CCM waombeni radhi Watanzania

CCM waombeni radhi Watanzania

CCM ni nani?​
Ni wale waliotengeneza fulana na kofia na kuzigawa nchi nzima zikiwa zimeandikwa CHAGUA CCM CHAGUA MAGUFULI. CCM ni wale wanaoamini kwamba bila ya chama chao hakuna Tanzania. CCM ni wale wanaobwatuka bwatu bila sababu kwamba nchi hii Ufisadi ni Lowassa na Bila Lowassa hakutakuwa na Ufisadi. Hao ni ndiyo CCM watu wa ghiliba, watumia dola kubaki madarakani!!
 
Tokea tupate uhuru nchi imekuwa ikiongozwa na serikali za chama kimoja tu, CCM [TANU].

Katika hii miezi mitatu ya utawala wa Magufuli tumeshuhudia uozo wa aina nyingi ukifunuliwa.

Nina imani kuna uozo mwingi zaidi ya huo ambao tumekwishauona.

Nisiseme mengi sana maana itakuwa ni kurudia yaleyale ambayo yamekwishasemwa huko nyuma.

Ila ningependa kutoa rai kwa Chama Chama Mapinduzi kiwaombe radhi Watanzania.

Kiwaombe radhi Watanzania kwa kushindwa kuwaletea maendeleo ambayo kwa kweli yalikuwa ndani kabisa ya uwezo wake.

Haiingii akilini katika karne ya 21 bado tuwe na wagonjwa wanaolala chini au watoto wanaosoma huku wamekaa chini kwenye mavumbi huku watu wachache wakiuhujumu uchumi na kujineemesha kupitia migongo ya watu maskini.

Haiingii akilini katika karne ya 21 umeme na maji ya uhakika zikawa ni huduma za anasa wakati ni huduma za msingi na kwa wakati huo huo kna mabilionea walioupata utajiri wao kupitia migongo ya walalahoi.

Hamjachelewa, waombeni radhi Watanzania kwani wanastahili kuombwa radhi kwa kushindwa kuwapa kile wanachokistahili.

Acheni kiburi, acheni ufedhuli, kuweni waungwana, ombeni radhi kwa Watanzania.

He he heee! Ngosha bana! Naona umewamisi ngómbe wa huku usukumani.
Unaishauri CCM hii hii ya kina Nape? Labda kwa vile hujawa hapa nchini kwa kitambo.
 
Ni wale waliotengeneza fulana na kofia na kuzigawa nchi nzima zikiwa zimeandikwa CHAGUA CCM CHAGUA MAGUFULI. CCM ni wale wanaoamini kwamba bila ya chama chao hakuna Tanzania. CCM ni wale wanaobwatuka bwatu bila sababu kwamba nchi hii Ufisadi ni Lowassa na Bila Lowassa hakutakuwa na Ufisadi. Hao ni ndiyo CCM watu wa ghiliba, watumia dola kubaki madarakani!!

Rejea kusoma mada husika kuanzia mwanzo na uisome yote na siyo juju juu tu na kukimbilia kuandika, halafu ndiyo uje unijibu kwamba CCM anayetakiwa aombe radhi ni nani?
 
magufuli anajarbu kutupooza machungu kwa jinsi chama chake kilivyotutenda lkn mda utazungumza
 
Rejea kusoma mada husika kuanzia mwanzo na uisome yote na siyo juju juu tu na kukimbilia kuandika, halafu ndiyo uje unijibu kwamba CCM anayetakiwa aombe radhi ni nani?
Kwani mnaposema kwamba CCM inaongoza mnamaanisha nini?
 
kwa niaba ya CCM tunawaomba radhi watanzania...
tunawaomba radhi mpaka leo hii hakuna vita vya kikabila, vita vya kidini, tunawaomba radhi mpaka leo hii mna uhuru wa kutoa maoni yenu...

tunawaomba radhi watanzania mtusamehe sana
 
He he heee! Ngosha bana! Naona umewamisi ngómbe wa huku usukumani.
Unaishauri CCM hii hii ya kina Nape? Labda kwa vile hujawa hapa nchini kwa kitambo.

Katika ujinga wangu nadhani labda walau wanaweza hata kutuomba radhi Watanzania kwa yale yote waliyoyafanya kuruhusu uwepo wa hali iliyopo.

Kwani Magufuli aliposema hii ndo Tanzania tuliyoikuta [sina hakika na nukuu halisi] anamaanisha nini?
 
Wanaotakiwa kuomba radhi ni CHADEMA wametunyima fursa ya mabadiliko ya kweli kwa kuuza chama kwa mafisadi. Pengine leo hii tungekuwa tunaongea mengine, ila tunashukuru Magufuli anaonyesha nia njema ya kuturudisha kwenye mstari.

Samahani vibaraka wa team Lowassa.
 
Ngabu
Upepo wa Magufuli huku Bongo ni mkali sana kwa sasa. Ila ninachojua ni kwamba Magufuli hawezi kuwa juu ya CCM. CCM is full of illusion and acrobatics. Ninaifahamu CCM kwa kiasi chake.
 
Miaka nenda rudi ya ufisadi chini ya CCM unahusiana nini na CHADEMA?
 
Halafu kama umestukia Magufuli ni kama anamrushia madongo Kikwete....kwenye hotuba ya leo.
Kuna vijana 46 nilisoma kwenye mitandao ambao walisaidia CCM kusonga mbele na bado wapo wengine wamejiunga JF Mei -Sept 2015 waulize yote wanajua kila kitu siwataji sababu mimi si bingwa wa majibizano na ni mzee nahitaji kula asprini kila baada ya muda asubuhi nusu, mchana nusu na jioni nusu.
 
Ngabu
Upepo wa Magufuli huku Bongo ni mkali sana kwa sasa. Ila ninachojua ni kwamba Magufuli hawezi kuwa juu ya CCM. CCM is full of illusion and acrobatics. Ninaifahamu CCM kwa kiasi chake.

Hilo hata mimi nalifahamu na ndo maana nasita kuamini kama kweli majipu yote yatatumbuliwa.

Kwanza tatizo wala si majipu. Tatizo ni saratani.
 
Mkuu hapa umeongea point ila ngoja uone ujinga wa baadhi ya watu hapa watavyokusakama...
 
Kuomba radhi kutakua na maana kama yale yanayotia kinyaa yakiweza kutatuliwa for good...
Magufuli leo anaonekana kama vile haamini why wamama wanalala chini Muhimbili
wakati ni nchi nzima wanalala chini
na wanafunzi wanakaa chini nchi nzima

na miaka kumi from now utakuja niambia tatizo halijaisha....
 
Back
Top Bottom