CCM wakamatwa na Rushwa Igunga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM wakamatwa na Rushwa Igunga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwalimu Makini, Aug 27, 2011.

 1. Mwalimu Makini

  Mwalimu Makini Member

  #1
  Aug 27, 2011
  Joined: Dec 5, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu heshima mbele.

  Ninaleta habari kutoka katika uwanja wa mapambano kule Igunga ambako CCM, CHADEMA na CUF wamekwishaanza mchakato wa kulitwaa jimbo kila mmoja kwa nmna yake.

  Taarifa zilizotolewa leo hii asubuhi ya saa 4 ni kwamba mbunge mmoja wa CCM kutoka katika mkoa wa Singida wilaya ya Iramba ameruka kiunzi cha maafisa wa TAKUKURU kiaina baada ya kukamatwa live wakigawa rushwa kwa wapiga kura huko Igunga.

  Mchezo ulikuwa ukifuatiliwa kwa karibu sana na makachero wa CHADEMA ambako siri ya eneo la tukio ilifahamika na hivyo mtego kuandaliwa mapema. Taarifa za kiinteligensia ziliwafikia makamanda wa CHADEMA kuhusu uwezekano wa kumkamata Mhe. Mbunge huyo na hivyo mbinu za kumweka mkononi kuwekwa.

  TAKUKURU walipofika eneo la tukio waliwachukua wote waliohusika bila kumkamata Mhe. mbunge. Hata hivyo kikosi cha kufuatilia nyendo za watoa rushwa wa CCM kiko makini sana. Na kwa hakika pamoja na kulindwa sana lazima watashikwa.

  Tutaendelea kujuzana
   
 2. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #2
  Aug 27, 2011
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Hii habari kuna ndugu yangu kanidokezea leo, nilifikiri ni uzushi.
  Naanza kupata picha kuwa ina ukweli.
   
 3. g

  gayo JF-Expert Member

  #3
  Aug 27, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 237
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Ufisadi ulizaliwa sisiemu na unalelewa na sisiemu na unazalia sisiemu na utakufa na sisiemu..
   
 4. a

  alute New Member

  #4
  Aug 27, 2011
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Atakua muweka hzina wachama.
   
 5. V

  Vatoi Member

  #5
  Aug 27, 2011
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hicho ki kifo cha mende, ccm are never smaart even for a single minute
   
 6. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #6
  Aug 27, 2011
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Atakuwa Mwigilu huyo.
   
 7. G

  GATZBY Member

  #7
  Aug 27, 2011
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Watahangaika sana lkn mwisho wao lazima ufike. Umefika wakati hata maDC wakihutubia wananchi wanatukana halafu wanauliza pembeni "Hivi nimetukana?" Kumbukumbu hawana tena.
   
 8. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #8
  Aug 27, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,519
  Likes Received: 1,689
  Trophy Points: 280
  Mtaje huyo mbunge vinginevyo huu utakuwa ni upupu
   
 9. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #9
  Aug 27, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  anaitwa mwigulu nchemba, na rushwa itampeleka pabaya, kama si duniani hata mbinguni.
   
 10. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #10
  Aug 27, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  huh...............mwisho wa siku utaskia hawana na hawakukamatwa na vithibitisho,picha la kihindi hili
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Aug 28, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  alikamatajwe live..?
   
 12. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #12
  Aug 28, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,969
  Likes Received: 2,963
  Trophy Points: 280
  Napata kichefuchefu kila nikisoma siasa za bongo.
  Waachieni wan igunga wamchague wanaemtaka.
   
 13. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #13
  Aug 28, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  That is the only remained weapon CCM have in hand.
   
 14. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #14
  Aug 28, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG][​IMG]
   
 15. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #15
  Aug 28, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Uongo na ukweli haviendi njia moja. Unaweza kumudu kusema uongo saa na wakati wote lakini huwezi ukawa yuleyule saa na wakati wote. Wakati wa kusema na kushuhudia uongo huwa tunazika karama ya utu tuliyopewa na Mungu. Lakini baada ya kushuhudia uwongo Mungu kwa huruma huturejeshea karama yetu na hapa ndio mateso yanaanza kwani nafsi zetu hukataa kubariki tuliyoyasema na kushuhudia kinyume na utu wetu. kwa sababu ya hilo huwa tunakosa ushujaa wa kushuhudia kwa macho ulimwengu unaotuzunguka ndivyo picha hii inavyotuambia kuhusu aliyoyasema Wassira katika mjadala kwenye kipindi cha TBC1. Saa ya uongo imepita sasa Wasira hawezi tena kuwa shujaa mbele za watu anaogopa hata kivuri chake na cha mpiga picha. Malipo ni hapa hapa duniani
   
 16. Ngaliba Dume

  Ngaliba Dume JF-Expert Member

  #16
  Aug 28, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,604
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  npo apa The Planet hotel...na hz ndo tetesi za mji mzma wa igunga...jamaa wameanza kumwaga fedha n balb?na jana kuna vijana wamekula hela ndefu toka makada wa CCM maeneo ya machinjio mapya njia ya kwenda nzega.,
   
 17. k

  kiloni JF-Expert Member

  #17
  Aug 28, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 575
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Bravo CDM endeleeni kufuatilia kusanyeni taarifa. Kumbukeni mahakama haziaminiki tena hao wezi wameshaangamiza kila mfumo. Kumbukeni Jaji Ramadhani alituambia alishaamuriwa atoe hukumu "wanavyotaka". My take; Our fate are on our hands.
   
 18. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #18
  Aug 28, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Kama ni kweli sitashangaa manake hawa jamaa wa kijani ni kawaida yao!
   
 19. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #19
  Aug 28, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Ngaliba sijakuelewa kwenye bold.
   
 20. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #20
  Aug 28, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ndio zao hizo. Mlungula kama kawa!
   
Loading...