Mwalimu Makini
Member
- Dec 5, 2009
- 65
- 23
Wakuu heshima mbele.
Ninaleta habari kutoka katika uwanja wa mapambano kule Igunga ambako CCM, CHADEMA na CUF wamekwishaanza mchakato wa kulitwaa jimbo kila mmoja kwa nmna yake.
Taarifa zilizotolewa leo hii asubuhi ya saa 4 ni kwamba mbunge mmoja wa CCM kutoka katika mkoa wa Singida wilaya ya Iramba ameruka kiunzi cha maafisa wa TAKUKURU kiaina baada ya kukamatwa live wakigawa rushwa kwa wapiga kura huko Igunga.
Mchezo ulikuwa ukifuatiliwa kwa karibu sana na makachero wa CHADEMA ambako siri ya eneo la tukio ilifahamika na hivyo mtego kuandaliwa mapema. Taarifa za kiinteligensia ziliwafikia makamanda wa CHADEMA kuhusu uwezekano wa kumkamata Mhe. Mbunge huyo na hivyo mbinu za kumweka mkononi kuwekwa.
TAKUKURU walipofika eneo la tukio waliwachukua wote waliohusika bila kumkamata Mhe. mbunge. Hata hivyo kikosi cha kufuatilia nyendo za watoa rushwa wa CCM kiko makini sana. Na kwa hakika pamoja na kulindwa sana lazima watashikwa.
Tutaendelea kujuzana