CCM Maarufu: Utafiti wa Synovate wabainisha!

CCM Maarufu: Utafiti wa Synovate wabainisha!

TandaleOne

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2010
Posts
1,644
Reaction score
709
Taasisi ya kujitegemea inayofanya Utafiti wa masuala mbalimbali ikiwemo Utawala bora na Demokrasia hapa nchini, Synovate imetoa matokeo yake ya utafiti wake uliomalizika hivi karibuni na kubainisha vipengele muhimu ambavyo vinabashiri mustakabali wa uhai na uimara wa vyama vya siasa hapa nchini.

Utafiti huo umebainisha kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndicho chama maarufu zaidi hapa nchini kwa sasa ambapo umaarufu wake umeongezeka maradufu, utafiti huo umeonyesha kuwa zaidi ya asilimia 52 ya wananchi wote wa Tanzania wangependa kuijiunga na CCM, na hivyo kudhihirisha kuwa CCM bado ni chama Imara na kinachopendwa zaidi na watanzania walio wengi.

attachment.php

Rekodi hiyo mpya ya CCM inakinzana na kuviacha mbali vyama vya Upinzani ambavyo graph yao imeendelea kushuka na kupoteza umaarufu kwa kiasi kikubwa, mfano wa chama ambacho kinaongoza kambi ya Upinzani bungeni Chadema kimeshuka sana na kwamba ni asilimia 31 tu ya wananchi ndio ambao wangefikiria kujiunga na Chama hiko. Pamoja na M4C, operesheni Sangara,n.k bado hali ya chama hiko ni dhaifu mno kulingana na tafiti hizi. Hali ni mbaya zaidi kwa CUF ambayo ina asilimia 4 tu ya kuungwa mkono na watanzania.

attachment.php

Utafiti huo pia umebainisha kuwa kupanda kwa CCM na kuongezeka kwa umaarufu wake kunatokana na Utekelezaji wa Ilani yake kwa kasi inayoridhisha, lakini zaidi ni kutokana na Uchaguzi wake ambao umetengeneza safu mpya ambayo ni bora na imara ya Uongozi ndani ya Chama hiko kikongwe na MAARUFU duniani.

Lakini pia tafiti ya synovate imeenda mbali zaidi na kubainisha kushuka kwa Umaarufu wa Dr Slaa maarufu kama "BABU" ambapo imeelezwa kuwa ameshuka kwa asilimia 25 ambapo tafiti ya awali ilibainisha kuwa umaarufu wake ulikuwa ni kwa asilimia 42 na kwa sasa umeshuka na kubaki kwa asilimia 17 tu sawa na kushuka kwa asilimia 25.

attachment.php
 
Attachments

  • synovate2.jpg
    synovate2.jpg
    29.8 KB · Views: 4,087
  • synovate1.jpg
    synovate1.jpg
    33.1 KB · Views: 4,014
  • ccm-inakubalika.jpg
    ccm-inakubalika.jpg
    45.7 KB · Views: 3,967
  • Synovate-Report-2011-2012.pdf
    Synovate-Report-2011-2012.pdf
    1.3 MB · Views: 112
Kabla hatujadili huu Uongo kwanza fafanua kuhusu EGM-Butimba TCC na Matokeo ya IV- 29---------G-D,M-F
 
Asilimia 52 ya wananchi wote Tanzania? Really?

Wamejuaje hilo? Wamehoji wananchi wote Tanzania? Kivipi?

Tunacheka waliofeli Form Four wakati miswaki galore.

Unapotoa figures kama hizi, unatakiwa kutoa sample space, methodology na margin of error.

Basic shyt.

Tusitake kupelekana kama ng'ombe. Angalieni Gallup polls zinavyoripotiwa.
 
Utafiti huo huo umeonesha Dr. Slaa ndiye anayekubalika zaidi kwa nafasi ya Urais kwa sasa. By the way, chama kinachokubalika kwa 31% dhidi ya 51% za chama kilichotawala kimabavu kwa miaka lukuki unawezaje kusema ni "dhaifu sana" kwa kuzingatia mfumo kandamizi uliopo?
 
Asilimia 52 ya wananchi wote Tanzania? Really?Wamejuaje hilo? Wamehoji wananchi wote Tanzania? Kivipi?Tunacheka waliofeli Form Four wakati miswaki galore.Unapotoa figures kama hizi, unatakiwa kutoa sample space, methodology na margin of error.Basic shyt.Tusitake kupelekana kama ng'ombe. Angalieni Gallup polls zinavyoripotiwa.
Nitumi email yako nikupe report kamli, with sample selection method, sample quality, timeframe na mengine yote. 🙂I have seen it, and I believe they have respected international standards in this regards. To me the results are sahihi.
 
Sina uhakika Na Hili ila nadhani Ofisi zote Za Synovate EA ziko bize Na uchaguzi wa keshokutwa KENYA. Kwa sasa wanafanya tafiti Za uungwaji Mkono wagombea Out of Kenya baada ya juzi ya Ndani as KURA YA maoni ya Synovate kuonyesha Uhuru Kenyatta amepanda hadi 44.8%, juu ya Raila Odinga 44.4%. Mudavadi 5.2%, Kenneth 1.6% Karua 0.8%.

Mengine yanayoendelea mmmh..! Sijui labda Kuna Synovate nyingine siijui..

Please TandaleOne Au Mwali mni pm hiyo sampling niiwasiliahe Kama ni Yao .. Mie niko mwazi sana .. Napenda kweli iwe kweli Na jamii ipokee kilicho kweli.
 
Last edited by a moderator:
Mh chama maarufu ni chadema chama cha zamani saana ni ccm hilo halina ubishi
 
Huyu jamaa ni muongo... hakuna ripoti yeyote ya synovate imetolewa... mnajadili hewa
 
Sina uhakika Na Hili ila nadhani Ofisi zote Za Synovate EA ziko bize Na uchaguzi wa keshokutwa KENYA. Kwa sasa wanafanya tafiti Za uungwaji Mkono wagombea Out of Kenya baada ya juzi ya Ndani as KURA YA maoni ya Synovate kuonyesha Uhuru Kenyatta amepanda hadi 44.8%, juu ya Raila Odinga 44.4%. Mudavadi 5.2%, Kenneth 1.6% Karua 0.8%.

Mengine yanayoendelea mmmh..! Sijui labda Kuna Synovate nyingine siijui..

Please TandaleOne Au Mwali mni pm hiyo sampling niiwasiliahe Kama ni Yao .. Mie niko mwazi sana .. Napenda kweli iwe kweli Na jamii ipokee kilicho kweli.

Hakuna research yeyote iliyofanywa na synovate siku za karibu...
 
Nitumi email yako nikupe report kamli, with sample selection method, sample quality, timeframe na mengine yote. 🙂I have seen it, and I believe they have respected international standards in this regards. To me the results are sahihi.

weka hapa jukwaani.... mwongo weee
 
Tuwekee population sample ya utafiti huo kabla ya kuingizwa chaka.
 
Asilimia 52 ya wananchi wote Tanzania? Really?

Wamejuaje hilo? Wamehoji wananchi wote Tanzania? Kivipi?

Tunacheka waliofeli Form Four wakati miswaki galore.

Unapotoa figures kama hizi, unatakiwa kutoa sample space, methodology na margin of error.

Basic shyt.

Tusitake kupelekana kama ng'ombe. Angalieni Gallup polls zinavyoripotiwa.

Huyu mtu anayejiita Tandale na id nyingie akiwa amevaa kike kapika hizi data kwenye kiPC chake hapo Lumumba...
 
Nyinyiemu wana 'mbinu' nyigi wanaanza kuandaa mazingira ya kuiba kura 2015 maana ni umaarufu gani huo wakati chaguzi zote zinazofanyika kwa sasa CDM wanazoa 85% and more iwe kwa wananchi au Mahakamani. Mimi sijawahi kukutana na mtu kahojiwa na hawa wachumia tumbo. Peopleeeeeeez
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom