CCM Maarufu: Utafiti wa Synovate wabainisha!

CCM Maarufu: Utafiti wa Synovate wabainisha!

ccm bado kina nguvu. lazima tuseme ukweli. kujiridhisha kwa kusema kuwa ccm kinaporomoka tunajidanganya. waliweza kutoka salama katika uchaguzi na uteuzi wa wajumbe wa halmashauri kuu na kamati kuu. jambo hilo limewasaidia kuwa imara hadi hii leo. kuhamia ccm kwa akina juliana na wenzake kumezidi kukiimarisha chama. wanazunguka nao mikoani kuiponda chdm

Acha wazunguuke mikoani na hao jamaa. Ila nasi tunajipanga kufanya research isiyokuwa yakifisadi wasije wakashika midomo humu jamvini kwani taarifa zao za kisynovate hazitawapeleka mbali hapo 2015
 
hatimaye Mnyika apinga matokeo ya synovate na kutaja matokeo ya utafiti wa barabarani usio na viwango katika kutetea hatua yake hiyo. Kimsingi hakuna ulazima sana wa kupigania usahihi ama upotoshaji wa tafiti ikiwa hali halisi inajulikana, uimara wa chama unathibitika na taarifa za utekelezaji wa sera za chama unaonekana waziwazi kwa wananchi.
Chadema imepoteza muelekeo na haiwezi kusimama tena.,imejivuruga ndani na kuwavuruga wafuasi wake nje., ni chama ambacho hakijitrangazi kwa sera wala ilani yake, ni chama cha harakati ambacho hakiwezi kutawala wala kuongoza. Wananchi wanayasikia na kuyaona yanayoendelea ndani ya chadema kamwe hawaweze kuiamini.,wataiamini kwa lipi..?

Mnyika usijisumbue kutumia nguvu nyingi kupingana na synovate ni bora ungelielekeza nguvu hizo katika kutatua migogoro yenu ya ndani na kufikia suluhu ya tofauti zenu.
 
Msipate shida kujadili report za hawa jamaa, nitawaelekeza maeneo ambayo mkienda muda kama huu mtawakuta vijana wao wanapika Data. Hapa nitataja baadhi ya maeneo tu ila nikipata muda nitawaeleza maeneo mengine zaidi. Arusha wapo Kismayo guest house ipo Levolosi pembeni ya ofc za magari ya Mwanza. moshi wapo Devotion guest house dar street, Mwanza wapo Lena Hotel ipo opposite Thaqaafa secondary school, Mbeya-Mariset iliyopo Mwanjelwa na Mafao ipo soweto karibu na Mbeya Carnival, dodoma- Kavula guest house ipo Bayi road, morogoro- Kwa babu au Shela park.
Nikikumbuka zingine nitawaletea ila haya ndio maeneo ambayo ukienda jioni lazima utawakuta na ni mabingwa wa kujiungia chumbani na kutengeneza data
 
Taasisi ya kujitegemea inayofanya Utafiti wa masuala mbalimbali ikiwemo Utawala bora na Demokrasia hapa nchini, Synovate imetoa matokeo yake ya utafiti wake uliomalizika hivi karibuni na kubainisha vipengele muhimu ambavyo vinabashiri mustakabali wa uhai na uimara wa vyama vya siasa hapa nchini.

Utafiti huo umebainisha kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndicho chama maarufu zaidi hapa nchini kwa sasa ambapo umaarufu wake umeongezeka maradufu, utafiti huo umeonyesha kuwa zaidi ya asilimia 52 ya wananchi wote wa Tanzania wangependa kuijiunga na CCM, na hivyo kudhihirisha kuwa CCM bado ni chama Imara na kinachopendwa zaidi na watanzania walio wengi.

attachment.php

Rekodi hiyo mpya ya CCM inakinzana na kuviacha mbali vyama vya Upinzani ambavyo graph yao imeendelea kushuka na kupoteza umaarufu kwa kiasi kikubwa, mfano wa chama ambacho kinaongoza kambi ya Upinzani bungeni Chadema kimeshuka sana na kwamba ni asilimia 31 tu ya wananchi ndio ambao wangefikiria kujiunga na Chama hiko. Pamoja na M4C, operesheni Sangara,n.k bado hali ya chama hiko ni dhaifu mno kulingana na tafiti hizi. Hali ni mbaya zaidi kwa CUF ambayo ina asilimia 4 tu ya kuungwa mkono na watanzania.

attachment.php

Utafiti huo pia umebainisha kuwa kupanda kwa CCM na kuongezeka kwa umaarufu wake kunatokana na Utekelezaji wa Ilani yake kwa kasi inayoridhisha, lakini zaidi ni kutokana na Uchaguzi wake ambao umetengeneza safu mpya ambayo ni bora na imara ya Uongozi ndani ya Chama hiko kikongwe na MAARUFU duniani.

Lakini pia tafiti ya synovate imeenda mbali zaidi na kubainisha kushuka kwa Umaarufu wa Dr Slaa maarufu kama "BABU" ambapo imeelezwa kuwa ameshuka kwa asilimia 25 ambapo tafiti ya awali ilibainisha kuwa umaarufu wake ulikuwa ni kwa asilimia 42 na kwa sasa umeshuka na kubaki kwa asilimia 17 tu sawa na kushuka kwa asilimia 25.

attachment.php
ili utafiti uonekane ni wa kweli waitishe uchaguzi wa kujaza nafasi za madiwani Arusha
 
Acha wazunguuke mikoani na hao jamaa. Ila nasi tunajipanga kufanya research isiyokuwa yakifisadi wasije wakashika midomo humu jamvini kwani taarifa zao za kisynovate hazitawapeleka mbali hapo 2015

CCM sio wazur wa marumbano kama ilivyo wapinzani kwani huku ni vitendo tu,jaribu kuchunguza hata humu jf mtaona jinsi mlivyo wengi na wazur kwa mabishano ila CCM ni wazur wa vitendo tu.Na hiz harakati zenu mtabadili majina(sangara,papa,mkizi&move 4change ila ikulu kwenu ni ndoto)
 
Msipate shida kujadili report za hawa jamaa, nitawaelekeza maeneo ambayo mkienda muda kama huu mtawakuta vijana wao wanapika Data. Hapa nitataja baadhi ya maeneo tu ila nikipata muda nitawaeleza maeneo mengine zaidi. Arusha wapo Kismayo guest house ipo Levolosi pembeni ya ofc za magari ya Mwanza. moshi wapo Devotion guest house dar street, Mwanza wapo Lena Hotel ipo opposite Thaqaafa secondary school, Mbeya-Mariset iliyopo Mwanjelwa na Mafao ipo soweto karibu na Mbeya Carnival, dodoma- Kavula guest house ipo Bayi road, morogoro- Kwa babu au Shela park.
Nikikumbuka zingine nitawaletea ila haya ndio maeneo ambayo ukienda jioni lazima utawakuta na ni mabingwa wa kujiungia chumbani na kutengeneza data

kutueleza wanapoishi kunamahusiano gani na data zao kua potofu,hata mimi najua unapokaa nikutajie?
 
Utafiti huo huo umeonesha Dr. Slaa ndiye anayekubalika zaidi kwa nafasi ya Urais kwa sasa. By the way, chama kinachokubalika kwa 31% dhidi ya 51% za chama kilichotawala kimabavu kwa miaka lukuki unawezaje kusema ni "dhaifu sana" kwa kuzingatia mfumo kandamizi uliopo?

kaka mfumo upi wa kigandamizi wewe unaoeleza. Huo mfumo ambao mwanachama akitoka anaambiwa kwaheri au kwa mwanachama akitoka anatukanwa na kutishiwa maisha.huu mfumo wa chadema wa kutishana ndio unaona wa kidemocrasia
 
Nitumi email yako nikupe report kamli, with sample selection method, sample quality, timeframe na mengine yote. 🙂I have seen it, and I believe they have respected international standards in this regards. To me the results are sahihi.
red! kwanini usiitupie hapahapa!!
 
kaka mfumo upi wa kigandamizi wewe unaoeleza. Huo mfumo ambao mwanachama akitoka anaambiwa kwaheri au kwa mwanachama akitoka anatukanwa na kutishiwa maisha.huu mfumo wa chadema wa kutishana ndio unaona wa kidemocrasia
Hiv bashe ni mtanzania au siyo matanzani. Maana ata kikwete alichezeshwa nyimbo hii, mlimkataa na mkamtumia,nyis ndio wabaguzi kama mnabaguana wenyewe kwa wenyewe basi nyie n hatari sana, karbun cdm
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom