Quinine,
Unaanza sasa kuwa kituko humu ndani. Mjadala sasa unaelekea kwenye KATIBA zaidi na tumeacha Propaganda.
Unaingiza vifungu vingi sana humu ndani ambavyo unaanza kuonekana kama Lisanamu la Michelin vile.....
Hapa tunajadili kitu kimoja tu "Chitanda alikuwa na haki ya kupiga kura au laa...."
Sasa haya ya Reggae, Mke wa mtu na kila aina ya mipasho yanatoka wapi? Kumbe Mkuu na wewe ni mtu wa Modern Taarab? Mwanzo nilikuwa nahofia kuwa unaelekea huko ila sasa nimepata uhakika kuwa ni PURE MIPASHO.
Kama kuna kuvunjwa sheria ya idadi ya wanachama wanaopiga kura 2/3 basi hebu lete hicho kifungu pia tukijadili na sidhani kama hata kitahitajika kujadili maana CCM na TLP kwa uhakika hawakufika 2/3 na hivyo Uchaguzi haukuwa HALALI.
CCM na hasa PM Pinda, alikuwa na uwezo kabisa wa kulimaliza hili. Ilitosha tu kuongea na uongozi wa JUU wa CHADEMA na wangelikwenda hapo na kuwajulisha jamaa wa Arusha SHERIA ikoje na uchaguzi ukafanyika. Sidhani kama Lema na kundi lake wangelibisha. Nashindwa kufahamu kwa nini hakulishughulikia hili ingawa alikuwa kaahidi kulifanyia kazi mwishoni na mwanzoni wa Mwaka kabla ya Mauwaji.
Juu ya IMANI yangu kichama, hadi sasa sina CHAMA na maishani sijawahi kupiga kura hata siku moja kuchagua Rais wala Mbunge. Sasa waweza kuniweka kwenye KAPU lolote unalotaka Mkuu na maadamu wewe ni Mipasho Man, wala sintabishana na wewe maana huko ndiko kwenye maeneo yako ya kujidai na inabidi tu Utunukiwe u-Dr wa Mipasho na UDOM.
Maadam REGGAE huzipendi, basi angalia hiki kibao Fundamentalist wa Chadema weee..........
YouTube - J Martins - Jupka (Remix) Ft. Fally Ipupa