CCM waombeni radhi Watanzania

CCM waombeni radhi Watanzania

Hata mimi nawashangaa wana ccm eti leo wanashinda mitandaoni wakimnanga jk kuwa alikuwa mzembe wakati yupo madarakani walikuwa wakimkenulia meno

Na walikuwa wa kwanza kumrushia mawe Mnyika aliposema Kikwete ni dhaifu. Leo serikali ya awamu ya 5 miezi mitatu sasa inajaribu kurekebisha madhaifu ya Kikwete. Kuna kipindi ninawaona wanaccm kama si watanzania halisi. Agenda yao ni ya nchi ni vitu viwili tofauti.
 
Na walikuwa wa kwanza kumrushia mawe Mnyika aliposema Kikwete ni dhaifu. Leo serikali ya awamu ya 5 miezi mitatu sasa inajaribu kurekebisha madhaifu ya Kikwete. Kuna kipindi ninawaona wanaccm kama si watanzania halisi. Agenda yao ni ya nchi ni vitu viwili tofauti.
Ccm ni machumia tumbo na ni sawa na mamba awapo mtoni
 
Tokea tupate uhuru nchi imekuwa ikiongozwa na serikali za chama kimoja tu, CCM [TANU].

Katika hii miezi mitatu ya utawala wa Magufuli tumeshuhudia uozo wa aina nyingi ukifunuliwa.

Nina imani kuna uozo mwingi zaidi ya huo ambao tumekwishauona.

Nisiseme mengi sana maana itakuwa ni kurudia yaleyale ambayo yamekwishasemwa huko nyuma.

Ila ningependa kutoa rai kwa Chama Chama Mapinduzi kiwaombe radhi Watanzania.

Kiwaombe radhi Watanzania kwa kushindwa kuwaletea maendeleo ambayo kwa kweli yalikuwa ndani kabisa ya uwezo wake.

Haiingii akilini katika karne ya 21 bado tuwe na wagonjwa wanaolala chini au watoto wanaosoma huku wamekaa chini kwenye mavumbi huku watu wachache wakiuhujumu uchumi na kujineemesha kupitia migongo ya watu maskini.

Haiingii akilini katika karne ya 21 umeme na maji ya uhakika zikawa ni huduma za anasa wakati ni huduma za msingi na kwa wakati huo huo kna mabilionea walioupata utajiri wao kupitia migongo ya walalahoi.

Hamjachelewa, waombeni radhi Watanzania kwani wanastahili kuombwa radhi kwa kushindwa kuwapa kile wanachokistahili.

Acheni kiburi, acheni ufedhuli, kuweni waungwana, ombeni radhi kwa Watanzania.
Why watuombe radhi why ujinga wetu wenyewe ndo umewaweka madarakani muda wote huo?
 
Vitendo dhidi ya maneno ndo njia sahihi ya kuwaomba radhi watanzania..Nadhani Magufuli ndo anachojaribu kukifanya kwa sasa
Nani alikuambia watanzania wanataka maendeleo? Sisi ccm kwanza maendeleo baadae,kama tungekuwa tunataka maendeleo kwa mfano 2010 tuliambiwa na Slaa kwamba atatoa elimu bure na cement itauzwa sh 5000 kama tutamchagua,ccm wakatuaminisha haiwezekani,na sisi kwa uzuzu wetu na kuupenda umasikini tukachangua ccm, 5 years after, we see dwe have started implementing the same tena tukitetea na kushangilia kwa nguvu zote,we are strnge people
 
Niajabu sana raisi nafika eneo anakuta mazingira anayo yajua nayalisha pigiwa sana kelele na wadau alafu anasema anatumbua majipu.Wana wadanganyika tunapiga makofi.Yaani mtu ana meza sumu alafu anaenda kunywa maziwa alafu mnampigia makofi kwa ametenda vyema
Hata Mzee wako akiacha ulevi utampigia makofi. Mtu hasifiwi kwa kufanya mabaya bali kuacha maovu na kutenda mema haijalishi alikuwa anayajua ama la.
 
Hapa mada inahusu msamaha kwa hiyo nipo ndani ya mada.

Kwa nini chadema ndio wanapaswa kuomba msamaha?

Kulikuwa na kilio kikubwa sana kuhusu ufisadi nchini lakini wananchi awakuonekana kujali wakiamini ndio maisha ya watanzania yameumbwa hivyo.

Chadema baada ya kulaumu sana jinsi watanzania walivyo wajinga kwa kuutazama ufisadi na kuendelea kuchagua mafisadi wakaamua wazunguke nchi nzima kutoa elimu juu ya ubaya wa ufisadi na namna mafisadi walivyoifirisi hii nchi na kufanya watu wawe masikini wa kutupwa.

Awakushia hapo wakayataja mafisadi yaliyotufirisi yakiongozwa na Lowassa pamoja na best yake Rostam aziz na wakatoa maneno mengi ikiwemo kutoa ushahidi walionao juu ya ufisadi wa lowassa.

Wananchi baada ya kuwasikiliza wakawaelewa sana tena sana na wakawaunga mkono mpaka wakamwaga damu zao na wengine kuacha mayatima wakipambana na ufisadi wa kina lowassa.

Mara ghafla ikafika kipindi cha uchaguzi wananchi wakijiandaa kuyaondoa mafisadi yanaotaka urais. Mambo yakawa kinyume ccm wakamkata fisadi na chadema wakampokea fisadi huyo na wafadhili wake kisha wakarudi kwa wananchi na kuwambia yule fisadi lowassa waliowaambia anatakiwa kuchomwa moto ndio wamchague awe Rais ili awaletee mabadiliko ya nchi ya maziwa na asali. Tena wakasema wasipomchagua lowassa basi hakuna tena mabadiliko mpaka mwisho wa dunia maana mabadiliko ni lowassa na lowasa ni mabadiliko.


Ata nikimuuliza mpya wangu Nguruvi3 atuambie kwa nini Chadema awatakiwi kutuomba msamaha kwa utapeli waliotufanyia?
Mpwa wangu, hapa kuna hoja mbili tofauti

Kuna tatizo la kujibu hoja kwa hoja nje ya hoja linalojitokeza.
Na hili limeanzishwa na L45 baada ya mmoja kupata uhakika leo. Anyways

Hoja ya bandiko ni ccm kuomba radhi kama alivyosema NN.

Sababu za kuombwa radhi ni ukweli kuwa CCM imetawala nusuru karne, na hakuna mtu wingine aliyewahi kuishi magogoni bila njano na kijani yenye jembe na nyundo

Hoja yake ipo katika msingi kuwa uchafu unaoonekana kama huu wa kupima mafuta kwa vijiti au mboni za macho, makontena kupotea yakipokelewa bandarini, wanyama kupanda first class wakielekea majuu, mchanga kuchujwa ulaya n.k. ni matokeo ya sera za CCM

Mh Nape alizunguka nchi nzima akitueleza mambo ni mazuri sana.
Mwaka huu kasema nchi ilifikia pabaya.

Huyu ni yule yule wa CCM akitumikia CCM ileile aliyoikuta.
Ndio maana NN anasema, hapana inatosha, hata kuomba radhi ni uungwana.

Kuna hoja ya mpwa wangu Judi wa Kishua kuwa Chadema nao waombe radhi

Bila kuwa na msingi wa kwanini waombe radhi na kwa madhara yapi, haionekani kama hoja inajibu hoja ya CCM kuomba radhi.

Hizi ni hoja mbili tofauti kabisa na wala moja haijibu nyingine

Ningekushauri mpwa, anzisha uzi na hakika naomba mwaliko ili tujumuike.

Kuijadili hoja yako hapa ni sawa na kuzungumzia chips za mihogo kwa mada ya mtairi ya magari

Shime mpwa anzisha uzi nipo bega kwa bega nawe katika kuchangia, huu wa NN tusi u-dilute kwa kuchomeka mengine.
 
CCM lini waliwahi kusema kwamba wamekosea!?

Kikwete walikuwa wanamtetea hapa masaa 24 ila alivyoondoka ndio wakaanza kujifanya wanaona mapungufu yake.... Lakini bado hawataki kuonba radhi

FaizaFoxy mpaka kesho haoni mapungufu ya mkwere na natakuambia hakuna uongozi bora kama wa msoga
 
Siyo waombe radhi tu bali wajiuzulu wote na kujiondoa kwenye siasa. Bora wawe majangili waziwazi tujue moja
 
Siyo waombe radhi tu bali wajiuzulu wote na kujiondoa kwenye siasa. Bora wawe majangili waziwazi tujue moja

Ccm kwa baadhi ya watu humu JF imekuwa kama imani ya kidini hivi. Wana macho mazima lakini watakuambia nyekundu ni nyeupe. Kuna hali fulani ya kiubwetere naiona ndani yao. We need to pray for seriously.
 
Ukiangalia historia, kuna CCM ya 1977-1991 na CCM ya 1991 hadi sasa. CCM ya kwanza ilikuwa na falsafa ya Ujamaa na Kujitegemea chini ya misingi ya Azimio la Arusha na ililenga kujenga jamii ya watu sawa (bila matabaka) na kuondoa aina zote za unyonyaji na ufisadi. Hii CCM ilijikita katika ustawi wa walalahoi (wakulima na wafanyakazi). Baada ya Azimio la Zanzibar la Februari 1991, CCM ikabadilika nyuzi 180! Chama kikabadili misingi yake yote ya kifalsafa na kidira. Kikaachana na kujitambulisha kama chama cha wakulima na wafanyakazi na badala yake kikakumbatia wawekezaji na matajiri uchwara; wezi; majangili; na 'wazungu' wa unga. Ufisadi ukarasimishwa rasmi katika chaguzi na miamala ya kiserikali. Kwa sera za CCM ya sasa, huduma kama afya na elimu bora ni bidhaa kwa ajili ya wenye pesa tu (CCM haina mpango na walalahoi). Pia ni kila mtu na lwake kwenye na ajira na hifadhi ya jamii! Ukilalamikia huduma mbovu unaitwa mwenye uvivu wa kufikiri! Kinachotakiwa hapa ni CCM kuomba msamahau au wewe kuinyima kura yako?
 
CCM hawana ustaarabu wa kuomba misamaha,hata wakiharibu wakiambiwa wawajibike utasikia "SIJIUZURU NG'O" "PATACHIMBIKA" "NIKIJIUZURU NCHI ITATETEMEKA HII"
 
Kama Alivyofanya Lowassa sio?
Mbona katibu wako mkuu mwenye kumiliki meli inayowarahisishia usafiri umemfunika uso ukaacha makalio? Au hilo nalo geni kwako? Meli yake haikukamatwa na pembe Hongkong mkauchubua na kuupotezea uzi ule. Uwe na kumbukumbu basi uache mahaba niue kwa hao wanaokusaidia kwenda chooni. Waacheni tembo waishi ninyi ccm!!!!!!
 
Back
Top Bottom