Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,900
- 944
IGUNGA: "TUMEAMUA KUACHANA NA VIKAO VYA CHINI YA MITI NA KWENYE STOO ZA PAMBA".
Mbunge wa Jimbo la Igunga Mhe Nicholaus George Ngassa ameendelea na Ziara ya Kikazi Jimboni, Ziara inayoambatana na zoezi la ujenzi wa Ofisi za Kata za Chama cha Mapinduzi (CCM). Akiongea na Wanachama wa CCM Kata ya Nguvumoja Leo tarehe 21 Mei, 2023 Mheshimiwa Ngassa (MB) amesema;
"... Ndugu zangu, tuendelee kushirikiana katika ujenzi wa Ofisi zetu za Kata... Igunga tuwe mfano kwenye kufanikisha jambo kubwa kama hili Nchini ambapo Kila Kata itakuwa na Ofisi ya Chama ya kisasa yenye ukumbi wa mikutano, Ofisi za Chama na Jumuiya zake na vibanda vya biashara (flames). Tufikirie kuachana na utamaduni uliozoeleka wakufanya vikao chini ya miti au kwenye stoo za pamba..."
Mheshimiwa Ngassa (MB) amehitimisha Ziara ya Kikazi ya Siku Tatu kwenye Kata Nne Jimboni na kurejea Dodoma kuendelea na Vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
"KAZI NA MAENDELEO"
Imetolewa na:
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Igunga