CCM na Wasomi wa Taifa Letu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM na Wasomi wa Taifa Letu

Discussion in 'Great Thinkers' started by Mchambuzi, Jul 22, 2012.

 1. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Kwa nyakati fofauti, wengi wetu tumejifunza katika historia ya nchi yetu kwamba moja ya sababu za msingi ambazo Mwalimu Nyerere alizitaja miaka 50 iliyopita kwamba ni kikwazo kwa Maendeleo ya taifa letu ni uhaba wa wataalam wa kusaidia kujenga taifa. Hivyo, katika miaka ya mwanzo ya uhuru, ilimlazimu Mwalimu na serikali yake kuagiza wataalam kutoka nje na hawa walikuwa wanalipwa na fedha za walipa kodi wa nchi yetu. Miaka 50 baadae, hali sio tofauti sana kwa maana ya kwamba bado kama taifa, hatuoni bado mchango wa kutosha kutoka kwa wataalam wetu katika kuendeleza nchi yetu. Tunabaki kujiuliza, tatizo ni nini hasa:

  · Je, bado kama taifa tuna uhaba wa wasomi/wataalum?
  · Je, tunao wasomi/wataalam lakini wengi ni wababaishaji (wachakachuaji)?
  · Je, tunao wasomi/wataalam lakini mazingira (social and economic institutions and infrastructure) zinawanyima nafasi kutumia uwezo wao kuchangia ujenzi wa taifa?
  · Je, tunao wasomi/watalaam lakini hawathaminiwi?
  · Je, tunao wataalam lakini wengi wamegeuka kuwa wanasiasa?


  Nia yangu sio kutoa majibu kwa maswali haya bali kuchokoza mada huku nikijaribu kutoa maoni yangu kadhaa juu ya jambo hili. Kwa sasa nitajikita zaidi kwenye kujenga hoja kwamba moja ya tatizo lililopo ni kwamba wasomi/watalaamu wetu wengi wamegeuka kuwa wanasiasa.

  Katika mazingira yetu, tunapozungumzia Siasa, ni vigumu kutenganisha neno hili na dhana ya Siasa ya Vyama. Kwa maana nyingine, in Tanzania, politics is partisan politics. By tradition, vyama vya siasa uhakisi na kukimu zaidi matakwa na mahitaji ya watawala kuliko matakwa na mahitaji ya jamii. Ni jambo la kawaida kwa vyama vya siasa kutumia muda mchache sana kujishughulisha na matatizo/changamoto zinazokabili jamii na badala yake kujikita katika masuala yanayohusiana na uongozi na kutwaa madaraka. Suala hili linapotokea kwenye jamii maskini kama Tanzania, jamii ambayo hakuna mjadala kwamba haina Dira ya Maendeleo inayoeleweka kitaifa, hili ni tatizo. Kwa mfano, ukimuuliza mtanzania wa kawaida kwamba, je dira ya taifa lako ni nini? Wengi watakujibu kwamba dira yetu ni MKUKUTA au MKURABITA. Ni watanzania wachache ambao watatamka "DIRA 2020" – na hata hivyo, huu ni upuuzi kwani Dira hii haikutengenezwa na watanzania bali wahisani kupitia IMF na World Bank. Kwahiyo sio Dira inayotokana na watanzania. Lakini mbaya zaidi ni kwamba, katika kujibu swali juu ya dira yetu ya taifa, watanzania wengi watakujibu kisiasa zaidi kwani huo ndio ufahamu wa wengi – yani katika mazingira ya ilani za vyama vyao vya siasa. Huu ni ujenzi wa janga kubwa sana la kitaifa kwa siku za usoni.

  Kwa mtazamo wangu, ni muhimu katika mijadala juu ya Maendeleo ya Taifa, tukaanza kupunguza siasa za vyama kwani inazidi kutugharimu kimaendeleo. Ni muhimu tukaanza kujadili na kupangiaa Maendeleo ya Taifa letu katika mazingira ambayo ni over and above partisan politics. Mimi nadhani wenye uwezo wa kutufikisha huko ni wasomi (ambao ntawaita - intellectuals). Kabla sijaenda mbali, ni vizuri nikafafanua an intellectual ni mtu wa namna gani: An intellectual ni mtu anaetumia akili yake kwa ubunifu, lakini muhimu zaidi mtu anaetumia intelligence zaidi kuliko emotions or instincts. Hapa, maana ya intelligence ni – uwezo wa kuchanganua, kutambua, na kuelewa jambo. Na na ndio maana intellectuals katika jamii yoyote ile wana uwezo mkubwa wa kuona masuala mbali mbali over and above partisan politics, hawa yale yenye maslahi kitaifa.

  Tofauti na miaka ya nyuma, Tanzania ya leo imejaliwa kuwa na wasomi wengi sana waliotokana na vyuo vyetu vikuu (ukiachilia wale waliosomeshwa na walipa kodi nje ya nchi). Vyuo vikuu ni taasisi zenye umuhimu wa kipekee wa kupangilia na kuendeleza a body of intellectual thought, kitu amhacho jamii inaweza kuakisi. This body of intellectual thought is supposed to be over and above mambo ambayo ni dhahiri/yanayoonekana/eleweka kwa urahisi. Jamii kama jamii hutingwa na many complex issues; na tatizo ukua zaidi wanasiasa wanapoingiza siasa katika complexity iliyopo tayari ndani ya jamii; kitendo hiki huzidi kuwagharimu na kuwaumiza watanzania kimaendeleo. Lakini kwa vile wasomi wana nafasi na uwezo wa kushughulika na masuala mbalimbali ya kijamii in a manner ambayo ni over and above partisan politics, hawa ndio wenye jukumu kubwa la kuisaidia jamii yetu iondokane na miaka 50 ya umaskini ambao kwa mshangao mkubwa na bila aibu, CCM imeutungia kauli mbiu ya Tumethubutu, Tumeweza na Tunasonga mbele.
  An intellectual body ni kama kioo cha jamii – kwa maana ya kwamba inaipa jamii taswira yake. Wasomi wa nyanja mbali mbali (politics, law, geology, engineers, journalism, medicine etc) wana uwezo na wajibu wa kutuelezea watanzania tunaonekana vipi kama jamii. Wasomi wana uwezo na wajibu pia to ‘articulate' our hopes and fears; kutupa tahadhari juu ya hatari iliyopo mbele yetu; na vile vile kutusaidia kutupatia maana ya vitu ambavyo wanasiasa wetu aidha wanavipotosha, hawavielewi au wanafanyia mzaa kwa faida zao binafsi.

  Ninapoizungumzia zaidi CCM ni kwa sababu hadi sasa, ni chama pekee ambacho miaka nenda miaka rudi (kwa miaka 50), ndicho kilichopewa dhamana ya kutuongozi kama taifa. Hivyo ni muhimu nikajadili aina ya viongozi wa CCM ya leo kwa mujibu wa maoni yangu. CCM in aina kuu tatu ya viongozi wa kisiasa:

  1. Wanaitikadi Feki: Wanaitikadi wa dhati CCM hawapo tena kwani waliondoka na Mwalimu Nyerere. Wanaitikadi wa leo ni wale wajipambanua kama wana itikadi wa kijamaa, lakini wanadanganya wananchi huku wakitambua wazi kwamba CCM hakikuwaandaa watanzania kuhamia kwenye mfumo wa soko huria kutoka kwenye ule wa awali wa Ujamaa. Ndio maana watanzania wengi leo hii wamebakia kuduwaa na wasijue jinsi gani ya kukabiliana na maumivu ya sera za soko huria huku viongozi wanaohimiza CCM ni chama cha kijamaa wakiishi maisha ya ubepari uliopitiliza. Ni wajibu wa wasomi kurekebisha hili, sio wanasiasa.

  2. Wapambe: Hili ni kundi la pili la viongozi wa kisiasa ndani ya CCM ya leo. Enzi za uchifu, hii ilikuwa ni ajira rasmi. Lakini leo hii, watu huteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali lakini unofficially, kazi yao ni upambe ambapo shughuli yao kubwa huwa ni to ‘amuse', ‘cheer' and ‘charm' their masters (waliowapa madaraka). Hivyo ndivyo wanavyofanikiwa kuhudumia matumbo yao na familia zao. Mbali na kufanya shughuli zao kupitia vyombo vya habari, wapambe wapo hata ndani ya bunge, CCM – NEC na kamati kuu ambapo kazi yao kubwa ni kuwafagilia wakubwa waliowapa madaraka au fadhili kampeni zao, lakini muhimu zaidi, kusaidia CCM to divert attention ya umma from major issues of the day. Wapambe ni nuksi na kama msomi, ukikwaruzana nao, ni rahisi sana kukumaliza kibiashara, career-wise na hata kimaisha.

  3. Wachochezi (Political trouble makers) – kundi la tatu ni lile la wachochezi. Kazi kubwa ya watu hawa ni kuushawishi na ku-bamboozle umma, na ni mabingwa wa kutumia vyema prejudices na stereotypes zilizopo kwenye jamii yetu kwa maslahi ya CCM. Viongozi hawa huwa hawaheshimu mantiki (logic), human decency, consistency na hawana muda kusoma alama za nyakati. Misamiati na kauli mbiu nyingi za CCM hutokana na viongozi wa namna hii wakisaidiwa na wenzao (wapambe na wanaitikadi feki). Lakini muhimu zaidi ni kwamba, hawa ni mabingwa wa kupika uongo mbalimbali kisha kuujengea hoja na propaganda kwamba huo ndio ukweli uliosadidika, usiopingika na unaotakiwa kuabudiwa. Na iwapo anatokea mtu mwingine kupingana nao, basi ubatizwa kila aina ya majina – muhasi, haramia, adui, mhuni, mkabila, n.k, na mara nyingine maisha yako yanaweza kuwa hatarini. Wachochezi hawana muda wa kuheshimu dhana ya uhuru wa mawazo; huwa hawaoni any merit on a political opponent (mfano tazama tabia na kauli zao dhidi ya upinzani bungeni) na badala yake wanajaribu kuwatuhumu wale wote wanaowa ‘challenge' kwa mbinu za udini, ukabila, ukanda, n.k. Viongozi wa namna hii ni mabingwa wa ku-appeal on stereotypes, prejudices, emotions, fears, na expectations za umma kwa kujenga propaganda based on themes za kidini, kikabila, ukanda n.k. Wachochezi ndio hutumika zaidi katika kuzima hoja za wasomi zinazolenga maslahi ya taifa.

  Nini nafasi ya wasomi?

  Tofauti na viongozi niliowajadili, kwa kawaida wasomi huwa ni ‘great thinkers'. Tofauti kubwa iliyopo kati ya wasomi na viongozi niliowajadili ni kwamba, wakati wanaitikadi feki, wachochezi na wapambe ni kawaida kujichukulia madaraka mikononi kuifanyia jamii maamuzi, wasomi wajibu wao ni kusaidia wananchi kujenga uwezo "to think for themselves". Ni tofauti hii kubwa baina ya viongozi hawa na wasomi ndio inayofanya viongozi wengi wa kisiasa kuwapiga vita wasomi kila wanapojitokeza kutoa maoni yao kuhusu muhstakabali wa taifa letu. Na mbaya zaidi ni kwamba, sehemu kubwa ya jamii bado inaamini wanasiasa na kuliko wasomi.

  Kwa viongozi wa kisiasa, wasomi ni watu wabaya na wa hatari sana. Hii ni tofauti na enzi za Mwalimu Nyerere kwani miaka ya 1960s – 1970s, kila wakati taifa lilipokuwa linakabiliwa na changamoto mbalimbali, Mwalimu alikuwa na utamaduni wa kwenda Chuo Kikuu (Mlimani) kukutana na kujadiliana na wanafunzi. Ndio maana tofauti na leo, ilikuwa ni mara chache sana kwa serikali ya Mwalimu kukwaruzana na wasomi. Moja ya matukio machache ni lile la kuwalazimisha wasomi kujiunga na JKT ambapo Samuel Sitta na wengine walijikuta katika matatizo pale walipopinga na Mwalimu juu ya hilo. Kwa ufupi, enzi za Mwalimu, Mlimani became "a symbol of expression of critical intellectual thought". Tofauti na enzi za Mwalimu, leo hii hatusikii wasomi wakishirikishwa na serikali katika mijadala na maamuzi ya kujenga taifa letu. Na ni nadra sana kusikia viongozi wa CCM wametembelea vyuo vikuu kwenda kubadilishana mawazo na wasomi. Ni kama vile wanawaogopa na hakuna jamii hata moja duniani iliyopiga hatua kimaendeleo kwa kuwaogopa au kutofautiana na wasomi. Katika Tanzania ya leo ni vigumu sana kuyasikia mawazo ya wasomi. Ikitokea bahati basi ni kupitia vipindi vya televisheni ambavyo sio watanzania wengi wanapata nafasi ya kuvitazama, let alone kujua in advance vipindi vitarushwa lini. Lakini mbaya zaidi ni kwamba hata mawazo na michango ya wasomi hawa huishia kuwa soga tu kwani ushauri wao haufanyiwi kazi yoyote na serikali.

  Ni desturi pia kwa viongozi wengi wa kisiasa (CCM) kujenga hoja (chini kwa chini) kwamba wasomi ni watu ambao wapo too academic, too theoretical; wasomi hawaelewi reality; wasomi ni arm chair critics na wamejaa destructive criticisms. Hoja hizi ni za kawaida hasa nyakati za chaguzi mbalimbali za CCM. Kwa mfano, mwaka 2005 kulikuwa na fitina nyingi sana kwamba mgombea – Professor Mwandosya hafai kuwa Rais kwani Tanzania haina mahitaji na Rais ambae ni professor. Hata katika nafasi za ubunge na udiwani, wasomi hujengewa chuki na fitina kubwa. Lakini viongozi hawa hawa wa kisiasa baadae hushangaza pale wanapopigana vikumbo kutafuta degree za kuchakachua, huku wengine wakitafuta degree za PhD kwa kila njia ili na wao waonekana wa maana mbele ya jamii.

  Tukirudi kwenye hoja kwamba wasomi hawafai kwani ni watu waliojaa theory pekee, as a matter of fact, kwa msomi wa kweli na alie makini,kuitwa too theoretical sio matusi kwani kazi kubwa ya msomi is to theorize reality na hivyo ndivyo msomii uzidi kuelewa ukweli wa suala husika. Lakini ukweli ulio wazi ni kwamba - Wanasiasa wa CCM wanaposema wasomi kazi yao kubwa ni ‘destructive criticisms', na sio ‘constructive criticisms', wanacho maanisha hapa ni kwamba: Yale yote ambayo wanasiasa hawa au CCM hawataki kuyasikia au hawataki wananchi wayaelewe, basi hayo yote ni desctructive; Lakini yale yote ambayo wao au CCM inayaunga mkono, yale ambayo hayakiweki CCM katika hatari ya kuanguka kisiasa, na hayasaidii kuamsha watanzania kutoka kwenye usingizi mzito wa miaka 50 ya umaskini, basi hayo yote ni constructive. Isitoshe, ni dhahiri kwamba katika Tanzania ya leo, hakuna msomi makini ambae anaweza kujenga hoja na asionekana hafai machoni mwa CCM. Kwa mfano, zipo taarifa zisizo rasmi kwamba hata ndani ya vikao vya baraza la mawaziri, wapo mawaziri kadhaa ambao uonekana na mawaziri wenzao kwamba wanachafua hali ya hewa kutokana na hoja zao kulenga zaidi maslahi ya taifa - over and above partisan politics.

  In actual fact, constructive criticism ni ile inayolenga kuondokana na existing dominant, unfair, unjust and unequitable relationship ndani ya jamii yetu ya Tanzania chini ya utawala wa miaka 50 wa CCM. Ndio maana it turns out kwamba any serious criticism ya wasomi ni Destructive kwani - such criticism uhimiza the need to Construct a new Tanzania. Kwa mfano, watanzania wamepitia tabu kubwa sana kutafuta katiba mpya ambapo kwa miaka mingi wasomi wamepigana kufa na kupona na utawala wa CCM (kihoja) na hatimaye kupata ushindi dhidi ya CCM. Ni muhimu kwa wasomi kuendeleza juhudi za aina hii kwani mbali ya suala la katiba Mpya ambalo dhahiri ni non-partisan, yapo mengine mengi ambayo wasomi wanaweza kusaidia ili watanzania wapigie hatua kimaendeleo.
   
 2. J

  JokaKuu Platinum Member

  #2
  Jul 22, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,955
  Trophy Points: 280
  Mchambuzi,

  ..lakini hii picha uliyotuchorea kuhusu CCM/Tanzania mbona inatisha hivi??
   
 3. y

  ycam JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2012
  Joined: Mar 17, 2012
  Messages: 755
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 180
  Umefanya uchambuzi mzuri Mkuu kuhusu nafasi ya msomi ndani na chini ya utawala wa CCM.

  CCM si kwamba hawajui umuhimu wa elimu na wasomi katika chama na katika kuisaidia serikali kuleta maendeleo kwa wananchi. Actually, sometimes huwa wanawatumia wasomi inapobidi. Broadly speaking, tatizo ni ufisadi. Mafisadi ndani ya Chama, sikuzote wapo tayari kumfanya mtu mwingine mwenye utaalamu na nia njema aonekane hafai, ili wao wapate wanachokitaka bila kukosolewa na bila kuzibiwa mianya yao ya uhalifu.

  Ndiyo maana, kama ulivyosema, utashangaa hata wao wakishapata huo uongozi kifisadi au kimizengwe baadae tena wanautafuta huo usomi kwa kujisomea online au kwa long-distance kusaka vyeti.
   
 4. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #4
  Jul 24, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  JokaKuu,
  Ukitazama siasa za CCM, hiki sio chama kinacho appreciate wasomi tena tofauti na miaka ya mwalimu. Nimetolea mfano jinsi gani wasomi wa chuo kikuu walivyokuwa wanashirikishwa katika mijadala inayohusu hali ya nchi kisiasa, kiuchumi na kijamii. Nina kitabu kimoja kinachoelezea pia ni jinsi gani Mwalimu Nyerere alipata ujasiri wa kuingiza nchi yetu kwenye ujamaa kutokana na wasomi wengi wa Mlimani kukubaliana na mtazamo wake, tatizo likaja tu baadae kwenye utekelezaji. Miaka ya sasa, tuna wasomi wengi sana na wenye hekima sana kutokana na elimu yao na uzoefu wao lakini hawatumiki ipasavyo na wakitumika ni kwa malengo ya kisiasa peke yake na wakishatumika na kufanikishia watawala malengo yao, shughuli yao imekwisha. Pia Tazama tume ya katiba, wengi ya walioteuliwa mle ni kwa malengo ya kisiasa tu; inastaajabisha kuona mawakili wa katiba (constitution lawyers) kama Professor Shivji wanaachwa katika tume hii; hakuna msomi anayejulikana ndani na nje ya nchi kuhusu utafiti wake katika masuala ya katiba kama Issa Shivji; Wasomi wengi walioteuliwa mle ni wale wenye political orientation ya CCM - hili halina mjadala, kama wapo wenye mtazamo ambao ni no-partisan basi ni wachache sana. Na wanasiasa wengi walioteuliwa mle ni kwa ajili ya to heal political wounds, na sio vinginevyo.

  Vinginevyo kwa miaka 20 sasa, taifa limeshuhudia zaidi malumbano baina ya wasomi na serikali ya CCM kuliko ushirikiano. That is the bottom line.
   
 5. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #5
  Jul 24, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Kimsingi nakubaliana na wewe, lakini kuhusu CCM kuwatumia wasomi inapobidi mara nyingi huwa na kwa malengo ya kisiasa, sio kwa maslahi ya taifa. Nazungumzia CCM baada ya Nyerere. Ndio maana hata katika mawizara yetu, watendaji ni wasomi (makatibu wakuu, wakurugenzi, wakuu wa taasisi mbali mbali za umma), lakini wizara hizi hizi pia zina wanasiasa (mawaziri na manaibu mawaziri) ambao ndio huteua bodi za wakurugenzi mashirika ya umma, na hata mara nyingine mawaziri wanakuwa na uwezo wa kukubali au kukataa makatibu wao wakuu. Kuna mifano mingi sana juu ya hili tukitazama kwa undani historia ya utendaji wa serikali ya CCM. The bottom line ni kwamba wasomi wanapotumika kama unavyosema, basi mara nyingi huwa on a partisan way (kwa malengo ya kisiasa - CCM), na sio non-partisan (kwa maslahi ya taifa over and above party politics).
   
 6. J

  JokaKuu Platinum Member

  #6
  Jul 24, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,955
  Trophy Points: 280

  Mchambuzi,

  ..lakini nadhani hata wakati wa Mwalimu kulikuwa na viongozi wa ajabu-ajabu ambao wanaweza pia ku-fit ktk hizo category ulizoziweka.

  ..kwa msingi huo sidhani kama nitakuwa nimekosea nikisema CCM imekuwa hivyo ulivyoielezea kwa kipindi kirefu sana.

  ..tofauti ya CCM ya Mwalimu na hii ya JK ni kwamba Mwalimu alikuwa na some sense of direction and ideological background/belief wakati JK hana. mazingira hayo ndiyo yaliyofanya tukawa na ahueni wakati ule wa Mwalimu kuliko ilivyo sasa hivi.

  ..Uongozi wa nchi yetu unategemea sana aina ya Raisi tuliyenaye. Wapambe wapo siku zote ktk siasa. Ikiwa hawa wa sasa hivi wanakukera ujue wanatokana na aina ya Raisi/Mwenyekiti wa CCM tuliyenaye.
   
 7. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #7
  Jul 24, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kabisa - na tofauti kubwa kati ya sasa and then ni kwenye hoja yako kwamba unlike now, enzi zile nchi ilikuwa na sense of direction kwa misingi ya itikadi ndio maana wanaitikadi/ideologues kama wanasiasa na viongozi walikuwa wanafanya kazi zinazoonekana, ingawa tatizo la utekelezaji wa sera pia lilikuwepo; vinginevyo kama unafuatilia siasa za wenzetu UK au US, siasa zinaendeshwa kwa itikadi za conservatives, liberals, moderates n.k, hivyo ndivyo viongozi wa nchi za wenzetu wanavyoongoza, wanavyotengeneza sera na pia wanavyouza sera zao to the electorate; sisi tunaongozwa na wanaitikadi feki, wakisaidiwa na wapambe na wachochezi, na wameshika kasi katika awamu ya sasa kuliko wakati mwingine wowote wa historia ya nchi yetu, na ndio maana nchi haiendi na hivyo ndivyo CCM itakufa.

  CCM inachungulia kaburi, ambao hawaoni hili ni wale wenye madaraka au wanaofaidika nayo, vinginevyo kuna kila dalili kwamba wachochezi, wanaitikadi feki na wapambe kama viongozi wa kisiasa wa CCM wanaiua CCM kwa maana moja kuu - siasa zao zimeshindwa kuki defend chama kila kinapokuwa attacked na mazingira - and this is the hall mark of an endangered species, which is CCM for that matter. ​CCM is a Dinosaur that will soon become extinct...
   
 8. J

  JokaKuu Platinum Member

  #8
  Jul 24, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,955
  Trophy Points: 280
  Mchambuzi,

  ..lakini viongozi wa juu wa CCM wa sasa hivi walikuwa ama wapambe, au wachochezi, wakati wa Mwalimu Nyerere.

  ..nakumbuka Mzee Butiku aliwahi kulalamikia viongozi wa sasa wa CCM ambao anadai zamani walikuwa "wakimbiza mwenge."

  ..kutokana na background ya viongozi wetu ndiyo maana unaona nchi inaendeshwa kwa program za "milipuko" tu.

  ..serikali na taifa kwa ujumla linaonekana halina vipaumbele wala mwelekeo wa aina yoyote ile.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. J

  JokaKuu Platinum Member

  #9
  Jul 24, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,955
  Trophy Points: 280
  Mchambuzi,

  ..lakini viongozi wa juu wa CCM wa sasa hivi walikuwa ama wapambe, au wachochezi, wakati wa Mwalimu Nyerere.

  ..nakumbuka Mzee Butiku aliwahi kulalamikia viongozi wa sasa wa CCM ambao anadai zamani walikuwa "wakimbiza mwenge."

  ..kutokana na background ya viongozi wetu ndiyo maana unaona nchi inaendeshwa kwa program za "milipuko" tu.

  ..serikali na taifa kwa ujumla linaonekana halina vipaumbele wala mwelekeo wa aina yoyote ile.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #10
  Jul 24, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Joka Kuu,
  Naiona hoja yako ya msingi lakini kwa mtazamo wangu, nyerere alikuwa na loyalists kuliko wapambe na hawa ni kina kawawa, sokoine n.k in my view; wachochezi kama walikuwepo basi ni wale walio onekana hivyo just because they were politically opinionated ingawa at times they had valid arguments - kwa mfano Mzee Aboud Jumbe, Hamad Rashid Mohamed, Maalim Seif, Dr. Masha etc;

  Kuhusu Mzee Butiku, mimi sio mfuatiliaji mkubwa sana wa siasa za Mzee huyu kwa kweli zaidi ya kujua kwamba he had a chance to extend legacy ya mwalimu kitaasisi lakini hajafanikiwa katika hilo, kwahiyo sitamjadili.

  Vinginevyo nakubaliana na wewe kwamba kama taifa, hatuna dira wala vipaumbele, just as baadhi ya viongozi wa CCM wanaviita vyama vya upinzani vyama vya msimu, CCM inaongoza kwa sera na programu za msimu.
   
 11. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #11
  Jul 24, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kwanza nikupongeze kwa kuchokoza mjadala. Naheshimu maoni yako ambayo sitayachambua bali nitachangia kwa vidokezo vyake.

  · Je, bado kama taifa tuna uhaba wa wasomi/wataalum?

  Tuna uhaba mkubwa sana wa wasomi kwa sababu waliopo ni wakuchonga. Madhumuni ya kuwa na wasomi ni kupanda mbegu ya bubujiko la fikra zinazojielekeza kutoa solution siyo kusubstitute solution. Nyerere kwenye maandiko na hotuba zake alisisitiza elimu inayoaddress mahitaji ya nchi; sasa hivi elimu yetu inaddress mahitaji ya vyeo kwa ajili ya madaraka serikalini. Jiulize baraza la mawaziri lilivyo na madokta wengi lakini wanashindwa kuweka mfumo fanisi wa kuendesha uzalishaji mali na utoaji huduma. EDUCATION WHICH DOES NOT GIVE SOLUTION kwangu ni sawa na hakuna. Kwangu mimi usomi = solution ya changamoto

  · Je, tunao wasomi/wataalam lakini wengi ni wababaishaji (wachakachuaji)?

  Tunao wasomi wa kuchonga si wababaishaji ni wakukariri ndivyo walivyo na pengine hawajijui.

  · Je, tunao wasomi/wataalam lakini mazingira (social and economic institutions and infrastructure) zinawanyima nafasi kutumia uwezo wao kuchangia ujenzi wa taifa?

  Bado nasisitiza usomi ni final product ya utatuzi wa matatizo ya maendeleo ya kiuchumi na ya kijamii pamoja na miundombinu. Ni wajibu wao kutafuta solution ndani ya mazingira haya, wameshindwa ila wepesi wa kulalamikia mazingira na stahili badala ya kutoa solution ya matatizo na kuzalisha vya kutosheleza kukidhi mahitaji.

  · Je, tunao wasomi/watalaam lakini hawathaminiwi?

  Tunao wasomi wa kuchonga wasiojua thamani yao. Pia ni bahati mbaya taifa letu kwa bahati mbaya au kwa makusudi wamezalisha wasomi wa aina hii. Hali ni mbaya zaidi kwa watawala/viongozi kwani wamefikia mwisho wa uwezo wao wa kufikiri kwa kiwango cha usomi wao.

  · Je, tunao wataalam lakini wengi wamegeuka kuwa wanasiasa?


  Tunao wataalamu wa kuchonga ambao hawana uvumilivu wa kisomi kukabiliana na matatizo. Ni wepesi wa njia za mkato kama siasa yenye maamuzi ya aibu kwa manufaa yao binafsi.


  1. Wanaitikadi Feki:

  Kweli na inawezekana itikadi yao ni kuchumia tumbo.

  2. Wapambe:

  Wengi wao wana fikra duni na ni tegemezi hao wapo ndiyo mawakala wa takwimu feki zinazoathiri maamuzi ya wanasiasa

  3. Wachochezi (Political trouble makers)

  Hawa hawapo kwa sababu silaha yao ni NGUVU YA HOJA ambayo haijaonekana

  Nini nafasi ya wasomi?

  Wasomi ndiyo uhai wa taifa; ukisikia CCM na serikali ziko ICU maana yake zimekufa kwa sababu ya ukosefu wa wasomi.

  HITIMISHO

  Tunahitaji kwa pamoja kuwa na dira na mwelekeo mmoja wa mustakabali wa taifa letu. Kuanzia hapo tutatayarisha elimu ya kuzalisha wasomi wa kutupeleka huko. HATUJAANZA lakini hatujashindwa kwa sababu hayo yako ndani ya uwezo wetu labda kama tumekufa ganzi.
   
 12. J

  JokaKuu Platinum Member

  #12
  Jul 25, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,955
  Trophy Points: 280

  Mchambuzi,

  ..we r not 100% on the same pg.

  ..kama nimekuelewa, kwenye post yako ya kwanza umewa-define wachochezi kama watu wa propaganda au funika-funika. hawa ni wale ambao wanajua kabisa kwamba mambo yanaharibika lakini kwa upande mmoja wanawalaghai wananchi, na upande mwingine wanawalaghai watawala kwamba mambo yanakwenda vizuri.

  ..in my opinion watu hao walikuwepo, wapo, na wataendelea kuwepo hata ktk awamu zijazo bila kujali chama gani kitakuwa madarakani.

  ..tatizo lililopo sasa hivi ni kwamba hao ambao mimi nimekuelewa kwamba walikuwa wachochezi wakati wa Mwalimu Nyerere, na awamu zilizofuatia, ndiyo sasa hivi wamepanda daraja na kuwa watawala. katika mazingira hayo it is obvious kwamba nchi itaendeshwa hovyo-hovyo kwa campaign slogans na siyo program zinazoeleweka.
   
 13. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #13
  Jul 25, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  In my contention, there is a very thin line between wanasiasa wachochezi na wale wa propaganda; wachochezi tunawaona kila siku kwenye bunge wakifanya vurugu ambazo nyingi huwa hazikemewi mle; wachochezi wanafanya kazi zao randomly, not in an organized manner na mara nyingi hufanya hivyo kujitafutia sifa ndani ya CCM, and not neccesarily kwamba wametumwa na chama rasmi kufanya wanayofanya ingawa mengi ya wanayoyafanya yanafuraiwa na wakubwa wao;

  On the other hand, wale wa propaganda wapo more organized kwani kazi yao kubwa ni kusambaza taarifa for the purpose of promoting some cause or belief kwenye jamii for the interest of the party kwa mfano upinzani hawaitakii mema nchi yetu, nia yao ni kuvunja amani na utulivu etc; idara hii chini ya CCM imeshindwa kazi kutokana na nguvu ya chadema, ndio maana hivi sasa kuna taarifa kwamba wanaifumua na kuisuka upya na itapewa jina tofauti;why? kwa sababu kazi kubwa ya propaganda ni kupika uongo na kulazimisha jamii ielewe kwamba ndio ukweli uliosadikika; it worked before lakini sasa hivi upinzani umeilemea CCM katika kuwafumbua macho watanzania; so CCM needs to come up with a new strategy;

  Kuhusu wachochezi enzi za mwalimu kuwa watawala nyakati za sasa, mimi nadhani kilichotokea ni kwamba - wengi walikuwa ni ideologues na wapambe nyakati zile, hapakuwa na wachochezi zaidi ya wale CCM dissents niliowataja awali - mzee wetu Aboud Jumbe, Hamad rashid mohamed, Maalim Seif etc ambao walikuwa na hoja za msingi kabisa; nikijaribu kufikiria wachochezi wa wakati ule ndani ya CCM besides political dissents, sipati mifano ya watu wa namna hii, unless unisaidie kwa hilo;
   
 14. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #14
  Jul 25, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Kimsingi nakubaliana na hoja zako. Lakini ningependa nigusie hiyo hapo juu kwa kukuuliza maswali matatu:
  1. Je, ni kwanini kama taifa hatuna dira wala mwelekeo mmoja?
  2. Nje ya CCM, kuna chama chochote cha siasa chenye jibu katika hilo - yani kina dira ya taifa iliyowazi to the electorate? Kama ipo, ni ipi?
  3. Ni aina gani ya uongozi au mazingira gani ya uongozi yanaweza kuturudisha kwenye mwelekeo kama taifa kama ilivyokuwa wakati wa nyerere? hapa sina maana ya kuanzisha mjadala wa failures za ujamaa, lengo langu ni self determination kama nchi inaweza kuzaliwa kwa namna gani katika mazingira ya leo ya soko huria.
   
 15. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #15
  Jul 26, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sawa mkuu najibu kama ifuatavyo:-

  1. Je, ni kwanini kama taifa hatuna dira wala mwelekeo mmoja?

  Nina sababu tatu

  i. Kuna dhana kuwa chama tawala ndiyo kila kitu, itikadi, sera, mikakati, usimamizi wa rasilmali kwa niaba ya kila mtu si kwa ridhaa ya kila mtu. Hapa yanafanywa maamuzi finyu yasiyogusa kila eneo la mahitaji ya nchi na mwananchi. Mifano mingi ipo; hoja inayotolewa nje ya chama haikubaliki mpaka iporwe na chama. Kwa bahati mbaya inapoporwa inaacha misingi mizuri ya hoja hiyo. (mfano wa karibuni ni wa katiba hapa tusigemee katiba inayokidhi matakwa ya wengi wenye hoja za msingi)

  ii. Tumegawika sana kivyama kwa sababu ya viongozi dhaifu usiotaka kukabiliwa na changamoto. CCM chama tawala ndiyo waasisi na watekelezaji wa mgawanyiko huu kwa vitendo. Nukuu "Chama kina wenyewe na wenyewe ni sisi"

  iii. Jitihada za kutafakari na kuingiza mawazo ya msingi ya kitaifa bila kujali yanatoka wapi hazitoshi. Iko sababu moja tu nayo ni maslahi binafsi si kitaifa, haya yananyima fursa ya msingi na mwanzo ya mwelekeo mmoja.

  Kutokana na hayo matatu jiulize na hususan CCM inazingatiaje sera muafaka ya uchumi? Ubinafisishaji ulieleweka na kuliridhiwa kwa hoja na wananchi? Mambo ya nje tumetoka kwenye ukombozi tumeingia kwenye sera ya nje inayoelemea kujenga na kuinufaisha nchi kiuchumi. Wangapi wanalielewa na kuliafika hili? Je liliridhiwa na mihili ya dola kwa taratibu muafaka? Jibu mwenyewe. Ulinzi na Usalama-Je huu ni ulinzi na usalama wa viongozi, watawala na chama tawala? Dhana hii haieleweki na kum"engage" kila mwananchi vilivyo. Utaifa!! Wote tunajua na tunakubali tulivyokua tunajivunia utaifa miaka ya 60/70. Hapo tuliweza kuwa na mwelekeo mmoja kwenye suala la kitaifa. Kwa sasa nina wasiwasi na hili.

  Kimsingi hatuna dira wala mwelekeo mmoja kwa sababu HATUNA jitihada za kufanya hivyo. Pia tumetelekeza tunu na fursa nyingi kwa udhaifu wa uongozi wa chama tawala kilichobinafsishwa.

  2. Nje ya CCM, kuna chama chochote cha siasa chenye jibu katika hilo - yani kina dira ya taifa iliyowazi to the electorate? Kama ipo, ni ipi?


  Honetly nina tatizo binafsi kuwa jinsi vyama vilivyoanzishwa mimi napata tabu sana kuona kama misingi yao ni kutuelekeza kwenye sera na mwaelekeo mmoja. Kwa sababu vimeanza kama wapinzani wa sera na mwelekeo uliopo katika mazingira ninayoyaona kama ya shinikizo. Wako hodari kupingana. Jibu rahisi hakuna. Kikubwa hapa masuala ya sera na mwelekeo wa taifa ni suala mtambuka linalohitajika kuwa ni zaidi ya chama na ambalo lina common denominator ya taifa. Hapa mimi ningependa vyama vishindanishe baadhi ya utekelezaji wa sera na mwelekeo wa kitaifa kama nilivyo ainisha baadhi hapo juu.

  Tatizo lililopo CCM imepoteza fursa ya kuongoza kipindi cha mpito kuelekea democrasia ya vyama vingi kwa kutosimika sera na mwelekeo muafaka wa kitaifa ambao ungeshindaniwa. Natabiri chama mbadala kikishika madaraka kitalibaini hili kwa sababu watakuwa na mbinyo wa kimazingira kufanya hivyo kwa ajili ya nchi kutawalika. Kwa sasa CCM inapigania kuishi na si ajabu inapigania usalama wake baada ya kutoka madarakani.

  3. Ni aina gani ya uongozi au mazingira gani ya uongozi yanaweza kuturudisha kwenye mwelekeo kama taifa kama ilivyokuwa wakati wa nyerere?

  Kuna aina moja tu ya uongozi wa namna hii, ni ule unaotokana na dhamira ya wapiga kura, ni ule wenye hisia na "facts to decide" zinazotokana na wananchi, ni ule wenye uthubutu wa kuanza na kufanikisha mambo kwa maslahi ya kitaifa. Mechanism ya kupata uongozi wa namna hii ndiyo jibu. Tumepiga hatua kiasi kwa jinsi tunavyowapata viongozi na mbeleni kuna fursa zaidi nje ya viongozi maslahi. Sababu yake ni kuwa kinachoendelea, hali ngumu ya maisha, hati hati za usalama, mdororo wa uchumi vimekuwa shule tosha kwa wapiga kura.

  NI FURSA ILIYOJITOKEZA YENYEWE si ajabu ni fursa pekee ya wapiga kura kubadilisha mambo.

  Mimi ni product ya Nyerere sina uhakika kama ni product ya ujamaa. Pia naamini kila penye failure kuna opportunity. Ombwe la uongozi kuanzia wakati wa Nyerere halikuzitumia fursa hizi "kikamilifu".

  Naamini kabla ya kuwanyooshea vidole viongozi ni muhimu kwangu kujihoji mimi nimechangiaje hapa. Watanzania tumejisamilisha kwa viongozi ambao wanatupelekesha bila kuwafanya lo lote. Ni kweli wametubana kwenye kupata elimu na taarifa sahihi kuhusu kinachoendelea; lakini humu humu kuna fursa za kufanyia kazi. Mfano mzuri ni sanduku la kura hapo mtu ana fursa ya kuwakataa viongozi wababaishaji.
   
 16. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #16
  Jul 26, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Ningependa nianze kwa kunukuu kauli yako pale unaposema:

  "Mimi ni product ya Nyerere sina uhakika kama ni product ya ujamaa."

  Hii ni kauli ya msingi sana kwa sababu watanzania wengi wanaomjadili Nyerere wamekuwa na tabia ya kumpima kwa mtindo wa matokeo ya sera yake ya Ujamaa. Na kwa vile wengi wanahisi Ujamaa umetugharimu kama taifa, basi humwangalia Mwalimu katika mazingira ya matokeo ya sera ya Ujamaa. Lakini kwa kauli yako hapo juu, ni dhahiri kwamba linapokuja suala la Ujamaa, unatenganisha NIA YA UJAMAA, UTEKELEZAJI WA UJAMAA NA MATOKEO YA SERA ZA UJAMAA. Kama nipo sawa, naomba niungane na wewe kwamba hata mimi ni product ya Nyerere, sidhani kama mimi ni product ya Ujamaa - kwa maana ya kwamba imani yangu kwa Nyerere ipo katika NIA aliyokuwa nayo Mwalimu kwa taifa letu, masuala la utekelezaji na matokeo ya sera za Ujamaa ni mengine kabisa. Ni muhimu sana kutenganisha haya kwani ndio njia pekee ya kuweza kutusaidia kujirudi na kutafuta dira na mwelekeo mpya wa taifa letu. Haina maana kwamba turudi kwenye Ujamaa; maana yangu hapa ni kuwa na self determination kama taifa.

  Miaka ya Mwalimu, baada ya uhuru tulianza na a shared belief kama taifa kwamba ili tuweze kusonga mbele na kuondokana na ukoloni wa kiuchumi baada ya kuushinda ukoloni wa kisiasa, ilikuwa ni muhimu kuweka pembeni tofauti zetu zote za kisiasa na ili kujenga umoja na mshikamano ambao ungetusaidia katika harakati za kujikomboa in the context of a single and elaborate vision. Ndio maana hoja ya kufuta mfumo wa vyama vingi vya siasa miaka michache baada ya uhuru ilijengeka kirahisi sana na ilipata mashiko. Changamoto tuliyokuwa nayo sasa ni je, ndani ya mfumo wa vyama vingi, self determination kama taifa inaweza kuzaliwa vipi katika mazingira ya sasa ya vyama vingi ambapo siasa za sasa ni za kuishambulia CCM kwa failures?

  Nikiingia kwenye hoja ya pili kuhusu chama nje ya CCM chenye dira na mwelekeo unaoeleweka wazi kwa electorate:

  Kwanza kabisa, ni dhahiri kwamba hata CCM imepoteza dira na mwelekeo kwa miaka zaidi ya 20 sasa (tangia Mwalimu ang'atuke mwaka 1985). Lakini cha kustaajabisha ni kwamba hata vyama vya upinzani katika nyakati hizi havijawekeza sana katika hili zaidi ya kujikita katika kukosoa mapungufu ya CCM huku vikiweka juhudu ndogo sana kuonyesha wana mbadala gani kwa CCM. Badala yake, tunacho ona ni kwamba wapinzani wakipata nafasi kuongoza nchi, watatekeleza sera zile zile za CCM kwa ufanisi zaidi – yani matakwa ya wahisani in the context of soko huru tulioingizwa kiholela na kwa nguvu na wakubwa wa nje kwa faida yao wakisaidiwa na vibaraka wao (matajiri/mabepari wa kitanzania), na ni dhahiri kwamba Tanzania ya 1986 – 2012 imezaa watanzania wengi maskini kuliko Tanzania ya 1961 – 1985.
  Given ukweli huu, ndani ya mfumo wa vyama vingi ambapo kila chama kina malengo yake kwa umma tena in a top – down approach na sio bottom up (kwa kushirikisha wananchi):

  1. Kwa mtazamo wako, unadhani ni rahisi kurudi tena kwenye mazingira ya kuwa na dira na mwelekeo mmoja kama taifa, ambayo ni over and above partisan politics? Mimi nadhani uwezekano upo lakini ni kazi ngumu na ya muda mrefu sana.

  2. Je unadhani ni masuala gani ambayo yanaweza ku play out kama maslahi ya taifa bila ya kujali siasa za vyama? Masuala haya yatatusaidia kuwa na mwelekeo mmoja kama taifa.

  3. Na kama kuna issues ambazo tunaweza kuzifanyia kazi beyond partisan politics, vyama vyetu vya siasa vitakuwa tayari kufanya hivyo bila ya kujiletea athari?

  Binafsi bado nafikiria majibu juu ya maswali yote haya na nikiyapata nitajaribu kutoa mawazo yangu.

  Mwisho ni kuhusu aina ya uongozi na mazingira ya uongozi ambayo yanaweza kuturidisha kwenye mwelekeo mmoja kama taifa kama ilivyokuwa miaka ya Nyerere:

  Nadhani kwa kiasi kikubwa itategemeana na uwezo wa siasa zetu kukomaa na kuvuka siasa za vyama katika mambo ya msingi kama ilivyokuwa kwa nchi za wenzetu ambako kuna baadhi ya masuala huwa hayajali siasa za vyama bali maslahi ya taifa. Tunahitaji kuanza kuelekea huko kwani siasa za vyama pamoja na umuhimu wake, zikiwa over played zitazidi kutugharimu kimaendeleo kama taifa.
   
 17. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #17
  Jul 26, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mimi natoa mawazo yangu huru kwa sababu ni fursa niliyo na uwezo nayo, zaidi nafaidika sana kusoma mawazo ya wengine.

  Changamoto tuliyokuwa nayo sasa ni je, ndani ya mfumo wa vyama vingi, self determination kama taifa inaweza kuzaliwa vipi katika mazingira ya sasa ya vyama vingi ambapo siasa za sasa ni za kuishambulia CCM kwa failures?

  By definition Changamoto (Chalenge) ni suala lililotambulika kuwa likitafutiwa mchakato na mkakati litatoa fursa au manufaa ya kusonga mbele. Tunavyo vyama vingi, self determination ipo ila haipo shared. CCM inashambuliwa kweli lakini siyo saana kwa baadhi ya sera ila katika mikakati iliyokengeuka kutokana na michakato inayolenga kujifaidisha kibinafsi. Kwa lugha nyingine CCM ndicho chama kilichotelekeza jukumu la kuwaunganisha watu kwenye shared sel determination ya kitaifa. Kumbuka kinyume cha failure ni success. Kwa hiyo hii failure ya CCM kama wengine wangekuwa makini na determined wangeigeuza success. Yaani wangejikita kuwaelimisha na kushawishi wapiga kura ku"focus" kwenye masuala ya kitaifa na ambayo yanahuisha utaifa wetu ambao nadhani wengi wetu tunautamani sana.

  1. Kwa mtazamo wako, unadhani ni rahisi kurudi tena kwenye mazingira ya kuwa na dira na mwelekeo mmoja kama taifa, ambayo ni over and above partisan politics? Mimi nadhani uwezekano upo lakini ni kazi ngumu na ya muda mrefu sana.

  Tunahitaji yafuatayo kurudi tena kuwa na dira na mwelekeo mmoja kama taifa:-

  a) Mabadiliko ya fikra ya masuala muhimu ("Mind set"). Hii inadai turudi mezani tuangalie suala la ya elimu yetu. Inahitajika izalishe mtanzania mwenye "mind set" ya kitaifa huku tukiacha utendaji usio na tija na mstakabali wa kitaifa.
  Hapa yapo mengi sana lakini nichukue mawili matatu.

  Utendaji wetu toka mtendaji mkuu hadi wa chini anapofanya kazi analenga kumfaidisha nani? Wengi mind set zetu hazipo kwenye utendaji unaoelemea kulifaidisha taifa bali mshahara wa kujikimu.

  Tunamuonaje mtu ambaye anaharibu au anakengeuka katika utendaji wake k.m mvivu, mwizi asiyetimiza malengo ya kazi kwa wakati? Mind set ya waliowengi ni kwamba mjanja amejikwamua au ametoka kwa wizi ni shujaa. Kazi kubwa inahitajika kufanyika kwenye eneo hili, nayo ni kurudisha nidhamu ya kufanya kazi kuanzia juu kabisa hadi kwa mtu wa chini kabisa bila kuziacha taasisi zote za kila aina ya mafunzo. KURUDISHA NIDHAMU YA UTENDAJI HAKUHITAJI MTAJI WA MAPESA

  Mwisho kunakitu kinaimbwa kama wimbo nacho ni USIMAMIZI NA UDHIBITI wa utendaji (Performance Monitoring and Evaluation). Hili halipendwi na viongozi na watawala wetu (taarifa ya CAG). Hili pia ni mind set kwa sababu chain yo yote ya utendaji inaishia kwenye hili. Ndiyo maana hatujui baadhi ya "impact" ya maamuzi yetu na utendaji wetu. Lakini "impact" hii ambayo ipo ndiyo kiini cha mfarakano wa dira na mwelekeo wa pamoja. Lakini hiki pia ndicho kingekuwa chechem ya shared dira na mwelekeo wa pamoja. Sivumbui jembe bali najaribu kutumia jembe lililovumbuliwa zamani kwa kulimia kiwango cha mahitaji yangu.

  2. Je unadhani ni masuala gani ambayo yanaweza ku play out kama maslahi ya taifa bila ya kujali siasa za vyama? Masuala haya yatatusaidia kuwa na mwelekeo mmoja kama taifa.

  Suala la kwanza ni uchumi; huu una msingi wa ku"exploit" resources (rasilimali) zote za nchi kwa lengo la kuzalisha mali na mitaji ya kunufaisha taifa. Kutengeneza ajira kwenye sekta ya jamii afya, elimu huduma za usambazaji. Ukilitazama hili kwa suala hili kwa undani utagundua kutegemea kwa kila sekta. Ina maana kuzorota kwa moja ya sekta kunaathri sana sekta zingine. Kwa hiyo ni uchumi ni kiunganishi muhimu cha dira na mwelekeo mzima. Mfano wa china ni linchi likubwa wako pamoja kwa sababu uchumi wao unawaunganisha. Kila mchina ni sehemu ya uchumi kama siyo mzalishaji ni mlaji katika mfumo wa uchumi.

  Suala la pili ni mfumo wa utawala; huu umepitia "reforms" ambazo na zenyewe zimeji"reform" kiasi kwamba tumepoteza "orientation". Madhara yake ni kuwa hata ukitafuta kiongozi kama malaika bila kuwa na mfumo rahisi na thabiti wa utawala uongozi utapwaya. Utawala si kuwepo kwa rais, wakurugenzi, etc ni zaidi ya hayo. Utawala ni kudeliver kukidhi matakwa ya maendeleo ya nchi.

  Mimi kwangu suala la Ulinzi na Usalama ni la msingi sana kuwaunganisha watu. Tupo hapa na hali tete ya usalama kwa sababu ya sintofahamu kwa uhakika kuwa wajibu wa hili suala na jukumu linatekelezwaje? Sipendi kabisa huu upuuzi wa ulinzi shirikishi kwa sababu ni kukiri hakuna ushiriki wa namna fulani. Ni kweli hakuna ushiri wa namna fulani kwa sababu ya kukosa uelewa wa kila mtu kuhusu wajibu na jukumu la ulinzi na usalama. Kuna mambo mengi hapa lakini kubwa ni upungufu mkubwa katika elimu yetu isiyokidhi mahitaji hayo.

  Kubwa zaidi katika yote kufanikisha yote haya ni KUFANYA KAZI; hii tabia ya kutofanya kazi imefikia hali mbaya mno. Tija katika ufanyaji kazi imeshuka mno. Ndiyo masuala ya nidhamu. Mimi binafsi nilifikia hitimisho kuwa tija katika utendaji umeshuka hadi chini ya asili mia kumi. Hadi tumefikia kuruhusu ajira za wageni. Kubadilisha hii tabia ni dhamira ya usimamizi madhubuti katika utendaji. Kivipi hii ni kiunganishi cha sera na mwelekeo wa kitaifa? Kufanya kazi maana yake kutimiza wajibu kwa majukumu yaliyopo ya kitaifa, ambayo yanamgusa kila mtu binafsi kwa kuchangiana juhudi. Katika utendaji wo wote kunajengwa mshikamano usiotangazwa lakini una nguvu sana katika kiwango cha msingi. Hapa ndipo unajengwa msingi wa mwelekeo wa pamoja. Watanzania kwa sasa hatufanyi kazi hata viongozi wetu wavivu katika kutoa maamuzi sahihi na kwa wakati.

  3. Na kama kuna issues ambazo tunaweza kuzifanyia kazi beyond partisan politics, vyama vyetu vya siasa vitakuwa tayari kufanya hivyo bila ya kujiletea athari?

  Kulijibu hili tugeuze swali je ni kweli kuna masuala nje ya itikadi za kisiasa (issues beyond partisan politics)? Ndiyo hayo ndiyo masuala ya kitaifa; uchumi unatugusa wote, ulinzi na usalama, uzalishaji, nidhamu etc. Hapa tusitegemee maisha bora kufanya kazi, na kufanya kazi kunahitaji mazingira rafiki yanayosimamiwa na utawala bora. "Impact" ya masuala haya yote ni kutuunganisha kuibua sera na mwelekeo muafaka wa kitaifa.
   
 18. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #18
  Jul 28, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Ningependa nichangie maeneo matatu based on how hoja zako have stimulated my thinking:

  1. Suala la mindset na pia la nidhamu kama taifa, ni kweli kabisa inabidi tubadilike, ila ni vigumu kujua tufanye nini ili kufanikiwa katika hilo, hasa ikizingatiwa kwamba nchi imehakuwa corrupted from the grass roots up, na chanzo kikubwa cha tatizo hili ni CCM yenyewe kwa maana ya kwamba – kwa mfano, atanzania wengi live in a context of total hopelessness anddespair kwani kwa muda sasa CCM na serikali yake imeshindwa kutengenzea watanzania mazingira yanayotoa opportunity for prosperity and success and an upoward social mobility kutokana na jasho la mtu. Matokeo yake ni kwamba ni watanzania wachache sana ndio wanafanikiwa kimaisha; ni katika hali hii, mtu akifanikiwa kiuchumi/kifedha, regardless of the means, anageuzwa kuwa hero na role model, hence the term ufisadi getting a positive connotation.

  2. Sijakuelewa vizuri kuhusu uwepo wa self determination kama taifa under vyama vingi hasa pale unaposema kwamba ipo lakini haipo shared. Ni kwamba sijakuelewa tu but I think you might have a very interesting point. Inawezekana the shared vision ipo katika masuala uliyoyazungumzia ya mtazamo wa kiuchumi, ulinzi na usalama, nidhamu na uzalishaji, na tatizo ni kwamba tu haukufafanua vizuri. All in all, umenipa a starting point towards uelewa as I am still digesting your thoughts; Lakini kuna kitu kinanitatiza hapa: Chini ya Ujamaa, the State (CCM) failed; miaka 27 baada ya soko huria kuingia, hadi leo hii the market has failed, hence the state (CCM); Je, tatizo hapa ni uwepo self determination that is not shared? Kwa mtazamo wangu, STATE FAILURE UNDER UJAMAA POLICIES AND MARKET FAILURE UNDER FREE MARKET POLICIES, means CCM na serikali yake have failed watanzania since independence na sioni any justification and legitimacy for the party to continue to rule the country unless kinakubali mapungufu haya na kuanzisha mabadiliko from the bottom – up, sio kufanya maamuzi kwenye vikao vyao in a top – down manner na kuja kutuletea taarifa kwenye television. Bila ya hivyo, CCM is getting into a collision course na umma uliochoka!

  3. Na mwisho ni kuhusu hoja yako juu ya masuala ambayo unadhani we can deal with in a non – partisan way. Nimependa your ideas on issues kama uchumi, ulinza na usalama, nidhamu, na uzalishaji. Nilikuwa nina maoni tofauti kidogo juu ya hoja yako hii:

  · Tukianza na uchumi – Hadi sasa, sio CCM wala Chadema ambayo inaweka bayana nchi itasonga mbele kwa kutumia mfumo gani wa uchumi; Sera na itikadi za vyama vyote zinalenga kutegemea kujaziwa bakuli na wahisani, kwani tangia Nyerere ang'atuke, sera zaetu, dira yetu ya taifa n.k zimekuwa zinatengenezwa na wakubwa wan je (wahisani – IMF na World Bank) kupitia economics za AID ambazo ni maafa makubwa sana sio kwa taifa letu tu bali nchi zote maskini. AID ndiyo njia pekee iliyobakia kwa wakubwa wa nje to justify kwamba their theories about the market and economic development will lead us into a take off stage. This is a fallacy.
  · Tukija kwenue ulinzi na usalama – tumeona jinsi gani vyombo vyetu juu ya masuala haya vilivyokuwa partisan. Sina haja ya kufafanua sana kwani mengi yapo dhahiri.

  · Nidhamu – tatizo lililopo ni kwamba nidhamu imekuwa ni suala voluntary, sio mandatory tena kwani viongozi hawaonyeshi mfano wa kuigwa, na badala yake, madudu wanayofanya ndio yana inspire hata watoto wetu. Ni kawaida kwa watto mashuleni nyakati hizi kuwa na malengo ya kumaliza elimu zao ili wakajijenge binafsi, sio wakatumikie taifa.

  · Uzalishaji – tangia uhuru, mkulima amekuwa anamzalishia mtawala mazao ya biashara ili auze nje ya nchi na kupata resources za kujijenga kitaasisi; kuzalisha mazao ya vyakula ili to feed the urban elites and bureaucrats; ku maintain law and order kwa kuwekeza kwenye ulinzi na usalama (polisi n.k); kuwapatia maisha bora watu wa mijini kwa kuwapatia ajira kwenye taasisi za umma na pia kuwajengea mazingira ya ujarisiamali (sababu wengi ni exposed, educated, elites…) na pia kuwajengea miundo mbinu na huduma mbali mbali za kijamii ili wasi revolt against the regime n.k. Yote hii happens at the expense of mzalishaji ambae ambae yupo kijijini (70% of the population) ambae serikali does very little to care for their social welfare.

  That being said, mimi nadhani hoja yako juu ya masuala haya stands katika kuzungumzia masuala that can be dealt with in a no – partisan way, lakini kwa mtazamo wangu, yote haya lazima yawekwe kwenye kasha ya UZALENDO.
   
