CCM Maarufu: Utafiti wa Synovate wabainisha!

CCM Maarufu: Utafiti wa Synovate wabainisha!

Hao Synovate(Ipsos) ni waongo sana,niliwah kufanya nao kazi tena nying sana na mimi nikawa ni mmoja wao wa kutindua madodoso kwa hyo hata hzo habari zao ni za uwongo
 
Kwanza nawasalimu ndugu zangu wote humu JF! Mwenzenu huwa mzimu wa REDET na tafiti zake unaniandama kila nisikiapo neno utafiti.Kuna viji taasisi vinaibuka na kushika kasi kila tunapoelekea kwenye uchaguzi nchini.Unaweza kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa au uchaguzi mkuu ambapo vitaasisi hivyo hujifanya kutoa tathmini za kisiasa bila kuainisha 'objectives of the study,population size,area of study e.t.c) Kama hutakuwa makini unaweza kuaminishwa ujinga nawe ukapoteza muda kujadili kitu ambacho hakipo ukiacha mambo muhimu kuhusu gesi,uranium,kushuka kwa kiwango cha elimu,migogoro ya ardhi,katiba mpya,vitambulisho vya taifa,vazi la taifa,kilimo na teknolojia eti tunajadili CCM kimekuwa maarufu. Nahoji,kati ya chama cha zamani na vyama vipya kipi kinaweza kupanda kuwa maarufu? Utafiti wa Synovate ulilenga nini,wametumia vigezo gani kupima umaarufu na wamewahoji watanzania wangapi? Nielewesheni!

issue ya msingi ni Babu kugeuza mke wa mtu na kuwa kimada wake nyie hapa JF mbinu mnayotumia yakuwa na account 30 30 si ndio mnavyojidanganya....ngoma uraiani raia wamesanda ariff
 
Ya kujikopesha ruzuku ya chama?

Swadatah. Watu wengi walidhani Babu kasingiziwa, ila alivyojitoa muhanga live kuwa ni mil. 20 tu, watu wamepoteza imani naye kabisa!!!

Sasa hivi wananchi wanahoji jengo lilipangishwa na chadema Kinondoni ni la nani na linalipiwa sh. ngapi kwa mwezi...
 
Jengo ni mali ya CHADEMA,wananchi wanahitaji kujua hatma ya rasilimali za Taifa,ambazo ccm wanazifisadi,endeleeni kujipa moyo kuwa ccm inakubalika,anguko la ccm li dhahiri
 
Ili muwe maarufu Chadema punguzeni mitusi na chuki za kidini.
 
Ya kujikopesha ruzuku ya chama?

Ninyi watu wa CCM huwa mnachekesha kweli. Mnajaribu kutafuta boriti katika jicho la Chadema kumbe kwenu yamejaa hata mmeshindwa kuyashughulikia kiasi mnaanza kuwa vipofu.
 
Kwanza nawasalimu ndugu zangu wote humu JF! Mwenzenu huwa mzimu wa REDET na tafiti zake unaniandama kila nisikiapo neno utafiti.Kuna viji taasisi vinaibuka na kushika kasi kila tunapoelekea kwenye uchaguzi nchini.Unaweza kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa au uchaguzi mkuu ambapo vitaasisi hivyo hujifanya kutoa tathmini za kisiasa bila kuainisha 'objectives of the study,population size,area of study e.t.c) Kama hutakuwa makini unaweza kuaminishwa ujinga nawe ukapoteza muda kujadili kitu ambacho hakipo ukiacha mambo muhimu kuhusu gesi,uranium,kushuka kwa kiwango cha elimu,migogoro ya ardhi,katiba mpya,vitambulisho vya taifa,vazi la taifa,kilimo na teknolojia eti tunajadili CCM kimekuwa maarufu. Nahoji,kati ya chama cha zamani na vyama vipya kipi kinaweza kupanda kuwa maarufu? Utafiti wa Synovate ulilenga nini,wametumia vigezo gani kupima umaarufu na wamewahoji watanzania wangapi? Nielewesheni!

Hata sifa mbaya ni sifa! Waweza kuwa maarufu kwa ubovu wako.....
 
Jengo ni mali ya CHADEMA,wananchi wanahitaji kujua hatma ya rasilimali za Taifa,ambazo ccm wanazifisadi,endeleeni kujipa moyo kuwa ccm inakubalika,anguko la ccm li dhahiri

we acha uongo jengo la CDM tangu lini? Ndivyo ulivyodanganywa hivyo? Pole!
 
Jengo ni mali ya CHADEMA,wananchi wanahitaji kujua hatma ya rasilimali za Taifa,ambazo ccm wanazifisadi,endeleeni kujipa moyo kuwa ccm inakubalika,anguko la ccm li dhahiri

This is news, limeshakuwa la chadema?!!! Toka lini???? Wamelinunua kwa nani???
 
Kitu cha muhimu katika research ni methodology na sio methods, waweza kuwa na methods and data nzuri lakini bado ukashindwa ku-draw/generalise warrantable inference.

Chifu, hilo ndilo la msingi katika utafiti. Kuna na njia ya uhakika katika kufikia jumuisho kuu.

Na katika kufikia jumuisho kuu (generalisation), namna ya kupata wahojiwa (sampling strategies and procedures) ni muhimu sana. Ingawa hakuna makubaliano rasmi ya kiasi cha wahojiwa wawakilishi (sample population) kinachotakiwa katika utafiti. Waandishi wengi wanasema uwakilishi wa kati ya asilimia 5 hadi 10 ya idadi ya jumla ya wahojiwa tarajiwa (total population or households; depending in the central unit of research and analysis) ndiyo stahili. Sasa kati ya watanzania milioni 45, kuna na wawakilishi (sampled population) ya watu 2000+ au si zaidi ya 10,000, ni aibu. Kwa namna hiyo huwezi kutoa jumuisho kuu (generalisation) katika aina ya sample iliyotumika!

