CCM na Wasomi wa Taifa Letu

Mchambuzi:Ningependa nichangie maeneo matatu (in italics) based on how hoja zako have stimulated my thinking:-

1. Suala la mindset na pia la nidhamu kama taifa, ni kweli kabisa inabidi tubadilike, ila ni vigumu kujua tufanye nini ili kufanikiwa katika hilo, hasa ikizingatiwa kwamba nchi imehakuwa corrupted from the grass roots up, na chanzo kikubwa cha tatizo hili ni CCM yenyewe kwa maana ya kwamba – kwa mfano, atanzania wengi live in a context of total hopelessness anddespair kwani kwa muda sasa CCM na serikali yake imeshindwa kutengenzea watanzania mazingira yanayotoa opportunity for prosperity and success and an upoward social mobility kutokana na jasho la mtu. Matokeo yake ni kwamba ni watanzania wachache sana ndio wanafanikiwa kimaisha; ni katika hali hii, mtu akifanikiwa kiuchumi/kifedha, regardless of the means, anageuzwa kuwa hero na role model, hence the term ufisadi getting a positive connotation.


Mimi (in Normal font)

Nashukuru kwa upanuzi wa "mind set" ilivyokengeuka niongezee tu HILI NI LA KUTENGENEZWA, wote sisi tumechangia kwenye hili. Kwa hiyo kila mtu ana fursa na nafasi ya kuwa "solution" kwenye hili. Hili lipo kwenye "category" ya SUALA LA KITAIFA.

2. Sijakuelewa vizuri kuhusu uwepo wa self determination kama taifa under vyama vingi hasa pale unaposema kwamba ipo lakini haipo shared. Ni kwamba sijakuelewa tu but I think you might have a very interesting point. Inawezekana the shared vision ipo katika masuala uliyoyazungumzia ya mtazamo wa kiuchumi, ulinzi na usalama, nidhamu na uzalishaji, na tatizo ni kwamba tu haukufafanua vizuri.

Sawa ngoja nijaribu kulifafanua. Kuna msomi mmoja hapa nchini mtaalam wa socialogy na psychology anaitwa Prof. Marjorie Mbilinyi (Naweza kuwa nimekosea spelling za jina lake). Kifupi, huyu anazungumzia ujenzi wa fikra "mind set" kwa walimu. Maana yake ni mchakato toka mtoto anazaliwa na mazingira anayokulia, ni mkakati wa kufikisha au kutekeleza maudhui ya elimu ili kuwa na binadamu aliye kamilika, kujitambua(balanced and self determined) na mwenye kumudu mazingira anayoishi. Hapa kilichopo ni kuwa taifa ni mkusanyiko wa watu waliozalishwa na mfumo wa elimu iliyokusudiwa si huria/holela. Wanaweza kuwa na kiwango tofauti lakini watatambulika kwa mtazamo wa vitu mbali mbali na uelewa wa mambo ya pamoja hasa ya taifa lao. Hayo ndiyo misingi ya self determination. Mfano familia tofauti zina kiwango tafauti cha hadhi katika jamii. Kuna familia zenye wasomi na wadilifu wanokubalika na zingine zina wasomi si waadilifu na hawkubaliki na jamii. Self Detemination za hizi familia zinapata mapokeo/zi tofauti ndani ya jamii. Unaweza kukuta hata mafanikio yao kiuchumi yana mtazamo tofauti katika jamii. Mfano mwingine nimeuona kwenye TV, mtu yupo kwenye 4WD na mke wake, anakunywa maji ya chupa ya lita moja. Baada ya kunywa maji, anaitupa ile chupa barabarani na inaokotwa na mtoto anamrudishia kupitia dirisha lake. Anaipokea baada ya kushawishiwa hivyo na mkewe na baada ya kufikishiwa ujumbe wa mazingira. Ujumbe hapa "mind set" ya mazingira kwa anaetupa chupa kama huyu bwana ipo ipo tu haiendani na jamii. Ili kujibu yote haya tujiulize wewe na mimi na yule na sisi tunalichuliaje suala la mazingira hususan baada ya kunywa maji ya chupa tunazifanyaje chupa tupu. Hizo ni chupa tupu, je tuna mtazamo gani wa pamoja (kitaifa)juu ya mambo mengine kama uchumi, afya, elimu na muhimu zaidi kuhusu KAZI? Ni suala la kitaifa kujenga "self determination" kujitambua kuwa na msimamo na kujiamulia mustakabali wetu.

All in all, umenipa a starting point towards uelewa as I am still digesting your thoughts; Lakini kuna kitu kinanitatiza hapa: Chini ya Ujamaa, the State (CCM) failed; miaka 27 baada ya soko huria kuingia, hadi leo hii the market has failed, hence the state (CCM); Je, tatizo hapa ni uwepo self determination that is not shared? Kwa mtazamo wangu, STATE FAILURE UNDER UJAMAA POLICIES AND MARKET FAILURE UNDER FREE MARKET POLICIES, means CCM na serikali yake have failed watanzania since independence na sioni any justification and legitimacy for the party to continue to rule the country unless kinakubali mapungufu haya na kuanzisha mabadiliko from the bottom – up, sio kufanya maamuzi kwenye vikao vyao in a top – down manner na kuja kutuletea taarifa kwenye television. Bila ya hivyo, CCM is getting into a collision course na umma uliochoka!

Kuna failure wengine hujawataja mimi, wewe na jamii. Serikali na CCM ni taasisi ambazo kiundani kuna watu nyuma yake. Hawa ni failure na ndiyo maana hizi taasisi ni failure. Tusisahau kuwa failure ya jamii ni kubwa zaidi, kwa sababu inawahusu individuals na taasisi. Naomba turejee kwenye "principles" shule na elimu kwa ujumla jukumu lake la kwanza ni kujenga taswira ya taifa. Hii ni suala muhimu la kitaifa, tukiri kuwa hapa ndipo kwenye mtindio wa mambo yetu. Mimi mwishoni mwa 70s na mwanzoni mwa 80s nilikuwa mdau wa elimu ya watu wazima. Humo ndani ya elimu hiyo tulikuwa na fursa nzuri ya kujenga "self determination" ambayo yalizingatia umoja wa taifa. Huwezi amini yalileta msisimko na mshikamano ambao ulikuwa na positive impact kwenye umoja, usalama na uchumi.

3. Na mwisho ni kuhusu hoja yako juu ya masuala ambayo unadhani we can deal with in a non – partisan way. Nimependa your ideas on issues kama uchumi, ulinza na usalama, nidhamu, na uzalishaji. Nilikuwa nina maoni tofauti kidogo juu ya hoja yako hii:

Tukianza na uchumi – Hadi sasa, sio CCM wala Chadema ambayo inaweka bayana nchi itasonga mbele kwa kutumia mfumo gani wa uchumi; Sera na itikadi za vyama vyote zinalenga kutegemea kujaziwa bakuli na wahisani, kwani tangia Nyerere ang'atuke, sera zaetu, dira yetu ya taifa n.k zimekuwa zinatengenezwa na wakubwa wan je (wahisani – IMF na World Bank) kupitia economics za AID ambazo ni maafa makubwa sana sio kwa taifa letu tu bali nchi zote maskini. AID ndiyo njia pekee iliyobakia kwa wakubwa wa nje to justify kwamba their theories about the market and economic development will lead us into a take off stage. This is a fallacy.

Kwanza nishukuru kuliona hilo; ni uthibisho kuwa hatuna agenda/dondoo ya kitaifa kuhusu uchumi. Je hapo kuna fursa yo yote? Ndiyo ipo wewe na mimi na wengine hatujanyimwa fursa ya kuiweka hiyo kama agenda/dondoo yetu ya kikatiba tujadili na kuiweka vizuri kwa muafaka. Mfano clause moja tu ya kuwa rasilimali zote za taifa hii zitamilikiwaje kitaifa si kitaasisi kwa sababu taasisi hizi zote zimefeli kwenye hili. Juu ya sera kuamuliwa nje ndilo linathibitisha usemi wa ukoloni mambo leo, na uwingi wa fikra tofauti hata ndani ya chama kimoja. Lakini udhaifu huu ni kutokana na uchumi dhaifu, viongozi dhaifu na sisi wananchi dhaifu. Hakuna mtu anawaamulia wachina kwenye mambo yao ya uchumi hata ya haki za binadamu. Rejea historia ambayo wachina wanaiheshimu sisi hatuiheshimu; Tanzania ndiyo iliyopigania kuiingiza China UN. Hizo gutts tumezipeleka wapi? Hakuna sababu ya kuwezeshwa ili TUWEZE. TUNAWEZA kujiamulia mambo yetu bila KUWEZESHWA; hiyo ndiyo self determination in action tuliyoipotelezea.

Tukija kwenue ulinzi na usalama – tumeona jinsi gani vyombo vyetu juu ya masuala haya vilivyokuwa partisan. Sina haja ya kufafanua sana kwani mengi yapo dhahiri.

Na mimi pia sina haja ya kufafanua ila kujitwika jukumu la kushare na wengine

Nidhamu – tatizo lililopo ni kwamba nidhamu imekuwa ni suala voluntary, sio mandatory tena kwani viongozi hawaonyeshi mfano wa kuigwa, na badala yake, madudu wanayofanya ndio yana inspire hata watoto wetu. Ni kawaida kwa watoto mashuleni nyakati hizi kuwa na malengo ya kumaliza elimu zao ili wakajijenge binafsi, sio wakatumikie taifa.

Umesema yote ila ungekwenda mbali ukatoa maoni yako juu ya mwelekeo uelekezwe wapi. Mimi naona ni matokeo ya kukengeuka kwa elimu yetu ambayo mimi naiita ya kukariri siyo ya kujikomboa. Kwangu ukombozi ni kufanya kazi. Kwa dini yangu kupata mshahara nisioufanyia kazi ni wizi (utumwa); ni bahati mbaya nimezungukwa na wenzangu wavivu. Ndiyo maana nashindwa kuelewa kwa nini watu wanadai mishahara ya kukidhi mahitaji yao bila kujihoji uzalishaji ukoje?

Uzalishaji – tangia uhuru, mkulima amekuwa anamzalishia mtawala mazao ya biashara ili auze nje ya nchi na kupata resources za kujijenga kitaasisi; kuzalisha mazao ya vyakula ili to feed the urban elites and bureaucrats; ku maintain law and order kwa kuwekeza kwenye ulinzi na usalama (polisi n.k); kuwapatia maisha bora watu wa mijini kwa kuwapatia ajira kwenye taasisi za umma na pia kuwajengea mazingira ya ujarisiamali (sababu wengi ni exposed, educated, elites…) na pia kuwajengea miundo mbinu na huduma mbali mbali za kijamii ili wasi revolt against the regime n.k. Yote hii happens at the expense of mzalishaji ambae ambae yupo kijijini (70% of the population) ambae serikali does very little to care for their social welfare.

Umesema vyema lakini kuna la ziada alilisema Nyerere siku zake za mwisho; yeye hakufanya yote mazuri lakini wenzake hata mazuri aliyoyafanya wameyaacha. Labda na mimi niungane naye kuwa yapo mengi mazuri ambayo yangekuwa ya tija katika uzalishaji. Hakuna aliyetunyima kuyarudia, lakini tunajibaraguza tu. Ni matumaini yangu serikali makini itakuja kuyarejea mazuri. Hata mabaya si ya kusahau ni mambo ya kuyafanyia kazi 'Challenges addressed are always Opportunities"

Samahani najibu kifupi kifupi ila naweza kuchangia in details kama nitatakiwa
That being said, mimi nadhani hoja yako juu ya masuala haya stands katika kuzungumzia masuala that can be dealt with in a no – partisan way, lakini kwa mtazamo wangu, yote haya lazima yawekwe kwenye kasha ya UZALENDO.

Kwenye fani ya Komputa kuna neno "semantic" na lingine "syntacs/x" likiwa na maana ya lugha inayokubalika/isyokubalika; sisi tuna maneno mengi sana ya namna hiyo moja wapo ni hilo. Ukweli maana yake ipo kwa mtumiaji. Kwa hiyo kwangu mimi sikubaliani na hilo kasha kwa sababu lina maneno yanayotumika kibinafsi. Mimi natambua kasha moja ambalo naona kama bado liko tupu nalo ni la UTAIFA.Nakuomba wewe na mimi na wasomaji wetu ebu tujikite kwenye kuitafakari dhana ya utaifa kiuchumi, kiusalama, kiuzalishaji (productivity) katika kila mahali tulipo ili tuwe wengi tunaojenga taifa tuwazidi wabomoa taifa letu.
 
Mkuu Mchambuzi,

Naomba nami nichangie japo kwa uchache:
1. Juu ya tafsiri ya Msomi: Ni kweli, lazima awe mbunifu, anayeongozwa na mantiki ya mambo na sio hisia zake, mwenye uwezo wa kuelewa na kuchambua jambo, lakini asiishie hapo haitakamilika kuitwa msomi ila pale atakapoweza kufanya maamuzi sahihi kwa nafasi yake aliyonayo. Uelewa tu hautoshi pasi Maamuzi Sahihi-yenye tija kwa umma.

2. Tukirejea tafsiri hiyo hapo juu, basi ni hakika kabisa, tuna wasomi wachache mno! Wengi wanaishia hatua ya kuwa mbunifu (lakini ni kwa maslahi yake) na ataelewa mambo na kuyachanganua vizuri, lakini kwenye kufanya MAAMUZI ndipo wanapokosa sifa za kuitwa wasomi, kwani Maamuzi yao huongozwa na HISIA ZAO na si Mantiki ya mambo waliyoing'amua! Ni watumwa wa fikra: Wanajifikiria wao kwanza, si umma! Hawa ni wapumbavu, si wasomi!

3. Wataalamu: Ni wazi kuwa kuna tofauti ya mtaalamu na msomi: Usomi ni zao la critical thinking hali kuwa Utaalamu ni zao la Training, ni Ujuzi-Skills. Tunao wataalamu, japo si wengi sana ila wangetosha kutufikisha mahali tofauti na hapa leo.

Tatizo ni.....
(a) Utaalamu wao unatumika kwa maslahi ya watu wachache, na hili ni zao la Kujifikiria binafsi-MIMI KWANZA.
(b) Wataalamu wengi wamekosa uzalendo-utaifa. Wanajifikiria binafsi-wanarubuniwa ng'ambo hali kwetu duni...wananunuliwa kwa gharama ya vifo vya watanzania wenzao! Madaktari wangapi na wakandarasi wako nje ya nchi, wangeifikisha wapi nchi?
(c) Utumwa wa kifikra tulionao raia, juu ya utaalamu! Mfano wengi wanapenda kutibiwa na wazungu na kutowaamini weusi wenzetu! Mkandarasi mweupe akiwa mweusi mbabaishaji!

UTAIFA KWANZA:
Hili ni suluhisho-mtaalamu angemthamini raia na raia nae angemthamini mtaalamu, mwishowe kila mtu angeshiriki ustawi wa mwenzake, hadi taifa zima!
*Ukishaanza kusema CCM imesababisha hiki na kile, ni kujitukana mwenyewe! Kwani CCM ilisimikwa na watanzania hawa hawa, kwanini tusiwalaumu wapanda mbegu kwanza kabla ya mpaliliaji?

Ni hayo tu.

Mungu wetu anaita!
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi kuna wasomi wengi ambao wangeweza kufanya kazi za ubunge, udiwani etc etc lakini wako benchi, na wachovu na wababaishaji ndio wamekalia viti. Naona hizi ndio issues ambazo watanzania tunatakiwa kujiuliza, ni kwanini. Lakinin pia kuna wasomi, maprofesa na wengine ni wanazuoni wakubwa kabisa, ukisikiliza wanapoongea unaweza kuuliza kama kweli wana akili, ni wazima au wameamua tu kuuvaa wenda wazimu, watu kama hawa nao hawana maana kabisa ni bora wakae nje. Kwa hiyo kuna complications kidogo.

