Mbunge Nicholaus Ngassa apongezwa na CCM wilaya ya Igunga kwa mchango wake ndani ya Chama Cha Mapinduzi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,165
1,026
📍 Igunga, Tabora

Habari Picha: Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Mbunge wa Jimbo la Igunga Mhe. Nicholaus George Ngassa akipokea cheti cha pongezi kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Igunga Ndg. Mafunda Temanywa kwa ajili ya kutambua mchango wa Mheshimiwa Mbunge kwenye ushiriki wa shughuli za uchaguzi wa Chama na Jumuiya zilizofanyika Mwaka 2022.

Ndg. Ngassa (MB) amewashukuru Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Igunga kwa kutambua mchango wake na kuahidi kuendelea kushirikiana na Chama cha Mapinduzi (CCM) katika kusimamia Miradi ya Maendeleo na kuhakikisha Fedha zinazotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan zinaleta tija kwa Wananchi wa Jimbo la Igunga.

Imetolewa na:
Katibu wa Mbunge
Jimbo la Igunga
21 Januari 2023
 

Attachments

  • indexmjiuop.jpg
    indexmjiuop.jpg
    108.6 KB · Views: 3

Similar Discussions

Back
Top Bottom