CCM na Wasomi wa Taifa Letu

Vile vile Marehemu Edward Sokoine; Kuna kitabu kimoja nimekisoma na kugundua jinsi gani kiongozi huyu asivyopewa heshima (hasa na viongozi uchwara waliomfuata baadae) anayostahili kwa mchango wake mkubwa sana kwa taifa letu (Tanzania); huyu mtu alikuwa anaelekea urais after nyerere on merit kabisa; wengi wetu tulimjua kwa suala la vita dhidi ya mafisadi (wahujumu uchumi tu), lakini kumbe mtu huyu alifanya mambo makubwa sana kwenye kilimo n.k; nikipata muda nita-share taarifa hii.

Mbali ya Nyerere, hakuna kiongozi mwingine wa ngazi za juu (mawaziri wakuu, makamo wa rais na marais) aliyelifanyia taifa hili mambo ya maana in terms of legacy kama Sokoine (ukimtoa mkapa ambae alijaribu kidogo) pamoja na elimu yake ya Form Four (i.e. Sokoine); bottom line is, you have a point kuhusu Mrema;
That is the point Mchambuzi.

Wasomi wanaofaa na wale wasio wasomi wanaofaa wote hawatakiwi na CCM. Ukiangalia watu wanaouawa hapa Tanzania unaweza kuona kuwa ni wasomi, au kama sio wasomi ni wale ambao wanajua mafisadi wanaitafuna vipi Tanzania. Kiaina naweza kusema kuwa kuna elements za jinsi wasomi walivyokuwa treated katika serikali tatu au nne zilizozpita Uganda.

Watu wote wenye elimu na wasio na elimu, lakini wanaoweza kulifanyia taifa mambo ya maana, hawana political future katika mazingira ya sasa ya Tanzania.
 
That is the point Mchambuzi.

Wasomi wanaofaa na wale wasio wasomi wanaofaa wote hawatakiwi na CCM. Ukiangalia watu wanaouawa hapa Tanzania unaweza kuona kuwa ni wasomi, au kama sio wasomi ni wale ambao wanajua mafisadi wanaitafuna vipi Tanzania. Kiaina naweza kusema kuwa kuna elements za jinsi wasomi walivyokuwa treated katika serikali tatu au nne zilizozpita Uganda.

Watu wote wenye elimu na wasio na elimu, lakini wanaoweza kulifanyia taifa mambo ya maana, hawana political future katika mazingira ya sasa ya Tanzania.

CCM haiwapendi wasomi ambao wanasimamia taaluma zao bali wasomi mamluki wanaoweza kuuza utaalam wao ili kukidhi matakwa ya mafisadi.

Ushahidi wa wasomi kutotakiwa na ccm unajidhihilisha wazi wakati wa chaguzi za ccm hasa wakati wa kura za maoni za ubunge; pale wasomi wanafanyiwa mizengwe na kejeli na mwisho wa yote wanachaguliwa waganga wa kienyeji kuwa wabunge badala ya wasomi!! Hiyo ndio ccm ambayo kama wanavyosema wao INA WENYEWE!!

Angalia tu uwakilishi wa Tanzania kwenye baraza la kutunga sheria la Afrika Mashsriki; ccm iliwachuja na kuwakataa wasomi mahili na badala yake kuwapendekeza watu wasiostahihi ,kati yao wakishutumiwa kuhusika na biashara ya madawa ya kulevya!! Sio hivyo tu karibuni wote kutoka ccm walichaguliwa kwa kutumia rushwa ya kuwahonga wabunge hasa wa ccm!!

Wasomi mahili hawawezi kununua ubunge kwa kutoa rushwa!!
 
Nichangie senti tano.
Kuna watawala na vongozi (Rulers and Leaders). Si kila mtawala ni kiongozi lakini kiongozi anaweza kuwa mtawala.
Nyerere kwa jinsi yoyote atakavyochuliwa bado anabaki na sifa moja ya kuwa kiongozi. Ni sifa hiyo ndiyo ilimpa nguvu ya kukutana na wasomi kila mara. Siku zote kiongozi husikiliza wafuasi wake na mtawala huamuru wafuasi wake.

Kuna kitu kinaitwa 'status quo' ambacho tunaogopa kukiongelea kila mara.
Nyerere alianza akiwa hana wasomi na alitumia waliokuwepo wachache akijenga kundi kwa siku za baadaye.
Zao la kundi hilo ndilo la wasomi waliopita na waliopo.
Ndani ya chama alilea viongozi kwa kuwajenga katika uzalendo.

Kwa bahati mbaya utaratibu wa kulea wataalam na viongozi umekwisha kwasababu ya kundi hasa ndani ya chama chake lililoamua hakuna mabadiliko na hali ibaki kama ilivyo(status quo).
Ni kwasababu hizo kundi hili halikubali msomi au maoni ya wasomi.

UZALENDO: Hakuna shule au kitabu cha kufundisha uzalendo. Uzalendo ni matokeo ya nidhamu kwa jamii (Discipline).
Kundi nililolitaja hapo awali limehodhi mamlaka ya nidhamu kwa kutumia kitu kinaitwa Katiba.

Katiba iliyopaswa kujenga nidhamu inatumika kulinda kundi dogo la watu kama tunavyoona serikali ya sasa na chama tawala.Kama hakuna Discipline nani atakuwa mzalendo? Utaongezaje kipato cha mbunge kwa siri huku ukimhimiza Daktari atangulize uzalendo! Bila kuwa na discipline inayojengwa na sheria na taratibu hakuna uzalendo.

WASOMI: Siamini kuwa tuna wasomi wababaishaji kama wengi wanavyosema. Kuna ushahidi wa kutosha wa wasomi wetu kutumika sehemu nyingine na kuleta tija. Nakubaliana na JingalaFalsafa anaposema wataalam ni zao la Taraining na wasomi ni zao la watalaamu kuwa na critical thinking.
Sisi hatuwajali wataalamu wetu tunategemeaje kupata critical thinking? na kwanini hapo wasionekane kama feki.

Bwana shamba yupo busy kufanya utafiti wa mbegu bora za mahindi, Daktari anafanya operesheni Kwa mishumaa, Engineer anabuni mradi nafuu sana wa umwagiliaji. Tumewaomba wafanye ubunifu wakiongozwa na uzalendo ili kuondoa umasikini. Jioni wanasikia Rais amesaini kwa mlango wa nyuma ongezeko la mishahara ya wabunge hadi milioni 11. Bado tunaomba wasomi na wataalamu wawe wazalendo! na tunataraji critical thinking, tunawahukum ni feki

MATOKEO YA UKOSEFU WA NIDHAMU: Ni kitu wanaita rule of the jungle( sheria za mwituni) mwenye nguvu atadumu (survival of the fittest). Ili msomi aweze kukabiliana na hali ya mwituni, naye hulazimika kutumia kanuni ya 'if you can't beat them join them'( Kama huwashindi waunge mkono). Wote wanatimkia katika siasa hata kama hawana karama hizo.

NDANI YA SIASA: Kwa vile wamejiunga kwa mahitaji na ulazima na si karama, wataalam na wasomi wengi huishia kubangaiza na hao ndio tunasema ni feki. Ufeki wao ni kuwa wapo ndani ya kundi miliki nililolisema awali na wanatakiwa wakubali hali ilivyo (status quo). Utatumia wapi usomi wako ukiwa ndani ya NEC au CC ya CCM kwa mfano mmoja tu.

WAPI PA KUANZIA: Ni lazima tuwe na nidhamu (discipline) na hakuna nidhamu iliyojengwa juu ya barafu. Nidhamu itaanza kwa kuwa na katiba itakayotufanya sote tuhisi ni wananchi na hakuna mtu au kundi la wenyenchi.
Hapo tutaweza kuwahukumu kila mtu na kila kundi kwa haki.

Wasomi wapo wazuri sana, system haiwaungi mkono au kuwapa nafasi.
Kwanini tunakinga visadolini, maguduria na bakuli na wengine kuning'inia katika chuchu za ng'ombe tukisubiri maziwa na uzalendo wake na kusahau kuwa hatujamlisha na amekondean?
Kwanini tunawahukumu wasomi na kuwatolea hukumu tukiwa na vipande vya ushahidi visivyoungika.
 
Mkuu Nguruvi3,

Wiki kadhaa zilizopita, ulileta hoja nzuri na za kusisimua sana kama mchango wako kwenye mjadala wangu juu ya CCM na Wasomi wa Taifa Letu. Leo hii tumesikia CCM ikijivunia kupata wasomi wengi kama wagombea wa nafasi mbalimbali ndani ya chaguzi za CCM zinazoendelea hivi sasa. Nadhani maneno yako sasa yana hit home zaidi kuliko awali kwa maana ya kwamba mifano hai sasa ipo wazi, na ningependa kuanza na ulichokisema kama ifuatavyo:
Utatumia wapi usomi wako ukiwa ndani ya NEC au CC ya CCM kwa mfano mmoja tu.

Kwa mtazamo wako, nini ni matarajio ya wasomi hawa in relation to swali lako hili. Pia ulinena yafuatayo:
Kuna watawala na vongozi (Rulers and Leaders). Si kila mtawala ni kiongozi lakini kiongozi anaweza kuwa mtawala. Nyerere kwa jinsi yoyote atakavyochukuliwa bado anabaki na sifa moja ya kuwa kiongozi. Ni sifa hiyo ndiyo ilimpa nguvu ya kukutana na wasomi kila mara. Siku zote kiongozi husikiliza wafuasi wake na mtawala huamuru wafuasi wake.

Je hawa wasomi wanakimbilia CCM kugombea hizo nafasi za NEC na vitu kama hivyo, wanafanya hivyo kwa kutegemea kwamba mchango wao kwa taifa utathaminiwa na mawazo yao kusikilizwa kupitia CCM?

Kuna kitu kinaitwa 'status quo' ambacho tunaogopa kukiongelea kila mara. Nyerere alianza akiwa hana wasomi na alitumia waliokuwepo wachache akijenga kundi kwa siku za baadaye. Zao la kundi hilo ndilo la wasomi waliopita na waliopo.
Ndani ya chama alilea viongozi kwa kuwajenga katika uzalendo.

Hoja hii inatoa ishara kwamba pengine CCM ilifanikiwa zaidi enzi zile ilipokuwa na wasomi wachache kulik hivi sasa ambapo ni kinyume; je hii ina uhusiano wowote na dis-economies of scale? Au je ni suala la uzalendo? au je ni simply CCM kutokamata tena hatamu na hivyo kutokuwa tena in the commanding heights za kuendesha uchumi kupitia parastatals mbalimbali ambapo zilijazwa wasomi wa kila aina?

Kwa bahati mbaya utaratibu wa kulea wataalam na viongozi umekwisha kwasababu ya kundi hasa ndani ya chama chake lililoamua hakuna mabadiliko na hali ibaki kama ilivyo(status quo). Ni kwasababu hizo kundi hili halikubali msomi au maoni ya wasomi.

Iwapo hoja yako hii ni sahihi, sasa hivi vigele gele na vifijo kwamba CCM sasa inakimbiliwa na wasomi ni vigelegele na vifijo vya nini hasa;

UZALENDO: Hakuna shule au kitabu cha kufundisha uzalendo. Uzalendo ni matokeo ya nidhamu kwa jamii (Discipline).

Kwa maana hii, wasomi kukimbilia CCM haina maana kwamba kuna lolote litakalo badilika?

Kundi nililolitaja hapo awali limehodhi mamlaka ya nidhamu kwa kutumia kitu kinaitwa Katiba. Katiba iliyopaswa kujenga nidhamu inatumika kulinda kundi dogo la watu kama tunavyoona serikali ya sasa na chama tawala.Kama hakuna Discipline nani atakuwa mzalendo? Utaongezaje kipato cha mbunge kwa siri huku ukimhimiza Daktari atangulize uzalendo! Bila kuwa na discipline inayojengwa na sheria na taratibu hakuna uzalendo.

Pengine ni kutokana na hili ndio maana wasomi wengi wanakimbilia CCM kwani angalau huko marupurupu na mishahara itaendana na juhudi walizopitia na kuenyeka kujitafutia elimu?

WASOMI: Siamini kuwa tuna wasomi wababaishaji kama wengi wanavyosema. Kuna ushahidi wa kutosha wa wasomi wetu kutumika sehemu nyingine na kuleta tija.


Je una maana tija hii ni nje ya siasa/CCM? kwani hiki ni chama tawala chenye mamlaka ya kuongoza nchi kiuchumi, kisiasa na kijamii, na maeneo haya yote huitaji wataalam na wasomi, jambo ambalo chama tawala linao wengi tu wa kuwachukua na kuwaweka kwenye taasisi husika;

Nakubaliana na JingalaFalsafa anaposema wataalam ni zao la Training na wasomi ni zao la watalaamu kuwa na critical thinking.

Kwa mtazamo wako, does CCM have any critical thinkers? Why or why not? na je, ni kwa sababu nyingine nje ya kuangalia maslahi mbele au ni suala la kimfumo zaidi?

Sisi hatuwajali wataalamu wetu tunategemeaje kupata critical thinking? na kwanini hapo wasionekane kama feki.[/qoute]

Kama hili ni sahihi, again, majivuno ya CCM kukimbiliwa na wasomi msingi wake ni upi?

[quote] Bwana shamba yupo busy kufanya utafiti wa mbegu bora za mahindi, Daktari anafanya operesheni Kwa mishumaa, Engineer anabuni mradi nafuu sana wa umwagiliaji. Tumewaomba wafanye ubunifu wakiongozwa na uzalendo ili kuondoa umasikini. Jioni wanasikia Rais amesaini kwa mlango wa nyuma ongezeko la mishahara ya wabunge hadi milioni 11. Bado tunaomba wasomi na wataalamu wawe wazalendo! na tunataraji critical thinking, tunawahukum ni feki.

Tatizo hapa ni nini hasa:
· Je, bado kama taifa tuna uhaba wa wasomi/wataalum? Kwa hoja yako, hili sio tatizo.
· Je, tunao wasomi/wataalam lakini wengi ni wababaishaji (wachakachuaji)? Kwa hoja yako, hili sio tatizo.
· Je, tunao wasomi/wataalam lakini mazingira (social and economic institutions and infrastructure) zinawanyima nafasi kutumia uwezo wao kuchangia ujenzi wa taifa? Kwa hili, sina uhakika unasimamia upande upi wa hoja, ingawa nadhani itakuwa unaungana na hoja yangu hii;
· Je, tunao wasomi/watalaam lakini hawathaminiwi? Kwa hoja yako, tatizo lipo hapa;
· Je, tunao wataalam lakini wengi wamegeuka kuwa wanasiasa? Hili nadhani unakubaliana nalo kama ulivyojieleza hapo chini kwamba;

MATOKEO YA UKOSEFU WA NIDHAMU: Ni kitu wanaita rule of the jungle( sheria za mwituni) mwenye nguvu atadumu (survival of the fittest). Ili msomi aweze kukabiliana na hali ya mwituni, naye hulazimika kutumia kanuni ya 'if you can't beat them join them'( Kama huwashindi waunge mkono). Wote wanatimkia katika siasa hata kama hawana karama hizo.
In summary hapa ni kwamba kwa mtazamo wako, tuna wasomi wengi lakini wamegeuka kuwa wanasiasa, na mimi nakubaliana na wewe katika hili;

.....Kwa vile wamejiunga kwa mahitaji na ulazima na si karama, wataalam na wasomi wengi huishia kubangaiza na hao ndio tunasema ni feki. Ufeki wao ni kuwa wapo ndani ya kundi miliki nililolisema awali na wanatakiwa wakubali hali ilivyo (status quo).

Kwa hoja hii, Msomi anageuka kuwa feki pale tu anapoingia ndani ya CCM, lakini akiwa nje, anaweza kuendelea kuwa au kuonekana ni msomi genuine; maana nyingine rahisi ya kuangalia hoja hii ni kwamba msomi akiingia CCM ni rahisi kuwa corrupted and rot; kwa maana hii, wasomi wengi waliojitokeza kuwania nyadhifa ndani ya chaguzi zinazoendelea wanaenda kuwa corrupted na kuwa rot, au?

Wasomi wapo wazuri sana, system haiwaungi mkono au kuwapa nafasi. Kwanini tunakinga visadolini, maguduria na bakuli na wengine kuning'inia katika chuchu za ng'ombe tukisubiri maziwa na uzalendo wake na kusahau kuwa hatujamlisha na amekondeana? Kwanini tunawahukumu wasomi na kuwatolea hukumu tukiwa na vipande vya ushahidi visivyoungika.
Je mtu akijenga hoja kwamba CCM inawaunga mkono na kuwapa nafasi ndio maana wanakimbilia kugombea nafasi za uongozi how would you counter this argument; Au je, mtu akijenga hoja kwamba kuwaunga mkono na kuwapa nafasi includes kuwapatia nyadhifa ndani ya chama, what would be your counter argument?
 
Mkuu Mchambuzi, niwaombe radhi wanajamvi kuwa hoja zako ni nzito na zinahitaji ufafanuzi wa kina.
Kwa upande wangu nitajitahidi kufupisha majibu na hata mengine kuayaaunganisha kama yatakuwa na ufanano.

Kwanza nirejee hoja yangu kuwa kuna viongozi na Watawala. Viongozi ni wale wanaowasikiliza watu, wakachanganua mambo na kutoa majibu kwa jamii yao. Watawala ni watu wanaotumia nguvu walizopewa kisheria au iwavyo kuwaongoza watu. Mara zote viongozi hutokea kuwa watawala wazuri na si kinyume chake.

Tukirejea historia ya ukombozi na miongo mitatu baadaye, ni ukweli kuwa Nyerere hakuongoza akiwa na wasomi. Bunge na serikali yake ilikuwa na watu kama madereva n.k.
Ni ukweli kuwa hatua tuliyopiga kuweka misingi ya utaifa, kijamii na hata kiuchumi ni kubwa kuliko miaka ya viongozi watatu waliofuata. Najaua kiuchumi wapo wanaoguna, ninachosema hapa ni misingi ya uchumi wa muda mrefu, siyo uchumi bandia tuanaouona.

Hilo liliwezekana kwasababu timu yake ilijaa wazalendo, ilikuwa na nidhamu na ili heshimu umma. Wataalam wachache walitumika vema katika kupanga mipango, na viongozi walitumia busara zao kuhakikisha kuwa mipango hiyo inatekelezeka kwa kile kilichokusudiwa. Kwa mfano, mapnago wa kupata medical assistants ulitoka nchi za nje kama Cuba n.k. Wasomi wetu wachache wakauweka katika mazingira ya ki-Tanzania hadi leo tuna MD kwa maelfu.

Viongozi walielewa wazi kuwa kupata wataalam ni jambo moja na kuwa na nyenzo ni jambo jingine. Busara ikatumika kuhakikisha kuwa kila kituo cha afya kilichotarajiwa kujengwa kilijengwa. Pita vijijini utaona 'zahanati imefunguliwa na.. mwaka 1963, 67, 72 n.k. Usimamizi ulifanywa na viongozi wengine wakiwa hawana elimu, lakini wakiongozwa na busara, hekima na uzalendo.

Ninachosema hapa ni kuwa usomi ni kigezo muhimu sana cha uongozi, but not a prerequiesite to good leadership.
Siyo kila msomi au mtaalamu anaweza kuwa kiongozi, na hiyo haifanyi utaalamu wake au usomi uwe na kasoro.
Uongozi ni zaidi ya hapo, ni busara, hekima, maono vitu anavyozaliwa navyo mwanadamu, tofauti ni kuwa kwa wengine ni recessive na baadhi ni dorminant. Kwa wingine exposure inasaidia wasio na fursa wanabaki mitaani

Nijibu hoja:
(i)Kwamba CCM inashangilia kuwa na wasomi.
Hakuna chama kilicho na wasomi wengi tena wenye uzoefu kama CCM. Kushangilia kuwa kuna wasomi wamejiunga na chama leo ni kutoelewa historia ya chama kama si mbiu za kisiasa za kuughilibu umma. Angalia ndani ya bunge la sasa, asilimia zaidi ya 85 ya wabunge wapo katika viwango vya usomi wa hali ya juu. Kipi leo kinaonekana cha ajabu ambacho CCM haakuwa nacho mwezi uliopita?

(ii)Kwamba wasomi sasa wanakimbilia CCM!
Katika kundi la jamii lisiloipenda CCM ni kundi la wasomi. Ninawajua marafiki zangu waliokuwa wapinzani kindaki ndani na walipotaka uongozi walihamia CCM.
Niliwauliza kwanini? Wakasema ili 'mambo yako yanyooke' ni lazima uwe ndani ya system.
Wakasema CCM wanauwezo 'pesa', wanadola (police, PCCB, tume ya uchaguzi n.k)

Katika chama kisichowapenda wasomi kwasasa hivi ni CCM. Na ndiyo sababu mtaji wa chama umekuwa vijijini.
Kinachotokea hapa ni ule msemo wa 'Nifae kwa mvua nikufae kwa jua'.

Itaendelea....
 
Inaendelea..
Kundi la wasomi linalokimbilia CCM ni wale ambao hawajiamini na wameshindwa kusoma mazingira.
Tanzania ya leo mtu anaweza kuwa Chama chochote na bado akapata nafasi ya kulitumikia taifa.
Vijana wadogo walioingia siasa na sasa wana nafasi kama za uwakilishi tena kwa kupambana na CCM.

(ii)Kundi la wasomi linafuata masilahi kwasababu nchini kwetu siasa ndiyo kazi inayolipa sana.
Ndiyo kazi mtu anaweza kuifanya bila kuwajibika.Hakuna msomi anayemfikia mbunge wa Tanzania kimapato.
Ni wasomi wachache wanaoeweza kufanya 'dili' zao zikafanikiwa wakiwa si wana NEC au CC, hata hivyo ni lazima wawe na link.Kuvutika kwao ndani ya CCM kuna nguvu ya ziada itakayowawesha kujikwamua kimaisha.

(iv)Je,CCM nawaunga mkono wasomi kugombea nafasi za uongozi.
Jibu ni hapana, mazingira ndiyo yanailazmisha.Wanachokifanya ni kuiga upinzani wakidhani kuwa umaarufu wa Chadema ni kutokana na wasomi, wasichokijua ni kuwa wao ndio chanzo cha kuupa upinzani nguvu, kwamba tatizo lipo ndani na wala si nje. Endapo wangelikuwa wanaunga mkono wasomi tusingesikia hoja za kuwatisha kila wanapotoa mawazo mbadala.

Watapewa nafasi ndani ya CCM kwa masharti ya kuwa watiifu, wafunge midomo na waitikie ndiyoo.
Angalia Wabunge wanavyodhalilika,wanaitwa chini ya kamati za chama na kutishwa kisa wanasimamia masilahi ya umma.
Angalia NEC na CC, ni kitu gani unachoweza kusema kinafanyika kwa mantiki ya usomi zaidi ya mipasho na majungu.

(v)Kwa maana hii, wasomi kukimbilia CCM haina maana kwamba kuna lolote litakalo badilika?
Hakuna kitakachobadilika, wataingizwa katika mfumo na kujikuta wanalazimika kufungia degree zao makabatini.
Tujiulize ni lipi lililoshindikana katika wingu la wasomi waliopo kufanya cha maana?

Ukishaingia katika system unakubali hata usichokiamini. Fikiria, profesa anapolazimishwa kutoa data za ajira milioni 1, tukijua wazi kuwa Tanzania hatuna mfumo wa kubaini ajira zilizotengenezwa au kupotea! huyo ni profesa.

(vi)J
e hawa wasomi wanakimbilia CCM kugombea hizo nafasi za NEC na vitu kama hivyo, wanafanya hivyo kwa kutegemea kwamba mchango wao kwa taifa utathaminiwa na mawazo yao kusikilizwa kupitia CCM?
Kukimbilia ndani ya NEC au CC hakuna maana ya kulihudumia taifa, ni njia ya kumiliki chama ili waidhibiti serikali na ni kwa mambo yatawanyookea. Kwanini Mbunge ang'ang'anie ujumbe wa NEC? Kwanini mawaziri wakuu wastaafu wang'ang'anie NEC?

(VI)
msomi akiingia CCM ni rahisi kuwa corrupted and rot; kwa maana hii, wasomi wengi waliojitokeza kuwania nyadhifa ndani ya chaguzi zinazoendelea wanaenda kuwa corrupted na kuwa rot,?
Huwezi ku-survive CCM ukiwa pristine. Uwepo wa yoyote ni lazima uambatane na corruptio.Absolutely!
Waliojaribu wamekiona cha moto, unakumbuka ya Spika na wale waliokimbia!

(vii)k
wa mtazamo wako, does CCM have any critical thinkers? Why or why not? na je, ni kwa sababu nyingine nje ya kuangalia maslahi mbele au ni suala la kimfumo zaidi?
CCM ina critical thinkers wengi sana, ina hazina ya wazoefu, wenye busara,hekima na wasomi.
Tatizo ni kuwa mfumo umeruhusu corrupted minds kumiliki chama.

Critical thinkers wanaonekana kama vibaraka, wanakiuka taratibu za funga mdomo, ni wasema hovyo na hawaoni kitu wakatulia. Mfumo unawatupa nje ya circle ya uongozi. Ukitaka kujua hili, mfumo umetengeneza kitu kinaitwa baraza la ushauri ili kuwaondoa baadhi ya 'wavurugaji' katika safu ya uongozi wa nchi.

(viii)
Je, tunao wasomi/wataalam lakini mazingira (social and economic institutions and infrastructure) zinawanyima nafasi kutumia uwezo wao kuchangia ujenzi wa taifa?
Hili hasa ndilo tatizo. Katika nchi za wenzetu wanasiasa ni wasimamizi wa hoja za wataalamu.
Katika nchi yetu wanasiasa ndio wanaowaongoza wataalamu.

Narudia mfano, hivi mwanasiasa anasimama vipi na kutangaza Hospitali X kuwa ya rufaa huku wataalamu wakiwa hawajui? Hivi mwanasiasa anasimamaje kupima uzito wa tatizo la nishati na kutoa maamuzi bila kuwasiliana na wataalam?
Hivi mwanasiasa anawezaje kusema kilimo kwanza bila kuwa na hoja za kitaalam kutoka kwa wataalam?
Inakuwaje mawaziri wakuu wawili katika kipindi cha miaka 5 wawe na 'sera' tofauti i.e Kilimo kwanza na Shule za kata?
Je hawa wanaongozwa na sera za chama au mawazo na utashi wao wa kisiasa

Kuna mtaalam au msomi gani alishirikishwa kama siyo kukurupuka tu na kuanzisha unsustainable projects.
Wapi ilitumika manifesto ya CCM iliyoandikwa na wasomi ambayo ukiiangalia ina uzuri wa kitaalam.
Sasa hapa CCM imewatumiaje wasomi, na kama siyo itawatumiaje serikalini.

(ix)
Kwa mtazamo wako, nini ni matarajio ya wasomi hawa in relation to swali lako...
Matarajio ya wasomi wanaojiunga na CCM ni kutumika tu. Kazi zao zitakuwa mapambo mazuri.
Watarajie kujiunga katika system, kuacha elimu zao majumbani na kumsikiliza katibu kata.
Watajifunza kuwa wanafiki, waongo na wasio na haya kuudanganya umma.
Wakishakubali hayo watapewa mkate wao.
Kama yupo anayedhani kuwa anaweza kuibadili CCM hapa ilipo basi kabla hajafanya hivyo achukue day off kumuona Daktari anayeshughulikia mfumo wa fahamu.

Mfumo mzima wa chama umetekwa nyara na kundi la maharamia.
Hali imefikia mahali pa kutafutana kuuana.
Msomi mwenye dhati ya kulikomboa taifa itamuia vigumu kujiunga nao.
Msomi anayedhani njia rahisi ya maisha ni kupitia CCM atafanya kila awezalo ajiunge na mfumo.

Vigele gele tunavyosikia ni kutuondoa katika hoja ya msingi, kujenga matumaini ya uongo na kuziba ufa ndani ya chama kwa kutumia pamba. Ukweli ni kuwa hakuna msomi anayejiunga na CCM kwa sasa tukatumaini ataibadilisha, wala hakuna atakayeweza kuvunja ngome iliyojijenga isipokuwa maasi kwa wanachama au mpasuko wa chama.

CCM inaelekea kaburini ikiwa na hazina ya werevu,weledi na wazalendo.
Mfumo unaolea makundi ya kurithishana uongozi kama ufalme, kutafuta uongozi kwa rushwa, kulindana kwa pesa na sumu unakimaliza chama.

Tatizo sio wasomi, wala rasilimali ni ukosefu wa watu wenye uzalendo, waadilifu na waliotayari kulikomboa taifa.
Tatizo ni kuwa na wasomi feki wasiojitambua, waliotayari kuuza intellect zao kwa ujira wa mafao.
Walio tayari kulisaliti taifa kwa kuficha elimu zao uvunguni ili wawe sehemu ya maangamizi ya taifa.

Kuna nyakati sauti za kilio zinaweza kufanana na kushangilia, hizi tambo za wasomi kujiunga, huenda ni sauti za kilio tunazosikia kama vigele vigele.
Huwezi kuwa na wasomi waliozaliwa tarehe 25/9/2012 huku ukishindwa kulitumia kundi ulilo nalo miaka 7 au 10 iliyopita.


 
Update...

Mkuu Mchambuzi, nadhani umesikia yaliyotokea Dodoma.

JK amethibitisha kwa maneno yake kuwa kuwania NEC ni kwa masilahi binafsi, akaonyesha jinsi watu wanavyotaka kuuana.

Umeona majina ya watu waliokatwa. Sababu kubwa ni kutumia hekima zao katika kuliendeleza taifa.

Hii inashadidia hoja yangu kuwa huwezi kuwa ndani ya CCM, msomi au wakawaida ukaleta mabadiliko.

Chama hakikubali mawazo mbadala, leo akina Filikunjombe waliosema hili si sahihi kwa taifa wanabaki wahanga (victims). Wakati hayo yakiendelea, 'wenye' chama na ambao tunajua uchafu wao kuanzia ubadhirifu, hila za kuuana, ufisadi n.k wamebaki ndani ya chama.

Hii maana yake ni kuwa wasomi tulioambiwa wanaingia ndani ya CCM, siyo kuwa wanakwenda kuleta mabadiliko la hasha! wanakwenda 'gerezani' na ili waendelee ni lazima wafungie akili zao kabatini, wafiche degree zao na vae vilemba vya unafiki, uongo na hata wendawazimu.

Kumbuka hawa wasomi ndio wataalam wa nyanja mbalimbali.

Je, tutawalaumu kuwa hawafai, usomi wao ni hafifu, hawalisaidii taifa n.k?

Nadhani yanayotokea Dodoama yanatetea mabandiko yangu na hoja kuwa, tatizo siyo wasomi, ni mfumo mzima. Niambie ni msomi gani ndani ya NEC au CC atakayeweza kutumia usomi wake kuleta mabadiliko katika taifa.

Nikupe hint kidogo kuhusu neno 'wenye chama':
Wapo walioenguliwa eti kwasababu wanataka kuuana. Hapa ni Bashe na Kigwangalla. Huko nyuma Spika Sitta alishawahi kuomba ulinzi kwasababu ilipangwa ajali kwa ajili yake. Kundi lililoratibu 'ajali' hiyo linajulikana, leo wameachwa kugombea tena wakiwa na nyadhifa za kamati mbali mbali za chama na bunge.

Hao ndio wenye chama!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Nguruvi3,

Asante sana kwa mchango wako mzuri uliojaa hoja nzito sana; Nitakurudia muda si mrefu;
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3,

Nashukuru sana kwa mchango wako uliosheheni hoja za maana sana. Naomba niseme tu kwamba kwa kweli hoja zako zimezidi kuchangamsha na kupanua sana fikra zangu; Nitajitahidi kujadili mambo ambayo naona ni muhimu, na iwapo kuna jambo ambalo utadhani nimeliacha, tafadhali usisite kunijulisha;

Kwanza, kuhusu nafasi ya wasomi katika Maendeleo ya taifa letu, naunga mkono hoja yako, hasa juu ya umuhimu wa watu hawa as ‘critical thinkers’, sio kwa CCM tu bali taifa kwa ujumla. Siku za nyuma, niliwahi kulijadili suala hili kidogo katika majibu yangu kwa mdau mwenzetu Pasco, na ukipata muda, naomba upitie thread ifuatayo, kwenye ukuruasa wa TANo Post Number 235: https://www.jamiiforums.com/tanzani...-edward-lowassa-then-2015-ni-ccm-tena-12.html

Kuhusu hoja yako juu ya Wasomi wanaokimbilia CCM ni kutokana na wao kutojiamini lakini pia kushindwa kusoma mazingira, kwa hili naunga mkono hoja, lakini naomba niongezee pia kwamba, mara nyingine wasomi hawa huwa na uelewa mkubwa tu juu ya mazingira lakini kutokana na ‘up bring’ yao na vilevile socialization processes walizopitia, they just decide to become ignorant kwani kwa njia hiyo ndio wataweza kurithishwa mfumo mbovu uliojengwa na wazee wao tofauti na popular expectations kwamba Vijana wasomi wanatakiwa kutumia fursa zilizopo wawe kama Agents of Change. Ni kutokana na ukosefu wa Uzalendo as you rightly have put it, ndio maana wanageuka kuwa wasomi uchwara na wa kimaslahi zaidi;

Kuna hoja zako nyingine mbili ambazo ningependa kuzijadili kwa pamoja ambazo ni: ile inayohusu Vijana wasomi kukimbilia CCM kwa imani kwamba siasa inalipa in terms of ajira, income n.k; na ile inayohusu Vijana kupewa nafasi za uongozi ndani ya CCM kwa masharti ya kuwa watiifu na wafunga midomo. Ningependa kutumia quotations mbili muhimu katika maoni yangu juu ya hili kama ifuatavyo: Ya kwanza ni ya Mwalimu Nyerere, kutoka kwenye barua ya Kujiuzulu Ubunge mwaka 1957, aliyomwandika Gavana wa kikoloni ndani ya kipindi kifupi cha uteuzi wake:


******
“[I have given everything that it was in my power to give and what I have given has been rejected. I came to the council expecting a little of the spirit of give and take. That spirit is not there. I would feel that I am cheating the people and cheating my own organization if I remained on the council, receiving allowances and attending sundowners as an Honorable Member, giving the impression that I was still of some service on that council, when in fact I know that I am useless. I had therefore no alternative but to tender my resignation and to ask that my resignation take effect from Friday, 14[SUP]th[/SUP] December, 1957, the day my last compromises were rejected by the government”].
******


Mkuu Nguruvi3, unalionaje hili katika mazingira ya leo hali isiyotoa matumaini yoyote ya maana kwa wananchi kwa mwendo ule ule wa miaka 50 ya uhuru? Wabunge uliowataja kama Filikunjombe na wengine ambao wameangushwa na Uzalendo wao, je mazingira yao hayafananii na haya ya Mwalimu mwaka 1957? Kinachowazuia wao kuchukua uamuzi mgumu ni kitu gani?

Naomba pia niweke quotation nyingine ambayo nadhani pia ni muhimu na relevant katika hili. Haya ni maneno ya mmoja wa Statesman wa nchini Marekani aliyeishi in the 18[SUP]th[/SUP] Century - Dean Acheson ambae alitamka kwamba:


******
“I will undoubtedly have to seek what is happily known as gainful employment, which I am glad to say does not describe holding public office”
*****

Mkuu nguruvi3, this quotation nails home hoja yako ya Vijana Wasomi kukimbilia CCM kwa ajili ya ajira – kipato na madili yenye kuwapatia fedha. Hakika kwa vijana wa nama hii kwa kiasi kikubwa, Siasa kwao ni: “GAINFUL EMPLOYMENT”. Na kama ulivyojadili, vijana hawa wanajua kabisa kwamba wanaende huko kutumikia masuala mengine yalio nje ya wananchi au maslahi ya taifa.

Kuna hoja yako nyingine ambayo imenivutia sana – ile inayohusu uanzishwaji wa baraza la ushauri la CCM ambalo lita play kama a critical thinking body; Nakubaliana na wewe, na naomba nikiri kwamba sikuwahi kulitazama kwa jicho hilo;

In the section that follows, naomba nijumuishe hoja zako nyingine kadhaa ambazo hakika nimezipitia mstari kwa mstari na kubaini kwamba kama kuna neno moja lingebeba hoja hizi, basi ni “MFUMO”. Sana sana nitaelezea maoni yangu based on how hoja zako stimulated my thoughts, hasa hoja yako kwamba - Kwa wenzetu wanasiasa ni wasimamizi wa hoja za wataalam lakini kwetu wanasiasa ndio wanaoongoza wataalam.

Kwa bahati mbaya sana, moja ya matatizo yatokanayo na colonial legacy ni SUPREMACY OF POLITICS over and above everything else – RULE OF LAW, ECONOMICS n.k. Bila ya matumizi ya siasa, ingechukua muda mrefu sana nchi yetu kupata uhuru. Tatizo lililojitokeza ni kwamba, supremacy of politics ililelewa hata baada ya uhuru hivyo ku-infect na kudumaza nyanja nyingine zote muhimu katika taifa; Leo hii, watawala wetu wapo mkao wa ku - exercise political supremacy at the expense of everything else; Ndio maana kwa mtazamo wangu ambao pengine ni finyu, pamoja na mapungufu mengi yaliyokuja na Economic and political Reforms, kwa kiasi kikubwa, reforms hizi zimekuja na faida yake moja kubwa, hasa kusaidia kupunguza supremacy of politics nchini; Wengi wetu tunakubaliana kwamba ni Viongozi wachache sana kama Mwalimu na Sokone ambao walitumia supremacy ya siasa kwa maslahi ya taifa; na hata pale walipokosea, bado tunaweza kusema kwa kujiamini kwamba viongozi hawa ‘DID NOT PROFIT FROM POLITICS; Lakini katika nyakazi hizi, how true is that? No doubt wengi wao wapo mkao wa KIBIASHARA ZAIDI.

Mwanazuoni mmoja kutoka Sweden – GORAN HYDEN ana dhana moja that I find very useful kutusaidia kuelewa nini kinaendelea katika taifa letu, in the realm of hoja zako kadhaa. Dhana hii sio nyingine bali ile ya “ECONOMY OF AFFECTION”. Key pillars za dhana hii ni tatu:


  1. WHO YOU KNOW is more important than WHAT YOU KNOW;
  2. SHARING PERSONAL WEALTH is more rewarding than INVESTING IN ECONOMIC GROWTH & SOCIAL DEVELOPMENT &
  3. A HELPING HAND today generates RETURNS TOMORROW;


TUNAJIFUNZA NINI KATIKA HILI?
Huu ndio uchumi unaoendekezwa na CCM ya leo i.e. THE ECONOMY OF AFFECTION; uchumi wa namna hii unaishi ndani ya uchumi wa aina yoyote na ni tofauti kabisa na Ujamaa na Ubepari; Katika uchumi huu, Money isn’t an end in itself, lakini pia serikali sio the primary redistributive mechanism; Badala yake, uchumi unaendekeza na pia kuyapa kipaumbele mambo yafuatayo:


  • Handshake kuliko Contracts; &
  • Personal discretion kuliko official and rational policies to allocate rasilimali za nchi kwa maslahi ya taifa;

Uchumi huu ni kaka VIRUS ya Ukimwi kwani una uwezo mkubwa sana wa kujipenyeza sehemu yoyote na pia kuharibu/kuua kinga yoyote; Muhimu zaidi, mfumo huu una survive katika mazingira ya Ujamaa, Ubepari, mixed economy etc, bila ya tabu yoyote, na ndio maana pamoja na madhara makubwa ya baadhi ya sera za soko huria kwa wananchi walio wengi, demand for changes au opposition on mapungufu ya Liberalization, Privatization and Marketization kwa watanzania walio wengi (hasa vijijini), hata siku moja mtazamo au opposition ya namna hii haiwezi kutokea from the top (watawala); Imekuwa ni utamaduni kwa watawala kupuuza vilio vya wengi towards that end; WHY? Kwa sababu, Economy of Affection inawasaidia watawala to get around any hurdles or rough edges za any system be it Socialism, Capitalism, Mixed etc…. na kusonga mbele kiuchumi at the expense ya wananchi walio wengi;

ROLE YA WASOMI KATIKA MFUMO HUU NI IPI?
Ni vigumu sana kwa wasomi kubadili mfumo huu kwa maslahi ya taifa; Nitajaribu kufafanua; Uchumi wowote unaendeshwa na the principles of “EXCHANGE”; Lakini kwa bahati mbaya, chini ya ‘ECONOMY OF AFFECTION’, exchanges are not registered officially, na badala yake all important exchanges in the economy either stay informal or happen Under the table; The Economy of Affection is an invisible economy, kwahiyo WASOMI (policy makers for instance) wenye roho nyepesi na pia uhaba wa Uzalendo kwa taifa lao wanashawishika kwa urahisi sana kujiunga na mfumo huu;

Kitu kingine kibaya zaidi ni kwamba, hata wataalamu kama vile wachumi, wanasheria n.k, wanapata wakati mgumu kutumia their conventional forms of analysis to incorporate mfumo huu; Matokeo yake ni kwamba, wasomi wengi wanakuwa frustrated kwamba hawawezi kuleta change, na kwa wale wenye roho nyepesi, wanajiunga na mfumo huu in practice; pia huwa inatokea kwamba wasomi wanapokuwa nje ya mfumo huu, ni kawaida sana kwa wao kuonekana ni mabingwa katika fani zao, wazalendo, n.k, lakini mara tu wanapotia mguu ndani ya System, mfano huko mawizarani, bungeni, ikulu n.k, wanaishiwa energy waliyokuwa na nayo na wanajikuta na three options: Jiuzulu, initiate policy reforms individually, au join the parade; wengi huishia ku ‘join the parade’ ya Economy of affection;

Naomba nimalizie mchango wangu kwa kujadili kidigo hoja yako nyingine muhimu sana – hoja kuhusu Mawaziri Wakuu Wawili ndani ya miaka mitano kuwa na misimamo tofauti kuhusu vipaumbele vya TAIFA. Kwa mtazamo wangu, chanzo kikuba cha cha tatizo hili pia ni Colonial Legacy; Serikali/State imekuwa katika mgogoro mkubwa sana kiutawala kutokana na muingiliano uliopo baina ya Taasisi za Umma (formal and civic institutions) na Community institutions. Mwalimu Nyerere alijaribu sana kurekebisha hili lakini hakufanikiwa kumaliza the project; nitafafanua;

Ebu tutazame kwanza Dhana ya “STATE”

The State (almost equivalent to serikali) kwa kawaida huibuka in response to mahitaji yaliyopo miongoni mwa makundi mbalimbali ndani ya jamii husika kama vile ulinzi na usalama, ustawi wa jamii, lakini muhimu zaidi umuhimu wa kutatua the never ending conflicting demands on scarce resources vis-à-vis unlimited wants, and for our matter – Suala la ELIMU KWANZA VS KILIMO KWANZA;

The state is made up of hierarchy of organizations mbalimbali established for the purpose ya kufanikisha malengo mbalimbali ya kiuchumi, kisiasa na kijamii; Watumishi wa serikali kwa kawaida hutegemewa na jamii to perform roles fulani fulani katika taasisi na ngazi mbalimbali za serikali towards that end; in the process, watumishi hawa wanatakiwa kuweka pembeni any pursuit of self interest na badala yake to act zaidi in the interest of the public; Mara nyingi utekelezaji wa dhana hii huwa ni mgumu sana katika nchi kama zetu i.e. ni vigumu sana kwa watumishi wengi wa umma kuweka mpaka unaoeleweka baina ya private and public interest au a personal and official issues; Ni kawaida sana kwa watumishi wa serikali wa ngazi mbalimbali kutumia dhamana yao waliyopewa na umma to favour their own interest at the expense of public interest; Je kwanini inatokea hivi?

Tunarudi pale pale kwenye colonial legacy ambayo Nyerere alijitahidi kuifuta lakini waliompokea hawakuendeleza juhudi zake; tutazame kidogo historia ili nieleweke vizuri zaidi; Wakati wa harakati za kutafuta uhuru, in principle, nationalist leaders kama Nyerere walikuwa wanaiogomea serikali ya kikoloni pamoja na taasisi zake ilizoziunda; In the process, nationalist leaders na wafuasi wao (mfano TANU) did not find civic institutions as legitimate; Kwa maana nyingine, legitimate institutions in this context zilikuwa ni zile zilizokuwepo ndani ya jamii, hasa zile informal na ni hizi ndizo Nyerere na wananchi walizipa uzito wa legitimacy kuliko zile za serikali; taasisi za serikali ya kikoloni ni hizi ambao tunazo leo kama vile mahakama, polisi, n.k, na taasisi za kijamii (community institutions) zilikuwa ni zile zilizotokana na imani mbalimbali za dini, mila, ukabila, occupation ya watanganyika mbalimbali n.k); Loss of legitimacy ya government institutions ndio ilipelekea eventually kwa serikali ya kikoloni kuporomoka, kwani haikuwa na uhalali mbele ya umma ikifananishwa na institutions za watanganyika weusi huko kweney community zao mbalimbali, institutions ambazo TANU iliwekeza sana katika harakati zake za uhuru;

Baada ya uhuru, Nyerere alijaribu to pursue development policies kwa aidha kuziweka inherited institutions toka kwa mkoloni ziwe mkao wa wananchi zaidi lakini mara nyingine kuanzisha nyingine mpya from scratch; in the end, nia ya Mwalimu ilikuwa ni kujaribu kuzifanya hizi institutions sasa ndio ziwe na legitimate role over and above zile community institutions za awali; mradi huu ulikuwa ni mgumu sana kwani nje ya Mwalimu, viongozi wengi walitokana na community institutions huko kwenye maeneo yao Kwahiyo walizidi kuendekeza such institutions at the expense of the state institutions; in other words, viongozi wengi nje ya Mwalimu, lakini sana waliomfuatia walijengwa na local community zao, hawakuwa viongozi wa kitaifa moja kwa moja, na utamaduni huu unaendelea hata leo;

Viongozi wengi wa leo tunaowasikia wakivuma huku na kule wamejengwa na community institutions za huko wanapotoka, whether ni upareni, umasaini, uhayani, ugogoni, n.k, hasa kwa kupitia nafasi zao za ubunge ambapo baadae ndio huchaguliwa kuwa mawaziri n.k, au viongozi wa kitaifa. Kwahiyo, hata kwa wengi ya viongozi hawa, loyatly yao kwanza ni wanapotoka, then taifa ndio hufuata; ndio maana unakuta mara nyingi kuna tendency ya wao kuheshimu zaidi community institutions za huko wanapotoka kuliko state or civic institutions na matokeo yake, wanafanya maamuzi mengi sana hata yanayohusishwa matumzi ya fedha za umma, kuendeleza loyalty yao huko makwao; Ndio maana suala la viongozi kuja na Agenda ya KILIMO KWANZA kwasababu huko kwao kilimo ndio ajira kuu, au kiongozi kuja na agenda ya ELIMU kwanza kwasababu kwao wapo nyuma kielimu, au ELIMU kwanza kwasababu wanaogopa kilimo kitaua ufugaji (recall ugomvi wa ardhi baina ya wakulima na wafugaji) etc etc, haya yanaendelea kuwa ni mambo ya kawaida miongoni mwa viongozi wengi, licha ya Usomi na ufahamu wao mkubwa;
 
Je hawa wasomi wanakimbilia CCM kugombea hizo nafasi za NEC na vitu kama hivyo, wanafanya hivyo kwa kutegemea kwamba mchango wao kwa taifa utathaminiwa na mawazo yao kusikilizwa kupitia CCM?

Hoja hii inatoa ishara kwamba pengine CCM ilifanikiwa zaidi enzi zile ilipokuwa na wasomi wachache kulik hivi sasa ambapo ni kinyume; je hii ina uhusiano wowote na dis-economies of scale? Au je ni suala la uzalendo? au je ni simply CCM kutokamata tena hatamu na hivyo kutokuwa tena in the commanding heights za kuendesha uchumi kupitia parastatals mbalimbali ambapo zilijazwa wasomi wa kila aina?

Mchambuzi kuna jambo moja unatakiwa kukumbuka. Siku hizi Chama ni conduit pipe. Ni wachache sana ambao wanaogombea uongozi ndani ya CCM ili kusukuma ajenda ya Ujamaa na kujitegemea ya CCM.

Wasomi wanakimbilia CCM kwa kuwa CCM ndio chama chenye nafasi kubwa kuingia madarakani, na CCM ikiwa madarakani wenye chance kubwa ya kupata nafasi za uongozi wa kisiasa serikalini ni wasomi. Si kama wana mapenzi na CCM, si kama wana ndoto ya kuiendeleza Tanzania kupitia chama, wanaitumia CCM kama daraja na ngazi ya kufikia malengo yao, binafsi.

Naweza kukuuliza swali moja, do you really believe that Edward Lowassa is in CCM because he believes in ujamaa na kujitegemea, or because he is longing to see Tanzania and Tanzanians are becoming better? NO way, anataka kujitajirisha tu, na kulewa madaraka. May be we leave him alone because he is an aspirant, hatujamuona akiwa rais.

Umeona JK katika miaka nane ya urais wake, unaweza kueleza ni nini kilimfanya atake kuwa rais na amefanya nini na urais huo? sana sana unaweza kusema ni mambo binafsi tu na kuridhisha nafsi yake. He did not do a thing that he can stand before Tanzania and say i did this for Tanzania.

Wabunge, na watu wa NEC same story........

Kwa hiyo wasomi nao ni binadamu wenye ndoto zao binafsi zinazoweza kutimia kwa kutumia daraja na ngazi ya CCM. Kama tungekuwa kama nchi za Ulaya na Asia, ambako maisha mazuri unapata kwa profesion yako na sio siasa, nadhani wasomi wetu wasingejihangaisha na siasa zetu za matusi, majungu na ushirikina. Marekani ukiwa Professa havard unaweza ku-make kuliko senator na congressman, ukiwa basketball player unaweza ku-make kuliko Obama, Uingereza kijana mdogo Theo Walcot ana make kuliko waziri mkuu. Lakini Tanzania wanao-make wengi ni wanasiasa, ndio maana watu wanapigana risasi, wanawekeana sumu kwa sababu ya siasa.

kuna siku Sumaye alisema "ukitaka mambo yako yakunyokee ingia CCM". Unajua inauma sana kuona mtu umesoma mpaka Ulaya na Marekani kwa taabu kwa hope kuwa utakuja kutoa mchango kwa nchi yako, unaishia kuwekwa kuwa ofisa utawala hospitali ya Muhimbili, ofisi inanuka na ina vumbi kama nini, viti ovyo hata kuliko tunavyoviona kwenye movie za charlie Chaplin, mshahara hautoshi hata chakula decent kwa mwezi.

Lakini ukiangalia mbunge ambaye hajamaliza hata kidato cha NNE, yuko well off kuliko hata professor, Dr au Engineer.

Moja ya sababu ya CCM kuyumba kwa sasa ni kuwa haina waadilifu na watu makini wakutosha. Kwenye centers za decision making za chama ukiangalia watu waliomo ni vichekesho, na wanaofaa kama kina Kinana ndio hao wameondoka.
 
Mkuu Mchambuzi,
Hiyo quote ya Nyerere wakati ana resign inasimama kama ilivyo leo hii.
Ni hiyo ndiyo inayoonyesha kiongozi ni nani na mdandia uongozi ni yupi.

Kwanini watu kama Filikunjombe wasichukue hatua kama za Mwalimu?
Hawa wana mapungufu yanayotokana na 'conflict of interest'. Wanahisi kuwa utamu walio nao kwasasa unawaweka uzuri kimaisha. Wakati huo huo kunadhamira inawasuta kuwa kinachoendelea si sahihi.
Utamu unawafanya wawe short sighted na wasiweze kuangalia mazingira kwa upana wake.

Wanashindwa kusoma mazingira kwa kutoelewa siasa kikamilifu, up and down zake na jinsi ya kujenga career for longterm. Wana 'upofu' wa kuamini kuwa yaliyomkuta Njelu au Ntagazwa yanaweza kuwakuta.
Ni up bring uliyosema inayowasumbua na hadithi za mitaani.

Kwanini wasijiulize Makongoro alimpinga baba yake na kupewa nafasi ya uongozi. Kwanini Mrema amekuwa na political come back nyingi na wanashindwa kutambua na kujiuliza Mtei alipotofautiana na Mwalimu jambo hilo lili reflect maisha yake politically n.k.

Vijana hawa wamesahau kuwa mwongozo wa TANU wa mwaka 1970 unasema 'Heshima ya mtu itatokana na huduma yake kwa jamii' na wameshindwa kusoma maandiko mbali mbali juu ya siasa na uongozi kama ulivyonukuu kwa uchache.
Huduma kwa jamii ni pamoja na kusimamia kile mtu anachoamini ni sahihi kwa watu wake

Lakini pia kuna vitu vinaitwa dhamira na makusudio.
Dhamira ni kile unachoamini, mathalani, Fred Mpendazoe aliamini kwa dhamira kabisa kuwa wakati wa kupigana nje ya CCM ulikuwa tayari. Akaondoka mchana kweupe.

Makusudio ni kile kitu mtu anafanya kwasababu ya! na mara nyingi hutokea katika siasa.
Haifanyiki kwasababu dhamira inamtuma mtu hivyo, la hasha! inafanyika pengine kutafuta political fame.

Kuhusu namna tunavyopata viongozi, nakubaliana nawe kabisa kuhusu viongozi kutoka katika institution za huko watotakako. Mfumo wetu ni mbaya na hakuna vetting system ya kupata viongozi.

Kwa nchi za wenzetu huchaguliwi kuwa Jaji au waziri bila kuwa na kitu cha kuonyesha 'performance'.
Angalia Mitt Romney anavyoandamwa na BAIN, watu wanamungalia kuanzia huko alikotoka kabla ya kumpa nafasi.

Na mwisho hatuna mfumo wa kisiasa wa ukweli. Kilichopo ni vurugu tu kama za mawaziri kuwa na sera tofauti pengine nje ya sera za chama chao. Ni personal interest zinafanya kazi na siyo system as whole.
 
Mkuu nguruvi3,

Asante kwa mchango wako. Nafurahi kwamba tunazidi kufanya diagnosis na kubaini chanzo cha magonjwa mbalimbali yanayokabili utawala wa nchi yetu; Ni matumaini yangu kwamba in the process, pia tutafanikiwa kuja na remedies ambazo ni practical na zinazozingatia pia changamoto zilizopo;

Nikianza na Fred Mpendazoe, mwanasiasa huyu kwa kweli alistahili kupewa heshima ya juu sana na wapenda mabadiliko lakini sielewi kwanini heshima hiyo hatuioni kutoka kwa wananchi, na wala viongozi wazalendo ndani ya CCM; Vile vile nahisi huko alipo (Chadema), hapewi uzito unaostahili;

Suala la mapungufu waliyonayo viongozi kama Fulikonjombe nadhani inatokana na ukweli kwamba nchi yetu haijawahi kupata viongozi wenye ‘strong sense of public service' kama Mwalimu. Kwa kweli ni vigumu sana kuelewa kwanini Mtu kama Mwalimu aliweza kumudu nafasi ile without profiting from Siasa, tena katika nyakati zile ambapo cold war ilitoa so many loopholes kwa viongozi kujinufaisha na siasa; How do we instill the same tone kwa viongozi wetu leo? Sitegemei uje na jibu, lakini wapo wanaosema tunahitaji Rais Dikteta, mfano wa Kagame, wapo wanaosema Katiba mpya ndio solution, Wapo wanaosema Chadema ndio mkombozi, the list goes on, lakini binafsi naona katika yote haya, changamoto ni nyingi kuliko tunavyofikiri.

Binafsi nazidi kusititiza kwamba tatizo tulilonalo kiini chake ni kwamba: POLITICS HAVE BECOME SUPREME TO EVERYTHING ELSE. Kutokana na hili, Kila kitu kingine kama vile RULE OF LAW, ECONOMICS, ACCOUNTABILITY, n.k are secondary to Politics; Na cha kusikitisha ni kwamba inapotokea WATAWALA wanatikiswa kidogo tu na UMMA demanding change, wanakimbilia hoja za AMANI NA UTULIVU, na haya vile vile ni mafanikio pekee ya CCM kwani nje ya mafanikio ya KISIASA, CCM imefeli katika mambo mengine karibia yote; Na hata kwa yale madogo ambayo imejitahidi kuyafanyia kazi, ni kutokana na msukumo wa kisiasa, na sio vinginevyo, ndio maana unakuta Maendeleo ya maeneo mbalimbali ya nchi yapo so inequitable, na pia income distribution so uneven; WATAWALA wapo more loyal to their local communities than the country at large;

We all know kwamba - Peace means AN ABSENCE OF WAR. Lakini kama MAO alivyowahi tamka - Politics is War without Bloodshed while War is Politics with Bloodshed; Kama utakubaliana na maneno haya ya MAO, basi kutokana na madhaifu yaliyopo katika utawala wa nchi yetu ambayo yanayopelekea wananchi walio wengi kukosa haki za msingi kabisa katika kila nyanja za Maisha yao – Political Injustice, Economic Injustice & Social Injustice, THEN TANZANIA IS ALREADY AT WAR.

Mwisho ningependa kuzungumia kidogo dhana ya WANANCHI; Hivi kwa mtazamo wako, dhana hii inatumika kwa maana ile ile nyakati hizi ikifananishwa na enzi za Mwalimu? Enzi za Mwalimu, dhana hii ilitawala karibia kila nyanja ya maisha ya watanzania na matokeo yake yalionekana wazi kabisa; Lakini leo hii, with ideas of individualism, private accumulation of wealth & the market, kwa mtazamo wangu, dhana ya WANANCHI haipo tena kama ilivyokuwa enzi za Mwalimu, hasa in the context of Socio-Economic Development; Katika nyakati hizi, hakuna tena Collective Leadership & Collective Responsibility, kama nilivyoelezea, watawala wapo more loyal to their local communities kuliko TAIFA, na pia more loyal to their inner circles, hasa kwa kutekeleza kanuni ya Economy of Affection: A HELPING HAND today generates RETURNS TOMORROW.

Kinachoendelea ni utawala wa kundi fulani la watu wanaojihisi kwamba wao ndio wenye mamlaka na nchi yetu kuliko wananchi wengine, and in the process, wanatumia ‘political office' kwa manufaa yao binafsi na wale waliowapa madaraka; Kwa mfano, katika kila Bajeti ya nchi, tunaona the government is growing faster kuliko sekta nyingine yoyote ya uchumi kwani humo ndipo nafasi ya watawala kupeana madaraka na miradi itakayowanufaisha wao badala ya wananchi; Ushahidi wa hili ni kuangalia bajeti za kila mwaka ambapo Matumizi ya Kawaida – Mishahara, Posho, Tenders n.k ndio huchukua fungu kubwa zaidi la bajeti kuliko matumizi ya Maendeleo ambayo haya essentially are meant kulenga Wananchi. Na hata katika fedha ndogo zinazopelekwa kwenye fungu la matumizi ya Maendeleo, huko pia kwa kiasi kikubwa ni sehemu ya ulaji kwani miradi mingi ya Maendeleo inayolenga WANANCHI, haitekelezwi miaka nenda miaka rudi.
Kuna kitabu kimoja ambacho ndani yake Mwalimu Nyerere anaelezea tofauti iliyopo baina ya Afrika na Asia in terms of Tatizo la Rushwa. Hadithi inaanza na ziara ya Waziri kutoka nchi ya Africa ambae alimtembelea Waziri mwenzake barani Asia na kuvutiwa sana na JUMBA lake la kifahari: I quote maneno kama ifuatavyo:

"How did you afford all this on a minister's salary?" he asked. Pointing through his living-room window, his host said: "Do you see that large bridge in the distance?" Yes, replied the African. ‘Well, part of its budget came my way," the Asian explained. The next year, reciprocating the visit, the Asian minister asked the same question. "Do you see that road down the valley?" asked the African. "No", he replied. "I see nothing". "Exactly", explained the African. "I financed this house instead".

Mkuu nguruvi3, we have done a lot of DIAGNOSIS & have determined the DISEASE; In your view, What's the CURE?
 
Bongolander,

Nashukuru kwa mchango wako; Kwa kweli sioni kama ni ajabu kwa mtanzania wa leo mwenye uelewa kuona kwamba tuna wanasiasa ambao ni kama wendawazimu pamoja na usomi wao; Kwa kweli mimi yule mweka hazina (nadhani unaelewa namzungumzia nani) ninamuonea huruma sana; Mimi nadhani kwa mwanasiasa kama huyu, iwapo kweli nguvu za giza zipo, basi zimetumika pale pengine kutokana na wanasiasa wengine kuitaka sana nafasi ile aliyonayo, vinginevyo matendo yake kwa kweli hayaendani na elimu/usomi na upeo tunaoambiwa anao, lakini muhimu zaidi, ni kinyume kabisa na generation yake;

Naweza kukuuliza swali moja, do you really believe that Edward Lowassa is in CCM because he believes in ujamaa na kujitegemea, or because he is longing to see Tanzania and Tanzanians are becoming better? NO way, anataka kujitajirisha tu, na kulewa madaraka. May be we leave him alone because he is an aspirant, hatujamuona akiwa rais.

Mimi binafsi sidhani anaamini katika Ujamaa na Kujitegemea, na sera hiyo sidhani kama ipo katika vocabulary yake ya siasa; Pamoja na ukweli huo, nadhani he is longing to see Tanzania/Tanzanians are becoming better off because any leader would want to leave a legacy behind him; Swali linalofuatia ni je, What Section of Tanzanians? Hapo sina uhakika kwani sijawahi kumsikia, pengine tusubiri pale atakaambia umma kama ana nia ya kugombea 2015; Vinginevyo kwa sasa, kauli yake kila akiulizwa swali hilo ni kwamba: "WE SHALL CROSS WHEN WE REACH THE BRIDGE.

Umeona JK katika miaka nane ya urais wake, unaweza kueleza ni nini kilimfanya atake kuwa rais na amefanya nini na urais huo? sana sana unaweza kusema ni mambo binafsi tu na kuridhisha nafsi yake. He did not do a thing that he can stand before Tanzania and say i did this for Tanzania.

Binafsi ningependa kuamini kwamba utawala wa nchi kwa kipindi cha 2005-2015 kabla ya kuingia madarakani ulikuwa na mikakati mizuri tu kwa taifa letu, lakini tatizo ni kwamba wahusika waliingia kama timu, huku pakiwa na midfield, defence, wingers, striker, lakini kwa bahati mbaya au pengine wengine wanaweza kusema ni bahati nzuri depending on how they profit with what is happening, timu hii iliyoingia bila ya kocha bali discipline za wachezaji wenyewe huku ikiwa na washabiki wa kupindukia, midfield ilipo collapse tu, matokeo yake ndio haya ambapo kuna kila dalili itashuka daraja 2015;

kuna siku Sumaye alisema "ukitaka mambo yako yakunyokee ingia CCM".

Binafsi sijawahi kuwa a fan of Sumaye kwa sababu imekuwa ni vigumu sana kuelewa anasimamia kitu gani hasa; lakini kwa vile muda bado upo na wengi wetu bado hatuna wagombea RASMI, pengine tukiwa wazima hatimaye tutaweza kuwaelewa kwa undani viongozi kama Sumaye wanataka kulifanyia nini Taifa lao, pale watakapotangaza nia zao rasmi;

Unajua inauma sana kuona mtu umesoma mpaka Ulaya na Marekani kwa taabu kwa hope kuwa utakuja kutoa mchango kwa nchi yako, unaishia kuwekwa kuwa ofisa utawala hospitali ya Muhimbili, ofisi inanuka na ina vumbi kama nini, viti ovyo hata kuliko tunavyoviona kwenye movie za charlie Chaplin, mshahara hautoshi hata chakula decent kwa mwezi. Lakini ukiangalia mbunge ambaye hajamaliza hata kidato cha NNE, yuko well off kuliko hata professor, Dr au Engineer.

Hapa sijakuelewa mkuu, kwani kwa haraka haraka mtu anaweza kudhania kwamba "You have a weak sense of public service in a poor country like Tanzania";

Moja ya sababu ya CCM kuyumba kwa sasa ni kuwa haina waadilifu na watu makini wakutosha. Kwenye centers za decision making za chama ukiangalia watu waliomo ni vichekesho, na wanaofaa kama kina Kinana ndio hao wameondoka.

Kwanza nakubaliana na wewe kwamba Kinana ni mmoja wa viongozi makini sana waliopo ndani ya CCM ya leo licha ya mapungufu yake ya hapa na pale; Mtu huyu angeweza kuwa waziri wizara yoyote, au katibu mkuu wa Chama, na hata Spika wa bunge kama angetaka lakini throughout ameamua kubakia na ujumbe tu wa NEC na Kamati Kuu kwa imani kwamba huko atakuwa na mchango mzuri zaidi kwa Chama chake; na kwa kweli Kinana amekuwa very instrunmental katika kujaribu kuiweka CCM sawa, lakini ni dhahiri kwa mtu kama yeye, pumzi lazima imuishie;

Mtu kama Kinana au Mangula (ambae ulimtaja kwenye mjadala mwingine) hawawezi kukubali kuwepo pale Lumumba kutumikia CCM ya leo ambayo literary speaking, imegeuka kuwa Taasisi ya Majungu, Fitina na 'Michongo' (Ulaji).
 
Mchambuzi nilikuwa najaribu ku-quote bandiko lako ili kujikita katika sehemu nilizotegemea kujibu, kwa kweli sikuweza.
Kila mstari unauhusiano na mwingine kimantiki.

Umesema in the process tunaweza kuja na remedies ambazo ni practical.
Nikupe kitu kimoja katika maradhi ya mwanadamu. Yapo magonjwa yanayosimama yenyewe na ukijua dawa yake yanatibika. Yapo yanayosimama yenyewe lakini huleta madhara katika sehemu zingine za mwili (complications).
Yapo maradhi ambayo yanashambulia sehemu muhimu sana za mwili na kuathiri kila kiungo kwamba kila sehemu ya mwili inakuwa vulnerable. Gonjwa la namna hiyo linaitwa (........Syndrome)

Matatizo ya nchi yetu ni 'syndrome' na hayana dawa moja.
Kwa lugha nyingine there is no silver bullet to solve all the problems in a day or fortnight kwa mwendo uliopo.
Sina maana haiwezekani, la hasha, lakini inahitaji radical intervention.
Anayeweza kufanya radical intervention ni surgeon. Ndipo ninapokubali hoja ya kuwa tunahitaji dikteta, si wa kuua bali wa kusimamia sheria za nchi hata kama inabidi anyonge mwanae.
Ndivyo china walivyofanya na kusemwa eti wana violate huma rights, lakini leo wapo sambamba na walimu wa human right economically.

Hoja ya kwanini hatuna watu calibre ya Nyerere? Hawa akina Nyerere waliwaangalia wananchi na kusema ninataka wafanikiwe bila kujali ujira au hadhi ya kisiasa. Ndio maana waliweza kusema 'ndugu wananchi' na wakasikilizwa tena kwa heshima. Hawa waliopo hata kutamka wananchi unaona nyuso zao zikiwa na haya,nafsi zao zinawasuta kwani maana ya mwananchi inayojulikana si ile wanayoitamka

Watu wa aina ya Nyerere wapo tena wengi. Wanalala wakifikiri watalifanyia nini taifa. Kwa bahati mbaya mfumo hauwapi fursa. Nadhani umeona urithi uliopo Dodoma wiki hii. Ni urithi huo huo upo kila idara na kila taasisi.

Unakumbuka BoT, kama chombo cha kusimamia uchumi ndipo palipokuwa mahali pa watoto wa wazee kujifunzia kazi.
Kwa mifano hii kama yupo 'Nyerere' nje ya System atawezaje kupata fursa ya kulitumikia taifa?
Tutawezaje kupata akina Nyerere kwa shule za kata?

Politics imekuwa suprement mahali pote duniani. Tofauti na wenzetu kwetu politics ndiyo imeshika mihimili yote ya nchi.
Hakuna check and balance na matokeo yake mwanasiasa mkubwa ndiye mkubwa wa serikali, bunge na mahakama.

Siasa kama siasa haina tatizo, tatizo ni wanasiasa wa nchini mwetu ambao wamejivika utaalaam hata wa kutengeneza rocket. Wamepewa nyenzo zote na hakuna anayethubutu kuwakemea.Ukijaribu utakutana na nguvu ya dola.

Kuhusu amani na utulivu, hili neno linatumika vibaya kinyume na maana halisi.
Hakuna mtu mwenye amani anayelala kwa uji wa mhogo, kutembea kutoka kimara hadi Posta, kwenda kulala hospitalini bila dawa au kuona mtoto ameshindwa shule kwa kukosa ada.

Kilichopo ni woga na si amani ndiyo maana jambo kidogo tu linazua hasira.
Ni petrol inayosubiri kibiriti lakini watawala wetu hujifariji kwa kulitumia hilo neno.

Kama nilivyosema hakuna silver bullets kutokana na upana wa tatizo, hata hivyo ni lazima kuwepo na mazungumzo ya wapi tuanzie na wapi tuelekee.
1. Nakubaliana na wanaosema tunahitaji rais dikteta. Udikteta uwe ule wa kusimamia misingi ya taifa, kanuni na sheria zinazotengeneza social fabrics.

2. Katiba mpya ilikuwa ni sehehmu ya suluhisho. Nasikitika kusema tumeiacha fursa hiyo na sasa matumaini hayapo.
Haiwezekani CCM walioshindwa kutupa majibu ya matatizo yetu kwa katiba iliyopo waje na katiba itakayotoa majibu tofauti. Katiba ndicho chombo kinachojenga misingi ya sisi kujitawala, sheria zinazotutawala, thamani na msingi ya taifa.
Hii iliyopo haikuweza kwanini tuamini CCM itakuja na muujiza mwingine! Tumewakabidhi rungu tusubiri maumivu

3. Chadema ndio mkombozi:
Sina uhakika kwasababu tuliwahi kusema NCCR, CUF na vyote vimepoteza matumaini.
Lakini kwanini tudhani CDM hata kabla ya kuangalia kama kinasimamia kile tunachotaka kama taifa.
Je, kuna utayari ndani ya CDM utakaorudisha nidhamu, uwajibikaji na utawala wa sheria.
Tumetumia vigezo gani kufikia hatima hiyo. Naelewa katika hali ya kutafuta mbadala hilo linaweza kuwa ni jibu la haraka, lakini ni jibu sahihi? Ni jibu pekee au ni sehemu ya jibu?

4. Mimi nadhani kuna vitu tunavyoweza kuanza navyo
(a) Tuhakikishe kuwa katiba ni yetu. Sijui tutawezaje lakini huo ndio ukweli hata kama tumeshabofoa.
(b)Katiba iwape wananchi uwezo wa kumiliki nchi yao kirasilimali na madaraka

(C) Turudishe nidhamu kwa kila mtu, kwamba mbele ya sheria hakuna bwana wala mtwana
(i) Tutaweza kuwawajibisha wasiowajibika
(ii) Kusimamia matumizi ya rasilimali zetu
(iii) Kugawa madaraka ili kuwe na check and balance
(iv) Kubadili muundo wa kujitawala na kutoa fursa kwa makundi kujiletea maendeleo kutokana na juhudi zao
(v)Kupunguza madaraka ya serikali kuu na kuyarudisha katika majimbo ya utawala

(d) Kujenga nidhamu ya kweli katika vyama vya siasa
(i) Kuwa na majadiliano hata kama ni kupingana bila kupigana
(ii) Kuhakikisha nidhamu ndani ya vyama ili kuwa na siasa zenye mantiki
(iii) Kuchagua sera na si mtu au watu

(e) Kutenga mihili ya dola bila kutegemeana. Kuweka vyombo huru vya kudhibiti mihimili hiyo isiingiliwe na serikali

(F) Elimu ya umma ili wajitambue wao ni nani na wana nafasi gani katika kushiriki shughuli za ujenzi wa taifa ikiwa ni pamoja na utawala wa haki na sheria. Wananchi waelewe kuwa wao ndio wameajiri viongozi na si kuajiriwa na viongozi
 
Nguruvi3,

Nimependa sana mtazamo wako kwamba MATATIZO YA NCHI YETU NI SYNDROME NA HAYANA DAWA MOJA. Vilevile kwa mtazamo wangu, upo sahihi kabisa kwamba moja ya njia kuu to ‘reverse' tatizo hili ni kuja na ‘a radical intervention'. Nipo katika kuandaa mjadala unaofanania na hoja yako hii, I will share mawazo yangu nitakapokuwa tayari;

Hoja yako juu ya umuhimu wa chombo kama Benki Kuu ambayo literally ni roho ya uchumi wa nchi imeniingia sana, ingawa ni jambo ambalo nalielewa kwa muda; Kilichonichoma hasa ni pale ulipozungumzia jinsi gani watawala wanavyo ‘abuse' chombo hiki muhimu kwa kukifanya kuwa sehemu ya watoto wao kwenda kufanya mazoezi ya kazi; Hii ni hoja nzito sana na inatoa mwanga mkubwa sana katika kiza cha "Kwanini uchumi wetu unaendelea kuwa uchumi UCHWARA". Lakini kwa bahati nzuri, sote tumeona product za chombo hiki zikiingia bungeni ni nini, suala ambalo linazidi kufikisha hoja yetu nyumbani juu ya Politics kuwa SUPREME to everything else; Kwa kweli inatia aibu kuona wasomi wetu ambao tunaambiwa ni wachumi wa kimataifa, wanapoishia kuwa watetezi wa UCHUMI UCHWARA kwa sababu za kisiasa;

Mimi nadhani chombo kama BOT ni muhimu kikapewa autonomy ya kweli ili kiache kuendeshwa kisiasa; kwa mfano, Gavana wa Benki Kuu pamoja na wasaidizi wake ni muhimu wakawa wanaidhinishwa/scrutinized na bunge, lakini pia ziwekewe performance indicators kupima utendaji wao ili kama wakishindwa kufikia malengo, basi wapishe wengine badala ya hali ya sasa ambapo wakuu wa taasisi mbalimbali za UMMA kila wanapovurunda, ni jambo la kawaida mtawala mmoja huko juu kumwambia maneno kama, "Hauna haja ya kujiuzulu, yatapita tu, usiondoke, nisubiri kwa miaka michache iliyobakia tuondoke wote."

Hoja nyingine iliyoniingia sana ni ile kuhusu Shule za Kata, hasa pale ulipohoji kwamba "Tutawezaje Kupata Nyerere Wengine Kwa Shule Za Kata"? In actual sense, shule hizi ndio zilitakiwa zitoe Nyerere wengine na sio vinginevyo; Shule nyingine hizi za English Medium mimi sioni maslahi yake kwa taifa kwani, nje ya kwamba watoto wanajifunza kiingereza, hakuna chochote wanachofundishwa watoto wetu kuhusiana na uzalendo au mapenzi kwa nchi yao; Inasikitisha unapokutana na watoto toka shule hizi na kuwauliza maswali kama: Nitajie mikoa kumi ya Tanzania, wanaishia kuja na majibu ya kubabaisha sana.

Lakini mimi nadhani wa kulaumiwa zaidi ni wazazi, sio watoto kwani wazazi ndio policy makers na waendeleza mitaala ya shule za Kata/serikali huko wizara ya elimu huku hawa hawa pia wakiwa ni mabingwa wa kupelekea watoto wao private schools za ndani na nje ya nchi kwa kuiba fedha za umma zinazotengwa kwa ajili ya shule za WANANCHI huko wizarani kama njia ya kujipatia uwezo wa kuwasomesha watoto wao private schools za ndani na nje ya nchi; Iwapo bureaucrats wetu hawa ndio wasimamizi wa Maendeleo ya shule za kata lakini watoto wao hawaendi shule hizo, hivi kweli watakuwa na mwamko gani wa kuziboresha shule hizi kama sio kuziua kwa kuiba fedha za bajeti ili kupata uwezo kusomesha watoto wao private schools au nje ya nchi? Na kama nilivyosema awali, wanachojifunza watoto hawa huko private schools na nje ya nchi have less to do na Uzalendo na mapenzi kwa nchi yao ya Tanzania; sana sana watawala wetu hawa wanapokutana, ni jambo la kawaida kufurahia kuadithiana jinsi gani watoto wao wanavyojua kiingereza. Issa Shivji ana hadithi very interesting inayohusiana na hili. Anasema hivi katika moja ya vitabu vyake:

****
"When I was at the University, we used to have a standing joke about a well – known politician who was then a minister of education. He visited schools in Britain and kept telling his people on his return that he was very impressed by the quality of education in Britain because even small children there spoke English"
***
Kwa bahati mbaya sana, this is becoming a very serious national perception now, na ndio hawa watoto wetu tunatarajia waje kuwa viongozi wetu wa baadae;

Mwisho naombe nizungumzie hoja yako kuhusu Politics kuwa Supreme to everything Worldwide; I agree with you on this one lakini zaidi naunga mkono hoja uliyotoa siku kadhaa zilizopita kwamba: "Katika nchi za wenzetu wanasiasa ni wasimamizi wa hoja za wataalam lakini kwetu wanasiasa ndio wanasimamia wataalam…."

Kwa mtazamo wangu, hili tatizo linachangiwa sana na dhana ya chama kushika hatamu, suala ambalo licha ya kuingia mfumo wa vyama vingi, bado lipo in practice kwa kiasi kikubwa sana katika Tanzania ya leo. Katika hotuba ya Mwalimu on Daily News mwaka 1974 anasema yafuatayo, na nadhani maneno haya bado ni relevant kwa kiasi kikubwa sana Tanzania ya leo:

******
"…kwa kuwa chini ya katiba ya chama kimoja, TANU imeshika hatamu. Inaweza kutoa maagizo ya sera za jumla kwa serikali sera ambazo zinatakiwa zitekelezwe kwa ajili ya Maendeleo ya nchi, na kinaweza kuwa na nguvu kutoa maagizo maalum juu ya mambo ambayo yanahitajika yapewe kipaumbele katika jambo lolote la uhai wa taifa. Zaidi ya hayo, itaweza kuitisha Baraza la Mawaziri, Waziri ye yote au mtendaji ye yote wa serikali, kujieleza juu ya shughuli zao au kutofanikiwa kwao katika utendaji wao"
******

Mwisho, nakubaliana na hoja zako kuhusu solutions to the SYNDROME inayotukabili. Umegusia maeneo muhimu ambayo ni Katiba Mpya, kurudisha nidhamu, kutenganisha mihimili ya dola na elimu ya uraia. Nitakurudia baadae kidogo na mtazamo wangu, hasa juu ya changamoto zinazotukabili katika maeneo haya.
 
Mchambuzi,
Kuhusu la shule za kata, ni kweli kuwa zilipaswa kutupa akina Nyerere. Nilichomaanisha ni kuwa zipo kama majengo lakini si utaalamu wala vifaa. Shule isiyokuwa na maktaba itatutolea mtaalam wa namna gani?
Nukuu mbali mbali unazotoa kila mara zinaenda beyond mathematics, biology and physics, it's all about knowledge and where to source it. Sisi tunadhani kuwa kuandaa taifa ni kuwafundisha physics na si kuwafundisha namna ya kukabiliana na mazingira ikiw ni pamoja na competitive world.

Hizi shule za wakubwa ikiwa ni pamoja na wanaopeleka huko ni matokeo ya 'mauaji' yaliyofanywa kwa Azimio la Zanzibar.
Sioni tatizo mtu kusomesha mtoto wake popote, tatizo ni pale mtu huyo anapokiuka maadili ya uongozi kwa kuiba hela za wagonjwa wa uti wa mgongo ili asomeshe mtoto wake. Azimio la Zanzibar lilisema fanya unavyoweza hakuna maadili, miiko au sahani. Kwahiyo hakuna kiongozi anayejua adha iliyopo katika shule za kata.

Kuna kitu umegusia muhimu sana, performance indicator(PI). Kama hatutakuwa na hicho kitu basi tutabaki kulalamika kila siku. Ili kuwa na PI ni lazima kuwe na kushikana 'uchawi' kuanzia kwa mkuu wa nchi hadi mfagiaji. Kwa bahati mbaya katiba itakayotupa uwezekano huo inaandaliwa na wale wale wasiotaka (pI) ziwepo.

BoT kwa namna yoyote ile lazima iwe chombo huru. Kwa nchi za wenzetu hata rais anapata ushauri kutoka Central bank na hawezi ku-manipulate data kama tunavyoshuhudia. Siyo BoT tu, Bureau of statistics zote zinatakiwa ziwe huru na kuwajibika sehemu kama bungeni kama inavyotakiwa kwa PCCB, DP n.k.

Nadhani unakumbuka wakati uchumi wa nchi ukiwa taabani Gavana wa benki kuu yupo busy kuangalia mabwawa ya kuogelea, wasaidizi ndio hao tunaowaona bungeni na wafanyakazi ni interns wa vigogo! Hapa hakuna tatizo kweli.

Kwa vile hii ni syndrome inabidi tuanze kuchagua system moja moja na kuiangalia kwa umakini.
Wananchi ni sehemu ya tatizo, badala ya kusimama na kusema shule za kata zina matatizo kila mmoja anakimbilia kupeleka mtoto english medium, mambo mengine yatafuata kwa msemo wa 'take care of today tommorrow will take care of itself'.

Vyama vya siasa ni sehemu ya tatizo. Mfano mzuri ni CCM ilijionyesha kuwa pamoja na uzooefu wa maika 50 haijaweza kujitambua achilia mbali kubadilika. Kwa vyama vya upinzani kama Chadema, endapo kweli wanataka kuisadia nchi kwanza lazima wajenge Nidhamu kwanza ndani ya chama.

Nidhamu hiyo ni pamoja na performance indicator, kuwajibika, ubunifu, kuheshimu mitazamo tofauti hata kama haikubaliana mmoja hadi mwingine, kuwa na vetting system ya viongozi, kuondoa opportunist, kutafuta talent, kuheshimu utaalamu na kusikiliza wananchi. Vyama hivyo visimamie kanuni, taratibu na sheria hata kama vinahusu mke au watoto wao. Chama kijengwe kama taasisi kwamba uwepo wake ni matokeo ya sera na wanachama na si mtu au watu.
 
Kwa nyakati fofauti, wengi wetu tumejifunza katika historia ya nchi yetu kwamba moja ya sababu za msingi ambazo Mwalimu Nyerere alizitaja miaka 50 iliyopita kwamba ni kikwazo kwa Maendeleo ya taifa letu ni uhaba wa wataalam wa kusaidia kujenga taifa. Hivyo, katika miaka ya mwanzo ya uhuru, ilimlazimu Mwalimu na serikali yake kuagiza wataalam kutoka nje na hawa walikuwa wanalipwa na fedha za walipa kodi wa nchi yetu. Miaka 50 baadae, hali sio tofauti sana kwa maana ya kwamba bado kama taifa, hatuoni bado mchango wa kutosha kutoka kwa wataalam wetu katika kuendeleza nchi yetu. Tunabaki kujiuliza, tatizo ni nini hasa:

· Je, bado kama taifa tuna uhaba wa wasomi/wataalum?
· Je, tunao wasomi/wataalam lakini wengi ni wababaishaji (wachakachuaji)?
· Je, tunao wasomi/wataalam lakini mazingira (social and economic institutions and infrastructure) zinawanyima nafasi kutumia uwezo wao kuchangia ujenzi wa taifa?
· Je, tunao wasomi/watalaam lakini hawathaminiwi?
· Je, tunao wataalam lakini wengi wamegeuka kuwa wanasiasa?


-----
.

Ndugu Mchambuzi,

Naomba nijitumbukize kwenye mjadala huu. Kitu cha kwanza, kushindwa kwa serikali au watanzania kwa ujumla kutatua matatizo yao au kuboresha maendeleo ya nchi, kusifanye tutafute visingio vya nani mchawi. Wasomi waliopo CCM sio kikwazo cha matatizo ya nchi. Matatizo makubwa ni kuwa Tanzania haikujiandaa au kuandaa wasomi wake na mfumo wa kiuchumi na maendeleo unaotumika sasa.

Wasomi waliopo CCM hawana tofauti na wasomi waliopo vyama vya upinzani kwani karibu wote wanaishi katika mazingira yaleyale na utendaji wao wa kazi ni sawa. Tofauti iliyopo ni kuwa waliopo CCM wanashikiria madaraka, hivyo lawama zote za kushindwa kwa nchi zinadondokea kwao.


Pili si kweli kuwa Tanzania ilifanya juhudi kubwa ya kusomesha watu. Juhudi kubwa Tanzania iliyofanya ni kuandikisha watoto na elimu ya msingi. Zaidi ya hapo, juhudi za kuwaendeleza watanzania na elimu ya sekondari na ya juu zilikuwa ndogo.

Na Tanzania kutoa idadi ndogo ya wanafunzi wa chuo kikuu ilikuwa ni mipango ya serikali ambayo mpaka sasa bado inafanyika. Na kama mnataka proof ninaweza kuchangia.

Katika hotuba za kubainisha sera zake za elimu, Nyerere alisema kuwa mfumo wa elimu wa Tanzania uwe kama jeshi. Uwe unatoa wanafunzi wengi na wazuri waliomaliza darasa la saba ambao watakuwa kama wapiganaji. Vilevile unatoa kiwango kidogo cha watu waliomaliza elimu ya kati ambao watakuwa kama makamanda. Na vilevile vyuo vikuu vitoe watu wachache sana ambao watakuwa majemadari (generals).

Katika sera hizi Nyerere alifanikiwa One elite university ambayo ilikuwa inatoa wanafunzi chini ya 500 kwa mwaka. Na wengi wao bila uzoefu wa kazi na ethics za kazi wakaenda kushika madaraka makubwa katika vyombo vya umma. Hawa watu hawakupata uzoefu wa kazi na leo tunataka waendeshe nchi kisawasawa.

One thing to remember is work ethic and performance are deliberate efforts. Tanzania did'nt prepare her educated population to be top perfomers, and I don't know why we expect miracles.

Nchi zote zilizofuata model hii ya kjeshi katika miaka ya 60,70,80, na 90 zina matatizo makubwa sana katika kipindi cha sasa cha globalization.

Tanzania inatakiwa kufanya reform kubwa jinsi inavyoelimisha watu wake. Mambo yanayofanywa sasa na CCM, sio matatizo ya kisiasa. Ni matatizo ya HUMAN CAPITAL and ideology hasn't got nothing to do with it.
 
Mkuu Zakumi,
Ningependelea utoe hiyo proof kama ulivyoainisha.

Pili, sikubaliani na hoja kuwa Nyerere alijenga chuo kimoja kilichotoa watu chini ya 500. Sentensi ilivyo ni kweli lakini maudhui yake yana walakini.

Hatuwezi kuongelea chuo kikuu kimoja au wasomi chini ya 500 bila kuiangalia historia na ukweli unaoambatana na huo.
Wakati anakabidhiwa nchi alikuwa na watu wa kiwango cha chuo kikuu wasiozidi 10. Kwa maneno mengine hata angewachagua wote wawe katika baraza la mawaziri bado alikuwa na upungufu.

Wakati hayo yakitokea alichukua nchi ikiwa haina chuo kikuu, vyuo vya elimu ya kati n.k. Hapo hujaongelea uwepo wa maprofesa wakufundisha vyuo hivyo.

Changamoto alizo kuwa nazo ni nyingi kuliko kiongozi yoyote aliyefuata. Illiteracy ilikuwa juu sana, hali ya afya ilikuwa mbaya, miundo mbinu hafifu, nishati mgogoro na wakati huo huo tukiishi katika dunia hii ya mafuta kutoka arabuni.
Majanga kama njaa, mafuriko hayakusita kumsubiri afanye kazi aliyotarajia.

Wapi aanzie katika hali dhaifu kama hiyo?
Kwanza ilikuwa kujenga vyuo vya elimu ya kati katika kila sekta ili kutoa wataalam wa kupunguza tatizo wakati nchi ikijenga uwezo. Tukaona kila tupliposafiri vyuo vya elimu, kilimo, medical assistant, technical college n.k.
Lengo halikuwa kupata madokta 100 kwa wakati mmoja watakaoishia katika hospitali za rufaa, lengo lilikuwa kupata wataalam wa akti kuzui yale yaliyokuwa katika uwezo wao.

Pengine ukiacha chuo kikuu cha UDOM nitajie chuo kingine cha elimu ya juu au ya kati kilichojengwa na marais waliofuata.
Wote walichofanya ni ku-upgrade vyuo vilivyokuwa tayari katika kada ya kati.

Pengine unitajie katika Hospitali za serikali zilizopo zipi zimejengwa nje ya utawala wa Nyerere.
Tafadhali nitajie vituo vya afya 20 kati ya 100 unavyojua vilijengwa baada ya mwalimu.

Katika nishati, tuliwahi kujadili kuwa hakuna rais aliyefuata aliyewekeza katika nishati kuliko Nyerere.
Kuwekeza sina maana ya kutumbukiza mabilioni kwa mtu mmoja na kumlipa milioni 167 kwa siku, nina maanisha kitu tunachoweza kusema huu ni uwekezaji kama Nyumba ya mungu, Kidatu n.k.

Nyerere aliwekeza katika viwanda vidogo ili kuinua thamani ya bidhaa za wakulima kama Pamba. Hakuna kiongozi aliyefuata ambaye amewekeza katika viwanda zaidi ya Mwalimu. Waliofuata wameaua vyote na kuacha tuagize mitumba na zile za china.

Miundombinu inayojengwa sasa ni kazi ya uwekezaji wa Nyerere.
Sikumbuki kiongozi aliyeanza kwa kuvunja pori ili kujenga bara bara, achilia mbali ujenzi wa reli zn.k.
Ni katika kipindi chake nchi iliingia vitani pamoja na kufa kwa EAC.

Katika kipindi cha miaka 23 ambayo ni michache kuliko pale alipoachia hadi sasa bado alifanya mambo mengi kuliko viongozi wote watatu kwa pamoja.

Ninachotaka kukueleza hapa siyo nini Mwalimu alifanya, nataka uiangalie picha nzima kutoka kila angle kabla ya kutoa takwimu za wahitimu 500. Uwezekano wa kutoa wahitimu 5,000 ulikuwepo, je hicho ndicho kilikuwa kipaumbele kwa wakati na changamoto zilizomkabili?

Kwanini tuangalie watu 500 au pungufu bila kuangalia ilikuaje na ingefanyikaje.
Nyerere kama mwanadamu ana mapungufu sasa ni wajibu wetu tuonyeshe mapungufu yako wapi na angefanya nini kwa wakati ule. Kuibuka na takwimu zachuo kikuu kimoja, wahitimu 500 bado hakujaweza kutueleza kosa lilikuwa wapi na kwamba takwimu hizo kwa kuangalia social-economic factors zinatoa ukweli.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom