CCM Maarufu: Utafiti wa Synovate wabainisha!

CCM Maarufu: Utafiti wa Synovate wabainisha!

Tandaleone,kama hujui kuwa wilayani magu kulifanyika uchaguzi mdogo wa vijiji na vitongoji basi huna hata idea na unachoandika hapa.Tangu baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 zimetokea chaguzi ndogo mbalimbali ambako CHADEMA ,imedhihirisha kuwa kinaaminiwa na watanzania,na kinazidi kuaminiwa,kama na hilo hulioni,basi utakuwa kipofu

Nafahamu kuwa hivi karibuni kulikuwa na uchaguzi katika kata 29 Tanzania bara na katika hizo matokeo ni kuwa 24 zilichukuliwa na CCM na nne (4) tu ndizo zilienda Chadema na Moja CUF..,je wewe una matokeo tofauti na hayo naomba unijuze..,ama matokeo haya yanatafsiri gani kwako, kwamba chadema ama ni CCM ndio maarufu na chenye nguvu zaidi..!
 
Mizuzu ni mizuzu tu hata yapelekwe wapi! Sasa hapa CCM wanamdanganya nani? Au watakuwa wanadanganyana wenyewe kwa wenyewe
 
Tandale ni mgonjwa, hivi kweli hajui uchaguzi uliofanyika karibuni kule Magu, au kwa sababu Ccm ilianguka vibaya sana basi ameamua kuifuta kwenye medula oblangata yake? Amazing
 
Rashidabdallah. Bado ni ukilaza mkuu kwasababu kama kuna mapungufu kwenye utafiti ni lazima wayaseme kwenye, 'limitation of the study' ili tunapotathmini data tuwe tunajua zilipatikana au hazikupatikana data zilizotarajiwa kwa kiasi gani.Ukweli nadhani ni kuwaambia wazi kwamba utafiti mbuzi wanaoufanya hauna nafasi kuelekea 2015.
 
Last edited by a moderator:
Ally Kanah. Watu wanapojadili masuala ya msingi,nawe unapochangia kumhusu mtu badala ya masuala bila shaka wanakudharau.Kumbuka ni vema ukakaa kimya ili watu wafikiri labda una busara,kuliko ukatoa mawazo yako kisha watu wakathitisha bila ya shaka kwamba wewe ni kilaza.
 
Last edited by a moderator:
ccm ni seduction masters,umeona ilivyowatongoza kwa pilau na visenti na kuwapakata shonza,mwampamba,bagenda,wassira,kabourou,etc etc etc
 
Kwanza nawasalimu ndugu zangu wote humu JF! Mwenzenu huwa mzimu wa REDET na tafiti zake unaniandama kila nisikiapo neno utafiti.Kuna viji taasisi vinaibuka na kushika kasi kila tunapoelekea kwenye uchaguzi nchini.Unaweza kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa au uchaguzi mkuu ambapo vitaasisi hivyo hujifanya kutoa tathmini za kisiasa bila kuainisha 'objectives of the study,population size,area of study e.t.c) Kama hutakuwa makini unaweza kuaminishwa ujinga nawe ukapoteza muda kujadili kitu ambacho hakipo ukiacha mambo muhimu kuhusu gesi,uranium,kushuka kwa kiwango cha elimu,migogoro ya ardhi,katiba mpya,vitambulisho vya taifa,vazi la taifa,kilimo na teknolojia eti tunajadili CCM kimekuwa maarufu. Nahoji,kati ya chama cha zamani na vyama vipya kipi kinaweza kupanda kuwa maarufu? Utafiti wa Synovate ulilenga nini,wametumia vigezo gani kupima umaarufu na wamewahoji watanzania wangapi? Nielewesheni!

Hii naona ni waganganjaa maana utafiti una utaratibu wake na unabidi kuwa wazi njia zilizotumika mpaka kutoa majibu ya tafiti. Sasa hii ya awa MAKAJANJA wa UCHAKACHUAJI naaminilengo lao ni kututoa kwenye mijadala ya msingi....
 
@Ryalo. Ni kweli mkuu na tumewashtukia kitambo,sasa hatujadili taarifa yao ila tunawajadili na kuwapa taarifa kwamba hatupotezwi njia na ujinga wanaopanga.
 
Wewe Tandale shule umefeli na ndio sio ajabu ripot umeiandika kiushabiki fikra zako zilivyo ndogo unafurahia. Cha ajabu wadogo zetu wamefeli hatujui na wala wewe hujui wataenda wapi halafu unaweka kidomo-domo chako mbele eti eti "imetokana chama kutekeleza ilan yake ya uchaguzi kwa kasi yenye kuridhisha"
Kwa ushauri tu ndugu yangu kama jinsi elimu yako ilivyo ya kuunga-unga a.k.a tia maji tia maji nenda karekebishe matokeo yako ya form four halafu utuelezee hiyo advance uliisomaje pale Tcc-butimba!

"Mwehu mwehu tu sio lazma akasafishe jalala"

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hakuna research yeyote iliyofanywa na synovate siku za karibu...
Hata kama ni kweli ni ripoti ya Snovate kwani wewe unawaamini? mimi binafsi siwaamini na ni mpuuzi peke yake ndio atawaamini hawa vinyago.

Wakishatowa ripoti zao za kitapeli wanaandikiwa cheque na ikulu kupitia kwa Salva Rweyemamu. open ur eyes msiwe wajinga kiasi hiki.
 
Nafahamu kuwa hivi karibuni kulikuwa na uchaguzi katika kata 29 Tanzania bara na katika hizo matokeo ni kuwa 24 zilichukuliwa na CCM na nne (4) tu ndizo zilienda Chadema na Moja CUF..,je wewe una matokeo tofauti na hayo naomba unijuze..,ama matokeo haya yanatafsiri gani kwako, kwamba chadema ama ni CCM ndio maarufu na chenye nguvu zaidi..!
Tueleze kwanza Division 4 point 29 uliwezaje kupata Masters ya mfukoni?
 
Nitumi email yako nikupe report kamli, with sample selection method, sample quality, timeframe na mengine yote. 🙂I have seen it, and I believe they have respected international standards in this regards. To me the results are sahihi.

I never trust tafiti za hawa jamaa hasa kwenye mambo haya ya kisiasa! Huko Kenya kwenyewe hawaaminiki. Si mnakumbuka 2010 wakati wa harakati za uchaguzi walivyokuwa wanatoa takwimu zisizokuwa na detail za kutosha na za uongo kwa kushirikiana na REDET. Yule Dr. wa UDSM kama sikosei Dr. Leyaru alipokuja na statistics na analysis za kuonyesha CCM na CDM itashinda wapi na vipi, hawa jamaa wakaonekana watupu. Utafiti wa yule Dr. ulikuwa almost to reality on the ground na matokeo yalipokuja yalionyesha vivyo hivyo. Leo hawa jamaa wanaibuka na ujinga wao tena wanadhani tumesahau. simply data miners!!!
 
This is news, limeshakuwa la chadema?!!! Toka lini???? Wamelinunua kwa nani???

Hivi Majengo ya CCM waliyanunua au waliyapora!!! Whether Chadema wamepanga au la, does not justify anything done by CCm kwa kupora majengo na viwanja vya Watanzania. Siku hizi tunaona hata viwanja vya wazi vinaporwa na CCM ili kuweka ma-kontaina ya ofisi.
 
Bila hata ya utafiti .. CCM ni baba bado
 
Sampuli yao inatia mashaka. Naona wamechukua respondents wengi kutoka Msata, Chalinze na Kisarawe. It does not represent the population.
 
Makala Jr

Hawa ni njaa kali tu. Tafiti zao zinaongozwa na matumbo yao. Wasitubabaishe na tafiti pori. Wanakolalia sisi ndiko tulikoamkia. Nimeambiwa utafiti wao mwingine unaofuata Mamvi na Zitto watapanda kidogo halafu Slaa atashuka tena kidogo....

