CCM Maarufu: Utafiti wa Synovate wabainisha!

CCM Maarufu: Utafiti wa Synovate wabainisha!

kuna watu wanakula alawanzi za mabwege, wacha wajifurahishe
 
NO SYNOVATE WALA SINAVOTE..........CCM huo ni utafiti wenu mnaoufanya kujpa Moyo na Imani kuwa bado mnathamininka,,,,,,,infact no 1 wants you anywhere and you can go to hell......TUMEWACHOKAHHHHHH.:shut-mouth::lying:
 
mwenzetu hiyo ripoti hata vyombo vya habari havijui wewe umeitoa wapi?
 
Tandale one,unamdanganya nani hapa?huwezi kulinganisha TZA1962 na T2015CDM,kajipange upyaa porojo zako.
 
ccm waendelee kujipa moyo kuwa wanakubalika,ndivyo tawala zote zilizokuwa zinaanguka,zilijipa moyo,ila mwisho wa siku zikaanguka,anguko la ccm haliwezi kuepushwa na utafiti kama huu
 
ccm maarufu.? Wapi ikiwa hata Lindi na Mtwara wameikataa.
 
Hii kampuni ni ya kitapeli na wala rushwa wakubwa. Msikubali kuingizwa chaka. Hakuna utafiti hapa ni maandalizi ya kumbeba mtu fulani na kumwangamiza mtu fulani. Dili lote kuna jamaa amesema analifuatilia na akifanikiwa kupata info atawaumbua. Habari za kuaminika ni kuwa hizi ni fedha za mzee mamvi zinaongea. Deal ni kwamba baada ya muda yatatolewa tena matokeo mengine ya kuonyesha Dr. Slaa/wagombea wengine wameshuka kwa percentage fulani na mzee mamvi ameongeza pcg fulani, halafu uchaguzi ukikaribia ndio Mamvi ''atapaishwa'' kwa kasi na kumpita Dr Slaa/wagombea wengine. Tuombe uzima jamaa akifaniwa atatuletea kwa undani na vielelezo vyote.

Pamoja mkuu, wenye akili tumestuka!
Hawa wachumia tumbo tu...CCM sasa hivi inakataliwa vijijini ambako imekuwa ikiongoza tangu uhuru..wenyewe wanasema umaarufu wao unaongezeka!

Aibu ya 2015 inawasubiri...na kama na wao wanataka wahusishwe na vurugu zitakazo tokea baada ya uchaguzi wataona..watz sasa tuko motomoto!! Patachimbika 2015!
 
Yani hawa jamaa kutishiwa tu kuwa watufukuzwa nchini bs wameamua kuibeba CCM? Wameivaa
 
Tatizo humu ndani JF hamkubali labda na nyie mfanye takwimu zenu.
CDM sasa hivi imepoteza mwelekeo, babu hana mvuto tena, asipoangalia atapotea kama alivyopotea Augustine Mrema.


Ndoto za PWAGU na PWAGUZI!
 
Taasisi ya kujitegemea inayofanya Utafiti wa masuala mbalimbali ikiwemo Utawala bora na Demokrasia hapa nchini, Synovate imetoa matokeo yake ya utafiti wake uliomalizika hivi karibuni na kubainisha vipengele muhimu ambavyo vinabashiri mustakabali wa uhai na uimara wa vyama vya siasa hapa nchini.

Utafiti huo umebainisha kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndicho chama maarufu zaidi hapa nchini kwa sasa ambapo umaarufu wake umeongezeka maradufu, utafiti huo umeonyesha kuwa zaidi ya asilimia 52 ya wananchi wote wa Tanzania wangependa kuijiunga na CCM, na hivyo kudhihirisha kuwa CCM bado ni chama Imara na kinachopendwa zaidi na watanzania walio wengi.

attachment.php


Rekodi hiyo mpya ya CCM inakinzana na kuviacha mbali vyama vya Upinzani ambavyo graph yao imeendelea kushuka na kupoteza umaarufu kwa kiasi kikubwa, mfano wa chama ambacho kinaongoza kambi ya Upinzani bungeni Chadema kimeshuka sana na kwamba ni asilimia 31 tu ya wananchi ndio ambao wangefikiria kujiunga na Chama hiko. Pamoja na M4C, operesheni Sangara,n.k bado hali ya chama hiko ni dhaifu mno kulingana na tafiti hizi. Hali ni mbaya zaidi kwa CUF ambayo ina asilimia 4 tu ya kuungwa mkono na watanzania.

attachment.php


Utafiti huo pia umebainisha kuwa kupanda kwa CCM na kuongezeka kwa umaarufu wake kunatokana na Utekelezaji wa Ilani yake kwa kasi inayoridhisha, lakini zaidi ni kutokana na Uchaguzi wake ambao umetengeneza safu mpya ambayo ni bora na imara ya Uongozi ndani ya Chama hiko kikongwe na MAARUFU duniani.

Lakini pia tafiti ya synovate imeenda mbali zaidi na kubainisha kushuka kwa Umaarufu wa Dr Slaa maarufu kama "BABU" ambapo imeelezwa kuwa ameshuka kwa asilimia 25 ambapo tafiti ya awali ilibainisha kuwa umaarufu wake ulikuwa ni kwa asilimia 42 na kwa sasa umeshuka na kubaki kwa asilimia 17 tu sawa na kushuka kwa asilimia 25.

attachment.php
Ongeza na Hii Hapa chini

[h=1]Utafiti: Dk Slaa aongoza vinara tisa urais 2015[/h]

Utafiti: Dk Slaa aongoza vinara tisa urais 2015 - Kitaifa - mwananchi.co.tz
 
Tumikia kafiri upate ujira kama imepitwa na wakati vile.
 
Huyu jamaa ni muongo... hakuna ripoti yeyote ya synovate imetolewa... mnajadili hewa
Unaweza kufuta kauli yako sasa.,kwa kutaka kupotosha umma kuwa ninachokiongea sio sahihi.,kwani tumeweka attachment ya graph na data muhimu zilizotumika katika tafiti hiyo.

Naomba uuthibitishie umma wa wanaJF kuwa wewe ni mtu wa kukurupuka na sio mtu ambae wanaweza kukuamini kwa lolote.
 
Tandaleone,umekuja na ripoti yako ya kishabiki,eti CHADEMA inaporomoka,pengine wewe haupo Tanzania hii,wala hujui dunia inakoelekea,Kwenye uchaguzi wa vijiji Magu tumeshinda kwa zaidi ya 75%,ambapo ni vijijini.Katika historia ya CHADEMA ;hakijawahi kurudi nyuma,bali ni kusonga mbele
 
Tandaleone,umekuja na ripoti yako ya kishabiki,eti CHADEMA inaporomoka,pengine wewe haupo Tanzania hii,wala hujui dunia inakoelekea,Kwenye uchaguzi wa vijiji Magu tumeshinda kwa zaidi ya 75%,ambapo ni vijijini.Katika historia ya CHADEMA ;hakijawahi kurudi nyuma,bali ni kusonga mbele
Kuna kila dalili inayonidhihirishia kuwa haujui unachokiongea.,kwanza kabisa hakuna uchaguzi wa serikali za mitaa wala uchaguzi wowote ambao unaendelea hivi sasa ambao unashindanisha kati ya vyama vya siasa. Hivyo kauli yako kuhusu "uchaguzi wa vijiji" sio ya kweli.

Lakini pia unanipa kila sababu ya kuamini kuwa uko mbali sana na yanayoendelea chadema hivi sasa na kushuka kwa credibility yao kwa wananchi. Nadhani unahitaji kuuliza kwa wanachadema wenzako wachache mliobaki juu ya kile kinachoendelea katika chama chenu.
 
Wana JF heshima kwenu wakuu;

Ni vyema mkalitambua hili laweza kuwasaidia Synovate na Redet ya Mkandala ni kama mtu na pacha wake, na madhumuni yake ni yale yale, hayajawahi badilika toka mwaka 2005. Lengo kuu la hizi taasisi ni kusafisha njia ya baadhi ya wale wenye ndoto za kuingia kwenye kinyang'anyiro cha Urais, na lengo lingine ni kutaka kututoa watanzania kwenye mstari, yaani tuachane na mijadala inayohusu mstakabali wa taifa letu na tuanze kujadili na kushabikia udaku ulio batizwa jina la utafiti.
 
Tandaleone,kama hujui kuwa wilayani magu kulifanyika uchaguzi mdogo wa vijiji na vitongoji basi huna hata idea na unachoandika hapa.Tangu baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 zimetokea chaguzi ndogo mbalimbali ambako CHADEMA ,imedhihirisha kuwa kinaaminiwa na watanzania,na kinazidi kuaminiwa,kama na hilo hulioni,basi utakuwa kipofu
 
Chadema wangeweka wazi mmiliki wa jengo walilopanga Kinondoni ni nani na wanamlipa sh. ngapi kwa mwezi labda wananchi wangeanza kuwaamini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom