Quinine,
Ninakuaminia sana kwa mambo ya Chadema. Ila kama mnataka kuwa tofauti na CCM, kama mnataka kuwa tofauti na POLISI WA TZ, kama mnataka kuwa tofauti na Kikwete, kama mnataka kuwa tofauti na Makamba nk basi ni LAZIMA muwe mnasikiliza wengine.
Mkulima kaweka POINT nzito na ushahidi wa waziwazi. Kuanza tu kurusha matusi ya mtu kupigwa na mkeo, inanikumbusha Makamba zaidi kuliko Quinine ninayemfahamu siku nyingi hapa. Tuwe tunatofautisha CCM aina ya akina MS na watu wanaokuja na POINT nzito.
Nimesoma na kufuatilia maneno ya Mkulima na kwa mbali naanza kukubaliana naye. Kwanza ni kweli CCM waliwazidi CDM kwenye Madiwani wa kuchaguliwa. Pili kama utakumbuka maneno ya Regia, aliamua KUIWAKILISHA Chadema kwao kilombero ingawa anaishi Dar. Angeliweza kabisa kuwa mbunge wa kuteuliwa na kuwa anafanya kazi zake Dar ila (kumbuka maneno yake), yeye ALIAMUWA kuwa KILOMBERO.
Labda hapa Chadema walifanya makosa. Wangeliweza kuwachukua akina Regia na kuwaandikisha kama wakazi wa Arusha.
Kuna haja ya KUWAONDOA hawa wabunge wa kuteuliwa kwenye mambo ya MADIWANI maana watakuwa wanaleta MATATIZO kila mwaka. Kwa mfano kwa Mwanza, wangeliweza kuwachukua wabunge kibao wa kuteuliwa Mwanza ili washinde kwenye uchaguzi wa madiwani na mwisho wawe na Meya wa Mwanza.
Katika Mabadiliko ya KATIBA, kuna haja ya hii kitu pia ibadilishwe ili KUPUNGUZA vyama vya siasa KU-FIX matokeo.
MKULIMA: Labda tu niseme kuwa SI KWELI kuwa unawakilisha
TU sehemu unayokaa. Regia anaishi Dar ila anawakilisha Kilombero.
Nafikiri inategemea baada ya kuchaguliwa,
unataka kuwakilisha wapi. Nakubaliana na wewe kuwa inabidi kuandikisha utawakilisha jimbo lipi maana kuna wale hawakugombea kabisa ubunge na wamechaguliwa. Sasa hawa watawakilisha wapi zaidi ya sehemu wanayotaka wao kuwakilisha (na mara nyingi ili kurahisisha maisha - SEHEMU WANAZOISHI.)
Wewe ni hopeless kabisa eti tumuulize Mwanakijiji inavyoonekana hata ukipigwa na mkeo huwa unamshitaki kwa MKJJ hovyoooo, kwanza takwimu zako feki hujui wabunge nao ni madiwani kwenye mikoa yao.