utakapowadia.Sijui ni jambo lipi huyu mkuu atakalolifanya kwa maslahi ya taifa bila kutanguliza maslahi yake.Lol!
   
 13. M

  Masatu JF-Expert Member

  #13
  Sep 5, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Rushwa haina chama ni tatizo la kitaifa ipo Chadema, CUF, Chausta nk
   
 14. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #14
  Sep 5, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Masatu,

  Nakubaliana na wewe juu ya hilo. Hata sisi wana JF hapa, wala na watoa rushwa wapo wengi tu kwi kwi kwi!!

  Tunahitaji chombo huru na makini kupambana na hili janga kubwa la taifa.
   
 15. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #15
  Sep 5, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  In what form?CCM rushwa yao wanaitangaaza nje nje na bila hata aibu wameibariki kwa jina la TAKRIMA!
   
 16. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #16
  Sep 5, 2008
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Shenzi wakubwa hawa, si wenyewe ndo walioianzisha na kuipitisha. Shenzi sana kwa unafiki.
   
 17. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #17
  Sep 5, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,694
  Trophy Points: 280

  Umeshaachana na hoja.Duh!
   
 18. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #18
  Sep 5, 2008
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,859
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 160
  Shenzi wakubwa, kama kweli wanania hiyo bungeni hawapajui? Waende wakaifute kupitia mswada. Si wapo wengi bungeni? Tofauti na hivyo ni unafiki na uzandiki mkubwa.
   
 19. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #19
  Sep 5, 2008
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Ni kweli lakini CCM haina utashi wa kisiasa kupigana dhidi ya rushwa, si unakumbuka utashi wa Mkapa na Tume ya Warioba? Hatujaona kitu hata sasa badala yake hata Mkapa aliyeunda tume katuchukulia Kiwira Coal Mine kwa bei ya bure.

  Chombo hicho huru kiundwe na nani na kwa manufaa ya nani? TAKUKURU ni ya nani na nani anatakiwa kuipa meno? Na ubutu TAKUKURU unasababishwa na nani?
   
 20. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #20
  Sep 5, 2008
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,723
  Likes Received: 1,218
  Trophy Points: 280
  Hiki chama cha mataahira wenye vyeti vya elimu ya darasani watakosa kutumia takrima? Litakuwa tukio lenye kustahili nafasi katika kitabu cha record cha guiness.
   
Loading...