 19. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #19
  Jul 28, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Ningependa nichangie maeneo matatu based on how hoja zako have stimulated my thinking:
  1. Suala la mindset na pia la nidhamu kama taifa, ni kweli kabisa inabidi tubadilike, ila ni vigumu kujua tufanye nini ili kufanikiwa katika hilo, hasa ikizingatiwa kwamba nchi imehakuwa corrupted from the grass roots up, na chanzo kikubwa cha tatizo hili ni CCM yenyewe kwa maana ya kwamba – kwa mfano, atanzania wengi live in a context of total hopelessness anddespair kwani kwa muda sasa CCM na serikali yake imeshindwa kutengenzea watanzania mazingira yanayotoa opportunity for prosperity and success and an upoward social mobility kutokana na jasho la mtu. Matokeo yake ni kwamba ni watanzania wachache sana ndio wanafanikiwa kimaisha; ni katika hali hii, mtu akifanikiwa kiuchumi/kifedha, regardless of the means, anageuzwa kuwa hero na role model, hence the term ufisadi getting a positive connotation.

  2. Sijakuelewa vizuri kuhusu uwepo wa self determination kama taifa under vyama vingi hasa pale unaposema kwamba ipo lakini haipo shared. Ni kwamba sijakuelewa tu but I think you might have a very interesting point. Inawezekana the shared vision ipo katika masuala uliyoyazungumzia ya mtazamo wa kiuchumi, ulinzi na usalama, nidhamu na uzalishaji, na tatizo ni kwamba tu haukufafanua vizuri. All in all, umenipa a starting point towards uelewa as I am still digesting your thoughts; Lakini kuna kitu kinanitatiza hapa: Chini ya Ujamaa, the State (CCM) failed; miaka 27 baada ya soko huria kuingia, hadi leo hii the market has failed, hence the state (CCM); Je, tatizo hapa ni uwepo self determination that is not shared? Kwa mtazamo wangu, STATE FAILURE UNDER UJAMAA POLICIES AND MARKET FAILURE UNDER FREE MARKET POLICIES, means CCM na serikali yake have failed watanzania since independence na sioni any justification and legitimacy for the party to continue to rule the country unless kinakubali mapungufu haya na kuanzisha mabadiliko from the bottom – up, sio kufanya maamuzi kwenye vikao vyao in a top – down manner na kuja kutuletea taarifa kwenye television. Bila ya hivyo, CCM is getting into a collision course na umma uliochoka!

  3. Na mwisho ni kuhusu hoja yako juu ya masuala ambayo unadhani we can deal with in a non – partisan way. Nimependa your ideas on issues kama uchumi, ulinza na usalama, nidhamu, na uzalishaji. Nilikuwa nina maoni tofauti kidogo juu ya hoja yako hii:

  · Tukianza na uchumi – Hadi sasa, sio CCM wala Chadema ambayo inaweka bayana nchi itasonga mbele kwa kutumia mfumo gani wa uchumi; Sera na itikadi za vyama vyote zinalenga kutegemea kujaziwa bakuli na wahisani, kwani tangia Nyerere ang'atuke, sera zaetu, dira yetu ya taifa n.k zimekuwa zinatengenezwa na wakubwa wan je (wahisani – IMF na World Bank) kupitia economics za AID ambazo ni maafa makubwa sana sio kwa taifa letu tu bali nchi zote maskini. AID ndiyo njia pekee iliyobakia kwa wakubwa wa nje to justify kwamba their theories about the market and economic development will lead us into a take off stage. This is a fallacy.
  · Tukija kwenue ulinzi na usalama – tumeona jinsi gani vyombo vyetu juu ya masuala haya vilivyokuwa partisan. Sina haja ya kufafanua sana kwani mengi yapo dhahiri.

  · Nidhamu – tatizo lililopo ni kwamba nidhamu imekuwa ni suala voluntary, sio mandatory tena kwani viongozi hawaonyeshi mfano wa kuigwa, na badala yake, madudu wanayofanya ndio yana inspire hata watoto wetu. Ni kawaida kwa watto mashuleni nyakati hizi kuwa na malengo ya kumaliza elimu zao ili wakajijenge binafsi, sio wakatumikie taifa.

  · Uzalishaji – tangia uhuru, mkulima amekuwa anamzalishia mtawala mazao ya biashara ili auze nje ya nchi na kupata resources za kujijenga kitaasisi; kuzalisha mazao ya vyakula ili to feed the urban elites and bureaucrats; ku maintain law and order kwa kuwekeza kwenye ulinzi na usalama (polisi n.k); kuwapatia maisha bora watu wa mijini kwa kuwapatia ajira kwenye taasisi za umma na pia kuwajengea mazingira ya ujarisiamali (sababu wengi ni exposed, educated, elites…) na pia kuwajengea miundo mbinu na huduma mbali mbali za kijamii ili wasi revolt against the regime n.k. Yote hii happens at the expense of mzalishaji ambae ambae yupo kijijini (70% of the population) ambae serikali does very little to care for their social welfare.

  That being said, mimi nadhani hoja yako juu ya masuala haya stands katika kuzungumzia masuala that can be dealt with in a no – partisan way, lakini kwa mtazamo wangu, yote haya lazima yawekwe kwenye kasha ya UZALENDO.
   
 20. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #20
  Jul 30, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mchambuzi kuna wasomi wengi ambao wangeweza kufanya kazi za ubunge, udiwani etc etc lakini wako benchi, na wachovu na wababaishaji ndio wamekalia viti. Naona hizi ndio issues ambazo watanzania tunatakiwa kujiuliza, ni kwanini. Lakinin pia kuna wasomi, maprofesa na wengine ni wanazuoni wakubwa kabisa, ukisikiliza wanapoongea unaweza kuuliza kama kweli wana akili, ni wazima au wameamua tu kuuvaa wenda wazimu, watu kama hawa nao hawana maana kabisa ni bora wakae nje. Kwa hiyo kuna complications kidogo.

  Kwa sasa mtanzania yeyote mwenye akili timamu hawezi kuisifia serikali ya sasa au kukisifia chama kwa sasa. Vyote viwili viko ovyo kabisa, na ukizungumzia siasa ya ujamaa Tanzania utakuwa mwendawazimu kabisa, kwani ukiangalie hata wale walijiapiza kuwa wakomunisti wanaonekana kuwa ni mabepari na mafisadi wakubwa. Sina nongwa na ubepari mwenyewe naupenda, lakini sikubaliani na ufisadi, au ubepari unaotokana na wizi. lakini sielewi kabisa kwanini ubepari tunauita ujamaa na na ufisadi tunauita changamoto inayotokana na maendeleo

  Sijui ni kwanini wasomi wanaanza kupotosha ukweli na kusema serikali ya sasa imefanya kazi nzuri, au chama kinafanya kazi nzuri. Sijui ni kujikomba kwa viongozi wanasiasa, kujipendekeza au kutoona nini kinafanyika. Au wasomi hao si wasomi kama tunavyodhani, au ndio zile MA na Phd za kuokota Ulaya na America, au za kupewa ambazo zimesambaa na kila mtu anataka kuweka title mbele ya jina lake bila hata sababu ya maana. Sasa hivi unaweza kuwasikia baadhi ya mawaziri wakipinda hadharani hali mbaya ndani ya chama na serikali, lakini hadharani wanaongea kingine, kuna wanasiasa wanaongea tofauti kabisa hadharani kwa maslahi ya chama, lakini pembeni wanajua kabisa kuwa taifa linaenda mrama, na wanasema tunaongea vile kwa kuwa tumeambiwa. Sijui ni woga au ujinga. Lakini hiyo ndio hali iliyopo. Ukivuka mpaka kuingia Kenya hali ni tofauti kabisa, wenzetu mamba wanamuita Mamba, sio kenge au mjusi.

  Jaribu kumsikiliza Prof Palamagamba kabudi akiongea au Dk Benson Bana akiongea, unaweza kudhani title zao zimekwisha muda wake, wanaochoongea hata mwanfunzi wa kidato cha nne anaweza kujua wazi kabisa kuwa ni upuuzi tu. Lakini ambacho hakijulikani ni kwanini akili zao zinakuwa kinyume na hali halisi. Lakini kuna baadhi ya wasomi tumeona jinsi serikali ilivyowafanya, mfano mzuri ni Dk Lamwai. Kwa hiyo issue naona is more
   
Loading...