Kwa sasa mtanzania yeyote mwenye akili timamu hawezi kuisifia serikali ya sasa au kukisifia chama kwa sasa. Vyote viwili viko ovyo kabisa, na ukizungumzia siasa ya ujamaa Tanzania utakuwa mwendawazimu kabisa, kwani ukiangalie hata wale walijiapiza kuwa wakomunisti wanaonekana kuwa ni mabepari na mafisadi wakubwa. Sina nongwa na ubepari mwenyewe naupenda, lakini sikubaliani na ufisadi, au ubepari unaotokana na wizi. lakini sielewi kabisa kwanini ubepari tunauita ujamaa na na ufisadi tunauita changamoto inayotokana na maendeleo

Sijui ni kwanini wasomi wanaanza kupotosha ukweli na kusema serikali ya sasa imefanya kazi nzuri, au chama kinafanya kazi nzuri. Sijui ni kujikomba kwa viongozi wanasiasa, kujipendekeza au kutoona nini kinafanyika. Au wasomi hao si wasomi kama tunavyodhani, au ndio zile MA na Phd za kuokota Ulaya na America, au za kupewa ambazo zimesambaa na kila mtu anataka kuweka title mbele ya jina lake bila hata sababu ya maana. Sasa hivi unaweza kuwasikia baadhi ya mawaziri wakipinda hadharani hali mbaya ndani ya chama na serikali, lakini hadharani wanaongea kingine, kuna wanasiasa wanaongea tofauti kabisa hadharani kwa maslahi ya chama, lakini pembeni wanajua kabisa kuwa taifa linaenda mrama, na wanasema tunaongea vile kwa kuwa tumeambiwa. Sijui ni woga au ujinga. Lakini hiyo ndio hali iliyopo. Ukivuka mpaka kuingia Kenya hali ni tofauti kabisa, wenzetu mamba wanamuita Mamba, sio kenge au mjusi.

Jaribu kumsikiliza Prof Palamagamba kabudi akiongea au Dk Benson Bana akiongea, unaweza kudhani title zao zimekwisha muda wake, wanaochoongea hata mwanfunzi wa kidato cha nne anaweza kujua wazi kabisa kuwa ni upuuzi tu. Lakini ambacho hakijulikani ni kwanini akili zao zinakuwa kinyume na hali halisi. Lakini kuna baadhi ya wasomi tumeona jinsi serikali ilivyowafanya, mfano mzuri ni Dk Lamwai. Kwa hiyo issue naona is more

Naunga mkono sehemu kubwa sana ya hoja zako, hasa kuhusu suala la Ubepari na Viongozi wetu. Nadhani kwa kiasi kikubwa sana, ukoloni ulituathiri sana kifikra, na tatizo hili linaendelea ndani ya mzaingira ya sasa ya ukoloni mamboleo. Mimi sidhani kwamba Ubepari per se ni mbaya, tatizo ni pale unapokuwa determined na external forces badala ya kujengwa na forces from within, huku mfumo huo ukitoa some sort of a Tanzanian Dream – kwa maana ya uwepo wa opportunities for prosperity and success kwa kila mtu bila ya kubaguliwa, na kila mtanzania asonge mbele kimaendeleo kutokana na wingi wa jasho lake. Lakini kinyume na hili, ubepari wetu ni ubepari uchwara, ubepari ule ule ambao Mwalimu alijaribu sana kupingana nao, sio kwa sababu ya kuuchukia, bali kujaribu kuuwekea speed governor ili utendee watanzania haki. Ubepari wa namna hii uliendelea kumpa sana shida Mwalimu baada ya uhuru kwani mawakala wa mabwanyenye wa nje walikuwa ni watu wale wale ambao walikuwa wanamzunguka Mwalimu – mawaziri, wakurugenzi wa mashirika ya umma n.k - wengi wakiwa ni wasomi wazuri kabisa kupitia fedha za walipa kodi.

Hawa agents wa ubepari uchwara sio kwamba hawakuwa wasomi na kutofahamu madhara ya shughuli zao kwa jamii yetu kwani walikuwa wameelimika kama Mwalimu, hata wengine kumpita Mwalimu, lakini walikosa kitu kimoja – Uzalendo na Upendo wa dhati kwa nchi yao. Matokeo yake wakawa ndio vinara wa kufanya sabotage kwenye mashirika ya umma ambapo walikuwa wamepewa nafasi ya ukurugenzi, yote ikilenga kuonyesha kwamba Ujamaa hauwezi kufanya kazi. Wasomi wetu ndani ya CCM wengi wao ndio wale wale walioua Azimoa la Arusha ili kurahisisha kazi yao ya uwakala wa mabwanyenye wa huko nje iwe rahisi zaidi kwani chini ya Azimio la Arusha, Mwalimu alikuwa ameziba mianya mingi exploitive to the mass. Mabepari hawa uchwara ambao wengi ndio wasomi na viongozi wetu ndani ya CCM na serikali yake hawana mentality tofauti na ile ya mabwanyenye wa nje ambayo simply – ni kutumia foreign capital in an "efficient manner", na maana ya efficiency to these economic hooligans simply means creating mazingira yanayojenga na kudumisha unequal exchange baina yetu na mataifa makubwa in the context of FOREIGN AID, TRADE and FOREIGN DIRECT INVESTMENT.

Hoja yako kuhusu viongozi wetu kuwa na multiple personalities when it comes to uongozi wa taifa letu ni sahihi kabisa. Nimetumie neno personalities kwasababu that is what leadership is all about in Tanzania. Wananchi hawachagui viongozi based on itikadi wanazosimamia bali personalities za viongozi husika. Umejaribu kubaini iwapo viongozi wetu wanatawaliwa na UWOGA au UJINGA. Nadhani vyote, lakini pia pamoja na UNAFIKI na UNAFSI. Na ni unafiki huu ambao umeupambanua vyema pale ulipotoa mifano jinsi gani unakuta kiongozi in one setting ana msimamo huu lakini in another setting ana msimamo tofauti kabisa and so irrational pamoja na elimu zao kubwa kubwa. Miaka 50 iliyopita, Mwalimu alipata kulizungumzia suala la unafsi miongoni mwa viongozi na nitamnukuu:

******************************
["…Dalili nyingine ya unafsi, na ambayo ni ugonjwa mbaya sana ni fitina. Kanuni moja ya TANU inasema hivi: "Nitasema Ukweli Daima. Fitina Kwangu ni Mwiko." Lakini bado tunao wanachama ambao ni wafitini wakubwa bila kujitambua. Ni wa aina mbali mbali. Wengine humwona mwenzao anafanya kosa. Badala ya kumwambia pale pale kijamaa kwamba atendalo ni kosa, watanyamaza kimya. Lakini hawanyamazi kabisa. Watakwenda kumteta katika vikundi vya siri. Mateto haya si ya kumsaidia mwenzao, ni ya kumdhuru. Hii ni aina moja ya fitina. Wengine hugawa watu katika mafungu. "Fulani" japo kafanya kosa kubwa sana hasemwi. Lakini "Fulani" wa pili akifanya kosa japo dogo, kosa lile hukuzwa likawa kama mlima Kilimanjaro. Hawa hutafuta sababu ya kumtetea "Fulani" wa kwanza, au za kumaulumu "Fulani" wa pili, ambazo hazifanani kabisa na ukweli. Kwa watu wa aina hii, ukweli ni jambo ambalo hutegemea mtu, si kitu kinachojitegemea chenyewe bila kujali mtu. "Fulani" wa kwanza akisema katika majadiliano kuwa mbili na mbili ni tano, wao watakubali. Lakini "Fulani" wa pili akisema sivyo, mbili na mbili ni nne, watamwona ni mtu mbaya kabisa ambaye hastahili hata kusikilizwa. Hawa hawajali ukweli, hujali nafsi tu. Kwao, ukweli ni maoni yao na matakwa yao.

Mwalimi anaendelea kusema kwamba:

"Hatuna budi, hasa katika majadiliano na mazungumzo yanayohusu jumuiya, tujifunze kusikiliza hoja zenyewe zinazotolewa na wenzetu, na kuzijibu zile hoja kwa kuzikubali au kuzikataa, bila kujali kama anaezitoa ni rafiki au si rafiki. Pia wanaopingwa hawana budi wakubali kuwa kinachopingwa ni zile hoja zao, sio wao wenyewe. Bila mazoea haya, mazungumzo hayana maana; yanakuwa ni kupoteza wakati, maana huwa tumekwisha kuzihukumu hoja za mtu hata kabla hajazitamka; kadhalika, hoja zetu zikijibiwa kwa kupingwa halafu tunawakasirikia waliozipinga tunafanya mazungumzo yasiwe na maana, kwa sababu tunapenda hoja zetu zikubaliwe tu hata kama si hoja safi. Ukweli una tabia moja nzuri sana. Haujali mkubwa wala mdogo; haujali adui wala rafiki. Kwake, watu wote ni sawa. Pia ukweli unayo tabia ya kujilipiza kisasi kama ukipuuzwa. Ukiniona nataka kulipiga teke jiwe kwa kuwa unafikiri kuwa ni dongo au mpira, natumaini utanionya. Lakini nikilipuuza onyo lako kwa sababu eti wewe ni mdogo au kwa sababu sikupendi, nikalipiga teke, basi litanivunja dole japo ningekuwa nani. Ukweli haupendi kupuuzwa."]

J.K.Nyerere, 1962.
********************************

Wasomi ndani ya CCM wanapuuza ukweli kwamba nchi ipo katika hatari ya kuingia katika machafuko kutokana na kuyumba kwa CCM katika nyanja zote za utawala, na nadhani wengi wetu tunakumbuka Mwalimu alionya kwamba CCM IKIYUMBA, NCHI ITAYUMBA. Na kama Mwalimu alivyosema: "Ukweli una tabia moja nzuri sana. Haujali mkubwa wala mdogo; haujali adui wala rafiki. Kwake, watu wote ni sawa. Pia ukweli unayo tabia ya kujilipiza kisasi kama ukipuuzwa."

Mimi nadhani tayari tumeanza kushuhudia Kisasi cha ukweli kwa wasomi ndani ya CCM, hasa bungeni.

Wengi tunasubiri kwa hamu hitimisho la CCM kama chama ambapo kitakuja kujifunza while it is already too late kwamba kumbe "Ukweli haupendi kupuuzwa."
 
JingalaFalsafa

Nashukuru kwa mchango wako mzuri.

Nakubaliana na hoja zako nyingi, na hasa juu ya umuhimu wa kutofautisha baina ya msomi na mtaalam. Hilo ni suala ambalo kidogo nilili over look na nadhani it makes a very big difference katika mjadala huu.

Kuhusu suala la UTAIFA KWANZA, inazidi kujenga hoja ya Mimibaba ambapo nilijaribu kusikia maoni yake juu ya nini ni muhimu zaidi in this context, je ni Uzalendo au Utaifa. Mimi nilikuwa nadhani Uzalendo ni muhimu zaidi lakini nazidi kuwa convinced kwamba pengine utaifa should be the over riding factor if we are to succeed.

Na mwisho, hoja yako kuhusu kutoilamu CCM bali wale walioiweka madarakani, hii ni hoja nzuri. Lakini je, ni sahihi pia kusema kwamba CCM ni ya kulaumiwa kwa sababu imewaangusha wale walioiweka madarakani na hawa watanzania waliosalitiwa inawawia vigumu sana kuiadhibu CCM kutokana na ukweli kwamba CCM imejijenga sana kwani tangia iachane na mkulima na mfanyakazi, lengo lake kubwa ni to consolidate power kupitia matumizi makubwa to maintain Law and Order vis a vis social wleafere, kwa mwendo wa LIWALO LIWE?
 
Last edited by a moderator:
Mimi Ni Baba:

Umezungumza mambo ya msingi sana, ningependa na mimi nichangie kwa haraka haraka, na kama sitaeleweka naomba niwie radhi na nifahamishe ili nitoe ufafanuzi zaidi.

Kwanza Ni suala la OUR FAILURE AS a SOCIETY. Suppose at the centre of our discussion tumweke mtoto na malezi yake, je akija kuwa mtu mzima wa umri wa miaka kumi na nane na kukutana na madudu ya leo, who has really failed this young fellow? Je, ni Wasomi (kitaasisi – vyuo vikuu)? Je ni Viongozi? Je ni Both?
Kwa mtazamo wangu, source ya failure ya kijana huyu ni both, lakini more importantly – ni attitude ya serikali to snob wasomi/wataalm wetu hasa michango yao kwa kuona kila kitu toka kwao ni destructive criticisms. Tuna vyuo vkuu vingi sana Tanzania ya leo lakini vingi ya hivyo (kama sio vyote) remain incapable of providing practical solutions katika kutatua our development dilemma. Na hii ni kutokana na ushirikiano duni kutoka kwa serikali, nje ya kutumia utaalam wa kina Dr. Bana na wengineo ambao kazi yao kubwa ni kuiambia serikali ya CCM what it wants to hear.

Ni dhahiri kwamba the state has largely failed to deliver kwa wananchi. Serikali yetu chini ya CCM imegeuka kuwa "Gatekeeper". Whereby, whether it delivers of no kwa wananchi, it is guarantee kupata fedha za kuendesha madudu yake by means of kodi za walala hoi, mikataba ya ovyo ovyo na wawekezaji, Foreign Aid etc. Uwepo wa resources za dezo bila uwajibikaji, unapelekea ushindani wa kisiasa usio na tija kwa wananchi na badala yake, ushindani wa kupata madaraka to enjoy the said resources. Ndio maana wahusika wakiyapata madaraka, primary objective kwao sio Economic Development or Social Welfare, badala yake kipaumbele inakuwa to tighten political control, tighten control on resources kwa manufaa ya regime husika (sio umma), lakini muhimu zaidi kujijengea mitandao na mabepari wa nje na kuwa mawakala wao katika kuliangamiza taifa kimaendeleo. Watawala wa namna hii hawana muda wa kujenga strong institutions (social, economic and political) za kusaidia kusukuma nchi kimaendeleo. Hali hii huchangia sana mporomoko wa nidhamu na wa ufanisi katika mazingira ya uongozi. Suluhisho lake ni kupata viongozi watakaoanza kujitambua, lakini muhimu zaidi ni umma kuonyesha viongozi kwamba wanajua nini kinachoendelea.

Pili naomba nizungumzie suala la MIND SET. Ni vizuri umeligusia hili. Mind set is simply a mental condition – sehemu kubwa ya jamii yetu ya Tanzania hatuna tena matumaini kwani tunaishi in hopelessness and despair, na kwa wengi, has wa vijijini wanaona Poverty is beyond recovery/irreparable. Ndio maana ni kawaida kwa wanavijiji to believe kwamba umaskini ni kitu cha kawaida, and to some it is even Desirable ili iwe rahisi kupata vitu vya bure bure, hasa nyakati za chaguzi kuu. Ni kawaida kwa watanzania wa hali hii to shift blame kuhusu umaskini wao kwa factors external to them. To make matters worse, wamegeuka kuwa watu wa kusubiria serikali iwafanyie kila kitu. Solution hapa ni kuanza kujenga dhana kwa watoto wetu wa leo kama ile ya JFK kwamba USIULIZE TANZANIA itakufanyia nini, bali jiulize UTAIFANYIA NINI TANZANIA. Lakini in the midst of all this, viongozi wa sasa lazima wajenge mazingira mazuri for watoto wetu to pursue their dreams.

Lakini pia kama jamii, tuna wajibu as you rightly put it kwani tatizo hili pia huchangiwa na malezi. Kwa mfano ni kawaida kwa watoto wetu kukua katika mazingira ya kuamini kwamba anything that is home grown is inferior; Mbaya zaidi, familia nyingi vijijini zina tabia ya kuhimiza kwa watoto wetu umuhimu wa kuwa wanyonge ili wapate misaada. Madhara yake ni kuwajengea watoto wetu "a begger mentality", hence kununulika na kurubuniwa kwa urahisi.
Pengine hapa nijadili kidogo suala la UMASKINI WA KITAMADUNI. Jamii yetu ya kitanzania inakabiliwa na umaskini mkubwa sana wa kitamadni. Tuna uhaba mkubwa sana wa taasisi zenye kujenga na kulinda utamaduni wetu kama taifa ambao ni muhimu sana in fostering development. Tanzania ni jamii isiyokuwa na msimamo; kama jamii, tuna tabia ya kubadilika badilika ovyo kama kinyonga kulingana na matukio na hali ya hewa ya wakati huo. Leo hii unakuta tunasimamia kushoto, kesho kulia, na ni mabingwa wa kwa kurukia tamaduni, beliefs, norms na ethics za wenzetu. The right intervention to reverse hali hii nadhani itatokana na mchango mkubwa wa media and entertainment industry yetu. Pia wasomi wetu kwani wengi wao kwa sasa for some reasons - intellectually wapo more curious kuhusu surroundings za utamaduni wa kigeni kuliko their own surroundings. Huu ni mtumwa and it is peculiar kuona msomi mtumwa karne hii.

Mwisho nigusie kidogo UMASKINI WA KISIASA unaotukabili. In short, Umaskini wa kisiasa ni hali ya jamii kukosa a common political ideology, au a political philosophy ya kuisaidia Jamii kuwa na Dira moja kama taifa. Katika ushindani wa kisiasa, viongozi compete based on personalities, not their ideological beliefs and vision. Ni muhimu vyama vyetu vya siasa kubadilika, na hii ni kwa vyama vyote, CCM, Chadema n.k, wote hawana mvuto wa kiitikadi bali personalities and events of the day.
 
Mchambuzi

1. Binafsi sioni tofauti kubwa ya Uzalendo na Utaifa! Hata naposema Utaifa kwanza ni sawa tu na Kusema Uzalendo kwanza. Uzalendo ni ile hali ya kutanguliza Utaifa katika kila ufanyacho! Taifa ni aridhi, watu na serikali. Hivyo mzalendo ni yule atakayethamini aridhi ya Tanzania, watu na Serikali yake!

2. Kwanini tuilaumu CCM hali kuwa sisi ndio tumeisimika? Tangu mwaka 77 ipo, bado tu tunawatupia lawama wao? Mfumo mbovu wenye baraka za watanzania, umesimika serikali mbovu kupitia ccm! Nafsi za watanzania, ndio adui yetu wa kwanza, "nafsi zetu" Wamefuga nyigu wanataka kuvuna asali! Mfumo umesema Hata vichaa 9 wakisema ndio, basi hata wenye akili 8 wakisema Hapana wameshindwa! Wengi wape, ni uvivu wa kufikiri-kurahisisha mambo! We can reason anything...for the best solution-not voting!

Jilaumu kwanini umekubali kufuga nyigu hali kuwa unataka asali!

Mungu wetu anaita!
 
Last edited by a moderator:
JingalaFalsafa

Nadhani kuna tofauti kati ya utaifa na uzalendo, ni kama komandoo na terrorist depending with the context.

Nadhani Uzalendo ni hali ya kuwa na majivuno na pia mapenzi na taifa lako, whether linafanya vizuri au vibaya katika mfumo wa ulimwengu (kisiasa, kiuchumi na kijamii).

Utaifa
ni hali ya kuwa na imani kwamba nchi yako ni bora na ni superior kuliko nchi nyingine na anaepingana na hilo ni adui. Lakini hatuna haja ya kuingia katika mjadala huu kwani nina uhakika hadi sasa tupo kwenye mstari mmoja kuhusu umuhimu wa utaifa au uzalendo katika maendeleo ya nchi.
 
Last edited by a moderator:
· Je, bado kama taifa tuna uhaba wa wasomi/wataalum?
· Je, tunao wasomi/wataalam lakini wengi ni wababaishaji (wachakachuaji)?
· Je, tunao wasomi/wataalam lakini mazingira (social and economic institutions and infrastructure) zinawanyima nafasi kutumia uwezo wao kuchangia ujenzi wa taifa?
· Je, tunao wasomi/watalaam lakini hawathaminiwi?
· Je, tunao wataalam lakini wengi wamegeuka kuwa wanasiasa?

.

1. Tukiangalia takwimu za idadi ya graduates wakati wa uhuru na sasa, tunaweza kuona kuwa sasa tunao wengi sana, hata wataalamu pia wameongezeka sana

2. Lakini ukiangalia quality ya wasomi na wataalamu wetu ni tofauti sana na ile ya wengine katika nchi za nje, au ni tofauti na ile ya wale wa miaka ya 60 na 70. Sio siri kuwa siku hizi kuna vihiyo wengi tu, Kuna watu wanajiita maDr na maProfesa, lakini ukiangalia uwezo wao unaona kabisa hakuna kinacholingana na uwezo wao. Kwa ufupo they are incapable au impotent

3. Kwa wale ambao wamequalify kweli, kwa wale ambao ni capable mazingira yetu si mazuri. Ukiangalia unaona kuwa sehemu nzuri ya kucheza hapa Tanzania ni siasa, si ajabu maprofesa wanataka ubunge ambao hata watu mbumbumbu kabisa pia wako humo humo. Kwa ufupi ni kwamba Tanzania siasa ndio professio inayoheshimiwa na kulipa kuliko uhandisi, udaktari, ualimu etc

4. Angalia ni nani anayelipwa zaidi, mbunge, mwalimu, mhandisi, mwanajeshi, daktari, ni nani anayepewa marupurupu makubwa zaidi, ni nani anayepewa heshima zaidi, utaona kuwa wataalamu na wasomi hawajapewa kipaumbele. Angalia yaliyomkuta Tido Mhando, mtaalamu aliyeheshimiwa na serikali ya Uingereza lakini hapa Tanzania aalifukuzwa na wanasiasa.

5. Hapa Tanzania ili uweze kukata vizuri keki ya pato la taifa ni kuwa mwanasiasa tu, ukiingia huko hata ukiwa jambazi, fisadi au tapeli utaheshimiwa. Angalia madaktari, wahandisi, walimu wanavyofanyiwa, au angalia ni wanasiasa wangapi wameacha uanasiasa na kuwa wahandisi, madaktari, walimu .....angalia ni wahandisi, madaktari, walimu wangapi wameacha taaluma zao na kuwa wanasiasa, utaona kuwa ni wengi sana.
 
...Si ajabu maprofesa wanataka ubunge ambao hata watu mbumbumbu kabisa pia wako humo humo.

..huku katiba ikisema sifa za elimu kwa mgombea ubunge ni angalau awe amefika darasa la saba;

...Angalia ni nani anayelipwa zaidi, mbunge, mwalimu, mhandisi, mwanajeshi, daktari, ni nani anayepewa marupurupu makubwa zaidi, ni nani anayepewa heshima zaidi, utaona kuwa wataalamu na wasomi hawajapewa kipaumbele.

Mwalimu miaka ya 1960 kwenye kitabu chake cha TANU na Raia alipata kusema:

"Tulipokuwa tukitawaliwa na wakoloni tuligawanywa katika mafungu matatu. Wazungu walikuwa juu, wahindi wakawa katikasi na waafrika walikuwa chini, kwah hali zao za elimu, mali navyeo. Yawezekana wachache wa kundi fulani la chini walipata bahati ya kuwa miongoni mwa kundi la juu, lakini kwa ujumla hivyo ndivyo tlivyokuwa. Shabaha ya TANU na serikali ya TANU ilikuwa ni kuondoa makundi haya. Milango ya elimu, mali na vyeo ambavyo jana ilikuwa imefungwa kwa waafrika, leo inafunguliwa. Wazungu na wahindi ambao jana walipita milango hiyo kwa urahisi kwa sababu ya cheti cha kupita kilikuwa rangi tu, wanaona kwamba cheti hicho siku hizi hakitoshi kumpitisha mtu asiyestahili kupita. Mambo haya tunayatenda hivi sasa na tutaendelea kuyatenda mpaka mafungu yale tuliyorithi kwa mkoloni yawe yameondoka. Jambo ambalo hatuna budi kujiuliza ni hili:

*Je vitendo hivi vina shabaha gani? Ni shabaha ya kuinua wanyonge wa jana?
*Au shabaha ni kuwatia waafrika wachache katika nafasi za wazungu na wahindi?
*Shabaha yetu ni kuondoa makundi kati ya raia au ni kuunda makundi mapya?

Tutakuwa na kundi la waafrika ambao hawajambo katika hali ya mali, elimu na vyeo, na kundi la waafrika ambao nia taabani katika mambo yote hayo"

J.K Nyerere, TANU na RAIA (1962, UK.6).

...Hapa Tanzania ili uweze kukata vizuri keki ya pato la taifa ni kuwa mwanasiasa tu, ukiingia huko hata ukiwa jambazi, fisadi au tapeli utaheshimiwa. Angalia madaktari, wahandisi, walimu wanavyofanyiwa, au angalia ni wanasiasa wangapi wameacha uanasiasa na kuwa wahandisi, madaktari, walimu .....angalia ni wahandisi, madaktari, walimu wangapi wameacha taaluma zao na kuwa wanasiasa, utaona kuwa ni wengi sana.

Mwalimu anaendelea kusema:

"Tuchukue mfano wa mishahara. Wakoloni walipokuwa hapa wanapanga mishahara bila kujali uwezo wa watu wetu kuilipa mishahara hiyo, na bila kuilinganisha mishahara hiyo na mapato ya watu wetu; Lakini wao ilikuwa ni ada yao kufanya hivyo. Serikali ya wageni haiwezi kujali maisha ya raia. Serikali yao ilikuwa ni serikali ya ubwana na ufahari; na walijitimizia ubwana wao na fahari yao, bila kujali uwezo wa watu wetu wa kugharamia ubwana huo na fahari hiyo;

Lakini baadhi yetu tulikuwa hatutambui jambo hilo. Waafrika wengi tulikuwa tumekwisha kusahau kwamba mzigo ule wa ubwana na fahari ni mzito mno na watu wetu hawawezi kuubeba. Kilichokuwa kikituuma ni kwamba ubwana ule na fahari ile wazungu waligawana wenyewe tu, bila kutugawia na sisi pia; baadhi yetu hatukuwa tunadai uhuru ili uwapunguzie watu wetu mzigo huu wa ubwana na ufahari, bali tamaa yetu ilikuwa ni kukalia viti vile vya ubwana na ufahari. Tamaa yetu haikuwa kushika vyeo tu vilivyokuwa vimeshikwa na wazungu, tulitaka na mishahara yao pia iliyokuwa ikifuatana na vyeo hivyo bila kujali kama watu wetu wanaweza kulipa mishahara hiyo, na bila ya kujali maisha ya watu wetu"

J.K Nyerere, TANU na Raia (1962, UK.7)
 
..huku katiba ikisema sifa za elimu kwa mgombea ubunge ni angalau awe amefika darasa la saba;



Mwalimu miaka ya 1960 kwenye kitabu chake cha TANU na Raia alipata kusema:

"Tulipokuwa tukitawaliwa na wakoloni tuligawanywa katika mafungu matatu. Wazungu walikuwa juu, wahindi wakawa katikasi na waafrika walikuwa chini, kwah hali zao za elimu, mali navyeo. Yawezekana wachache wa kundi fulani la chini walipata bahati ya kuwa miongoni mwa kundi la juu, lakini kwa ujumla hivyo ndivyo tlivyokuwa. Shabaha ya TANU na serikali ya TANU ilikuwa ni kuondoa makundi haya. Milango ya elimu, mali na vyeo ambavyo jana ilikuwa imefungwa kwa waafrika, leo inafunguliwa. Wazungu na wahindi ambao jana walipita milango hiyo kwa urahisi kwa sababu ya cheti cha kupita kilikuwa rangi tu, wanaona kwamba cheti hicho siku hizi hakitoshi kumpitisha mtu asiyestahili kupita. Mambo haya tunayatenda hivi sasa na tutaendelea kuyatenda mpaka mafungu yale tuliyorithi kwa mkoloni yawe yameondoka. Jambo ambalo hatuna budi kujiuliza ni hili:

*Je vitendo hivi vina shabaha gani? Ni shabaha ya kuinua wanyonge wa jana?
*Au shabaha ni kuwatia waafrika wachache katika nafasi za wazungu na wahindi?
*Shabaha yetu ni kuondoa makundi kati ya raia au ni kuunda makundi mapya?

Tutakuwa na kundi la waafrika ambao hawajambo katika hali ya mali, elimu na vyeo, na kundi la waafrika ambao nia taabani katika mambo yote hayo"

J.K Nyerere, TANU na RAIA (1962, UK.6).



Mwalimu anaendelea kusema:

"Tuchukue mfano wa mishahara. Wakoloni walipokuwa hapa wanapanga mishahara bila kujali uwezo wa watu wetu kuilipa mishahara hiyo, na bila kuilinganisha mishahara hiyo na mapato ya watu wetu; Lakini wao ilikuwa ni ada yao kufanya hivyo. Serikali ya wageni haiwezi kujali maisha ya raia. Serikali yao ilikuwa ni serikali ya ubwana na ufahari; na walijitimizia ubwana wao na fahari yao, bila kujali uwezo wa watu wetu wa kugharamia ubwana huo na fahari hiyo;

Lakini baadhi yetu tulikuwa hatutambui jambo hilo. Waafrika wengi tulikuwa tumekwisha kusahau kwamba mzigo ule wa ubwana na fahari ni mzito mno na watu wetu hawawezi kuubeba. Kilichokuwa kikituuma ni kwamba ubwana ule na fahari ile wazungu waligawana wenyewe tu, bila kutugawia na sisi pia; baadhi yetu hatukuwa tunadai uhuru ili uwapunguzie watu wetu mzigo huu wa ubwana na ufahari, bali tamaa yetu ilikuwa ni kukalia viti vile vya ubwana na ufahari. Tamaa yetu haikuwa kushika vyeo tu vilivyokuwa vimeshikwa na wazungu, tulitaka na mishahara yao pia iliyokuwa ikifuatana na vyeo hivyo bila kujali kama watu wetu wanaweza kulipa mishahara hiyo, na bila ya kujali maisha ya watu wetu"

J.K Nyerere, TANU na Raia (1962, UK.7)

Inawezekana kabisa sababu ya TANU na JKN ku africanize leadership ilikuwa ni kwa msingi kuwa wakiwa waafrika watafanya kazi kwa jili ya waafrika waliowengi, wale wazungu walikuwa chini ya serikali ya Uingereza na waliongozwa na maslahi ya nchi yao halafu wakaongozwa na maslahi ya Tanzania na watanzania hayakuwepo akilini mwao, so kimsingi naweza kukubaliana kabisa na wazo la mwalimu na TANU.

Inawezekana kuwa wakati ule hatukuwa na akili za kutosha kujua umuhimu wa ofisi ni nini. Lakini sasa hivi ni kama tuko worse kuliko wakati ule, angalia watu wanagombea ubunge kwa nini, au wanatafuta kuteuliwa kuwa mawaziri kwa nini, si kwa ajili ya kuserve taifa, ni kwa ajili ya maslahi yao binafsi.

hata utoajai wa mishahara au financial rewards nyingine una vigezo vya ajabu sana, haujali ume-invest kiasi gani kwenye elimu yako wala una deliver kiasi gani kwenye kazi yako.

Hata ukijaribu kuangalia watu wanapoteuliwa utasikia kuna neno moja la kijinga sana linatumiwa......amepewa uwaziri, amepewa ubunge, amepewa ukuu wa wilaya......infact ni kweli watu wengi wanapewa tu, hawa qualify na hawa-deserve.
 
Mchambuzi kuna wasomi wengi ambao wangeweza kufanya kazi za ubunge, udiwani etc etc lakini wako benchi, na wachovu na wababaishaji ndio wamekalia viti. Naona hizi ndio issues ambazo watanzania tunatakiwa kujiuliza, ni kwanini. Lakinin pia kuna wasomi, maprofesa na wengine ni wanazuoni wakubwa kabisa, ukisikiliza wanapoongea unaweza kuuliza kama kweli wana akili, ni wazima au wameamua tu kuuvaa wenda wazimu, watu kama hawa nao hawana maana kabisa ni bora wakae nje. Kwa hiyo kuna complications kidogo.

Kwa sasa mtanzania yeyote mwenye akili timamu hawezi kuisifia serikali ya sasa au kukisifia chama kwa sasa. Vyote viwili viko ovyo kabisa, na ukizungumzia siasa ya ujamaa Tanzania utakuwa mwendawazimu kabisa, kwani ukiangalie hata wale walijiapiza kuwa wakomunisti wanaonekana kuwa ni mabepari na mafisadi wakubwa. Sina nongwa na ubepari mwenyewe naupenda, lakini sikubaliani na ufisadi, au ubepari unaotokana na wizi. lakini sielewi kabisa kwanini ubepari tunauita ujamaa na na ufisadi tunauita changamoto inayotokana na maendeleo...

Nakubaliana na Mchambuzi na wewe Bongolander kuwa wasomi wetu wa leo have betrayed their professions; wengi wao sio wakweli kama utaalam wao unavyotaka wawe bali wamekuwa wanafiki ili kuwapendezesha watawala wawape vyeo / washibishe matumbo yao!! Ni ajabu sana kwani kuna wasomi wamepewa kazi za ushauri na kutunga sera mbalimbali za nchi ,lakini utashangaa jinsi watawala wanavyotoa maamuzi kutokana na ushauri wa wasomi hawa , maamuzi na sera ambazo hazina national interests.

Mifano ni mingi toka kwenye mikataba ya madini, ubinafsishaji wa mashirika, uuzaji wa ardhi kwa wawekezaji wageni na zaidi ya yote hatujifunzi kutokana na makosa tuliyafanya huko nyuma bali inaelekea tuta fanya makosa yale yale kwenye uchimbaji na uuzaji wa gesi asilia tuliyoigundua hivi karibuni!! Wasomi wetu hawana uzalendo period na ili kurudisha uzalendo uliopotea ni lazima tuanzie kwenye the type of education tunayotoa kwa watoto wetu.

Ni lazima tuwathamini waalimu wetu ili waweze kufundisha vizuri; ni lazima madaktari wetu wawe motivated ili tuwe na taifa lenye afya na hili litawezekana tu pale taifa litakapoweza kuzalisha chakula na mazao ya kutosha kuweza kujitosheleza. Taifa lazima liwe na sera ya kujitegemea kutokana na maliasili tulizo nazo na kamwe hatuwezi kuendelea kwa kuwa taifa la omba omba!! Lazima nchi ipate uongozi wenye vision ya maendeleo ya nchi na sio kuiibia nchi.

We must have policies that advocate an equitable distribution of the national cake among the populace.
 
Last edited by a moderator:
...........
Tukirudi kwenye hoja kwamba wasomi hawafai kwani ni watu waliojaa theory pekee, as a matter of fact, kwa msomi wa kweli na alie makini,kuitwa too theoretical sio matusi kwani kazi kubwa ya msomi is to theorize reality na hivyo ndivyo msomii uzidi kuelewa ukweli wa suala husika. ..............

RED: Maeneo mengine katika post hii nimekuelewa vizuri sana na nakubaliana na wewe katika maeneo mengi uliyoyazungumzia. Lakini katika hili napata shida kukubaliana na wewe. Kama wasomi wanatakiwa wawe hivyo kama unavyoelezea basi kuna tatizo juu ya maana ya neno msomi. Binafsi, najua msomi anaelewa jambo na kulitolea mapendekezo muafaka, na mapendekezo haya anaweza ama asiweze kushiriki moja kwa moja kuyatekeleza.

Lakini pia maelezo haya yanapingana na maelezo yako juu ya wasomi haya ya mwisho wa posti hii. Haya hiyo inaeleza kuwa wasomi wanaweza kutumia theories kuelewa jambo husika, lakini hawaishii hapo tu kuelewa jambo husika, wanatoa suluhisho lililo bora kwa jamii kama jambo walilolielewa linahusiana na matatizo yanayowakabili wanajamii (rejea katika mfano wako wa wasomi na katiba).

Mchambuzi kusahau suala la kutoa mapendekezo na utekelezaji wa mapendekezo ya wasomi kwa mambo amabayo wameyafanyia utafiti na kuyaelewa si sawa. Vinginevyo, nisaidie kunifafanulia ulimaanisha nini katika hiyo sehemu niyoiweka rangi nyekundu.
 
RED: Maeneo mengine katika post hii nimekuelewa vizuri sana na nakubaliana na wewe katika maeneo mengi uliyoyazungumzia. Lakini katika hili napata shida kukubaliana na wewe. Kama wasomi wanatakiwa wawe hivyo kama unavyoelezea basi kuna tatizo juu ya maana ya neno msomi. Binafsi, najua msomi anaelewa jambo na kulitolea mapendekezo muafaka, na mapendekezo haya anaweza ama asiweze kushiriki moja kwa moja kuyatekeleza.

Lakini pia maelezo haya yanapingana na maelezo yako juu ya wasomi haya ya mwisho wa posti hii. Haya hiyo inaeleza kuwa wasomi wanaweza kutumia theories kuelewa jambo husika, lakini hawaishii hapo tu kuelewa jambo husika, wanatoa suluhisho lililo bora kwa jamii kama jambo walilolielewa linahusiana na matatizo yanayowakabili wanajamii (rejea katika mfano wako wa wasomi na katiba).

Mchambuzi kusahau suala la kutoa mapendekezo na utekelezaji wa mapendekezo ya wasomi kwa mambo amabayo wameyafanyia utafiti na kuyaelewa si sawa. Vinginevyo, nisaidie kunifafanulia ulimaanisha nini katika hiyo sehemu niyoiweka rangi nyekundu.

Mkuu,
Sahamani, unaweza kunifafanulia hiyo in blue, sijakupata vizuri;
 
Mkuu,
Sahamani, unaweza kunifafanulia hiyo in blue, sijakupata vizuri;
Kwa maneno mengine ni kuwa wasomi wa kweli na makini hawaishii kuelewa theories pekee za mambo yanayohusu jamii, bali wanaenda mbali zaidi kutumia theories hizo kutoa mapendekezo ya kuisaidia jamii kwa kadri walivyoelewa mambo husika. Pia wanashiriki kwa namna moja ama nyingine kufanya utekelezaji wa mapendekezo yao.

Hivyo kusema wasomi ni watu wa theories na kuelewa mambo tu basi, sio sahihi na na hisi yale maelezo niliyoyapaka rangi nyekundu hapo awali yalikuwa yana wakejeli wasomi.
 
Kwa maneno mengine ni kuwa wasomi wa kweli na makini hawaishii kuelewa theories pekee za mambo yanayohusu jamii, bali wanaenda mbali zaidi kutumia theories hizo kutoa mapendekezo ya kuisaidia jamii kwa kadri walivyoelewa mambo husika. Pia wanashiriki kwa namna moja ama nyingine kufanya utekelezaji wa mapendekezo yao.

Hivyo kusema wasomi ni watu wa theories na kuelewa mambo tu basi, sio sahihi na na hisi yale maelezo niliyoyapaka rangi nyekundu hapo awali yalikuwa yana wakejeli wasomi.

Pengine sikueleweka vizuri vinginevyo hakuna sehemu ninakejeli wasomi; nilicholenga hasa ilikuwa kuelezea jinsi gani wasomi wamekuwa hawatumiki ipasavyo; kuhusu theories...nilichokuwa namaanisha ni kwamba wasomi (hasa wa chuo kikuu/professors) wakitoa maoni yao kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu mustakabali wa taifa, wanasiasa huwa wanawakejeli kwamba they are too academic, they are too theoritical, they dont understand reality, they are just armchair critics who enjoy destructive criticisms and so forth and so forth; ndio nikasema kwamba msomi kusemwa kwamba yupo too theoritical isiwe suala la kumvunja moyo kwani kazi yake ya msingi ya msomi (PhDs kwa mfano), ni pamoja na to "theorise reality", hivyo kusaidia jamii kuelewa reality vizuri zaidi;

Isitoshe, dhamira kuu ya ku-theorize, kwanza ni to make sense of reality (kutokana na observation fulani kwenye jamii au issue), halafu based on the observed reality, kukusanya evidence na kufanyia hii evidence tathmini itakayosaidia kuelewa zaidi the reality observed...
 
Pengine sikueleweka vizuri vinginevyo hakuna sehemu ninakejeli wasomi; nilicholenga hasa ilikuwa kuelezea jinsi gani wasomi wamekuwa hawatumiki ipasavyo; kuhusu theories...nilichokuwa namaanisha ni kwamba wasomi (hasa wa chuo kikuu/professors) wakitoa maoni yao kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu mustakabali wa taifa, wanasiasa huwa wanawakejeli kwamba they are too academic, they are too theoritical, they dont understand reality, they are just armchair critics who enjoy destructive criticisms and so forth and so forth; ndio nikasema kwamba msomi kusemwa kwamba yupo too theoritical isiwe suala la kumvunja moyo kwani kazi yake ya msingi ya msomi (PhDs kwa mfano), ni pamoja na to "theorise reality", hivyo kusaidia jamii kuelewa reality vizuri zaidi;

Isitoshe, dhamira kuu ya ku-theorize, kwanza ni to make sense of reality (kutokana na observation fulani kwenye jamii au issue), halafu based on the observed reality, kukusanya evidence na kufanyia hii evidence tathmini itakayosaidia kuelewa zaidi the reality observed...


Mchambuzi nakubaliana kabisa na wewe kuhusu hayo unayosema. Tatizo kubwa sana la wasomi wetu ni kuwepo Tanzania kimwili lakini kinadharia wanaishi sehemu tofauti, wengi huwa wanafanya makosa makubwa sana ya kutumia nadharia za vitabuni kwa mazingira ambayo ni tofauti na nadharia zilikotoka.

Unajua ni sawa na kutumia AK 47 kuua mbuzi, au kutumia dawa ya kuua mbu kujaribu kumuua kenge. Kuna baadhi ya mambo, au mambo mengi ya Tanzania, yanaweza kutatuliwa kwa kuwa practical, kuangalia reality on the ground na ku deal na reality. Wasomi wetu wengi wanashindwa kuangalia hilo.

Unaweza kumuuliza msomi hapa Tanzania kwanini kuna tatizo la umeme, baada ya kusema jibu ni kwamba viongozi wetu ni mafisadi wanahujumu umeme, jibu litakuwa mvua, mikataba ya kimataifa, mito imekauka, upepo umepata moto, au trnasti imecorss na ku bend, tea, sugar, soap.....na mengine mengi ambayo hayaeleweki. Tena anaweza kuanza hata kukwambia suluhisho ni theory A na CD etc etc etc, wakati mwananchi wa kawaida jibu ni moja na ndio linatakiwa kushughulikiwa. Hili ndio tatizo kubwa la wasomi wetu, most are completely out of touch.

Ndio maana mtu kama Mrema ambaye ni mchivu kielemu aliweza kuwa effective kwenye wizara ya mambo ya ndani kuliko hata wasomi wengine waliomfuata, so as Pombe Magufuli. They are practical si wapiga blaa za kisiasa.
 
.........Ndio maana mtu kama Mrema ambaye ni mchivu kielemu aliweza kuwa effective kwenye wizara ya mambo ya ndani kuliko hata wasomi wengine waliomfuata, so as Pombe Magufuli. They are practical si wapiga blaa za kisiasa.
Vile vile Marehemu Edward Sokoine; Kuna kitabu kimoja nimekisoma na kugundua jinsi gani kiongozi huyu asivyopewa heshima (hasa na viongozi uchwara waliomfuata baadae) anayostahili kwa mchango wake mkubwa sana kwa taifa letu (Tanzania); huyu mtu alikuwa anaelekea urais after nyerere on merit kabisa; wengi wetu tulimjua kwa suala la vita dhidi ya mafisadi (wahujumu uchumi tu), lakini kumbe mtu huyu alifanya mambo makubwa sana kwenye kilimo n.k; nikipata muda nita-share taarifa hii.

Mbali ya Nyerere, hakuna kiongozi mwingine wa ngazi za juu (mawaziri wakuu, makamo wa rais na marais) aliyelifanyia taifa hili mambo ya maana in terms of legacy kama Sokoine (ukimtoa mkapa ambae alijaribu kidogo) pamoja na elimu yake ya Form Four (i.e. Sokoine); bottom line is, you have a point kuhusu Mrema
 
Sasa Mchambuzi nimekuelewa ulichomaanisha.

Bongolander nikupe kisa kimoja:

Kuna mwanafunzi fulani (mtanziani) aliyekuwa anasoma katika chuo kikuu fulani hapa tanzania ambaye alitaka kufanya usanifu (ni kimaanisha designing) kifaa cha kutatua tatizo la kijamii katika masuala ya kihandisi kama sehemu ya kuanda repoti ya mradi ambayo inatakiwa ili kuhitimu elimu ya chuo.

Mwanafunzi huyo alimfuata mwalimu, tena inasemekana ni Full Professor sio Associate Professor,huku akiwa na PhD katika masuala yanayohusiana na hicho kifaa kitakapotumika. Mwanafunzi alimueleza mwalimu huyo wazo lake hilo na namna atavyofanya kulitekeleza. Mwalimu huyo alimuuliza kama amepitia machapisho yoyote kwenye internet au hata makitaba kama kuna watu waliwahi kutengeneza kifaa hicho. Mwalimu huyo aliongeza kuwa kama hakuna chapisho lolote linaloelezea kifaa hicho aachane na wazo hilo kwani hataweza ingawa wazo lake ni muhimu kwa jamii. Mwanafunzi alijitahidi kufafanua kuwa ataweza kwani hata gharama ya kukitengeneza anakadiria itakuwa ndogo sana pia muda utamtosha. Mwalimu huyo alikataa katakata na kumueleza kuwa kama hawezi kuachana na wazo hilo atafute mwalimu mwingine.

Sasa waweza kuona baadhi ya walimu tulionao katika vyuo vyetu.
 
Mimi naamini mwalimu ajiwajali sana wasomi ila wasomi wale waliokuwa na nia ya kuharibu taifa kwa hakika alijitahidi sana kuwapotezea. ila kipindi kile pia wasomi walikuwa wachache.

Sasa hivi CCM inao wasomi wengi ila wasomi tatizo wanatumiwa kukilinda chama kilichoshikwa na wachache wenye maslai fulani hivyo kufanya wasomi ndani ya chama kutotumia taaluma kwa uwazi na haki kwa maslai ya taifa na chama ila kwa matumbo ya wachahce na kusababisha wasomi hao kupindisha taaluma zao na kuwa kama mazoba.
 
3. Wachochezi (Political trouble makers) – kundi la tatu ni lile la wachochezi. Kazi kubwa ya watu hawa ni kuushawishi na ku-bamboozle umma, na ni mabingwa wa kutumia vyema prejudices na stereotypes zilizopo kwenye jamii yetu kwa maslahi ya CCM. Viongozi hawa huwa hawaheshimu mantiki (logic), human decency, consistency na hawana muda kusoma alama za nyakati. Misamiati na kauli mbiu nyingi za CCM hutokana na viongozi wa namna hii wakisaidiwa na wenzao (wapambe na wanaitikadi feki). Lakini muhimu zaidi ni kwamba, hawa ni mabingwa wa kupika uongo mbalimbali kisha kuujengea hoja na propaganda kwamba huo ndio ukweli uliosadidika, usiopingika na unaotakiwa kuabudiwa. Na iwapo anatokea mtu mwingine kupingana nao, basi ubatizwa kila aina ya majina – muhasi, haramia, adui, mhuni, mkabila, n.k, na mara nyingine maisha yako yanaweza kuwa hatarini. Wachochezi hawana muda wa kuheshimu dhana ya uhuru wa mawazo; huwa hawaoni any merit on a political opponent (mfano tazama tabia na kauli zao dhidi ya upinzani bungeni) na badala yake wanajaribu kuwatuhumu wale wote wanaowa ‘challenge' kwa mbinu za udini, ukabila, ukanda, n.k. Viongozi wa namna hii ni mabingwa wa ku-appeal on stereotypes, prejudices, emotions, fears, na expectations za umma kwa kujenga propaganda based on themes za kidini, kikabila, ukanda n.k. Wachochezi ndio hutumika zaidi katika kuzima hoja za wasomi zinazolenga maslahi ya taifa.

Huyu ana fit perfectly kwenye Kundi hili:
attachment.php


attachment.php

Nape-Nnauye1-538x600.png
 
Back
Top Bottom