CCM: Tuna madiwani 16 Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM: Tuna madiwani 16 Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyambala, Jan 10, 2011.

 1. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wakuu hii habari inaukweli wowote? Maana simwamini kabisa Hiza Tambwe na ofcourse kwenye hiyo 16 ndiyo pia kuna mbunge wa Tanga na aliyejiuzulu wiki iliyopita.

  CCM: Tuna madiwani 16 Arusha


  Source: Bofya Hapa
  Na John Daniel

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimedai kuna taarifa za uongo zinazosambazwa kuhusu idadi ya madiwani wake katika Manispaa ya Arusha na kueleza kuwa chenyewe ndicho kinachoongoza kwa kuwa na jumla ya madiwani 16 wakiwemo
  wabunge watatu.

  Chama hicho pia kimesisitiza kuwa kama kingeshindwa kisingeweza kugombania kiti hicho cha umeya kwa kuwa sera na ilani za uchaguzi zitakazotekelezwa na kiongozi huyo bado ni za CCM na si vinginevyo.

  Akizungumza na waandishi wa habari ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumulumba, Dar es Salaam jana, Naibu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda, Bw. Tambwe Hiza alisema ni aibu kwa watu wanaojiita viongozi kudaganya wananchi kuhusu idadi ya madiwani bila kuona aibu.

  "Kuna taarifa za uwongo zinazoenezwa kwamba CCM imepora umeya Arusha, ukweli ni kwamba CCM ndio ina madiwani wengi kuliko CHADEMA, tuna madiwani 10 wa kuchaguliwa, watatu wa viti maalumu na wabunge watatu, jumla 16.

  CHADEMA wana madiwani wanane wa kuchaguliwa, viti maalum watatu, wabunge wawili wa viti maalum na mbunge moja wa kuchaguliwa jumla 14, jamani hapo nani ana madiwani wengi?" alihoji Bw. Tambwe na kuongeza:

  "Kwanza CCM hatuwezi kugombani umeya wa Arusha maana sera na ilani ya uchaguzi inayotekelezwa ni ya CCM, asilimia 90 ya fedha za maendeleo za halmashauri zote ikiwemo Arusha zinatoka serikali kuu ya CCM, sasa hata meya akitoka chama gani atatekeleza mipango ya ilani ya CCM, lakini kilichopo Arusha ni ukweli kwamba tulishinda umeya," alisisitiza Bw. Tambwe.

  Alisema anasikitishwa na CHADEMA kuhoji uhalali wa Mbunge wake wa viti maalumu, Bi. Mary Chatanda, kuwa mmoja wa wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo wakati sheria ziko wazi kuhusu eneo gani mbunge wa viti maalumu atawakilisha.

  "Tarehe 10.12.2010 CHADEMA wenyewe walimwandikia barua Mwanasheria Mkuu wa serikali kuomba ufafanuzi wa kisheria kuhusu wajumbe wa halmashauri kisheria na katika majibu yake kupitia barua yenye kumbukumbu na. JC-A.130-74 ya 16.12.2010 aliwapa ufafanuzi kuwa ni maamuzi ya chama husika kuamua mbunge wake wa viti maalumu atawajibika halmashauri ipi.

  "Na hii waliuliza baada ya wao CHADEMA kuamua wabunge wake wawili, Bi. Grace Kiwelu na Bi. Lucy Owenya wawakilishe Halmashauri ya Hai na Mkurugenzi wa Wilaya hiyo kuwakatalia, lakini baada ya ufafanuzi huo wale wabunge waliruhusiwa, sasa wanachohoji ni nini kama si kupotosha tu wananchi kwa makusudi ili wajitafutie umaarufu bure," alisema Bw. Tambwe.

  Alisema kwa mujibu wa sura ya 287 ya kifungu cha 35 1 D wabunge wa viti maalumu wanatokana na idadi ya kura za chama husika, lakini ni wapi wafanye kazi zao ni uamuzi wa mamlaka husika ya chama kilichowateua na kutoa mfano kuwa kwa upande wa CHADEMA kazi hiyo hufanywa na Kamati Kuu.

  "Sisi tunasema kama CHADEMA wanadai kuna ukiukwaji wa sheria waende mahakamani badala ya kuchanganya watu, mbona wanadai wameshindwa kuhoji ushindi wa rais eti sheria inawazuia kwenda mahakamani, ndio maana wanataka katiba mpya mbona hili la meya wanaruhusiwa kwenda mahakamani lakini hawaendi kama wana haki," alihoji.

  Alikana CCM kutaka kufanya mazungumzo yoyote na CHADEMA kuhusu suala hilo na kusisitiza kuwa chama chake kiko sahihi, hivyo hakina sababu wala nia ya mazungumzo.
   
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Na ofcourse kama this is the case ile vizia vizia ya kufanya uchaguzi ilikuwa ya nini. Na kwa nini waligoma kurudia uchaguzi wakati wao wana madiwani wengi?
   
 3. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #3
  Jan 10, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,446
  Likes Received: 5,833
  Trophy Points: 280
  Kwani diwani wa CCM hawezi mpigia kura mgombea wa CHADEMA?Uchaguzi si siri ya mtu ? hii Tambwe iko gonjwa kabisa...kama dhani ndiyo hiyo uchaguzi wa nini si ingekuwa kuteua mara moja tu?
   
 4. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #4
  Jan 10, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Na bado mimi najiuliza kama wao walikuwa wengi na ni loyal kwa chama chao kwa nini kulikua na vizia vizia ya kupiga kura in the first place?
   
 5. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #5
  Jan 10, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kwa nafasi aliyonayo Tambwe Hizza CCM yuko kitengo cha PROPAGANDA so you can imagine
   
 6. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #6
  Jan 10, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hahaha ahaha ahaha, ndiyo maana nikai-highlight hiyo nafasi yake.
   
 7. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #7
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,705
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo hao madiwani ni rubber stamps? Na meya na madiwani wanapokea maelekezo kutoka serikali kuu? Kama ni hivyo kwa nini tunakuwa na uchaguzi wa madiwani? Badala ya kuingia gharama zote hizo, chama tawala kingepewa mamlaka ya kuteua madiwani na mameya ambao watatekeleza ilani zake za uchaguzi. Naona hapa Mheshimiwa huyu anastahili pongezi kwa kuliweka swala hilo wazi na kutuonyesha namna tunavyoweza kupughuza matumizi yasiyo ya lazima.

  Amandla....


  Amandla.....
   
 8. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #8
  Jan 10, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,446
  Likes Received: 5,833
  Trophy Points: 280
  CCM ikiyumba haraka sana atatafuta chama huyu...very disloyal dude CCM->NCCR->TLP->CUF->CCM->?????
   
 9. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #9
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,771
  Trophy Points: 280
  haya diwani wa CCM kata ya sombetini kajitoa, pia naibu Kivuyo wa TLP aliyewasaidia CCM 1st time kajiuzulu, mbona hajazungumzia ili uyu jamaa, atake asitake uchaguzi utarudiwa tu na CDM watashinda.
   
 10. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #10
  Jan 10, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  CCM huwa wanapenda kutumia watu fulani kama puppets wao one of them ni huyu TAMBWE and the other one is MAKAMBA
   
 11. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #11
  Jan 10, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Exactly bro! ila hii aina ya wanasiasa tulionao Tanzania inasikitisha na huyu ni kutoka chma tawala na kikongwe, and yet his superiors wanakubaliana naye kwamba huo ndiyo msimamo wa Chama!!!!!!!
   
 12. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #12
  Jan 10, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  wasiwasi wa ccm ni kwamba waligundua kuna madiwani wawili ambao wako upande wa cdm ndiyo maana hawa kufata njia sahihi ya uchaguzi na kati ya madiwani hao ni huyo alie jitoa ccm
   
 13. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #13
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  CUF alipanyea hawezi kurudi hata kama ataletwa na maaskofu au Mashehe.
  Alipandishwa chati na CUF alivyoona hakuna ulaji akakimbilia kwa Makamba, ni kama mbeba mikoba ya katibu mkuu wa CCM.

  Akiongea sihitaji kusoma au kusikia alichokisema maana anatia kichefuchefu!
   
 14. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #14
  Jan 10, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Kumbe wana madiwani wengi,basi Uchaguzi urudiwe ili washinde kihalali tatizo nini..?
   
 15. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #15
  Jan 10, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Huyu jamaa ni hopeless kabisa hajui maana ya uchaguzi.
   
 16. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #16
  Jan 10, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,446
  Likes Received: 5,833
  Trophy Points: 280
  Anajua kuchagua mchele tu.....
   
 17. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #17
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Naulza: Hivi Hizza anaposema CCM ina Wabunge 3 ambao ni madiwani, ni wa wapi hao? bila shaka ni kutoka majimbo ya uchaguzi yale mengine ya mkoa wa Arusha yaani wilaya nyingine ambazo zina halmashauri zao na hivyo wanakuwa madiwani wa huko. Kadhalika hao wabunge wa chadema ambao pia ni madiwani kisheria.

  Au tuseme 'madiwani' wa namna hii ambao ni wabunge hujichagulia wenyewe waende halmashauri gani wakapige kura?

  Lazima kuna kanuni kuhusu hili ama sivyo mambo yatakuwa shghala baghala.

  Nawasilisha
   
 18. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #18
  Jan 10, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Shangaa na wewe!!
   
 19. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #19
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  naamini CDM wanachopigia ni ufuataji wa taratibu za uchaguzi wa meya. Kwa hiyo alichotakiwa kusema ni uzingatiaji na ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi na si chama gani kina madiwani wengi.,. si kila diwani wa CCM ampigie mgombea wa CCM na si kila diwani wa CDM aipigie CDM (otherwise hamna haja ya uchaguzi).
   
 20. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #20
  Jan 10, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nakumbuka mwaka 2004 kabla ya Uchaguzi mkuu, Dr. Slaa na Mbowa walipohutubia mkutano wa hadhara na kutoa ufafanuzi wa maana ya propaganda ni nini. Tukiwa na hamu kubwa Mh. Mbowa kamanda wa jeshi la anga alisema "Ndugu zangu maana halisi ya propaganda nia KUBADILSHA UWONGO KUWA UKWELI NA UKWELI KUWA UWONGO" kwa hiyo CCM na serikali yake imekuwa inafanya propaganda kwa karibu miaka 45" wakati ule ambapo sasa ni miaka 50 toka uhuru.

  Nakumbuka tena jangwazi wakati wa zoezi la kuhitimisha uteuzi na udhamini wa Dr. Slaa kuwa mgombea urais kauli hii ilirudiwa tena na Dr. Slaa na Mbowe tangu wakati ule huyu Tambwe hiza alikuwa kimya baada ya waTZ kujua anachokifanya. Maana hata wana CCM wanakerwa na kauli zake. Alipigwa kadi nyekundu na hakuongea tena hadi uchaguzi ulipoisha sasa naona amefufuka tena.

  Huyu jamaa na CCM ni wakupuuza kabisa tusiwasikilize hata kidogo.

  Peoples Power.
   
Loading...