Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,499
- 145,893
Tokea tupate uhuru nchi imekuwa ikiongozwa na serikali za chama kimoja tu, CCM [TANU].
Katika hii miezi mitatu ya utawala wa Magufuli tumeshuhudia uozo wa aina nyingi ukifunuliwa.
Nina imani kuna uozo mwingi zaidi ya huo ambao tumekwishauona.
Nisiseme mengi sana maana itakuwa ni kurudia yaleyale ambayo yamekwishasemwa huko nyuma.
Ila ningependa kutoa rai kwa Chama Chama Mapinduzi kiwaombe radhi Watanzania.
Kiwaombe radhi Watanzania kwa kushindwa kuwaletea maendeleo ambayo kwa kweli yalikuwa ndani kabisa ya uwezo wake.
Haiingii akilini katika karne ya 21 bado tuwe na wagonjwa wanaolala chini au watoto wanaosoma huku wamekaa chini kwenye mavumbi huku watu wachache wakiuhujumu uchumi na kujineemesha kupitia migongo ya watu maskini.
Haiingii akilini katika karne ya 21 umeme na maji ya uhakika zikawa ni huduma za anasa wakati ni huduma za msingi na kwa wakati huo huo kna mabilionea walioupata utajiri wao kupitia migongo ya walalahoi.
Hamjachelewa, waombeni radhi Watanzania kwani wanastahili kuombwa radhi kwa kushindwa kuwapa kile wanachokistahili.
Acheni kiburi, acheni ufedhuli, kuweni waungwana, ombeni radhi kwa Watanzania.