Kumbe lengo ni kumfifisha dr slaa eee! Sasa watz wa leo sio kama wa miaka 10 iliyopita. Hata ss tulioko huku wanavyosema wenyewe pembezoni mwa nchi tushaistukia ccm kuwa si lolote na hatuyumbishwi na tafiti za kizushi kama hz. Viva cdm!
 
Last edited by a moderator:
ccm bado kina nguvu. lazima tuseme ukweli. kujiridhisha kwa kusema kuwa ccm kinaporomoka tunajidanganya. waliweza kutoka salama katika uchaguzi na uteuzi wa wajumbe wa halmashauri kuu na kamati kuu. jambo hilo limewasaidia kuwa imara hadi hii leo. kuhamia ccm kwa akina juliana na wenzake kumezidi kukiimarisha chama. wanazunguka nao mikoani kuiponda chdm
 
Sampuli yao inatia mashaka. Naona wamechukua respondents wengi kutoka Msata, Chalinze na Kisarawe. It does not represent the population.

Inanikumbusha utafiti wa Redet 2010 uliochukua sample toka makada wote wa CCM ndani ya kata wazifanya utafiti ili kutoa matokeo yanasupport CCM kuwa itashinda uchaguzi. Ukiona kina synovate wanaanza kutoa ripoti zinazolinganisha Dr slaa na CCm ujue maji yameifika shingoni CCM wanatafuta njia yoyote ya faraja na ku justify kukaa kwao madarakani ki mbavu!!

Nani asiyejua kuwa sasa CCM imetikisika vibaya hasa baada ya sakata la vurugu za udini zinalindwa na serkali? Nani asiyejua kuwa matatizo ya maji sasa yanaitikisa serkali baada ya kukataa suluhisho la kujadili wazi bungeni leo kila kukicha wanatafuta kuzima hasira za watu kukosa maji muda wote D'salaam badala ya kutafuta njjia ya kutatua tatizo kwa kuleta maji. Nani asiyejua kuwa wengi walio maliza f4 na wazazi wao wana uchungu kwa mwenendo mbaya wa elimu Tanzania? Zaidi ya wanafunzi 5 waliomaliza f4 wamekwisha jiua!! Kuna njia nyingine kubwa zaidi ya kuonyesha uchungu alio nao mtu zaidi ya kuwa tayari kutoa uhai wake!! Synovate itakuwa inaamanisha watanzania ni watu wa ajabu kama chama chenye kuongoza serkali inayosababisha haya yote yanayotia uchungu kimeendelea kuimarika na kupendwa zaidi!!

Hapa kuna jambo liliojificha katika matokeo ya ya utafiti wa synovate.
 
Kichwa cha mada kinapotosha sana. CCM maarufu au umaarufu wa CCM umeporomoka? Chama tawala kuwa na acceptance level ya 52% sio jambo la kushangilia kwa chama hicho. It is a huge huge thing. By the time elections come CCM will have less than 30% and end this corrupt regime

Kaka unajidanganya sana.,tena unajitia upofu wa macho na akili.,upofu ambao hautaleta afya nzuri ya kisiasa kwako na kwa Chama chako.

Naomba usome hapa;

Kushindwa kwa CDM;
Kulingana na yanayoendelea hivi sasa ndani ya CDM kikiwa kama chama kikubwa cha upinzani kunaonyesha dhairi kushindwa kwake katika kufikiri juu ya njia sahihi na mbinu piganizi katika kuyashughulikia matatizo yanayowakabili watanzania kiuchumi, kiutawala, pamoja na kijamii.
Na nitayazungumza machache na kwa mifano ili watu wapate kuelewa kiunaga ubaga
1: Katika ufisadi, CDM haijaonesha mipango thabiti juu ya kulishughulikia suala la ufisadi nchini zaidi ya kuitisha maandamano yasiyo na tija na kudai kuwa mafisadi wanabebwa na mahakama na kusahau kuwa wao ndio wanatoa mawakili wa kwenda kusimamia mafisadi mahakamani (Mabele Marando), lakini ni wazi kuwa kama CDM wangelikuwa na nia thabiti ya kulisimamia hili wanao uwezo wa kisheria kama chama cha siasa na haki ya kikatiba ya kupendekeza mchakato wa namna ya kuwakamata na kuwashughulikia wala rushwa na mafisadi na hata kutoa direction ya adhabu na kanuni zinazosimamia utekelezaji wa mikakati hiyo ya kupambana na rushwa bali tumeona kuwa wapo viongozi katika CDM ambao wanapropagate ufisadi katika nafasi walizonazo hali inayotoa ishara ni kwa kiasi gani wanaweza kuwa pindi wakipata nafasi kubwa, kumbuka ya Mshahara wa Dk Slaa, kumbuka Magari ya Mbowe, kumbuka ukwepaji wa kodi wa chama, yale ya diwani kule Mara, na sasa kashfa ya Dr slaa kuchukua fedha ya ruzuku kwa matumizi yake binafsi.

2: Katika nchi ambayo demokrasia ni msingi na daraja la kuendea utawala wa sheria, wananchi (wapiga kura) lazima wawe na ufahamu wa kutosha juu ya maamuzi wanayotakiwa kuyachukua pindi wanapotumia fursa yao ya kupiga kura, Katika hili CDM wamekuwa mbele kulalamika na kupinga matokeo bila kufanya study yakinifu juu ya uhalisia wa wapiga kura Tanzania, wakiwa wanatumia sample space ambayo ni irrelevant kwa wakazi wa mijini na watumiaji wa mitandao pekee katika kufanya tathmini zao za ushindi ama kushindwa., katika uchaguzi mkuu uliopita na zingine ndogondogo kama igunga, Mwanza na (hata chaguzi za hivi karibuni za kata 29 ambazo CCM ilishinda kata 24 kati ya hizo) tathmini za kwenye mitandao zilionyesha kuwa CDM itashinda kwa kishindo na matokeo yamekuja tofauti mara zote katika chaguzi zote, na ni baada ya matokeo ndipo CDM hukakamaa na kunadi kuibiwa kura baada ya kutulia na kujifanyia tathmini yakinifu. UKWELI NI KUWA..,wapiga kura walio wengi ni watu waishio vijijini ambako CDM hawakubaliki na propaganda zao hazifiki huko, Siasa za CDM ni za mlalo na zimeegemea upande mmoja , zipo jamiiforums zikiipiga vijembe CCM, zipo Arusha wakiandamana kila uchao na kulala nje, wakiamasisha kujitenga na kujitawala, wakiunadi ukanda na kupinga utaifa, lakini kuigawa siasa ya Tanzania kwa kigezo cha kanda na kuimarisha baadhi ya watu Fulani kwa kuwapa stahili kubwa katika chama, na nafasi za uongozi, hayana mvuto wala uhalisia wa siasa za Tanzania,CDM ipo Arusha kwa kila nguvu kana kwamba hakuna maeneo yenye kuhitaji usimamizi wa karibu wa kisiasa na kiuchumi bali ni Arusha pekee.

Lakini kama hayo hayatoshi, ni kuwa wakati wakiibeza na kuishutumu serikali ikishindwa kusimamia fedha na miradi inayoelekezwa katika maeneo ya vijijini CDM inashindwa kuweka mkakati wa ufuatiliaji na taasisi ya kuhoji matumizi na utekelezaji ( hili linawezekana kisheria) ambapo kupitia taasisi hiyo usimamizi utaimarika lakini pia wapiga kura watapata mrejesho na kushuhudia nia ya kweli ya wanasiasa wao ya kuwaletea maendeleo.

3: Kulingana na mfumo wa sasa wa kiuchumi wa soko “holela” ambapo wenye nacho hupata fursa ya kujitajirisha zaidi, CDM inayofursa ya kutoa muelekeo wa uchumi na mfumo unaojali na kugusa pande zote kwa kushauriana na wachumi walionao (kama ZITTO) na kuandaa proposal ya sera zenye kulenga mabadiliko chanya kwenye sekta ya fedha,kodi, biashara, mishahara,na miamala mbalimbali katika sekta tofauti za kiuchumi hususani kilimo, ambapo watanzania walio wengi wamejiajiri huko. Na hili lazima lifanyike chini ya wataalamu wa uchumi na fedha.
4: katika mambo ambayo wapinzani (hasa CDM) wanayapigia kelele ni pamoja na undugunization katika ajira na mgawanyo wa vyeo na madaraka, katika hili CDM tuliamini watakuja na mbinu tofauti ya kuhakikisha kuwa vyeo na madaraja ya kazi yanagawanywa kulingana na uwezo, elimu na nafasi ya mtu,lakini tofauti na matarajio ya wengi bado ipo system ya kulimbikiziana vyeo ndani ya CDM, watu kama mnyika na wengineo wanavyo vyeo zaidi ya vitano wakati mmoja kana kwamba hakuna vijana wengine katika CDM walio na uwezo na elimu ya kushika nafasi hizo. Lakini pia upo upendeleo wa dhahiri wa kupeana vyeo kwa nasabu na ukoo, ipo mifano katika hili, Tundu lissu na dada yake, Slaa na hawara yake,Ndesamburo na mwanae,mbowe na familia ya Mtei n.k

5: kupoteza umaarufu na kushindwa ushawishi kwa jamii.,hivi sasa kwa mtu aliye makini na siasa za ndani ya nchi, anaweza kugundua kwa urahisi na kukubaliana moja kwa moja na ripoti ya synovate (ambayo kwangu ni sahihi) kuwa CDM wamepoteza umaarufu na ushawishi kwa watanzania makini, umaarufu ambao ulipatikana kwa gharama kubwa na akili nyingi, hii inatokana na kauli za kibaguzi za viongozi wa CDM kama Mzee Mtei (Muasisi CDM), Joshua Nassar (Mb, Arumeru) na Wenje (Mb, Nyamagana) na kupoteza uelekeo kwa media outlet zinazotumiwa na chadema, mfano wa magazeti kama mwanahalisi,mtanzania,Tanzania daima,mwananchi na social medias kama jamii forums ama jambo forums,amua sasa blog n.k ambazo kwa mara ya kwanza zilikuwa na mvuto mkubwa kwa watanzania wapenda habari lakini kutokana na kuandika kwa mlengwa mmoja na kwa muda mrefu bila kubadilika zimepoteza ladha na thamani yake kwa watanzania, upendeleo, uzushi, upotoshaji wa dhahiri pamoja na uchochezi vimechangia kuondoa hadhi na heshima ya vyombo hivi kwa watanzania wanahabari na wapenda habari.
6: Migogoro ndani ya chama.,CDM kikiwa chama kilichojitokeza mbele ya watanzania kama chama cha wapenda mabadiliko, wapenda vijana na wanaharakati wenye kutaka Tanzania yenye neema ipatikane, bahati mbaya CDM kimekuwa kikijiingiza ndani ya migogoro ya mara kwa mara tena kwa viongozi wake wa ngazi za juu., ili linatokana na ukweli kuwa wapo wapenda madaraka wasiotaka kupisha wenzi wao katika nafasi za kiutawala ndani ya chama, wenye kutaka kutoa kauli za mwisho zisizopingwa wala kukosolewa.,wenye ukanda, udini na ukabila hali hii inatia mashaka kwa watanzania walio wengi hivyo kupoteza ari na hamasa katika kukipenda na kukiamini CDM. Kisa cha Zitto na Slaa kipo dhahiri katika kutoa picha ya suala hili. Shibuda, Arfi, Mwanpamba, Shonza etc against “godfathers” ndani ya CDM.

Haya na mengine mengi yamewafanya watanzania wapoteze imani kabisa na chama hiko cha siasa kulingana na mfumo huo mbaya wa siasa zao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom