CCM waombeni radhi Watanzania

CCM waombeni radhi Watanzania

Hapana.

Si kila inapotajwa CCM basi lazima na CHADEMA iwepo.

CCM inapotajwa kama ndo chama ambacho kimeunda serikali zote za Tanzania hapo CHADEMA haipo.

Acheni kiburi. Waombeni radhi Watanzania.

CHADEMA hawajasababisha hali kama hii kwenye video hapa chini huku wakiukumbatia ufisadi.


Chadema wamesababisha hii hali kwa kuwadanganya Watanzania kwamba wanapinga ufisadi huku wakiukumbatia kwa kumchukua fisadi mkuu waliyekuwa wakimsema na baadaye kumfanya kuwa mgombea wao wanafiki wakubwa malengo yao ni maslahi binafsi
 
Nyani Ngabu, mimi namuomba Raisi John Pombe Magufuli apate ujasiri, kwa niaba yake binafsi na kwa niaba ya CCM, awaombe radhi Watanzania halafu ndio sote tukae pamoja tushirikiane kulijenga upya taifa hili. Akifanya hivyo nitaamini kwamba kweli sasa tunafungua ukurasa mpya kwa sababu pamoja na jitihada anazofanya kujiweka mbali na tawala zote zilizopita kabla yake, hawezi kukwepa ushiriki wake katika kutufikisha hapa tulipo kama taifa. Lazima kwanza akiri ushiriki wake, atuombe radhi na ndipo hapo ataweza kutushawishi kwamba kazaliwa upya na hivyo kutuondolea shaka katika kumuunga mkono ili tufanye kazi pamoja.

Hatujawahi kuwa na Mkuu wa nchi, Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Wizara, Mkuu wa Chombo chochote cha dola (Jeshi, Polisi, Usalama wa Taifa), Mkuu wa Shirika lolote la serikali, Mkuu wa Mahakama (Jaji Mkuu), Mkuu wa Bunge (Spika), Mkuu wa taasisi yoyote ya serikali n.k. ambaye kigezo kilichotumika kumteua si U-CCM wake. Machafu yote ndani ya nchi hii yalipandwa, yakachanua, yakalelewa, yakakomaa chini ya uongozi wa wote niliowataja hapo juu na ndio wahusika wakuu. Magufuli, kwa niaba ya CCM, pia aliombe radhi taifa kwa kukosa katiba iliyotokana na maoni ya wananchi wake kwa shinikizo la CCM.

Si rahisi kwa mtu mchafu kuongoza mapambano dhidi ya uchafu mpaka kwanza ameoga na kuwa msafi na asipofanya hivyo lazima wasafi watasita kumuunga mkono. Na ndivyo ilivyo kwa Magufuli, aanze kwa kutubu na ingawa inawezekana ana nia ya dhati ya kimageuzi lakini shati lake la njano, linalohitaji maji na sabuni, linamuumbua.
 
Chadema wamesababisha hii hali kwa kuwadanganya Watanzania kwamba wanapinga ufisadi huku wakiukumbatia kwa kumchukua fisadi mkuu waliyekuwa wakimsema na baadaye kumfanya kuwa mgombea wao wanafiki wakubwa malengo yao ni maslahi binafsi

Sasa kudanganya kwa CHADEMA ndo kumesababisha hawa wamama kulala chini?

 
Ndiyo maana wasingedanganya wangeshinda hivyo wangetengeneza vitanda akina mama wasingelala chini

Wangeshinda uchaguzi gani wakati tume ya uchaguzi ya CCM ndo ilikuwa inaendesha uchaguzi?

Hebu acha kujitoa fahamu wewe.

Halafu kwa nini hujajibu swali langu?

CHADEMA ndo sababu ya watoto kukaa chini na wamama kulala chini?
 
Hiki Chama kimeshazeeka sasa, hakijaleta manufaa yenye kudhihilika kwa wananchi wake na badala yake kina longolongo nyingi sana. Tunashuhudia kwa baadhi ya viongozi wanaingia katika ngazi mbalimbali na kuanza kutafuta mitaji ya kuendesha biashara zao na hawawatumikii wananchi ipasavyo. Hii nchi imeshanuka kwa uozo wa chama chenye kung'ang'ania madaraka.
 
Wangeshinda uchaguzi gani wakati tume ya uchaguzi ya CCM ndo ilikuwa inaendesha uchaguzi?

Hebu acha kujitoa fahamu wewe.

Halafu kwa nini hujajibu swali langu?

CHADEMA ndo sababu ya watoto kukaa chini na wamama kulala chini?
Kwani mlivyoshinda ubunge majimbo mengi tu ilikuwa ni tume ya Chadema au ccm na anayejitoa fahamu ni mm au wewe? Wa kukaya acha hizo
 
Kwani mlivyoshinda ubunge majimbo mengi tu ilikuwa ni tume ya Chadema au ccm na anayejitoa fahamu ni mm au wewe? Wa kukaya acha hizo

Ubunge na urais upi wenye hadhi na thamani zaidi?
 
Tokea tupate uhuru nchi imekuwa ikiongozwa na serikali za chama kimoja tu, CCM [TANU].

Katika hii miezi mitatu ya utawala wa Magufuli tumeshuhudia uozo wa aina nyingi ukifunuliwa.

Nina imani kuna uozo mwingi zaidi ya huo ambao tumekwishauona.

Nisiseme mengi sana maana itakuwa ni kurudia yaleyale ambayo yamekwishasemwa huko nyuma.

Ila ningependa kutoa rai kwa Chama Chama Mapinduzi kiwaombe radhi Watanzania.

Kiwaombe radhi Watanzania kwa kushindwa kuwaletea maendeleo ambayo kwa kweli yalikuwa ndani kabisa ya uwezo wake.

Haiingii akilini katika karne ya 21 bado tuwe na wagonjwa wanaolala chini au watoto wanaosoma huku wamekaa chini kwenye mavumbi huku watu wachache wakiuhujumu uchumi na kujineemesha kupitia migongo ya watu maskini.

Haiingii akilini katika karne ya 21 umeme na maji ya uhakika zikawa ni huduma za anasa wakati ni huduma za msingi na kwa wakati huo huo kna mabilionea walioupata utajiri wao kupitia migongo ya walalahoi.

Hamjachelewa, waombeni radhi Watanzania kwani wanastahili kuombwa radhi kwa kushindwa kuwapa kile wanachokistahili.

Acheni kiburi, acheni ufedhuli, kuweni waungwana, ombeni radhi kwa Watanzania.
bila kukamata viongozi waliosababisha hujuma hizo ni kazi bure , hebu angalia wale wazee waliodakwa kwenye sakata la TRL ni wenyewe kweli wale ?
 
Tena msemaji anatakiwa awe Jk, akiambatana na Mkwapa, na mzee ruksa. Kila mmoja aombe msamaha
 
Tokea tupate uhuru nchi imekuwa ikiongozwa na serikali za chama kimoja tu, CCM [TANU].

Katika hii miezi mitatu ya utawala wa Magufuli tumeshuhudia uozo wa aina nyingi ukifunuliwa.

Nina imani kuna uozo mwingi zaidi ya huo ambao tumekwishauona.

Nisiseme mengi sana maana itakuwa ni kurudia yaleyale ambayo yamekwishasemwa huko nyuma.

Ila ningependa kutoa rai kwa Chama Chama Mapinduzi kiwaombe radhi Watanzania.

Kiwaombe radhi Watanzania kwa kushindwa kuwaletea maendeleo ambayo kwa kweli yalikuwa ndani kabisa ya uwezo wake.

Haiingii akilini katika karne ya 21 bado tuwe na wagonjwa wanaolala chini au watoto wanaosoma huku wamekaa chini kwenye mavumbi huku watu wachache wakiuhujumu uchumi na kujineemesha kupitia migongo ya watu maskini.

Haiingii akilini katika karne ya 21 umeme na maji ya uhakika zikawa ni huduma za anasa wakati ni huduma za msingi na kwa wakati huo huo kna mabilionea walioupata utajiri wao kupitia migongo ya walalahoi.

Hamjachelewa, waombeni radhi Watanzania kwani wanastahili kuombwa radhi kwa kushindwa kuwapa kile wanachokistahili.

Acheni kiburi, acheni ufedhuli, kuweni waungwana, ombeni radhi kwa Watanzania.
Umenena vema mkuu. Lakini kabla ya ccm kuomba radhi, wote waliohama ccm hasa kipindi cha serikali ya awamu ya nne warudisheni ccm. Hatuwezi kuomba radhi watz pamoja na wale ambao wana sehemu katika matatizo ambayo ccm imewasababishia watz. Baadhi yao kabla ya kuja kwenu, wakiwa ccm, mliwashutumu sana kwa ufisadi uliowanyima watz maendeleo.

Mnataka tuwaombe watz msamaha, wana ccm wote waliojilipua warudisheni ccm chini ya ulinzi wa polisi, mtukabidhi halafu........ Kinyume cha hapo ninyi mnatakiwa muwaombe watz msamaha kwa siasa za kilaghai za kubadili gia angani.

Kwa dhamira ya DHATI ya jpm ya kuwaletea watz maendeleo, watz wameisha isamehe ccm. Huoni furaha waliyonayo? Wamejaa matumaini. Wanasema yaliyopita si ndwele..........malizia sasa.
 
Umenena vema mkuu. Lakini kabla ya ccm kuomba radhi, wote waliohama ccm hasa kipindi cha serikali ya awamu ya nne warudisheni ccm.

"Warudisheni CCM"? Akina nani hao na hilo linahusiana nini na kushindwa kwa serikali za CCM kuwaletea Watanzania maendeleo?
 
Kama una grievances zako dhidi ya CHADEMA nakushauri uwaanzishie mada yao maalumu.

Hii nimeianzisha kwa makusudi na inaihusu CCM.

CHADEMA haijawahi kuongoza nchi. Hapa tunajadili chama ambacho kimekuwa madarakani tokea tupate uhuru..
Hapa mada inahusu msamaha kwa hiyo nipo ndani ya mada.

Kwa nini chadema ndio wanapaswa kuomba msamaha?

Kulikuwa na kilio kikubwa sana kuhusu ufisadi nchini lakini wananchi awakuonekana kujali wakiamini ndio maisha ya watanzania yameumbwa hivyo.

Chadema baada ya kulaumu sana jinsi watanzania walivyo wajinga kwa kuutazama ufisadi na kuendelea kuchagua mafisadi wakaamua wazunguke nchi nzima kutoa elimu juu ya ubaya wa ufisadi na namna mafisadi walivyoifirisi hii nchi na kufanya watu wawe masikini wa kutupwa.

Awakushia hapo wakayataja mafisadi yaliyotufirisi yakiongozwa na Lowassa pamoja na best yake Rostam aziz na wakatoa maneno mengi ikiwemo kutoa ushahidi walionao juu ya ufisadi wa lowassa.

Wananchi baada ya kuwasikiliza wakawaelewa sana tena sana na wakawaunga mkono mpaka wakamwaga damu zao na wengine kuacha mayatima wakipambana na ufisadi wa kina lowassa.

Mara ghafla ikafika kipindi cha uchaguzi wananchi wakijiandaa kuyaondoa mafisadi yanaotaka urais. Mambo yakawa kinyume ccm wakamkata fisadi na chadema wakampokea fisadi huyo na wafadhili wake kisha wakarudi kwa wananchi na kuwambia yule fisadi lowassa waliowaambia anatakiwa kuchomwa moto ndio wamchague awe Rais ili awaletee mabadiliko ya nchi ya maziwa na asali. Tena wakasema wasipomchagua lowassa basi hakuna tena mabadiliko mpaka mwisho wa dunia maana mabadiliko ni lowassa na lowasa ni mabadiliko.


Ata nikimuuliza mpya wangu Nguruvi3 atuambie kwa nini Chadema awatakiwi kutuomba msamaha kwa utapeli waliotufanyia?
 
Hapa mada inahusu msamaha kwa hiyo nipo ndani ya mada.

Hapana.

Mada inahusu wito kwa CCM kuwaomba radhi Watanzania.

Ni mada mahsusi kabisa.

Kwa nini chadema ndio wanapaswa kuomba msamaha?

Sina raghba na radhi ya CHADEMA. Hawaongozi serikali. Hawajawahi kuongoza serikali.

Kulikuwa na kilio kikubwa sana kuhusu ufisadi nchini lakini wananchi awakuonekana kujali wakiamini ndio maisha ya watanzania yameumbwa hivyo.

Chadema baada ya kulaumu sana jinsi watanzania walivyo wajinga kwa kuutazama ufisadi na kuendelea kuchagua mafisadi wakaamua wazunguke nchi nzima kutoa elimu juu ya ubaya wa ufisadi na namna mafisadi walivyoifirisi hii nchi na kufanya watu wawe masikini wa kutupwa.

Awakushia hapo wakayataja mafisadi yaliyotufirisi yakiongozwa na Lowassa pamoja na best yake Rostam aziz na wakatoa maneno mengi ikiwemo kutoa ushahidi walionao juu ya ufisadi wa lowassa.

Wananchi baada ya kuwasikiliza wakawaelewa sana tena sana na wakawaunga mkono mpaka wakamwaga damu zao na wengine kuacha mayatima wakipambana na ufisadi wa kina lowassa.

Mara ghafla ikafika kipindi cha uchaguzi wananchi wakijiandaa kuyaondoa mafisadi yanaotaka urais. Mambo yakawa kinyume ccm wakamkata fisadi na chadema wakampokea fisadi huyo na wafadhili wake kisha wakarudi kwa wananchi na kuwambia yule fisadi lowassa waliowaambia anatakiwa kuchomwa moto ndio wamchague awe Rais ili awaletee mabadiliko ya nchi ya maziwa na asali. Tena wakasema wasipomchagua lowassa basi hakuna tena mabadiliko mpaka mwisho wa dunia maana mabadiliko ni lowassa na lowasa ni mabadiliko.


Ata nikimuuliza mpya wangu Nguruvi3 atuambie kwa nini Chadema awatakiwi kutuomba msamaha kwa utapeli waliotufanyia?

Hayo yanahusikaje na CCM kushindwa kuwaletewa Watanzania maendeleo ya kuridhisha?
 
"Warudisheni CCM"? Akina nani hao na hilo linahusiana nini na kushindwa kwa serikali za CCM kuwaletea Watanzania maendeleo?
Come on Nyani. Akina nani? Unauliza jibu? Ok lowassa, mgana, sumaye, kingunge, guninita, medeye na wengineo. Warudisheni hawa kwani wanasehemu katika matatizo ya watz. Tunaombaje wakiwa huko. Basi nanyi muwaombe msamaha watz. Nyie ni ccm 'b'. Nyani usijitoe ufahamu, mlikuwa na uhalali wa kuwataka ccm wawaombe watz kabla ya kubadili.gia angani. Mlipokuwa na super star Dr. Slaa. Leo hii hamna makali tena, ninyi ni sawa na joka la kibisa.
 
Back
Top Bottom