macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 29,226
- 60,296
Hawa Synovate walikodiwa na CCM kufanya huu utafiti CHADEMA wameichomeka hapo kutimiza malengo ya CCM, lakini mimi sioni shida acha waendelee kujidanganya! Maswali karibia yote yanaihusu CCM, kama Dr. Slaa ndo atakayeshinda ukifanyika uchaguzi, inakuwaje chama chake kisiwe maarufu umaarufu wa chama uwe kwa ccm! Uongo mtupu!
Hii kampuni ni ya kitapeli na wala rushwa wakubwa. Msikubali kuingizwa chaka. Hakuna utafiti hapa ni maandalizi ya kumbeba mtu fulani na kumwangamiza mtu fulani. Dili lote kuna jamaa amesema analifuatilia na akifanikiwa kupata info atawaumbua. Habari za kuaminika ni kuwa hizi ni fedha za mzee mamvi zinaongea. Deal ni kwamba baada ya muda yatatolewa tena matokeo mengine ya kuonyesha Dr. Slaa/wagombea wengine wameshuka kwa percentage fulani na mzee mamvi ameongeza pcg fulani, halafu uchaguzi ukikaribia ndio Mamvi ''atapaishwa'' kwa kasi na kumpita Dr Slaa/wagombea wengine. Tuombe uzima jamaa akifaniwa atatuletea kwa undani na vielelezo vyote.