Kwa idadi hiyo ni vigumu kupata representativeness katika sampled population. Bila representativeness, pia inakuwa si stahiki kufanya generalisation.

Vagueness katika applied sampling strategies na procedures pia inasababisha ugumu katika replication ya utafiti. Bila replication, generalisation becomes questionable and the whole research becomes unscientific!
 
Hizi ni propaganda za akina nape nnauye kuhamisha mada ya elimu na kufeli kwao, synovate wanashughulika na kenya hawawezi kuhangaika na umaarufu wa vyama vya tanzania
 
Hata Tyson hakuamini siku alipopigwa na Lewis.
Kila siku tunashuhudia CCM yagalagazwa vijijini wiki iliyopita wamegalagazwa vibaya Magu wiki mbili zilizopita Bukoba vijijini, wakati CCM wakipumbazika na mbeleko za Synovate na REDET, on the contrary CHADEMA watumie ripoti hizi kuchapa kazi kweli kweli mwisho wa siku watajikuta wamefanya zaidi ya walivyotegemea.
 
Molemo. Umenena mkuu,nadhani hawa watu wanatafuta ulaji.Ni vema kwa taifa kuwa na taasisi za utafiti wa kisiasa ambazo ni huru kabisa.CCM ni maarufu siku zote ila siyo imara kama 2000-2010.Labda ndugu zetu wana tafsiri nyingine ya umaarufu.Lakini pia najiuliza,CCM kimekuwa maarufu kwenye nyanja gani na kivipi?

Ni maarufu kwa sababu akina nepi na chemba kazi yao ni kutuukana tu jukwaani hawana hoja na kwa sababu huo mtindo ni mpya ndio maana kinajipatia umaarufu,hongereni ccm endelezeni matusi
 
Last edited by a moderator:
issue ya msingi ni Babu kugeuza mke wa mtu na kuwa kimada wake nyie hapa JF mbinu mnayotumia yakuwa na account 30 30 si ndio mnavyojidanganya....ngoma uraiani raia wamesanda ariff

Ulitaka akugeuze wewe au Dadako?
 
Umaarufu???Umaarufu kwa uzuri au ubaya??Umaarufu wa matusi na ukatili uso na utu wala soni?KWA LIPI WAJAMENI?CCM IPI?HAYA NI MAANDALIZI YA USANII MWINGINE UNAOTARAJIWA KURUSHWA LIVE OCTOBER-2015.~~~KWA UWEZO WA ALLAH WA SUBHANA wasanii wote wanaotarajiwa kushiriki tamasha hili la dhulma kwa jamii wachanganyikiwe na washindwe kufanikisha show hii.Amin.***Ben where is Kivuitu now???
 
My crystal ball tells me that huu utafiti umekuwa funded na CCM, na umefanywa within the parameters walizotaka wao CCM. Na hii inaongeza uwezakano wa biaseness /'directive' research ili wapate matokeo ambayo walitaka wao. Hebu angalia hizi graphs hapa chini:

To me hizi graph zinatoa clue nzuri sana, kwamba utafiti ulikuwa wa CCM na hasa walitaka (CCM) kujua situation ikoje baada ya uchaguzi wao wa ndani. Wanauliza mgawanyiko ndani ya CCM na kama uchaguzi wa NEC utasadia kuponya makundi ndani ya chama.

Funny enough, almost half (45%) of the respondents wamesema uchaguzi wa NEC CCM haukuwa huru wala haki! Na wala hawana imani kuwa huu uchaguzi wa NEC utamaliza makundi. This is not a good sign. Unaanza kazi na team ambayo watu wanaamini 'wamepachikwa?

I am also suspecious na matokeo ya watu wanaodhaniwa kuwa wangefaa kuwa rais. Naona kama CCM wanawaanda wananchi kisaikojia! Hivi jamani, kati ya Pinda na Magufuli, nani anakubalika zaidi? Walikuwa wanauliza maswali gani hawa watu, na walifanya utafiti maeneo gani?

attachment.php
 
Hii tafiti wanayofanya synovate inaitwa SPEC AU SHADA na huwa kwa mwaka wanaifanya mara tatu.
Katika hii kampuni kuna malalamiko mengi sana kutoka kwa data collector kwa kulipwa pesa kidogo na hata wages zao kucheleweshewa wakati mwingine hadi miezi minne au mitano.Sasa kwa matatizo haya hawa data collector wataleta taarifa za kweli?

Na katika hii SPEC hawa data collector wanakaa siku hadi nne mkoani hawatumiwi night out siku wanapotumiwa wanalazimishwa kafanya hadi dodoso kumi kwa siku sasa hapo utapata taarifa za kweli? Wakati mwingine dodoso zinafanyiwa guest house!!

Mimi binafsi siwezi kuamini hata kidogo matokeo ya utafiti ya synovate.
Kama mnakumbuka uchaguzi mkuu uliopita synovate walitoa matokeo ya tafiti jimbo la Arusha mjini na kusema kuwa Dr Batilda Buriani anakubalika na wananchi wa Arusha mjini ile data ilipikwa na kilichomkuta Dr Batilda ni kushindwa vibaya na Godbless lema wa Chadema sasa kama tafiti ile ingefanyika na kampuni makini Dr Batilda angefahamu na angejipanga.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom